Bombing: Tanzania frees 3 Emiratis

Bombing: Tanzania frees 3 Emiratis

Msijaribu kulazimishia mambo! Sio lazima waliolipua wawe Waarabu. Kwani ndo walikuwa wakilipua makanisa? Ndo waliowapiga mapadri risasi kule Zenj? Kwani ndo waliousiwa na Sheikh Ilunga kuwa wauwe viongozi wa wakristo? Waarabu wa watu walikuwa na shughuli zao halali ikatokea watiliwe mashaka na kukamatwa na baadaye uchunguzi umebaini kuwa hawahusiki. Tafsiri yake ni kwamba dhana ya kuwa hilo ni shambulizi la kigaidi toka nje ta Tz sio sahihi. Kama sivyo thanabaki na shuku yetu iliyobaki kuwa lilikuwa shambulio lenye mlengo wa kidini kama mwendelezo wa yale mengine, na kitulacho ki nguoni mwetu. Kazi kwenu vyombo vya ujasusi vya Tanzania.
 
Kuna story ilikuja hapa kuhusu yule kijana aliyemkimbiza mmoja wa washukiwa mpaka akamkamata baada ya mshukiwa kuchoka kukimbia. Kwa kuonyesha zaidi kama alikuwa ni mshukiwa, yule kijana akawa anadai walimkuta na mfuko mwingine ambao ulikuwa na mabomu zaidi.
story ndiyo hii,

MATUKIO » ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA
ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA


ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.
Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.
Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza.
“Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana,” alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo, walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!
Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa.
“Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake.
Unaona huyu mbulula anataka kutu-diverge attention zetu na magazeti yake ya ma-house girls wa darasa la saba! Wewe kama unatumia kichwa kweli kufikiri unaona hiyo story ina ukweli wowote?
 
Jeshi la Policcm linafanya kazi kisiasa, Alipotekwa Dr.Ulimboka tuliambiwa mkenya. Mlipuko wa Mabomu wasaudia. Sikatai kama wameshiriki au hapana, uchunguzi wa kina lazima ufanywe kabla ya kuwabambikia watu kesi nzito.
 
Hakuna kitu kibaya kama kuwa taifa nyonge. Hivi unafikiri wangekuwa ni watanzania wamekamatwa Uarabuni kwa tuhuma za ugaidi au kosa lingine lolote lile, unafikiri wangeachiwa kirahisi namna hiyo? Nakumbuka hata kuna afisa ubalozi wa nchi fulani ya mashariki ya kati alibaka dada wa kitanzania, na alipokuwa anajaribu kutoroka alikamatiwa uwanja wa ndege Dar. Baada ya kukamatwa nchi yake ilikataa kumwondolea kinga ili ashtakiwe na badala yake wakasema arusishwe nyumbani waangalie utaratibu mwingine. Hapo tukawa hatuna ujanja zaidi ya kufyata mkia na kumwachia muhalifu arudi kwao kuendelea na maisha yake kama kawaida. angekuwa ni Afisa ubalozi wa Tanzania huko Uarabuni nawaakikishia kingenuka. Kweli unyonge mbaya sana.

wewe mkuu kwa akili yako ndogo hata kama hawana hatia unataka waendelee kushikiliwa kisa tu ni wa nje huo mbona ni ushamba mkubwa sana ulionao mkuu.
 
Kesi ya ugaidi wa kimataifa watuhumiwa akna alfayed wanaachiwa ndani ya wiki akna ambrose bado wataozea ndani..tunaipeleka wap nchi hii jaman...
Kwa hiyo unataka kulazimisha watu wa kukamatwa?au huamini kama akina victor wanaweza kuhusika na hilo tukio. Muulize pengo atakuambia nani wamehusika. Ndomaana wamekaa kimya hawajatoa tamko lolote kitu ambacho si cha kawaida
 
Wewe unarudiarudia kitu kisicho na mantiki kabisa. Kukamatwa au kuhisiwa watu wasiohusika kwenye tukio kama hili ni jambo la kawaida. Lakini unampomkamata mtu na kukaa nae muda huo wote halafu baadae unamwachia kama unafanya magendo ya karafuu lazima utakuwa unakaribisha hisia za kila aina.
Sasa mkuu, kama kuna mloo ! tufanyeje? Wenezu wanalenga mbali. Huwa hawaeleweki.
 
Wewe acha kutunga hoja za kihuni mbona alipokamatwa lwakatare na ugaidi hukuongea haya nawakati guest walikuwa wengi.

double standard Lwakatare Kikwete anakaza kamba aozee ndani waarabu akikumbuka suti anazohongwa anatuma waziri wake kwenda kuwatoa ,Kikwete kuna siku utajibu haya
 
Watu wengine kwa kujifanya upolisi na ushushushu na kutuletea majibu mepesi kwa issue nzito! Tuwaache wahusika wafanye kazi zao kwa uhuru na haki.
Tusipende kuingiza hisia na dhana kwenye mambo nyeti ambayo yamehusisha na raia wa nchi nyingine.
Rais mstaafu Mwai Kibaki alishawahi kwenda kupiga magoti kuomba msamaha Emirates kwa kuwaweka raia wake rumande bila ya kuwa na ushahidi.
 
Duh.. wangeozea jela hawawajui polisi wetu nini? yaani kwenye ukachero ni zero - wanachojua ni kamatakamata tu. wamebakia kuwalinda viongozi, kubambikia watu kesi na kuua tembo wetu "ujangili". Katika hili wataumia wengi sana ambao hata hawahusiki kabisa ili kukamilisha mradi wa funika kombe mwanaharamu apite!
Wewe ungekuwa hata na sura ya aibu polisi usiku kucha wanapambana na matukio kibao na wewe unaongea ubwabwa wako humu jf.
 
Wabunge mnaotoka maeneo yanayolima pamba chunguza jambo hili, nini TCB,TGT,DC,RC wanachofanya kwa wakulima wa pamba paza sauti wakulima wanadanganywa!!!!!!!!!!!!
 
Kwa hiyo unataka kulazimisha watu wa kukamatwa?au huamini kama akina victor wanaweza kuhusika na hilo tukio. Muulize pengo atakuambia nani wamehusika. Ndomaana wamekaa kimya hawajatoa tamko lolote kitu ambacho si cha kawaida

Kwa Kikwete Victor Ambrose ni gaidi si ndio maana Kwa Neema radio waliifunga ili kuwafurahisha wale waliokuwa wakiipenda radio ya morogoro aminia serikali ya Kikwete waarabu wanatoa mshiko mkubwa huko loliondo au sio
 
Atongwele, natumia mchina.
Kwahiyo unataka kuniambia Suala la mabomu(UGAIDI) kulipuka hapa Tz kazi hiyo tumewaachia FBI. Ok, kama ni hivyo ni kwamba usalama wa taifa na vyombo vya usalama hapa kwetu ni zero na kama ni hivyo hata suala la Lwakatare tungewaachia FBI kwasababu kulikuwa na shitaka la Ugaidi.
 
Unaona huyu mbulula anataka kutu-diverge attention zetu na magazeti yake ya ma-house girls wa darasa la saba! Wewe kama unatumia kichwa kweli kufikiri unaona hiyo story ina ukweli wowote?
Mkuu, hilo si gazeti la ma house girls. Ni gazeti la mmoja wa wafadhili wa chadema, gazeti la Nipashe. Ninaamini kuwa story hiyo iliandikwa kutokana na ushahidi wa mashuhuda. Hawakukurupuka. Isipokuwa kuna watu wanataka kulazimisha tukio hili ili ionekani watu wa dini nyingine ndo wamehusika
 
Very crazy! Definately the Saudi(s) will be released soon! Itabidi waendesha bodaboda watengenezewe ushahidi ili wafungwe otherwise serikali itaonekana haifanyi kazi. It doesnt click in mind that they were not suspects but were arrested because they happened to be on the crime scene! How many people were there? Why didnt they arrest all the people at crime scene?

Kwakuwa ni waarabu basi.
 
Atongwele, natumia mchina.
Kwahiyo unataka kuniambia Suala la mabomu(UGAIDI) kulipuka hapa Tz kazi hiyo tumewaachia FBI. Ok, kama ni hivyo ni kwamba usalama wa taifa na vyombo vya usalama hapa kwetu ni zero na kama ni hivyo hata suala la Lwakatare tungewaachia FBI kwasababu kulikuwa na shitaka la Ugaidi.
Mkuu, vita dhidi ya ugaidi duniani kote ipo chini ya marekani. Wao ndo hupanga nani awe gaidi na naniasiwe gaidi. Ni kutokana na maelekezo yao ndo maana mashtaka ya ugaidi lwakatare amefutiwa. Angalia hata kule cuba ambako kuna gereza la guantanamo linalosimamiwa na wamarekani. Pale hata serikali ya cuba haina mamlaka napo. Sembuse hapa bongo?
 
Uktaka kujua huu ni mkakat wa siri wa serkali angalia guest apo chni waliotumwa kupma upepo watanzania tuamke 2015..hakuna kuwarudsha hawa watu madarakan

There are currently 2221 users browsing this thread. (94 members and 2127 guests)

Safari bado ndefu sana.
 
Msishabikie tu.... Ulizeni Kenya walifanywa nini
walipowakamata raia wa Emirates???? Kibaki aliomba msamaha
Raia wa SAUDIA watatu wamefungwa life sentence in Kenya juzi tuu kwa taarifa yako!!!
 
GODBLESS LEMA alivyoongea mkamuana mgomvi..haya sasa tusubiri walipue lingine, labda watakamatwa..
 
Taarifa zinatangulia uarabuni kutoka wakati hapa nyumbani bado hatuna taarifa.
 
Back
Top Bottom