Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,480
Mkapa hiki kitabu kakiandika kwa woga, ujanjaujanja na uongo wa mapengo.
Hakutaka kufunguka kwa "ukweli na uwazi" kama anavyojitapa. Ndiyo maana kaandika kitabu kifupi. The main text is about 260 pages with added facts, figures, Azimio la Arusha excerpts etc that stretches it to about 320 pages.
Nimekisoma kitabu baada ya kusoma kitabu cha Samantha Power. Granted, Power simjui kama ninavyomjua Mkapa. I grew up with the Mkapas in Upanga. Ndiyo maana namjua Mkapa mpaka maongezi ya dinner table kwake na jinsi anavyokataza watoto kunywa maji mpaka wamalize kula kwanza. Mchizi wangu alikuwa ananilalamikia " Mshua noma sana, tukila anakataza kunywa maji. Anasema hakuna mtu kunywa maji mpaka umalize kula".
Lakini, ukimsoma Samantha Power unaona alivyokuwa open kuhusu maisha yake. Vulnerably so. Mkapa katupa hadithi nzuri ya maisha yake, ukweli kauficha.
Ujue unavyoandika zaidi, unafunguka zaidi. Ndiyo maana Mkapa kaandika kifupi sana.
Nakumbuka kwenda party moja ya kwa Mkapa, ali mu introduce Peter kama mwanaye ambaye anajivunia sana. Peter ni mtoto wa kufikia wa Mkapa, kwa Mama Anna na Basil Mramba.
Basi ungekuwepo kwenye hiyo party ungeona kwamba Mkapa anampenda Peter kuliko hata hao wanawe wa kibaiolojia kina Nico na Stephan.
Nimekuja kusoma kitabu, nakuta Peter kawa deleted kabisa. Hakutajwa hata sehemu moja. Katika watoto wanatajwa Nico na Stephan tu, kama Peter si mtoto wa nyumba ya Mkapa. Ukisoma kitabu bila kuijua familia, utafikiri Mkapa alimkuta Mama Anna bila mtoto. One can argue that this is a professional memoir with less emphasis on family, but then, if so, why mention Nico and Stephan?
Nikasononeka sana kwa unyanyapaa huu.
Sasa huo ni mfano mdogo tu wa maneno yaliyoachwa kuandikwa katika kitabu hicho ambayo watu wasioijua familia ya Mkapa kwa karibu hawatayajua.
Lakini wengine tunaojua ya ndani zaidi tumesoma kitabu tukaona hapa kaacha kusema hiki, hapa kaacha kile.
Mfano, Mkapa alikuwa na nafasi nzuri ya kuwa role model katika ndoa changa na za zamani zenye matatizo ambazo zinayakabili matatizo na kuyashinda.
Kuelekea uchaguzi wa 1995, familia ya Mkapa ilikuwa inasambaratika. Mama alikuwa amechoka ubabe wa mzee. Talaka ilikuwa inanukia (ingawa Mkapa alisema Wakatoliki talaka mpaka idhini ya Papa, na yeye alikuwa radhi kuishi sehemu tofauti na Mama Anna lakini hakuwa tayari kumtaliki). Msaada pekee ukawa Nyerere. Akamwambia Mkapa wewe unaenda kuongoza nchi, sitaki kusikia maneno ya talaka wala kuachana, mtakaa chini, mtazungumza, mtamaliza tofauti zenu na mkeo.
Wakakaa chini, wakazungumza, wakamaliza tofauti. Nyerere ndiye aliyewasuluhisha. Haya ni maneno ya kutoka kwa wanafamilia wenyewe.
Ukisoma kitabu utafikiri wamekuwa kwenye ndoa ya furaha mwanzo mwisho. Huo ni uongo by omission.
Ningemsamehe zaidi kama asingejinadi kwa ukweli na uwazi.
Huyu ndiye baba wa "Ukweli na Uwazi".
Sasa sisi wasela tusemeje?
Hapo nimegusia familia tu, ambako hakuna kesi. Ukienda zaidi unakuta kitabu kinaacha maswali mengi zaidi ya majibu. Yani kaandika mambo kirahisi rahisi sana kama wote wajinga na hatujui kitu.
Sent using Jamii Forums mobile app