Bomu la IMTU limeshalipuka, bado la UDOM!

Bomu la IMTU limeshalipuka, bado la UDOM!

haya bhana naona heri zenu mnaosoma vyuo vya taifa, mtuache na kata zetu maana tumeshaanza kuitana muhimbili na yule'wa Udom
Haikuanza leo hiyo!! Ilikuwa Makererean vs Muhimbili ,ikaja Muhimbili Vs Eastern blog na sasa ni Muhimbili vs IMTU,KCMC,UDOM.
Muulize Sarungi ukimuona!!!
 
Wakufunzi wengi wa UDOM wametoka SUA, UDSM na MZUMBE.Kama issue hawajui kufundisha, basi vyuo walivyotoka hao wakufunzi ndio vitakuwa na matatizo makubwa kuliko UDOM yenyewe.
Swala si kutoka chuo gani nielewe,Swala ni kwanini mhitimu wa degree ya kwanza apewe darasa afanye lecture,badala ya kuanzia kuwa tutorial assistant,aanze kwa kusimamia seminar kwanza.
 
1. Those days may be, ndio maana nasema hii ni "conservatism" wakati watu wa account wanaanza kuachana na form six wanakatia diploma from form four kukimbia pata potea ya form six wewe bado unakomaa na medicine ni muhimu???!! Sifa ya kuitwa daktari wakati kila siku migomo ya posho na mzingira mabaya nani anataka nyakati hizi???!!! sio muhimu ni wachache sasa kama uchache ndio umuhimu sawa na ndio kiwewe sasa cha kuona wanakuwa wengi na kuanza kubaguana kwa vyuo wakati MAT ni moja!!!!! Walizoea kuonekana "high" sababu ya demand supply chain! !!!! Nini "noble" katika hiyo fani zaid ya mapokeo tu??????

2. Hiyo 75% ya Korea ukiivunja, udaktari unabaki na ngapi???!!!

3. Suala la mikopo ni stigma tu kwa sura nyingine, mtu anataka kuwa muhasibu na wazazi wake wanakatwa kodi huwezi mnyima mkopo halafu umpe Mbunge ambaye hata diploma hana, ubaguzi tu hamna jingine!!!! Kama hili unaona la maana sawa ila kwangu huu ni "

4. Nilikuambia na narudia dunia inabadilika mambo ya sifa za fani yanabadilika mwanao mwambie tu kuwa atachoamua lazima akifanye vizuri kwa hali ya juu kabisa sio kumlazimisha "noble" kwa mujibu wako!!!! Hao unaowaita "noble" wanaajiriwa na familia za watu successfull wanalipwa na kutumikishwa tu kama kawaida!!!!

mkuu mimi sio daktari, nilivyo maliza PCB wazazi walitaka nikawe daktari lakini kwa kuangalia future yangu sikwenda. lakini hili bado halisababishi nisione uadhimu wa hii fani. nchi nyingi duniani hasa zilizo endelea 'staarabika' madaktari ndio hulipwwa pesa nyingi. ni serikali yetu haioni unobility wa fani hii ndio maana wanawalipa kidogo na pia ndio sababu wanaanzisha mabomu ya substandards medical schools. tatizo ni kwamba serikali yetu ndio muajiri mkubwa. private sector lazima wangechagua wa MUHAS badala wa UDOM au ifakara.

udikteta wa elimu" sababu unamfundisha mpaka form six na mtihani unampa halafu unaweka vikwazo vya kuendelea wakati ulimpa option ya kuchagua fani akiwa form three???!!!!
hapa unapoint, serikali inatakiwa isolve hii ishu kuanzia huko chini, inatakiwa kupunguza idadi ya wwanafunzi wanao chukua michepuo isiyo muhimu na kuongeza wale wa michepuo muhimu.

sio tuwalazimishe kuchukua kozi fula, tunatakiwa kuwaambia kozi tofauti zina uzito tofauti katika jamii.
 
Mmh gazeti la nipashe nimewahi soma kampuni moja wanatoa nafasi za ajira,vigezo GPA kwa waliohitimu Udom na SAUTI isiwe chini ya 3.8 na kwa vyuo vngne kama udsm,mzumbe nk GPA isiwe chini ya 2.9!
 
Eeeeeeeeeeeeeeeeeeehhhhhhhhhhhhhhhh balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
mkuu mimi sio daktari, nilivyo maliza PCB wazazi walitaka nikawe daktari lakini kwa kuangalia future yangu sikwenda. lakini hili bado halisababishi nisione uadhimu wa hii fani. nchi nyingi duniani hasa zilizo endelea 'staarabika' madaktari ndio hulipwwa pesa nyingi. ni serikali yetu haioni unobility wa fani hii ndio maana wanawalipa kidogo na pia ndio sababu wanaanzisha mabomu ya substandards medical schools. tatizo ni kwamba serikali yetu ndio muajiri mkubwa. private sector lazima wangechagua wa MUHAS badala wa UDOM

Mkuu uchumi unahamia kwenye gesi na mafuta wanaopiga hizi kozi kukiwa na sera nzuri basi shavu lao kama walivyopiga geologists na ujio wa madini!!!!!

Kama unaamini fani fulani ni muhimu sana kuliko nyingine tukubali kutofautiana tu sababu mimi naona kila mtu ana umuhimu wake bora tu awe "super" katika fani yake. Ni yale yale ya "learned fellows" naona!!!!
 
Mmh gazeti la nipashe nimewahi soma kampuni moja wanatoa nafasi za ajira,vigezo GPA kwa waliohitimu Udom na SAUTI isiwe chini ya 3.8 na kwa vyuo vngne kama udsm,mzumbe nk GPA isiwe chini ya 2.9!

GPA ni indicator tu sio confirmatory!!!!
Waulize hao watu kwenye interview hali ilikuwaje??!!!
 
Tunaposema huu upuuzi wa vyuo vya kata hautakiwi watu wanasema tuna dharau bora jamii inajionea yenyewe.
Ati mtu alifeli kidato cha nne leo hii anapewa cheti cha kuwa daktari...ukiuliza nini eti ooh tunapunguza uhaba wa madaktari...pambaff sana.

MY TAKE

  • SERIKALI INATAFUTA KURA
  • G.ABACHORI ANASAKA NOTI
  • MLALAHOI ANASAKA AJIRA YA URAHISI

Ku feli ni "accelerator" ya kufanya vizuri zaidi usoni, kwa wenye uelewa wanaelewa hilo, sitegemei kwa punguani kuelewa hilo.

Aliingiaje A level kama kafeli au alirudia mtihani wa alichofeli na akapasi?

Hii nyuzi yako imekaa kimajungu-majungu.

Kuna daktari mmoja maarufu sana ana PhD na hana degree hata moja. Unamjuwa?

Halafu kuna failure mwengine wa 0 kabisa. Eti ni Mwenyekiti wa chama fulani cha upinzani na anawaongoza wasomi zaidi yake, na haambiliki. Unamjuwa?

Wacha porojo na kuhororoja, njoo na vitu vyenye mashiko.
 
Mliosoma UDOM inabidi mkasome tena vyuo vingine Post Graduate!!! Elimu ya udom bado sanaaa...

huo utumbo wako naweza kulinganisha nataahira aliyesema kuwa "wale wote mliozaliwa na Kina mama wa kule mashinani (kijijini) miaka hiyo mrudi mlikotoka mkazaliwe upya na akima mama wa kisasa /kileo (wamama wa mujini) kisa kikiwa ni kizazi cha analogia hakiwezi shindana na kizazi cha digitali ...nani ka kwambia kuwa elimu ya mtu inapimwa kwa jina la chuo ulichosoma...? kwa taarifa yako mi naona kuwa unawatukana washikaji zako uliosoma nao Shule ya sekondari ..kisa wewe ulisoma chuo kikongwe,... na wao chuo kipya .... "education for emancipation" bado sana hapa TZ.na unaonaekana kuwa u'r suffering from critical mental slavery...
 
Umenipa raha sana, nashukuru kwa kuwa na upeo mkubwa sana. Unanifanya niwaze juu ya ndoa za siku hizi! !!!
 
huo utumbo wako naweza kulinganisha nataahira aliyesema kuwa "wale wote mliozaliwa na Kina mama wa kule mashinani (kijijini) miaka hiyo mrudi mlikotoka mkazaliwe upya na akima mama wa kisasa /kileo (wamama wa mujini) kisa kikiwa ni kizazi cha analogia hakiwezi shindana na kizazi cha digitali ...nani ka kwambia kuwa elimu ya mtu inapimwa kwa jina la chuo ulichosoma...? kwa taarifa yako mi naona kuwa unawatukana washikaji zako uliosoma nao Shule ya sekondari ..kisa wewe ulisoma chuo kikongwe,... na wao chuo kipya .... "education for emancipation" bado sana hapa TZ.na unaonaekana kuwa u'r suffering from critical mental slavery...

Jamaa anaonekana anamgando wa mawazao maana anadhani kusoma chuo kongwe ndio kujua mambo na kufundishwa vitu vizuri...... #CHUOKONGWE HAKINA WAALIMU WAPYA??? Chuo kipya hakina WAALIMU WAKONGWE?????? Thatz why kuna watu WANAWAITA WENGINE NYANI, SI KWA MUONEKANO ILA KWA AJILI YA AKILI FINYU....... MONKEY INTELLIGENCE
 
Haikuanza leo hiyo!! Ilikuwa Makererean vs Muhimbili ,ikaja Muhimbili Vs Eastern blog na sasa ni Muhimbili vs IMTU,KCMC,UDOM.
Muulize Sarungi ukimuona!!!

Sarungi profesa,daktari wa mifupa?Vipi ilikuwaje ishu yake kwani?
 
ID yake inamtuma kuandika alichoandika!
 
Sioni uhusiano wa kichwa cha habari na content, pia mwandishi anaonekana ni mfuasi wa ligi za vyuo plus hakipendi UDOM, binafsi nimesoma UDOM na nafurahi kuwa msaada kazini na kwa jamii inayonizunguka kutokana na maarifa niliyopata. Swala la IMTU linaonekana lilikua la cost saving na kubanwa na deadline ya ukaguzi, sijui wanafunzi wao wanaingiaje hapo. Mwisho wa siku muhusika anaenda kusimamia uwezo wake na chuo alichotoka kitakua hakina msaada. Hata UDSM ina watu wametoka pale na kuwa msaada mkubwa sana kwa hii nchi lakini kuna wengine wametoka pale kama wametumwa kuwakatisha tamaa Watanzania.
 
Kuna rafiki yangu mmoja alisomea udaktari Muhimbili,akaenda Marekani kwa lengo la kufanya kazi kama daktari.Baada ya kukutana na vikwazo vya mitihani ya bodi,akaamua atafute kazi nyingine na sasa ni mfanyabiashara.

Rafiki yangu mwingine naye alisomea udaktari hapo hapo Muhimbili.Baadaye akafanya specialization(ubingwa)Muhimbili au Bugando kwa muda wa miaka miwili au mitatu kama sikosei.Sasa yuko nchi moja Ulaya mwaka wa pili anahangaika kurudia kozi za udaktari upya na kisha anatakiwa afanye mitihani ya udaktari ya wizara ya afya ya nchi husika au bodi ya madaktari, na kama atafaulu ndipo atapewa leseni ya kumruhusu kutibu wagonjwa.

Halafu hapa watu wanajisifia kuwa chuo chao cha Muhimbili ni bora zaidi.Kama nyie wazuri,mbona mkiletewa kesi mnazi refer India na South Africa?Vifaa hakuna na wataalam hakuna;kwasababu kama huna vifaa vya kutosha na vya kisasa shuleni,hutaweza pia kutengeneza wataalam wazuri.

Tufanyeje ili tutoke?Tufanyeje walau na sisi tuwe na wataalam competent na hospitali hata 3 tu nchi nzima zenye viwango kama vya India na South Africa?Tufanyeje ili India na Ulaya nao siku moja watamani kuleta wagonjwa wao Tanzania iliyosheheni wataalam wenye sifa zinazoheshimika duniani kote?Nadhani haya ndiyo yakujadili kama tunataka kuboresha sekta ya afya nchini.

Huwezi kusema wewe ni bora kuliko IMTU au UDOM wakati kwenye soko la dunia wote mnatupwa kapu moja na ili mpate ajira ya udaktari,wote mnalazimishwa kufuata utaratibu unaofanana kulingana na nchi mliyosomea udaktari wenu.
 
mkuu kinachoangaliwa ni passion na ujuzi wa mtu. nenda hata india ukaone wanaosoma hayo mambo ni division 3 na 4. sasa endeleeni kuangalia ufaulu mkubwa. dunia imebadilika

Hiyo india ndiyo chanzo cha mifumo ya kibiashara kwenye medical field.tena hadi biashara za viungo
 
Ku feli ni "accelerator" ya kufanya vizuri zaidi usoni, kwa wenye uelewa wanaelewa hilo, sitegemei kwa punguani kuelewa hilo.

Aliingiaje A level kama kafeli au alirudia mtihani wa alichofeli na akapasi?

Hii nyuzi yako imekaa kimajungu-majungu.

Kuna daktari mmoja maarufu sana ana PhD na hana degree hata moja. Unamjuwa?

Halafu kuna failure mwengine wa 0 kabisa. Eti ni Mwenyekiti wa chama fulani cha upinzani na anawaongoza wasomi zaidi yake, na haambiliki. Unamjuwa?

Wacha porojo na kuhororoja, njoo na vitu vyenye mashiko.
Eti kufeli ni accelerator ya kufanya vizuri!
Kufeli ni kufeli tu hata ukibadilisha jina!
Kwa hiyo mmewaambia walimu wafelishe ili baadae watu wafaulu?

Yaani umefeli shule ya msingi,sekondari halafu leo umeibuka na PHD!
Hii iko Tanzania tu na ndio maana tunajionea vimbwanga!

UDOM na IMTU limekuwa kimbilio la wale walioshindwa na kuingia makazini kwa kada za clinical officers,AMO,n.k

ilitakiwa kuwe na program tofauti ya kuwaendeleza watu hawa na sio kuwapa elimu nzito ya udaktari kisa wanataka kupandishwa vyeo!

Hapa ni sawa na issue ya kila kijana kutaka kuimba bongo fleva hata kama ni bubu!
 
Back
Top Bottom