Brazameni akadhani Arusha…….!


Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Likes
1,319
Points
280
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 1,319 280


Ingawa tukio hili lilimtokea rafiki yangu katika mghahawa mmoja maarufu ulioko katikati ya jiji hili la Dar es salaam, lakini mpaka leo nimejikuta sitamani kukanyaga katika mghahawa huo.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Ijumaa ya Mei 2005, majira ya saa saba mchana nilikuwa nimetoka benki kuchukua vijisenti vyangu vya mshahara wa mwezi huo wa Mei, mara simu yangu ikaita. Nilipotazama namba ya mpigaji nikagundua kwamba ni ya rafiki yangu niliyewahi kufanya naye kazi miaka ya mwanzoni mwa 1990 kwenye kampuni moja ya utalii jijini Arusha.

Mimi ndiye niliyetangulia kuacha kazi na kukimbilia jijini Dar kwa ajili ya kusoma na rafiki yangu naye alikuja kuacha kazi baadae na kuja Dar pia ambapo alipata kazi kwenye Hoteli moja maarufu ya nyota tano.

Nilipokea ile simu na kuzungumza naye. Kwa kifupi alinijulisha kwamba, ameacha kazi na alikuwa ananiomba nimuandikie barua ya kumdhamini kwa kuwa amepata kazi mahali pengine. Nilimkubalia na kumwelekeza tukutane kwenye huo mghahawa ulioko katikati ya jiji mkabala na ilipo British Council ili nimwandikie hiyo barua ya kumdhamini.

Ukweli ni kwamba rafiki yangu huyo alikuwa ni mtu wa kujikweza sana na alikuwa ni mtu anayependa promo na kuishi maisha asiyostahili, nilikuwa nagombana naye mara kwa mara kutokana na tabia yake hiyo maana mara nyingi ilikuwa ikimuweka katika wakati mgumu. Ajabu ni kwamba hata alipohamia jijini Dar hakuweza kuacha tabia yake hiyo.

Nakumbuka mimi ndiye niliyetangulia kufika kwenye ule mghahawa na nilipofika nilikaa kwenye viti vilivyopo nje ili iwe rahisi kumuona pindi atakapofika. Haikuchukua muda mrefu jamaa alifika, tulisalimiana na bila kupoteza muda akatoa makabrasha yake aliyokuwa ameyaweka kwenye mkoba wake mweusi ili niweze kumuandikia hiyo barua ya udhamini.

Mara ghafla kama aliyeona kitu cha kushangaza alinyanyuka na kuniambia nimfuate upande wa pili wa ule mghahawa ambapo kulikuwa na wateja wengine wakijipatia mlo wao wa mchana. Nilinyanyuka na kumfuata. Alipofika pale alivamia meza waliyokuwa wamekaa watu wawili, mvulana mmoja mtanashati hivi na msichana mmoja mrembo wa kuvutia hasa na mwenye umbo la kibantu lakini lisilochusha…. Alikuwa amejaaliwa kijikalio cha kiushikaji na nyonga iliyokatika na kutenganisha eneo la juu na la chini kwa uwiano wenye kuvutia, alikuwa na kifua kipana kilichobeba matiti makubwa kiasi. Chini alikuwa amebeba miguu iliyoendana na umbo lake. Kwa kweli alikuwa ni binti mzuri na anayetamanisha hasa.

Rafiki yangu alimuuliza kwa ukali yule binti kuwa anafanya nini pale na yule mvulana. Katika hali ya kumshangaa rafiki yangu, yule binti alimjibu kwa dharau huku akiwa amebetua midomo yake kwamba, yuko lunch na mpenzi wake na wakati huo alimkumbatia yule mvulana na kumpiga busu shavuni.

Yule rafiki yangu huku akionekana kufura kwa hasira alimvuta yule msichana na kuanza kumfokea kwamba kwa nini anamdhalilisha mbele za watu wakati anajua wazi kwamba yeye ni mchumba wake na aliahidi kumvisha pete ya uchumba hivi karibuni........

Wakati haya yote yanatokea, mimi nilikuwa pembeni nikishangaa, kwani sikujua lolote na watu waliokuwa kwenye ule mghahawa wakiwemo wapita njia wote waliacha shughuli zao na kuanza kufuatilia ule ugomvi kama kawaida ya wakazi wa jiji hili.

Yule mvulana aliyekuwa amefuatana na yule binti alikuwa amekaa kimya huku akimuangalia yule rafiki yangu kwa dharau. Alikuwa akimpandisha na kumshusha kwa macho kama vile anamfanyia tathmini. Yule msichana kwa dharau alimsukuma rafiki yangu na kumwambia, ‘usinishike na ukome kabisa kuniita mpenzi wako, mimi ni ghali sana na huwezi kumudu gharama zangu, hebu nenda huko uswahilini ukatafute visichana vya bei rahisi vitakavyositiri aibu yako, usiniletee shombo mie, MH%#*&%@.'

Rafiki yangu kusikia hivyo alikurupuka akitaka kumvamia yule binti ili ampige. Ilibidi nifanye kazi ya ziada kumdaka na kumzuia ili asizushe tafrani.

Yule binti huku akishangiliwa na wasichana wenzie waliokuwepo pale kwenye ule mghahawa aliendelea kumpaka mshkaji, ‘tena uniondokee na huyo mjinga mjinga mwenzio (yaani mimi)usinitie nuksi bure kwa mchumba angu na kama ni suala la pete ya uchumba, baba umechelewa, pete hii hapa (huku akionyesha pete yake ya uchumba ambayo ilionekana dhahiri kwamba ni ghali) siyo kile kipete chako ulichonipimisha cha 60,000/-"

Rafiki yangu kusikia hivyo alianza kuporomosha matusi akimtukana yule mvulana na yule msichana.

Yule mvulana akionekana mwenye busara alimtuliza yule binti na kisha kunyanyuka kutoka kwenye kiti na kumfuata rafiki yangu pale aliposimama. ‘hivi umemuelewa huyu binti au unataka kuwapa watu faida? Si amekwambia hakutaki, sasa unalazimisha nini?' yule mvulana alimuuliza rafiki yangu kwa dharau.

Rafiki yangu hakujibu kitu, alibaki kimya akiwa ameshikwa na butwaa asiamini kile kinachotokea mbele yake.

Yule mvulana alimshika yule binti na kuelekea kwenye gari lao aina ya Prado na kuondoka zao huku wakiacha vyakula vyao pale mezani ambavyo walikuwa hata hawajavigusa.

Tulibaki pale tukiwa kama tumemwagiwa maji. Wale wasichana waliokuwa wakimshabikia yule binti pale mghahawani waliendelea kutucheka na kutukebehi kwa vijineno vya kejeli. Nilijikuta nikiondoka mahali pale kimya kimya na kutoweka bila kumuaga rafiki yangu. hivi ninavyoandika huu mkasa, jamaa alisharudi Arusha na hata namba yake ya simu alishabadilisha na sijawasiliana naye hadi leo.

Nahisi yuko humu JF, na kwa sasa najaribu kuunganisha Dots kwenye threads za Erickb52, maana isije ikawa ndiye yule mshkaji wangu.

Habari za mchana bwana Erickb52…..LOL
 
Nicas Mtei

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Messages
11,566
Likes
117
Points
160
Nicas Mtei

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2010
11,566 117 160
Huyo atakuwa either Filipo, Mungi, Arushaone or Liverpoolfc, Mzee wa Rula, Erickb52. Ntaeleza sababu baadaye
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Likes
1,319
Points
280
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 1,319 280
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Messages
23,001
Likes
11,325
Points
280
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2010
23,001 11,325 280
Huyo atakuwa either Filipo, Mungi, Arushaone or Liverpoolfc, Mzee wa Rula, Erickb52. Ntaeleza sababu baadaye
Ha ha ha,
Mzee wa Rula!!!!!?
Hapana bana, can't be him aisee
 
Last edited by a moderator:
fazaa

fazaa

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2009
Messages
2,985
Likes
15
Points
0
fazaa

fazaa

JF-Expert Member
Joined May 20, 2009
2,985 15 0
Aisay rafiki yako alikosea angejifanya hamjui kabisa yule mwanamke....nice mafunzo:biggrin1:


Umeona kifuo hicho, yani time zote unataka kukilalia tu, hata sura yake ina leta 7/10
 
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,192
Likes
592
Points
280
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,192 592 280
ndo balaa la kuvamia hilo bila kujua
Unajitututmua kutaka kuishi maisha ya juu kumbe mwenzangu ni wa maisha ya chini madhara yake ndo hayo aise
Mpe pole sana rafikio na mwambie ajifunze ustaarabu
Inawezekana ni Erickb52 maana hiyo issue ashawahi kuisema sema hivi
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Likes
1,319
Points
280
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 1,319 280
ndo balaa la kuvamia hilo bila kujua
Unajitututmua kutaka kuishi maisha ya juu kumbe mwenzangu ni wa maisha ya chini madhara yake ndo hayo aise
Mpe pole sana rafikio na mwambie ajifunze ustaarabu
Inawezekana ni Erickb52 maana hiyo issue ashawahi kuisema sema hivi
Oyaaaa, Nicas Mtei, njoo pande hii aisee....!
Mr Rocky amesha confirm kuwa ni mshakji Erickb52, kwani alishawahi kuwasimulia walipokuwa pale Arusha Night Pack ila alipotosha ukweli.....LOL
 
Last edited by a moderator:
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,192
Likes
592
Points
280
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,192 592 280
Mtambuzi usisanue deal aise ataninyima ndyofu bure maana huyu jamaa akisikia tuu ni ugomvi aise
 
Last edited by a moderator:
Mabreka

Mabreka

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2012
Messages
709
Likes
5
Points
0
Mabreka

Mabreka

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2012
709 5 0
Oyaaaa, Nicas Mtei, njoo pande hii aisee....!
Mr Rocky amesha confirm kuwa ni mshakji Erickb52, kwani alishawahi kuwasimulia walipokuwa pale Arusha Night Pack ila alipotosha ukweli.....LOL
hapo kwenye red,
mkuu hiyo haifahamiki kwa jina hilo,.... weka jina lake bwana
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,717
Likes
3,387
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,717 3,387 280
Mwanaume hapaswi kugombana na mwanamke...wanawake ving'asti huringia sana vitobo vyao utadhani huwa havivundi
 
LiverpoolFC

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Messages
11,018
Likes
178
Points
160
LiverpoolFC

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2011
11,018 178 160
Mtambuzi, Mkubwa ndiyo umeamua kunianika hivi! Ina maana hata umeshindwa hata kuniPM na ukaamua kunianika mchana kweupe hivi!

NB:
Ngoja na nitakuja na ile aibu yako iliyokukuta siku ile pale Picnic na naweka live kama ilivyokuwa akianani!

Mtambuzi kweli rafiki yangu unanianika hivi hivi mchana kweupe,hamna shida!
 
Last edited by a moderator:
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,192
Likes
592
Points
280
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,192 592 280
LiverpoolFC kumbe mpo wengi masharo wa arusha mnaofanya vituko eeehh Erickb52 na Arushaone yashawakuta kama haya na wana simulizi nyingi tuu na ndo maana huwezi wasikia wameenda dar sana sana wanaishia mwanza au moro au dodoma
 
Last edited by a moderator:
jouneGwalu

jouneGwalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
2,688
Likes
85
Points
145
jouneGwalu

jouneGwalu

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
2,688 85 145
Makalio Bar...................!
Ah sasa wabongo mmezidi jamani hata jina la sehemu mnalibadili kisa linataja maumbile yetu???

Pale ni M.A.T.A.K.O Bar bwana hebu jembe liitwe jembe wajameni....

Afu hii sred imekaa kiugomvi kabisaaa

Natamani niwe @Eirickb52, au sijui ninunue ugomvi?

Mambo gani ya kukumbushana machungu haya we jamaa!
 

Forum statistics

Threads 1,250,178
Members 481,248
Posts 29,723,271