Bomu lategwa nyumbani kwa RC Mulongo

Bomu lategwa nyumbani kwa RC Mulongo

Mkuu, hao jamaa itakuwa ni hawa wavaa suruali fupi. Na nashangaa kwanini serekali inawachekea
Ni majuzi tuu mkuu wa mkoa aliweka wazi nkuwa tukio la kushambuliwa sheick limetokana na mgogoro unaofukuta huko AR baina ya waumini wa dini hiyo ambapo hata mufti alikwenda kusuluisha sasa sijui wamempa message?Nafikiri hawa walipua mabomu wanatoka miongoni mwa jamii, na hata wafanye siri vipi lazima kuna watu wanajua , mimi ninadhadhani badala ya kuendelea kulaumu vyomabo vya ulinzi na usalama kwenye haya makosa ambao ni organized , jamii wangetoa ushirikiano kwani wakiendelea kulifumbia macho litaendelea kukua na madhara yaweza kuwarudia siku moja
 
Asubuhi hii askari Polisi na wa Jeshi wameizingira nyumba ya Serikali ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo iliyopo jirani na Mahakama Kuu Arusha wakijaribu kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kikiwa kimetegwa katika geti la kuingilia nyumba hiyo na watu wasiojilikana.

Hat kinjia kinachokatiza maeneo hayo kutokea Mt Meru Hotel nacho kimefungwa kwa muda.

Wakati huo huo kuna taarifa za usiku zikieleza watu kadhaa wamejeruhiwa katika Mgahawa mmoja maeneo ya Gymkhana Jijini hapa na wawili kati yao wako katika hali mbaya.

Hili litakuwa tukio la sita kutokea katika Jiji la Arusha ndani ya muda mfupi, kuanzia May 2013 mpaka sasa.

Tukio la kwanza lilikuwa Kanisani Olasiti watu watatu wakafa.

Baadee katika Mkutano Chadema Soweto watu watatu wakafa tena na mamia kulemaa

Ikafuata Usa River siku ya Mkesha wa mwaka mpya kwa wamama waliokuwa wanatoka kanisani

Halafu katoka Bar ya Arusha Night Park

Juzi hapa ikawa kwa nyumbani kwa Sheikh maeneo ya Majengo

Na sasa katika hiyo Vama Restaurant na chupuchupu kulipua nyumbani kwa RC!

Uwepo wa chadema Arusha ni shida kubwa sana kwa watanzania na wapenda amani wote duniani kwa ujumla.
 
Binafsi nina mashaka na Mbunge wa Arusha. Ahojiwe...
Mnatapatapa kwa kushindwa kuwakamata wahusika angali mnawajua,kila kukicha Lema,tudhibitishieni uhusika wake..
Siku nchi inachafuka kwa siasa chafu ntaanza na bendera ya ccm...
 
Hilo bomu halijategwa kwa ajili ya discourage utali. Vama ni restaurant ndogo sana hivyo hao sio magaidi ni vibaka hata uharibifu co mkubwa .hivyo inanifanya niamini sio al shabab.
Pili mi nashawihika sana kwamba hao walio lipua hilo bomu ni visa tu vinavyohusishwa kati yao na mkuu wa mkoa baada ya kauli ya yake kwa hao wa islam hivyo kutaka kumfundisha adabu[huo mgahawa upo krb sana na kwa mkuu wa mkoa)
 
Ubalozi unalindwa ila nao walikiri kua udhaifu ulitokea katika security yao na ndio maana sasa hivi wameimarisha ulinzi zaid.Mandla naomba uwe muelewa na na mwenye kufikiri na sio kupelekwa tu na mtazamo wa chama flani.Mimi sina chama chochote hapa kwetu ila nasikiliza hoja,ukinipa hoja nzuri lazima nikukubali.
Mbona mabomu mengine hatujaskia jambo lolote lyk majibu ya serikali kuhusiana na hayo mabomu au hatujaskia watuhumiwa wamekamatwa au lah au serikali inawafatlia au lah,au kwa kua hayakuwagusa wakubwa wa nchi?
mambo mengine ni kufikiria kwanza na sio kulipuka tu

Mkuu usitegemee jibu lolote la msingi toka kwa huyo jamaaa, jambo linalohusu usalama wa nchi au lenye maslahi yeyote kitaifa, lazima ataonyesha rangi zake,, kuna member mmoja amehoji juu ya elimu ya huyo jamaa yako unaetaka akujib.

Labda anaelewa mambo na ameamua kujifanya haelewi, au yote mawili yanawezekana.
 
Ubalozi wa Marekani unalindwa na nani??? ........nilishakuambia nina wasiwasi na elimu yako.

Hivi hili bomu "fake" lililotegwa kwa mkuu wa mkoa lina uhusiano gani na ulinzi wa Ubalozi wa Marekani? Au unataka kuhusianisha hili bomu fake na lile lililolipuka kwenye ubalozi wa marekani some years back? Kama hujui kilichotokea ni kwamba lile alikuwa bomu la kutegwa, lilikuwa ni bomu lililokuwa limebebwa na gari na lilipofika getini mjitoa muhanga akalilipua. Sasa hii ina uhusiano gani na tukio la kwa mkuu wa mkoa?

Wasomaji wataamua kati yangu na wewe nani ana umri wa kutiliwa mashaka.

Tiba
 
Je kama wamejitegea? Maana dola hii ambayo sina imani nayo nitakua wa mwisho kuamini kuwa hawajajitegea.

kujitegea nini?sizani mkritu anaweza kushiriki kuuwa mkristu mwenzake au mwislam kuuwa mwislam mwenzake eti kwasababu katumwa na taasisi flan,unatakiwa umakini nani wa uchunguzi,viongozi wa kiroho pande zote wameasirika.
 
Kama Bomu limetegwa kwa Rc nani kagundua kabla ya kulipuka? Tunataka majibu ya kina? Swali lenye utata inakuwaje kwingine kote yanalipuka kwa Rc lisilipuke liteguliwe? Tunataka majibu

Hilo ndo swali la msingi,wanacheza na akili za watu hawa.
 
Duh!! Kuna mengi hapa, haya hebu tupe dodoso juu ya kikao hicho cha Morogoro kaka.

Mbona siyo siri kikao kilikuwa ni kati ya mwigulu Mkuu Wa mkoa Wa Arusha na wajumbe wengine wakati huo ni siku chache toka mwigulu atoke China
 
kujitegea nini?sizani mkritu anaweza kushiriki kuuwa mkristu mwenzake au mwislam kuuwa mwislam mwenzake eti kwasababu katumwa na taasisi flan,unatakiwa umakini nani wa uchunguzi,viongozi wa kiroho pande zote wameasirika.

Mkuu umeandika nini hapa?, hivi una hakika kuwa hakuna mfuasi wa dini ambae anaweza kuua mfuasi mwenzie?? Unaishi dunia gani ambayo hiki ulichoandika hakipo.
 
Kwanini fujo kama hizo hazitokei majimbo mengine ya chadema??
 
Huu ni usanii tu. Nyumba ya mkuu wa mkoa inalindwa na FFU 24/7. Hao waliotega hilo bomu kwa nini hawakuonwa na hao askari na lilitegwa getini?

Nasema tena ni usanii.

Tiba

mkuu nakupa like kubwa umesema nilichotaka kusema,inashangaza nyumba ina askari wenye bunduki masa 24 ucku na mchana majira yote ya mwaka how come wategaji watege bila kuonekana tena getini,ccm na serekali yenu acheni kucheza na brain zetu,wajinga tu ndo wata amin huu usanii.
 
chadema wameharibu mji wa Arusha. Huku Dodoma hatutaruhusu huu ujinga utokee.

aliyekuloga amekufa,jibu swali hili kwa ufasaha,je wale field force wanaokesha na bunduk day an night getini kwa huyo mkuu wa mkoa wako pale kwa kaz gan?tena inasemwa bomu limetegwa getini hawa askar walikua wapi?huu usanii wenu ni wakipuuz sana mnajarbu mbinu zote ili jimbo lirud kwenu hakika mmechelewa sana kifo chenu ki dhahir sana
 
Mkuu, hao jamaa itakuwa ni hawa wavaa suruali fupi. Na nashangaa kwanini serekali inawachekea

Sasa badala ya hawa "great thinkers" kuja na ushauri wamebaki na siasa za ccm na Chadema.

Ukiunganisha dots ya matukio yote na aina ya mabomu yanayotumika ni dhahiri kuwa kuna kikundi fulani kinahusika...na ni kweli hawa jamaa wa suruali fupi wanazidi kuongezeka haswa Arusha, na haingii akilini kama serikali imekaa pembeni tu na kurelax bila kufuatilia huwa wanafundishana nini popote pale wanapokutana.

Tuendelee tu kupuuza kwa ujinga wa kusema ni siasa, tutakuja kulia na kusaga meno...na kati ya matokeo ya kuongezeka kwao ni hizo tofauti zilizopo hata ndani ya nyumba za ibada.

Sina uhakika kama serikali inaendelea na msako wa zile CD zilizokuwa zimezagaa haswa Arusha, kwani ukipata fursa ya kuzisikiliza yaliyomo kwenye zile cd ni hatari sana.
 
Hata kama umechoka kwa njaa zako.Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.Huyu ni mkuu wa Nchi huwezi kutukana kama hivi kichwa maji

Hana adabu ni watu aina ya Lema.
 
Maswali ya kawaida kujiuliza ni kwamba; kwa nini mabomu arusha na zanzibar? what is common between the two cities? TOURISM then jiulize who is our number one competitor kwenye tourism east africa? ishu za mabomu ya arusha na zanzibar hazina uhusiano na siasa .we are closing up a gap towards the real perpetrators

Yawezekana pia, lakini kumbuka siku chache tu zilizopita walimtarget kiongozi wa kidini, tena baada ya kumtumia vitisho.
 
Kwanini hilo la nyumbani kwa mulongo walifahamu na kulitegua kabla ya kulipuka ila la kwenye mgahawa washindwe? Hizi sio mind games kweli?
 
Serikali haijaonesha juhudi za makusudi za kuzuia milipuko ya mabomu arusha.
Baada ya mkutano wa chadema kupigwa bomu,ilitangazwa kuwa bomu ni la kivita na limetengenezwa China;pia linafanana na lililolipuliwa kanisani Olasiti.
Hapo tuu palitosha kwa serikali kuzuia uingizaji wa mabomu maana wanajua yanatoka wapi!
Uhusiano mkubwa wa shaka kati ya chama tawala cha Uchina na chama tawala cha Tz wa kuwezesha mpaka kumvalisha sare balozi wa china nchini nao ungefaa uchunguzwe na TISS !
Hili la kwa mkuu wa mkoa naungana na mdau Tiba na Ben Saanane 100%
 
Back
Top Bottom