Bongo Star Search ni janga la kitaifa

Bongo Star Search ni janga la kitaifa

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,549
Kwa mtu yeyote intellectual ambaye huwa anatazama Bongo Star Search atakubaliana nami kuwa mchakato huo wa kusaka mwanamuziki bora mwenye kipaji umejaa dharau,kejeli na kukatisha tamaa,hawa Master Jay na Salama Jabir ni majaji feki kabisa wanaowakatisha tamaa vijana wenye vipaji.

Namsifu sana Madam Rita,dada huyu hajawahi kumkatisha tamaa mshiriki yoyote,hata anapoonekana kushindwa yeye humtia moyo ama kukaa kimya,lakini Salama na Master jay huwatolea maneno ya kejeli,vijana wangu wa Tanzania wenye vipaji mbalimbali msikatishwe tamaa na hizi taasisi za kihuni zinazojifanya zina uwezo wa kubaini vipaji vyenu.

Leo hii Diamond,Lady Jay dee,Prof Jay,Dully sykes na wengineo wangeenda kutafuta vipaji vyao Bongo Star Search wangerudi wakiwa wamekata tamaa kwa kukutana na kina Master jay na Salama, simameni wenyewe achaneni na hawa wahuni,mtapoteza vipaji vyenu bure.

Historia inaonyesha kuwa,hakuna mtu aliyefanikiwa maishani kwa kuwekwa katika mizani ya ushindani bali alifanikiwa kwa kujituma mwenyewe akiamini atafanikiwa.
 
Hakika huu ni ukweli jamani,mwenye hoja ya kupinga anakaribishwa.
 
Ulitaka wasifiwe hata kama hawana uwezo wo wote wa kuimba?

Hizo sifa zisizo na mpango ndizo zinazowalegeza watanzania.

Mimi huwa naangalia na kuna wengine wanaimba kama kobe, wengine kama ngamia na wengine hawana hata idea nini wanatakiwa kufanya. Sasa wapewe sifa za nini?
 
Ila bora umwambie mtu ukwel...ya nn umfche...halafu wanachukua watu wachache sana
Mbeya walijtokeza vijana km mia tisa ila wakachukuliwa 6
 
dilemma

Vipaji viko vya aina 2 tuu. Kuna kipaji cha kuzaliwa na kipaji cha kujifunza. Wengi wanaoenda palle hawana hata kimoja. Kuimba sio kulegeza mdomo tuu na sauti nyembamba ukasema unaweza. Je unaweza kupangilia mahadhi ya sauti yako na kilebunachokiimba.
Mi nadhanai wangekaa na bakora hasa coz wengine wanaenda kufanya mzaha na kuonekana.
 
Last edited by a moderator:
Mimi huwa siangalii tena huo upuuzi azam wapo kwanin nijitese na maisha yenyewe ni haya mafupi
 
Ulitaka wasifiwe hata kama hawana uwezo wo wote wa kuimba?

Hizo sifa zisizo na mpango ndizo zinazowalegeza watanzania.

Mimi huwa naangalia na kuna wengine wanaimba kama kobe, wengine kama ngamia na wengine hawana hata idea nini wanatakiwa kufanya. Sasa wapewe sifa za nini?

aaaaah mkuu taratibu.wanaimba ka kobe! hizi kamba live live
 
dilemma

Hao Master Jay na salama wamesoma wapi huo muziki? Ni wahuni kama wahuni wengine tu wenye njaa kama ilivyo ada Bango!
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini wenye mawazo tofauti msianzishe shindano mbadala? Dunia haiwezi kuendelea kwa kulalamika. Hii ni opportunity, seize it man!
Dar City, to seize opportunity is not simple! Unaanza vipi kama unatoka katika familia masikini kama za kwetu! Hawa unaowaona kuna mahali walianzia tena usiseme kama ni wanawake- men are at work. Ila nakubaliana na wewe kuwa na mawazo mbadala na kuwa na wazo la kukattaa udhalilishaji. Kama ulivyosema ni vizuri kuwa-encourage vijana kuthubutu. Jay na Salama ni wadhalilishaji wa vijana masikini wanaotafuta pa kuponea
 
Mara unamsifu Madam Rita, mara unaponda taasisi yake, mbona hueleweki wewe.!? au wivu..!? master j amesoma muziki na ni produz haswa, salama ni mtangazaji wa siku nyingi, yaani wote wanaujua muziki au unatafuta kiki..:what:
 
Hawa BSS nadhani wasiwe wanapewa hizo mil 50.Ila mshindi aambiwe kuwa atarekodi bure nyimbo zote atakazotunga may be kwa miaka mitatu au mitano.Audio na video na kupewa nafasi ya kupiga collabo na wasanii wakubwa.Kuwapa m50 ni kuwahatibu tu
 
Asilimia kubwa ya kinachoniburudisha kwenye onyesho hili ni tabia ya waamuzi. Nawapongea sana kwa mtindo wanaotumia. Ni burudani tosha.
 
Ulitaka wasifiwe hata kama hawana uwezo wo wote wa kuimba?

Hizo sifa zisizo na mpango ndizo zinazowalegeza watanzania.

Mimi huwa naangalia na kuna wengine wanaimba kama kobe, wengine kama ngamia na wengine hawana hata idea nini wanatakiwa kufanya. Sasa wapewe sifa za nini?

Hivi hiki kipindi kinaonyeshwa channel gani na saa ngapi?
 
Ila bora umwambie mtu ukwel...ya nn umfche...halafu wanachukua watu wachache sana
Mbeya walijtokeza vijana km mia tisa ila wakachukuliwa 6

Na kumbuka hao sita kuna wengine walikutoka Arusha walikoshindwa wakafunga Safari mpaka Mbeya kuja kushiriki.

Kuhusu Majaji Hasa Salama nimemfatilia hataki kumsikiliza mtu akishakuona tu kwa jinsi ulivyovaa basi kasha ku "judge" kuwa huwezi kitu hivyo hata ukiendelea kuimba anakuelekezea mlango uliko.
Masta jay kidogo anakusiliza ila akiona tu mwanzo unavyoanza basi hapo hapo ana kutimua.

TUKUBALI TUKATAE KWENYE TUKIO LOLOTE HASA LA KUTAFUTA VIPAJI MBWEMBWE, VITUKO HUWA HAVIKOSEKANI NA WENGINE HUWA WANAENDA KAMA KUJUFURAHISHA TU ILI MRADI WAONEKANE NA HAPO NDIPO INAPOWAPA KAZI MAJAJI.
 
Nampenda sana Salama, hakika asipokuwepo judge km yeye bongo star search itakufa.
Hakuna mambo ya kubanabana pua,
 
Back
Top Bottom