Bomu la Arusha: Gari la Polisi PT 1179 lilitumika

Bomu la Arusha: Gari la Polisi PT 1179 lilitumika

huna uzalendo. raia mwema lazima aisaidie serikali kudumisha amani na kufichua maovu.

Uwasaidie kwani hawajui anayehusika! Wanachotaka kujua ni nani anajua kwa kiasi gani. Wakijua kwamba unajua kwa kiasi kikubwa lazima wakuondoe kwenye uso wa dunia! Labda watuletee wachunguzi toka nje na si akina Chagonja ambao kwanza familia yake haina maadili, mkewe kawadhurumu vijana kwa kuwatapeli pesaeti anao uwezo wa kuwapatia kazi polisi na Usalama wa taifa.
 
.....nimekumbuka mtoto wangu alikuwa anakuja na mikanda imetafasiliwa kiswahili na mtu anaitwa lufufu alivyokuwa akisema "hapo sasa Picha yetu ndo sasa inaanza"

Lufufu Mukanda (a.k.a mukandala) hivi huyu mtu yungalipo kweli? Au japo mikanda aliyotafsiri?
 
alielalamika ni chdm. ccm wakapuuza kwa kusema dalili ni kwamba wamejilipua wenyewe. kama chdm hawalalamiki na hawako tayari kutoa mkanda, basi yaishe. tuendelee na ujenzi wa taifa. amka usingizini dogo!
Hivi we hapo kwenye nyekundu una akili timamu? Yaani watu wamekufa we unasema yaishe?
Muuaji lazima apatikane awe Polisi, Chadema, CCM au yeyote yule na apewe stahili yake.
Damu ikimwagika hakuna "basi yaishe"! scramble
 
Last edited by a moderator:
Mengi yameanza kujulikana baada ya shuhuda aliyemuona mtu aliyerusha bomu kusimulia, akishuhudia chini ya kiapo mbele ya wakili anasema:

Jeshi la POLISI tunakanusha kuwa HATUNA GARI ZENYE NAMBA HIZO!
Usubiri kama Advocate Nyombi hajaja hapa kukanusha!!!!!!
 
Uwasaidie kwani hawajui anayehusika! Wanachotaka kujua ni nani anajua kwa kiasi gani. Wakijua kwamba unajua kwa kiasi kikubwa lazima wakuondoe kwenye uso wa dunia! Labda watuletee wachunguzi toka nje na si akina Chagonja ambao kwanza familia yake haina maadili, mkewe kawadhurumu vijana kwa kuwatapeli pesaeti anao uwezo wa kuwapatia kazi polisi na Usalama wa taifa.
kama unalidharau jeshi la polisi na serikali ya Tanzania, bac katafute kwengine pakushtaki. ushahidi wa video kama upo, kwa nini wasipewe waandishi wa habari ili video ioneshwe kwa watanzania? video ngapi zimewekwa hapa jamii forum? mbowe hana video. NI UONGO MTUPU
 
Mengi yameanza kujulikana baada ya shuhuda aliyemuona mtu aliyerusha bomu kusimulia, akishuhudia chini ya kiapo mbele ya wakili anasema:
Kama alifanikiwa kusoma namba ya gari la polisi, iweje ameshindwa kusoma hilo gari la kiraia? Halafu hawa mashuhuda mbona wanajichanganya? Wadau, si mnakumbuka yule aliyesema kuwa alimwona mrusha bomu akiwa amevaa kaptula ya jinsi ikiwa imechanika chanika? Tuelewe lipi sasa?
 
Nakuhakikishia sasa hivi hilo gari limeshatolewa kwenye system ya magari ya Polisi
 
Hivi we hapo kwenye nyekundu una akili timamu? Yaani watu wamekufa we unasema yaishe?
Muuaji lazima apatikane awe Polisi, Chadema, CCM au yeyote yule na apewe stahili yake.
Damu ikimwagika hakuna "basi yaishe"! scramble
kama mbowe ana ushahidi na kaukalia tusemeje? hana uchungu na waliouawa. aite wandishi wa habari awachezee video. aweka mkanda hapa JF. mbowe alikurupuka. kauli yake imedumaza upelelezi wa polisi. kama ushahidi upo, kwa nn wapeleleze. kwanza mbowe aombe radhi kuwa aliwadanganya watanzania, ndiyo mambo mengine yatafuata. kama haombi radhi laana ya waliouawa itampata.
 
mbowe atoe mkanda kumaliza utata. hivi ana nakala moja tuu? haiwezekani kuurudufu ziwe nakala nyingi? awape polisi au rais, wakikaa kimya kwa muda kama wa wiki mbili, aite waandishi wa habari makao makuu ya chadema na aucheze mbele yao. waandishi wataanika kwenye taarifa za habari. sijui ugumu uko wapi hapa. kiala mtu mwenye akili timamu ameshauri hivyo. labda kama mbowe alisema uongo hana mkanda. wanasiasa hawaaminiki!
Hii ishu ya Arusha ushahidi hauwezi kutolewa kirahisi tu.Kama serikali ni mtuhumiwa namba moja,huu ushahidi kwa nini upeleke kwa mtuhumiwa huyo huyo(serikali)?Katika hili tume huru na ya kimataifa ndio suluhisho.USHAHIDI UTATOLEWA KWA CHOMBO MUAFAKA na wala sii polisi au vyombo vya habari as it stand!Kwani ishu ya Mwangosi,Dr Ulimboka,EPA,Richmond,Mlipuko wa bomu Kanisani polisi wamefanya nini so far?Leo hii kuna wezi wa fedha za umma ,wameficha mamilioni kwenye off shore accouncts huko Uswiss.Hapo napo mnataka evidence ili muwashike wakati mambo yapo wazi?If anything polisi walete eveidence basi kwamba wao hawajahusika(Kwa kumleta mtuhumiwa)
 
watu wameuawa. mbowe kasema ana ushahidi. ww unasema halazimiki kuutoa hata kuupeleka ofisi za un au kuitisha press conference na kucheza video yake!
Ngoja kwanza Chagonja na tume feki yake wajichanganye kama walivyojichanganya kifo cha Mwangosi video ilipotoka wakaaibika vibaya, safari hii tunaka tuwaonyeshe watanzania na dunia jinsi polisi wa Tanzania wanavyolinda wananchi na mali zao.
 
Mimi binafsi nilikuwepo eneo la tukio na nilikua takriban mt 8 na lilipotua Bomu baada ya kurushwa.
Ilikua ni mida ya saa 11:50. Mwenyekiti Mbowe alishuka kwenda kukusanya pesa(SADAKA) kwa ajili ya Kugaramia chakula na vinywaji kwa mawakala siku inayofuatia ambayo ndio siku ya Uchaguzi.

Mara tu Mbowe aliposhuka Bomu likarushwa kutokea MASHARIKI KASKAZINI mwa uwanja kuelekea alipokuwa Mbowe akikusanya pesa.
Mimi nilikuwepo takriban mt 9 kwa upande wa Mashariki na ilipoanguka Bomu.Kwa wale wanaojua Jiografia ya Uwanja wa Soweto Jukwaa kuu lilikua upande wa Mashariki mwa uwanja likiangalia Mgharibi kulikokua wamekaa watu.. Na nyuma ya Jukwaa (GARI LA MATANGAZO) ni barabara na ngambo ya barabara ni Nyumba(Kotaz) za AICC. mbele ya nyumba hizo kuna KICHAKA cha Maua ya Bogavilia.
Bomu liliporushwa lilpita juu yetu likiwa limefungwa na kitu cheusi kama Soksi au Nailoni.Hakika binafsi kabla ya bomu hilo kutua chini na kulipuka nilipoona ikipita juu nilidhani ni Popo alietoka kwenye mti uliopo Jirani na Jukwaa kwa upande wa mashariki mwa uwanja.

Polisi walikuepo uwanjani upande wa Kusini magharibi mwa uwanja na jukwaa kuu.! Bomu lilipo lipuka yaonekana kabisa Mrusha bomu alikua kajificha kwenye kichaka cha Maua ya bogavilia ngambo ya barabara Mashariki mwa Uwanja nyuma ya Jukwaa kuu ndio maana hakuweza kuonekana.

KILICHOTOKEA KATI YA POLISI NA RAIA:
Baada ya Mlipuko na watu kuanza kukimbia huku na kule ndipo Polisi bila kujua nini kilichotokea kwa kua walikua mbali wakadhani watu wanawakimbiza wao. Muda huo tayari watu wachache walikua chini wakiwa wamejeruhiwa na BOMU na Polisi nao walikua kwanza ndio wamezunguka kuja upande wa Mashariki mwa uwanja kulipotokea Mlipuko.

Lakini kwa bahati mbaya Watu wengi na Polisi haswa waliokua mbali hawakujua kwamba mlipuko huo ni wa Bomu. Wengi walijua ni bomu la Machozi limerushwa na Polisi.

Pale ndipo Watu wakawa wanawafuata Polisi na polisi nao wakaanza kurusha risasi hovyo kuelekea jukwaa kuu na baadhi ya risasi kupiga watu na zingine kutoboa tanki la mafuta ya Lori la matangazo ambalo ndilo lilikua Jukwaa kuu.watu wengi walijeruhiwa na Risasi zilizokua zikirushwa na polisi na sio bomu.

Baada ya hapo ndipo watu wakaanza kuwarushia polisi mawe na muda huo tangia bomu kurushwa ni zaidi ya dk 7 au 10.

Polisi baada ya kuzidiwa nguvu walikimbia ndipo watu wakaanza kuwachukua majeruhi kuwapeleka Hospitali. Polisi walirudi baadae baada ya kama dk 45 wakati hali ikiwa imetulia.

Huu ndio ukweli na mh LUKUVI kudanganya kuwa eti watu wa CDM ndio walimtorosha mtuhumiwa sio za kweli.ni za uongo na za KUPOTOSHA UMMA.

Uongozi wa JF Naomba msiunganishe mada hii na nyingine. Ijitegemee.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...shwa-mengine-ni-propaganda-5.html#post6610017
 
Ndugu zangu wana Jamvi tuwe makini sana na habari tunazoambiwa ,lakini pia jambo moja la msingi hapa tujenge mazoea ya kuwa Inquisitive and investigative tukisha kumiliki stadi hizi,Sasa twende mbali zaidi kupanua upeo wetu katika matukio mbalimbali na tujitahidi sana kuwa na uwezo wa kuoanisha matukio yanayojili katika maeneo mbalimbali katika maktadha wa habari tunayokuwa tunashughulika nayo.Kamwe hatuishii hapo tunajaribu tena kuoanisha matamko ya viongozi wa ngazi mbalimbali katika jambo husika mbali zaidi,kwa uhalali wa kutoa hoja na kujiridhisha unatembelea eneo la chanzo cha gumzo,unakutana na vyanzo mbalimbali vinavyounga mkono au kupinga mada tunakusanya.Teknologia ya habari na mawasiliano imekuwa sana,Tunashukru sana.Hakuna cha kujificha,Kwa mfano la Arusha wakati tunarumbana kwa matamko yasiyoridhisha. Ebu tujiulize masawali haya madogo.Je ikipatikana picha ya mhusika akiwa anarusha bomu,huu ni mfano tu,akapatikana anayemtuma.Kwa usahihi akazungumza kwa hofu ya MUNGU. unajua dhambi inatesa rohoni.Kwani wakati huu ndo litukie?.Kwanini mkutano A sio B?. Maswali yanakuwa mengi sana.Mimi nina hakika ukweli utabainika hata kama ukichelewa kidogo,tukafa, tukabaki kwa maumivu ya ulemavu na maradhi.Siku ipo na si mbali.Madhira yanapoongezeka.Its SUNRISE.Kumepambazuka anayemkanyaga mwenzake ni kwa makusudi.
 
Hii ishu ya Arusha ushahidi hauwezi kutolewa kirahisi tu.Kama serikali ni mtuhumiwa namba moja,huu ushahidi kwa nini upeleke kwa mtuhumiwa huyo huyo(serikali)?Katika hili tume huru na ya kimataifa ndio suluhisho.USHAHIDI UTATOLEWA KWA CHOMBO MUAFAKA na wala sii polisi au vyombo vya habari as it stand!Kwani ishu ya Mwangosi,Dr Ulimboka,EPA,Richmond,Mlipuko wa bomu Kanisani polisi wamefanya nini so far?Leo hii kuna wezi wa fedha za umma ,wameficha mamilioni kwenye off shore accouncts huko Uswiss.Hapo napo mnataka evidence ili muwashike wakati mambo yapo wazi?If anything polisi walete eveidence basi kwamba wao hawajahusika(Kwa kumleta mtuhumiwa)
mkuu haya ni maneno matupu ambayo hayavunji mfupa na chadema wanahangaika sana kutunga uongo .
 
kama mbowe ana ushahidi na kaukalia tusemeje? hana uchungu na waliouawa. aite wandishi wa habari awachezee video. aweka mkanda hapa JF. mbowe alikurupuka. kauli yake imedumaza upelelezi wa polisi. kama ushahidi upo, kwa nn wapeleleze. kwanza mbowe aombe radhi kuwa aliwadanganya watanzania, ndiyo mambo mengine yatafuata. kama haombi radhi laana ya waliouawa itampata.

Kwenye hicho chumba atakachowaita waandishi wa habari watalipuliwa wote na mabomu yanayonunuliwa kwa kodi zetu
 
kwani kwenye mkutano wa siasa magari ya polisi huwa hayaruhusiwi? hakuna uwezekano kuwa ni kweli hilo gari lipo arusha lkn zimetajwa namba zake ili kuhalalisha ushahidi wa uongo? kwa nini mbowe anaedai ana mkanda wa tukio Zima asiutoe? upuuziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Kwa nchi hii ambapo gari ya RC au DC hubandikwa number za kiraia pasi na kujua zimetengenezwa wapi na kwa nini, Muda si mfupi hio gari utaambiwa haipo na haijasajiliwa TZ. Wanaweza kuwa walikuja na plate number ya tukio lile. kama ipo video inayoonyesha gari ile, kitu ambacho nina hakika kitakuwepo na kitawekwa wazi kama ushahidi mahakamani, ccm mtaumbuka.
 
kama mbowe ana ushahidi na kaukalia tusemeje? hana uchungu na waliouawa. aite wandishi wa habari awachezee video. aweka mkanda hapa JF. mbowe alikurupuka. kauli yake imedumaza upelelezi wa polisi. kama ushahidi upo, kwa nn wapeleleze. kwanza mbowe aombe radhi kuwa aliwadanganya watanzania, ndiyo mambo mengine yatafuata. kama haombi radhi laana ya waliouawa itampata.
Well I don't care what Mbowe or anyone else do or say.
The thing is the offender should get his right!
Tusilete mchezo inapokuja suala la vifo. Uhai wa waliofariki hautarudi na LAZIMA mauaji nchi hii yakome la sivyo tunajiletea laana kama taifa. Hatutakaa tufanikiwe kama kila siku Tunamwaga Damu ya watu wasio na hatia.

Lazima haya mauaji yafike kikomo! scramble
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom