Hoja yako yaweza kuwa na ukweli fulani lakini wakati mwingine inaweza isiwe kweli. Zamani watu walikuwa wanasoma wakiwa na umri mkubwa. Wapo walioanza shule wakiwa na miaka 15 au 12, siku hizi huanza shule na miaka 6 au 7. Zamani busara ilipimwa kwa kuwa na mvi kichwani sasa hivi hupimwa kwa vyeti alivyonavyo mtu. Miaka ya 1992 wakati serikali inaiondoa Mhimbili kuwa tawi la Chuo Kikuu cha DSM watu walipinga tena kwa migomo. Leo hii MUHAS inakubalika na kila mtu hata kimataifa. Jambo la msingi lilowapa MUHAS kukubalika ni utendaji wa wanafunzi wanaotoka MUHAS na sio jina la University of Dar es Salaam.
Cha kusikitisha ni kuwa wanaolalamikia kutofaa kwa UDOM ni wanafunzi au waalimu wa Muhimbili. UDOM na MUHAS kwa sasa ni washindani (competitors) au line staff. Katika ulimwengu wa ushindani hawezekani mshindani akusifu wala haikubaliki mkurugenzi wa kitengo fulani amtathimini mkurugenzi mwenzie wa kitengo kingine.
Hoja ya IMTU kutupa taka jalalani sioni ni jinsi gani linahusiana na ubora wa wanafunzi wanaohitimu IMTU na UDOM. Nilidhali hili linahusiana na uongozi wa chuo. It is more managerial issue rather than an academic issue. Lakini nijuavyo mimi wanafunzi waliohitimu Muhimbili mara zote wamekuwa wakijisifia kuwa wao ni bora zaidi kuliko madaktari waliosoma mahali pengine popote. Mfano wamekuwa wakiwabeza wanafunzi waliosoma Urusi, China, Hungary, Cuba nk nk. Sio ajabu kwa madaktari hawa hata wakiwabeza wenzo wa IMTU au UDOM. Kwa bahati mbaya waalimu wengi wanaofundisha katika vyo hivyo wanavyovibeza wanatoka Muhimbili hapohapo. Inakuwaje walimu haohao wakifundisha Muhmbili wanafundisha vizuri na wakifundisha IMTU wanashindwa kufundisha. Kama wanafunzi wa IMTU hawafai, wanafauluje sasa na marking scheme ni ileile! Hivi daktari aliyepasua kichwa badala ya mguu alisomawapi vile? Maana hii iliingizwa kwenye kitabu cha Guinness.
Mkuu ni kweli wakati MUHAS inaanzishwa tulipinga sana hasa hasa kwa kuzingatia management itakayoongoza MUHAS na reputation ya wanafunzi watakaotokana na MUHAS.hii ilikuwa ni haki yetu na kiukweli bado huwezi linganisha UDSM-MUCHS na MUHAS!
Uanzishwaji wa MUHAS ni muendelezo wa iliyokuwa FACULTY OF MEDICINE UDSM then MUCHS under UDSM, huu ni muendelezo uliokuwa na mpangilio kama ilivyokuwa SUA the then faculty of agriculture ya UDSM !
Kamwe huwezi linganisha uanzishwaji wa MUHAS/KCMC/CUHAS/SUA vs IMTU au UDOM!
IMTU na UDOM zimeanza kimagumashi au kisiasa au kibiashara zaidi na matokeo yake ni kama haya tunayoyaona au tusiyoyaona!
Tunachukulia uhuni unaoendelea marekani au India au Nigeria kuwa ni mfano yaani kila unayekutana naye ni graduate bila kutambua ukweli wa kwamba hawa nao wana taasisi bora walizozijenga na kamwe hazichakachuliwi au kubezwa au kulinganishwa na uyoga wa taasisi feki!
Ndio maana leo hii kina lukuvi na nchimbi na mrema wanajiita madokta wakiwa vifua mbele!
Hakuna usawa wa kiakili au kimauimbile katika dunia hii!ni lazima tuwe na wasomi,watendaji,waburudishaji,wababe,wehu,wategemezi n.k huu ni ukweli mchungu.
Tumefanya makosa kwenye sekta nyingi lakini makosa katika sekta ya afya ni hatari kwani yanagharimu maisha!
Naendelea kusisitiza kuwa leo hii tumeshuhudia bomu la IMTU lakini kesho tutashuhudia mabomu mengi,tukianzia na UDOM.
Leo hii almost kila chuo kinafundisha degree ya nursing ambayo ni changa sana hata kwa MUHAS !Tusije kulia baadae matokeo ya maamuzi haya!