Bosi anasemaje kuhusu mkasa huu wa kukamatwa Askari wake?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,885
12,327
Nauliza kama boss ana taarifa, au habari inayohusu kamata kamata ya askari wake?

Kama anayo taarifa, je amechukua hatua gani kuwasaidia, au ukishamlipa mtu akufanyie kazi basi litakalompata huko mbeleni ni juu yake?

Au askari wake wamevuka mipaka ya kile alichowaagiza, kwa kuanza kumshambulia mkuu kwa njia ya matusi, na kupanga mambo maovu dhidi yake badala ya hoja?

Boss Karamagi, Prof Tibaijuka (mama wa vimboga mboga vya milioni 10) na wakwepa kodi wengine wa bandari, tafadhalini jitokezeni kuwasaidia Askari wenu.

Maana walipokuwa wakimtukana mkuu, mlifurahi na kuwapongeza, badala ya kuwaonya mapema kuhusu athari ya matusi yao.

Ukimya wa mkuu ulifanya wasahau kuwa wao wameshika makali, na mkuu ameshika mpini. Acha wagombanie panga tuone nani atakatika vidole.

Wengine wamesahau kuwa kila mchuma janga hula na wa kwao tu. Sasa hivi Karamagi anafuatilia tukio radioni tu na familia yake, masikio baridi kabisa.
 
Mkuu mnashangilia sana ila nina uhakika asilimia 100 ndugu zako wako wanao teseka sana kwa sababu ya upuuzi wa watawala wa CCM walio pita na waliopo sasa, ila mnajitia upofu na kushabikia ujinga, Binafisi ndugu zangu wana maisha magumu kijijini huko yanayo sababishwa na hawa watawala na hakuna siku moja nitakubaliana na upuuzi wao na hakuna hata siku moja nitashangilia
 
Ee MUNGU MKUU tunakuomba utujalie mwisho mwema, utupe upendo na amani, utuepushe na hila, wizi, mifarakano, kuuana na hadaa za unyanganyi.

Sote ni ndugu tupendane na tutendeane wema hakika tutaishi vema leo na kesho.
Maombi yako ni mazuri, ila kuna mtu au watu hawakuyaona ndomaana walikuwa wanazunguka kanda ya ziwa na maeneo mengine ya nchi kumtukana mkuu kwamba ana akili za matope.

Waliona wakiongelea mkataba tu bila kuingiza matusi wasingeeleweka.
 
Watu kama ninyi mlikuwepo enzi za ukoloni huku mkimshangaa Nyerere kuacha kazi ya ualimu ili alipiganie Taifa.
Hata Lisu aliona kuwa habari ya Nyerere kuacha ualimu ili apiganie uhuru ilikuwa ni porojo tu.

Screenshot_20230814-221425.png
 
Wao wanaikandia serikali,na moto wao umekua mkali sana,hivyo serikali iwape kashikashi,then baadae itawaachia.Soma mchezo chief.
Nimekusoma mkurugenzi... ila kumbuka kwenye msafara wa mamba kenge nao wapo.

Si kila kinachofanywa na mwanasiasa ni cha kuiga. Waswahili wanasema ukimuiga tembo kunya .......
 
Mkuu mnashangilia sana ila nina uhakika asilimia 100 ndugu zako wako wanao teseka sana kwa sababu ya upuuzi wa watawala wa CCM walio pita na waliopo sasa, ila mnajitia upofu na kushabikia ujinga, Binafisi ndugu zangu wana maisha magumu kijijini huko yanayo sababishwa na hawa watawala na hakuna siku moja nitakubaliana na upuuzi wao na hakuna hata siku moja nitashangilia
Yeye mwenyewe ni kapuku wa kutupwa
 
Nauliza kama boss ana taarifa, au habari inayohusu kamata kamata ya askari wake?

Kama anayo taarifa, je amechukua hatua gani kuwasaidia, au ukishamlipa mtu akufanyie kazi basi litakalompata huko mbeleni ni juu yake?

Au askari wake wamevuka mipaka ya kile alichowaagiza, kwa kuanza kumshambulia mkuu kwa njia ya matusi, na kupanga mambo maovu dhidi yake badala ya hoja?

Boss Karamagi, Prof Tibaijuka (mama wa vimboga mboga vya milioni 10) na wakwepa kodi wengine wa bandari, tafadhalini jitokezeni kuwasaidia Askari wenu.

Maana walipokuwa wakimtukana mkuu, mlifurahi na kuwapongeza, badala ya kuwaonya mapema kuhusu athari ya matusi yao.

Ukimya wa mkuu ulifanya wasahau kuwa wao wameshika makali, na mkuu ameshika mpini. Acha wagombanie panga tuone nani atakatika vidole.

Wengine wamesahau kuwa kila mchuma janga hula na wa kwao tu. Sasa hivi Karamagi anafuatilia tukio radioni tu na familia yake, masikio baridi kabisa.
Amna chochote
 
Ukitokea Dr Slaa kafia kwenye mikono ya hao wasiojukikana au hata mmoja wao yoyote, serikali itakua na sura gani?
Kwahiyo watu waachiwe tu wamtukane mkuu kuwa ana akili za matope kisa wakikamatwa wanaweza kufia mikononi mwao?

Mbona kina Tibaijuka, Pengo na wengine wengi wamemkosoa mkuu kistarab kuhusu mkataba na hawakuguswa?

Tatizo mdomo uliponza kichwa, walivyokuwa wanatukana na kumdhihaki mkuu huku watu wanacheka na mkuu yupo kimya wakaona kwamba wao ndio wenye haki ya kuongea chochote, sehemu yoyote na muda wowote, bila kupima wala kuangalia athari za maneno yao.
 
Back
Top Bottom