Bongo Star Search 2009: Burudani kweli!?

Hata huyo Ritha mwenyewe nidhamu sifuri mbele ya luninga! i naona progamme nzima inaboa tu watoto wa watu!
 
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=IiC6eJBnjss&feature=channel_page"]YouTube - Kila kazi na kiburudisho chake hiki toka BSS[/ame]

Sipati picha simon cowel angemjibu vipi hiki kipaji nadhani jamaa angekula shavu.....
 
Date::5/23/2009
Udhalilishaji huu Bongo Star Search haukubaliki
Fidelis Butahe

MWANZONI mwa mwaka huu niliandika makala kuhusiana na vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na majaji wa shindano la kutafuta vipaji vya uimbaji la Bongo Star Search (BSS) uliokuwa unaongonzwa na aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha televisheni cha EATV, Salama Jabir.

Niliandika makala hayo kuwataka waandaaji wa shindano hilo ambao ni Kampuni ya Benchmark Production kuweka majaji ambao watakuwa msaada kwa vijana mbalimbali watakaojitokeza kuonyesha uwezo wao wa kuimba.

Msaada kwa maana kuu mbili ya kwanza ni kuwapa moyo washiriki ambao wataonekana kuwa na nia ya kuimba lakini hawana uwezo, pili kuwaonyesha njia nzuri za kufuata washiriki ambao wataonekana kuwa na vipaji. Na pia kuwapa moyo wale wote watakaojitokeza katika usahili.

Kipindi hicho kwa kuwa shindano hilo lilikuwa halijaanza niliwatolea mfano majaji wawili ambao walikuwepo katika shindano hilo mwaka jana ambao ni Salama Jabir na mtayarishaji wa muziki Master Jay.

Mfuatiliaji gani wa shindano la BSS asiyewakumbuka majaji hawa wawili jinsi walivyokuwa wakiwaumbua na kuwadhalilisha washiriki wa shindano hilo wa mwaka jana na mwaka juzi.

Nasema ni udhalilishaji kwa sababu washiriki walioonekana kutokuwa na uwezo mzuri wa kuimba walitukanwa ‘live’ na majaji hawa bila kujali kuwa kipindi hicho kinarushwa hewani na mamilioni ya Watanzania wanakitizama.

Mshiriki mmoja wa mwaka jana ambaye alifanikiwa kuingia kumi bora alipandwa hasira na kuzungumza maneno machafu mara baada ya kuambiwa na Salama Jabir kuwa hana uwezo wa kuimba na alifika katika hatua hiyo kwa bahati za mwenyezi Mungu.

Mambo kama haya yameonekana mapema katika hatua za mwazo za usahili kujirudia, na hata kutaka kuleta mtafaruku kati ya Chief jaja Madam Rita na P Funk katika usahili wa Mwanza. Na sio Mwanza pekee bali katika mikoa mbalimbali ambayo wamesha zunguka kutafuta vipaji.

Majaji hao wamejisahau kuwa rais Jakaya Kikwete hivi sasa yupo katika mapambano ya kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anaishi katika maisha bora, hao vijana ambao wamejitokeza katika usahili ni dhahili wanakwenda kushindana ili waibuke washindi na kujinyakulia fedha na zawadi mbalimbali zitakazowasaidia katika maisha yao, wanapodhalilishwa namna hii na majaji hapo tunaijenga Tanzania tunaibomoa?

Sikushangaa juzi serikali ilipotoa tamko la kusikitishwa na kulaani vikali udhalilishwaji unaofanywa na majaji wa BSS kutokana na tabia yao ya kutumia lugha chafu isiyostahili kutumika mbele ya jamii iliyostaarabika.

Tamko hilo lilitolewa na Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ghonche Materego alisema wao kama wasimamizi wakuu wa sanaa nchini wanalaani vikali vitendo vinavyofanywa na majaji wa BSS.

Alisistiza kuwa majaji hao ambao ni Rita Paulsen, Master Jay na P Funk wamekuwa wakivuka mipaka kwa kuwadhalilisha washiriki kitu ambacho ni kinyume na maudhui ya programu hiyo kwa mujibu wa maobi ya Benchmark Production.

Tangu kuanza kwa shindano hilo kumekuwa na malalamiko mengi yanayotolewa na washiriki wa shindano hilo pamoja na mashabiki na watizamaji wa BSS juu ya lugha zinazotolewa na majaji hao lakini kwa mwaka huu malalamiko haya yamezidi na kuvuka mipaka.

Master Jay na P Funk ni wafanyabisahara na wanamiliki studio za kurekodia muziki, siamini kama huko kwenye studio zao wanawadhalilisha wasanii kama wanavyofanya katika shindano hilo.

Kama ni njia ya kunogesha kipindi basi wahusika hawana budi kubadilisha njia hiyo, tunajua kuwa majaji hawa wanapata changamoto kubwa ya kukutana na vijana wengi kwa muda mfupi lakini hicho kisiwe kigezo cha kuwatukana na kuwatolea lugha chafu.

Materego alisema itakachokifanya BASATA ni kukutana na uongozi wa Benchmark Production kujadili suala hilo na kama wahusika wataendelea na unyanyasaji watasimamishwa na kufutiwa kabisa leseni ya programu hiyo.

Sasa hili ni suala jingine, itakuwa bora wafungiwe kama wakiendelea na udhalilishaji huu kwa sababu upo uwezekano wakaibuka washindi ambao watakuwa hawajali udhalilishwaji wanaofanyiwa na majaji hao kwa sababu wenye vipaji vya kuimba na kutunga wanaweza wakashindwa kuonyesha cheche zao na pengine kujiengua katika shindano kwa kuogopa kutukanwa na majaji hawa au kotojitokeza kabisa.

Mwaka juzi Jumanne Iddi ndio alikuwa mshiriki wa kwanza wa BSS kuibuka kidedea na kujizolea zawadi nyingi pamoja na kupata ofa ya kurekodi nyimbo katika studio ya Benchmark, washiriki wengine waliotinga katika hatua ya tatu bora ni Leah Muddy na Kala Jeremiah.

Mwaka jana mshiriki kutoka Bagamoyo, Misoji Nkwabi aliibuka mshindi huku nafasi ya pili ikinyakuliwa na mkali wa kubadilisha sauti na kupiga gitaa, Rogers Lucas huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na 'dogo' Aboubakar Mzuri ambaye hivi sasa anatamba na nyimbo ya Samahani.

Ni wazi kuwa washindi hawa walikumbwa na wakati mgumu sana mbele ya majaji hawa na inawezekana kulikuwa na washiriki wenye vipaji zaidi ya washindi hawa lakini kutokana na udhalilishaji wa majaji walishindwa kuonyesha cheche zao jukwaani.

Rais Kikwete aliahidi kutoa ajira milioni moja baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, BSS ilivyoanzishwa mwisho wa siku ni lazima mshindi apatikane, sasa kama ushindi wenyewe ndio huu wa kudhalilishwa sidhani kama kuna haja ya kuendelea kuwepo kwa majaji wa namna hii ndani ya BSS.

Mwisho

0754 597315

butahefidelis@yahoo.com
 
Mkuu kabla hujaanzisha thread ni vyema uangalie kama unacholeta jamvini kinastahili na kina upekee wa kuletwa. Mambo ya BSS kuna thread kibao zimeshazungumzia hili suala, tuwapunguzie MODS kazi. Ustaarabu ni pamoja na kuto-recycle niuzi.
 
hawa watu mbona wapo fake fake..are they really serious? hahaha imenichekesha sana
 
hata hivyo thread yake haina maana. anzisha ya kwako kama unaona hiyo haina maslahi

kuna vijana kibao wametoka kupitia BSS sasa hao unasema nao walizalilishwa?

habari za kuchongea sasa hivi jamii forums hazina mahala pake

siye tunataka mambo ya kweli na siyo fitina
 
mtu yeyote ili afanikiwe, mambo mengi humkuta ikiwa ni pamoja na kukatishwa tamaa kuwa huwezi. mimi naamini kuwa majaji wanawapa changamoto washiriki ili kama kweli mtu anadhani ana kipaji na kujiamini basi akaze buti kuyafuata mafanikio sio mafanikio yamfuate yeye. utakubalina na mimi kuwa kuna wengine hawaendi kushiriki bali kulete utani na hasa wakijua kuwa wataonekana kwenye luninga, kwa kufanya hivyo wataonekana mashujaa kwa wale jamaa zao watakao waona kwenye luninga kuwa na wao waliishawai onekana kwenye luninga tene kwenye BSS. wengine kuonekana tu kwenye tv ni sifa kwao haijalishi atakachokifanya ni sahihi ama sio.
napenda kusema kwa mtu aliye na nia na mafanikio changamoto kama hizo zinazotolewa na majaji wa BSS ataziona ni sehemu ya mapambano dhidi ya mafanikio yake,
wengi wa waliofanikiwa waliishawahitokanwa sana na kukatisshwa tamaa na zaidi ya yote waliambiwa hata iweje hawawezi kufika mbali but ukweli wengi waoni matajiri na wenye mafanikio tele kuzidi wale waliowakatisha tamaa.
sishabikii matusi na udhalilishaji ila nachojua hiyo ni changamoto kwa washiriki kuonyesha ujasiri wao kuwa wanaweza hata kama watakatishwa tamaa kiasi gani.
 
hata hivyo thread yake haina maana. anzisha ya kwako kama unaona hiyo haina maslahi

kuna vijana kibao wametoka kupitia BSS sasa hao unasema nao walizalilishwa?

habari za kuchongea sasa hivi jamii forums hazina mahala pake

siye tunataka mambo ya kweli na siyo fitina
Ukiona mtu anaongea maneno ya hovyo ujue amefilisika kichwani.

Sidhani udhalilishaji mnaoutetea kwa ngunvu zote ni sera za BSS na kama ndivyo basi nina mashaka na uwezo wa kufikiri wa waliotoa vibali vya shindano hili.

Pia nilisoma last week majibu ya Rita kwa BASATA ambapo kama ndo alisema yeye yale maneno basi huyu mama hana wazazi na wala hatufai kwani anaendesha kipindi kinachomwingizia hela nyingi lakini hajali utu wa WATU.

Mie nimeacha kuangalia hiki kipindi kwani hakina jipya zaidi ya kuwaharibu kisaikolojia washiriki. Na kama vipi kifutwe wakajipange upya ili wakija waje wakiwa na adabu kamili
 
Wajirekebishe..maan yale maneno yao hapana aiseee yanakatisha tamaa.....wangekuwa wastaarabu japo kidogo......maana bila hao vijana wanaojitokeza...na baadae kutuma sms hakuna huo mchezoo wala hawatapata pesa wanazotegemea......waachane na ubabe na radhau
 
Aa umenikumbusha siku ile alipozuka huyo jamaa na kucheza mbele za majaji,wale majaji huwa wanajidai wana vibomu kwa wasanii mbona huyo alipoingia walinywea ile mbaya na hawakuongea kitu jamaa akacheza alipomaliza huyo akaondoka zake,sikusikia yale maneno yao mara mlango ule,sijui muziki haukupendi hayo hayakuwepo siku hiyo ilikua burudani ya aina yake.
 
Mnamo saa moja lililopita nilikuwa miliman city hapa jijini Dar!kwakweli KWA MARA YA KWANZA nimeona 'matunda halisi' ya bongo star search!hawa vijana wawili feisal na madaha WANAUZA ALBUM ZAO MBILI pale ndani unapoingia SHORITE,dah!NI UBUNIFU WA HALI YA JUU!nisingependa kukumalizia utamu we cha kufanya unaporudi ofisin pitia pale kakamate album hizo mbili zikiwa katika audio na video kwa sh 11000 zote mbili,UTAZIPENDA TU

hongereni saaaana pilipili!MMELETA KITU KIPYA KABISA SIO SIRI!watanzania tuwape support hawa wasanii,na hii lebel!NIMEWAPENDA KWA UJUMLA!

hapa nipo zangu maeneo napitia pitia forum ya 'wajanja' huku nakula musics yao hapa!dah!

BRAVO-WADOGO ZANGU
 
Mnamo saa moja lililopita nilikuwa miliman city hapa jijini Dar!kwakweli KWA MARA YA KWANZA nimeona 'matunda halisi' ya bongo star search!hawa vijana wawili feisal na madaha WANAUZA ALBUM ZAO MBILI pale ndani unapoingia SHORITE,dah!NI UBUNIFU WA HALI YA JUU!nisingependa kukumalizia utamu we cha kufanya unaporudi ofisin pitia pale kakamate album hizo mbili zikiwa katika audio na video kwa sh 11000 zote mbili,UTAZIPENDA TU

hongereni saaaana pilipili!MMELETA KITU KIPYA KABISA SIO SIRI!watanzania tuwape support hawa wasanii,na hii lebel!NIMEWAPENDA KWA UJUMLA!

hapa nipo zangu maeneo napitia pitia forum ya 'wajanja' huku nakula musics yao hapa!dah!

BRAVO-WADOGO ZANGU


You must be a good marketer! Pilipili should not dare to loose U.
 
Nafikiri baada ya kusemwa sana, BSS inanoga. Nimeinjoi kwa kweli, hasa master j
 
yaap! ni mambo juu ya mambo, wazo kuu na la msingi la mbuzi ni majani, so ucshangae sana hao wana BI ESI ESI NA VIMAMBOVYO SI NDO UCELEBRITI HUO, THOUGH KIUKWELI INAUMIZA WAKTI MWINGINE, KI2 BORA NI KUANZISHA NYINGI KADRI INAVOWEZEKANA LABDA HAO WAAMUZI WATAHESHIMU WASANII HAWA WACHANGA! KIP KUL MAN! JAPO INAUMA SANA BRO!!
 
Napenda kutoa dukuduku langu katika mashindao haya. In fact naguswa sana na washiriki. I feel over the moon ninapowasikiliza. Kuna kelvin mbati, msechu na ntepa. Twende nao survivors hadi tamati
 
bongo star serch ni uharo mtupu...
na ndio maana hivyo vipaji vyao vinavyoibukaga na ushindi mwisho wa siku vikija kwenye game vinapotea kama ushuzi
 
Back
Top Bottom