Bongo Star Search (BSS) na mshindi mzungu!!

Rita is so HIGH she's on cracks, weed or something...so wack..
Mimi siwezi sema hayo maana sijui lakini hata wakati wa kupresent zawadi yeye yuko mbele nilimwona anafoka sijui ni nini kilitokea!
 
All the above. Ila ili shindano limetia aibu kabisa. Hususani uyo anaejiita chifu jaji,alikua yuko chicha la tilalila! Yani full kurembua na kufanya vituko. Na alivyomkumbatia yule kijana duh! Ni hatari na aibu. Payne or Bela deserved to be a winner! Namshauri Bela aende Tusker Project Fame na akawadhiirishie kua yeye ni mkali.
 
Ukaburu ni Ukaburu tuu. Ukaburu hauwezi kuwa mbaya wakati anaeonewa ni Mwafrika tuu. Hata ukiuelekeza kwa yule asiye na sura na hulka kama zako, huo bado ni ukaburu. Tuache fikara za kutupa viwango vya chini kimafikara.

Mtu apewe heshima kutokana na utu wake, mwelekeo wake na huduma zake kwa jamii sio vinginevyo.
 
Ukaburu ni Ukaburu tuu. Ukaburu hauwezi kuwa mbaya wakati anaeonewa ni Mwafrika tuu. Hata ukiuelekeza kwa yule asiye na sura na hulka kama zako, huo bado ni ukaburu. Tuache fikara za kutupa viwango vya chini kimafikara.

Mtu apewe heshima kutokana na utu wake, mwelekeo wake na huduma zake kwa jamii sio vinginevyo.

mbona sijakupata vizuri
 
Mzungu yuko poa.he had a big challenge of singing in swahili fortunately aliweza,he did his best,he deserved to be Bongo Star!!!
 
Uchambuzi wangu:

Payne ni mzuri katika kuimba (sauti) lakini ki saana vile. Uchaguzi wake wa nyimbo ulikuwa mzuri sana. Kucheza na beats nina mrank wa mwisho (kky).
Kweli ushabiki wa kumpenda Payne ni psychological zaidi kuliko the intrinsic talents in him. Yaani ulichangiwa na 'mtu mgeni' asiye tegemewa kuimba kiswahili kilichonyooka kwa usanifu. Mfano ni mtu kutoa Afrika akianza kufanya maajabu katika say Ice / figure-skaters' dance, watu wanaweza kukupenda sana maana si kawaida sana.

Juu ya shindano la BSS kwa ujumla. Mshindi kwa kwanza yaweza kuwa sawa, pengine kwangu ningemweka wa pili lakini huyo mshindi wa pili I doubt kabisa! Ana sauti moja nzito tu hawezi kupanda juu na pia hata nyimbo zake si zinazogusa sana ukilinganisha na wengine.Yaani kuna waliokuwa wazuri sana kuliko yeye akina Chiby na Salum.

Majaji (ukiondoa Mzungu kichaa) wameonyesha upupu mkubwa kwa kutoa comments za kishabiki kuliko ile kazi ya ufundi ambayo kwayo imewaweka hapo. Wameshindwa kuficha pia feelings zao na kuonyesha waziwazi yule walitaka ashinde eti oh huyu ana mvuto na lazima ashinde oh mimi huyu ndiye wangu namba moja n.k , oh nitajiua huyu aki.......... . Hakika sikuamini kuwa maneno kama hayo yanaweza kutamkwa na Jaji aliyepewa dhamana na shughuli iliyodhaminiwa na makampuni mamilioni ya fedha.

Kibaya kuliko vyooote ni kumuruhusu Payne kushiriki toka mwanzo maana baadaye kawa na washabiki wengi na niseme kuwa performance yake ya mwisho ilikuwa kiboko sasa baadaye mkishasoma alama za nyakati eti mnajifanya kumweka kuwa wa tatu! lo aibu sana! yaani mlichemsha kabisa. Huyu hakustahili kufanya kazi hii bila work permit inayomruhusu kufanya kazi hii. hata kuna yule msichana pia aliyepewa zawadi ya moza Kiili house naye wakati anashiriki Master J alikuwa anamnyanyepaa kuwa anafaa akaimbe hizo nyimbo zake huko kwao ( Yaani naye Kiswahili kilikuwa mgogoro). Ninachosema ni kuwa hamna haja ya kuwaruhusu wageni kushiriki halafu mnawaponda kutoknana na uraia au matamshi yao au lugha zao!

BSS rudini kwenye meza mkae chini mjiulize kusudi la BSS ni nini? Sidhani kama mnakusudia kutufurahisha watazamaji au kunyanyua vipaji vya watu wowote duniani au ndivyo? Kama ni vkwa ajili ya vijana wa kitanzania basi: mdefine umri wa kushiriki na pia mtu awe raia wa Tanzania full stop.

Halafu next time 2011, fanyeni kweli. Rita wewe kaa pembeni kama Mkurugezi na Mratibu Mkuu, acha kabisa kuwa jaji. Jopo la majaji liwe na:
Producer mwingine mmoja (si master J tena) , Mtaalamu wa maonesho ya Sanaa mmoja, na waalimu wawili waliobobea katika Muziki acheni blabla ndiyo maana mtu akijaribu kuwasahihisha washiki kwa kutaja terminologies za music ninyi akina Salama mnambeza! Haya ni mashindano ya kutafuta mkali wa KUIMBA si kuuza tu sura wala kukata ma...... waka hata kucheza na vyombo ingawa hivyo vinatakiwa kuwa vikolombwezo kwenye kipawa cha msingi cha uwezo wa kuimba!
BTW Kwenye shindano lolote malalamishi hayakosekani lakini mnaweza kuyapunguza kama mtafaya kazi hiyo strategically na kwa kuwa wakweli!

Rita, make your mind and your project shall be of a success and of benefits to the Tanzanian youth!
 
Mariam Mohamed ndiyo Mshindi wa BSS 2010 na Mzungu kachukiwa nafasi ya tatu na ya pili James Kapange. Ila majaji wapunguzo matusi na pombe wameniboa leo.
 
Mzungu kachakachuliwa...mshindi wa tatu Ni joseph Pyne,.james Martin nafasi ya 2 na mshindi ni MARIAM MOHAMEDI
Hakuna uchakachuaji hapo. Any one among the best 5 could b a winer. Tuacheni ushamba wa kushobokea wazungu.
 
Tatizo kubwa sana ambalo linatupeleka watanzania pabaya ni kutetemeshwa na kuridhishwa kupita kiasi na rangi pamoja na sura kwa ujumla.watanzania wanashobokea zaidi sura na muonekano wa nje wa mtu kuliko uwezo wake binafsi.fikiria tumefikia hatua mpaka rais anapigiwa kura kwa vigezo hivyo!!
 
Kwa mnaofatilia Bongo Star Search mnasemaje?

Mzungu kweli kastahili kuwa wa tatu?

Naona madame Rita kachakachua na kuweka uzalendo mbele. Hata hivyo nimempenda mshindi aliyetuchagulia maana ni peke yake anaimba Rusha Roho hivyo hana wa kulinganishwa naye.
 
Hili shindano ni usanii mtupu hakuna haki yoyote mshindi huwa anajulikana mapema.

Hao majaji nao wagangaa njaa tu wizi mtupu.
 
mariam pamoja na kuimba rusha roho (which isnt my taste of music at all) alistahili ushindi. ana sauti ya muziki, anapurudisha akiwa jukwaani(maringo ya kimuziki yapo)
Mzungu alikuwa akiimba vizuri lakini hakuwa na coordination ya viungo vya mwili wangu lilikuwa janga. Nadhani hicho pia kiliwafanya watu 'wamfurahie'
 
Back
Top Bottom