Wakuu mnamkumbuka Joseph Pyne, mzungu aliyeitikisa BSS 2010

Wakuu mnamkumbuka Joseph Pyne, mzungu aliyeitikisa BSS 2010

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mwaka 2010 uliingia kwenye vitabu vya historia ya Bongo Fleva kama moja ya miaka ya kipekee kupitia shindano la Bongo Star Search (BSS).

Ndani ya jukwaa hilo maarufu la kusaka vipaji, alijitokeza Mzungu aliyejulikana kwa jina la Joseph Pyne. Pamoja na kuwa si Mtanzania kwa kuzaliwa, Pyne alionyesha umaridadi wake katika kuimba nyimbo za Kiswahili kwa ustadi wa kuvutia, akizikonga nyoyo za mashabiki wengi waliomshangilia kama mmoja wao.


Licha ya kushika nafasi ya tatu, Pyne aliwakonga watanzania jambo lililosababisha sintofahamu kwa baadhi ya mashabiki waliodai kuwa alipaswa kuwa mshindi wa kwanza wa shindano hilo.

Lakini stori haikuishia hapo, kupitia majukwaa ya mtandaoni kama Jamii Forums, kulizuka tetesi nzito kuwa Pyne hakuwa tu mshiriki wa kawaida, bali eti alikuwa ni kachero kutoka shirika la kijasusi la Marekani, CIA, aliyekuwa na jukumu maalum nchini Tanzania.

Wengine walidai kuwa uwezo wake wa "kujichanganya" kirahisi na jamii, pamoja na umahiri wa lugha, ndio uliomfanya apenye hadi kwenye mashindano ya muziki maarufu.

Japo madai haya hayakuthibitishwa rasmi, pyne anabaki kuwa sehemu ya historia ya BSS.

Je, ulikuwa wapi kipindi Pyne anafanya yake?

Chanzo: 7sevenmediatz
 
😂😂 Bila ya kujali tumekuja na shemeji Halima
 
Nimetoka zanzibar kijijini huko wazungu ni wengi kuzidi watanzania na wanajichanganya sana

Inawezekana mtalii tu akaona anaweza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom