meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,828
- Thread starter
- #201
Kuna rafiki yangu mmoja alisomea udaktari Muhimbili,akaenda Marekani kwa lengo la kufanya kazi kama daktari.Baada ya kukutana na vikwazo vya mitihani ya bodi,akaamua atafute kazi nyingine na sasa ni mfanyabiashara.
Rafiki yangu mwingine naye alisomea udaktari hapo hapo Muhimbili.Baadaye akafanya specialization(ubingwa)Muhimbili au Bugando kwa muda wa miaka miwili au mitatu kama sikosei.Sasa yuko nchi moja Ulaya mwaka wa pili anahangaika kurudia kozi za udaktari upya na kisha anatakiwa afanye mitihani ya udaktari ya wizara ya afya ya nchi husika au bodi ya madaktari, na kama atafaulu ndipo atapewa leseni ya kumruhusu kutibu wagonjwa.
Halafu hapa watu wanajisifia kuwa chuo chao cha Muhimbili ni bora zaidi.Kama nyie wazuri,mbona mkiletewa kesi mnazi refer India na South Africa?Vifaa hakuna na wataalam hakuna;kwasababu kama huna vifaa vya kutosha na vya kisasa shuleni,hutaweza pia kutengeneza wataalam wazuri.
Tufanyeje ili tutoke?Tufanyeje walau na sisi tuwe na wataalam competent na hospitali hata 3 tu nchi nzima zenye viwango kama vya India na South Africa?Tufanyeje ili India na Ulaya nao siku moja watamani kuleta wagonjwa wao Tanzania iliyosheheni wataalam wenye sifa zinazoheshimika duniani kote?Nadhani haya ndiyo yakujadili kama tunataka kuboresha sekta ya afya nchini.
Huwezi kusema wewe ni bora kuliko IMTU au UDOM wakati kwenye soko la dunia wote mnatupwa kapu moja na ili mpate ajira ya udaktari,wote mnalazimishwa kufuata utaratibu unaofanana kulingana na nchi mliyosomea udaktari wenu.
Safi sana mkuu kwa kuelewa somo langu!waingereza au wamarekani hawataki kabisa kuruhusu uchakachuaji wa fani ya udaktari au afya kwa ujumla.
Ni haki yao kuiita MUHAS,UDOM,IMTU n.k kama vyuo visivyo na viwango kulingana na viwango walivyojiwekea.sasa nakushangaa sana unapochukia kuona watanzania tukiita IMTU haijakidhi viwango vya kitanzania.
Kuna kipindi ilikuwa ni lazima kupita internship Muhimbili kama hukusomea udaktari hapo Muhimbili!sasa ni bora liende!