Bombing: Tanzania frees 3 Emiratis

Bombing: Tanzania frees 3 Emiratis

Sina shaka yo yote kuwa madereva wa bodaboda hawahusiki na ulipuaji wa bomu kanisani! Mlipuaji bado yuko mitaani anadunda!

Cha kushangaza askari wetu walishindwa hata kuchukua alama za vidole katika pikipiki aliyopanda huyo gaidi!?
sasa alama ya vidole inasaidia nini kama hakuna database?..labda tusubiri hivyo vitambulisho vya taifa ili wachukue fingerprint za raia wote ziwe kwenye database ndo tutaweza kamata wahalifu kwa ushahidi wa fingerprint.
 
Twiga wamekwenda na sisi tunakwenda...tusubiri watuletee aioc na mhakama ya kadhi...mungu tuhurumie watanzania na tuepushe na hili janga
 
Ushahidi wa kuwatia hatiani unaweza usiwepo lkn cha kujiuliza uchunguzi umeshakamilika ktk muda huu wa juzi tu??
Lwakatare hata mfano wa bomu hakuwa nao lkn kakaa lupango mpaka leo hawa waarabu juzi tu ushahidi tayari.

SERIKALI YA CCM ndiyo inayopanga mauaji haya ili kuwavuruga watz nchi iingie ktk machafuko. Liko wazi.
Kama Victor alikamatwa Nchimbi akasema mwenyewe 2days after IGP anakuja anatangaza dau la 50m kwa atakayempata mlipuaje, hivi hapa J.K & Co wanaona kila mtu ni mjinga kama wao?
 
Nina wasiwasi wa wahusika kutokutiwa nguvuni, zaidi ya hao washukiwa
 
Kama kweli wameachiwa ni wazi kuwa hawakubusika. FBI walifika eneo la tukio na wamewahoji wahusika na wamejiridhisha kuwa hawana conncetion yoyote na tukio hilo. So tuendelee namaisha yetu
 
baada ya uchunguzi yawezekana imebainika kuwa hawajahusika kwa nini waendelee kushikiliwa.
 
Uktaka kujua huu ni mkakat wa siri wa serkali angalia guest apo chni waliotumwa kupma upepo watanzania tuamke 2015..hakuna kuwarudsha hawa watu madarakan
 
Ushahidi wa kuwayia hatiani unaweza usiwepo lkn cha kujiuliza uchunguzi umeshakamilika ktk muda huu wa juzi tu??
Lwakatare hata mfano wa bomu hakuwa nao lkn kakaa lupango mpaka leo hawa waarabu juzi tu ushahidi tayari.

SERIKALI YA CCM ndiyo inayopanga mauaji haya ili kuwavuruga watz nchi iingie ktk machafuko. Liko wazi.
Kama Victor alikamatwa Nchimbi akasema mwenyewe 2days after IGP anakuja anatangaza dau la 50m kwa atakayempata mlipuaje, hivi hapa J.K & Co wanaona kila mtu ni mjinga kama wao?
Mkuu, fbi wamefanya kazi yao. Suala la lwakatare lipo chini yetu na hatujahusisha fbi. Lwakatare ni hatari zaidi na yeye amakamatwa kutokana na ushahidi wa ilevideo
i
 
ukitaka kujua kama wewe ni mdini ndio utajipima kwenye matukio kama hayo,,yaani huna chengine chochote cha kufikiria milipuko kma hiyo inaweza kusababishwa,wewe unawanyoshea watu wa upande wa pili ndio waliohusika,,sasa jamani tunataka tuumalize udini,jeee tutaumaliza?
 
Kesi ya ugaidi wa kimataifa watuhumiwa akna alfayed wanaachiwa ndani ya wiki akna ambrose bado wataozea ndani..tunaipeleka wap nchi hii jaman...
 
Hakuna kitu kibaya kama kuwa taifa nyonge. Hivi unafikiri wangekuwa ni watanzania wamekamatwa Uarabuni kwa tuhuma za ugaidi au kosa lingine lolote lile, unafikiri wangeachiwa kirahisi namna hiyo? Nakumbuka hata kuna afisa ubalozi wa nchi fulani ya mashariki ya kati alibaka dada wa kitanzania, na alipokuwa anajaribu kutoroka alikamatiwa uwanja wa ndege Dar. Baada ya kukamatwa nchi yake ilikataa kumwondolea kinga ili ashtakiwe na badala yake wakasema arusishwe nyumbani waangalie utaratibu mwingine. Hapo tukawa hatuna ujanja zaidi ya kufyata mkia na kumwachia muhalifu arudi kwao kuendelea na maisha yake kama kawaida. angekuwa ni Afisa ubalozi wa Tanzania huko Uarabuni nawaakikishia kingenuka. Kweli unyonge mbaya sana.
 
Jioni njema hutokea kukamata randomly; Mwezi jana kwenye tokeo la Boston Marathon bomu, Tangazo la kwanza kabisa wamerekaniUS na taaluma zote za kiintelijensia baada ya mripuko tu walitangaza eti Msaudi ndo mhusika na ni kijana mwanafunzi tumemkaribia kumweka nguvuni !! (hapo boston peke kuna wanafunzi zaidi ya elfu5 wa kisaudia) Looh,
Wakuu hao baadaye kupeleleza waka geuza kibao na kuomba radhi na kutoa taarifa ingine kuwa walotenda ni wa CHECHENIA/warussi. eti wanafanana, Sasa mambo kama haya yanatokea kukamata mtu katika " WRONG PLACE and WRONG TIME"...
Lakini tusubiri reporti ya FBI hao mababa riwaya yao ni nini? Hakuna siri itakayo fichwa milele!!
good luck.

Wewe unarudiarudia kitu kisicho na mantiki kabisa. Kukamatwa au kuhisiwa watu wasiohusika kwenye tukio kama hili ni jambo la kawaida. Lakini unampomkamata mtu na kukaa nae muda huo wote halafu baadae unamwachia kama unafanya magendo ya karafuu lazima utakuwa unakaribisha hisia za kila aina.
 
Mimi hata sielewi tofauti ya bomu kuwa la kgaidi na la kidini nisaidieni jamani? kwani wa suni na washia kule Iraq si ugaidi na udini humo humo??? Hata sielewi kabisa jamani nisaidieni.

kweli wewe unahitaji elimu kubwa ngoja nile nitakuelimisha.
 
Duh.. wangeozea jela hawawajui polisi wetu nini? yaani kwenye ukachero ni zero - wanachojua ni kamatakamata tu. wamebakia kuwalinda viongozi, kubambikia watu kesi na kuua tembo wetu "ujangili". Katika hili wataumia wengi sana ambao hata hawahusiki kabisa ili kukamilisha mradi wa funika kombe mwanaharamu apite!
 
Inashangaza kwamba utendaji kazi wa jeshi letu la polisi ni kama Zima moto. Tukio likitokea basi utasikia tumewakamata watu kadhaa kwa mahojiano. Mambo yakishapoa wanaachiwa huru na mambo yanakuwa kimyaaa!! Jeshi linatakiwa lifanye kazi kimkakati si kukamatakamata watu kwa mahojiano na hakuna kitu cha zaidi ya hapo. We ona mafisadi wanaofikishwa mahakamani kesi zao zinavyosuasua kule Kisutu. Utasikia wote wameachiwa mahakamani! just give them time. Nimepata kufuatilia kesi moja ya jinai pale Kisutu nikagundua kwamba state attorneys wengi hawapo makini kuhakikisha conviction ya watuhumiwa inapatikana. Wanaletwa na basi lao pale Kisutu, wanapekuapekua mafaili hata kujiandaa vizuri hakuna, wanaingia kwa gakimu hawajajipanga. Wengi hawako motivated na wanafanya kazi bora siku imepita. Kila mtu anatamani siku moja nae awe wakili wa kujitegemea. Wachache ambao umri umekwenda wanajitutumua ili angalau siku moja ngekewa imwangukie ateuliwe jaji!! Kwa hali hii kweli kuna mtuhumiwa smart atapatikana na hatia? Rushwa yenyewe pale Kisutu inatolewa nje nje!! Kwa hiyo unakuta polisi hawafanyi kazi yao vizuri ya kukusanya ushahidi, mawakili wa serikali nao wapo wapo tu, mwisho hakimu anamuachia huru mtuhumiwa hata kama anajua kabisa kesi hii ingemwangukia lakini afanye nini. Unachotakiwa kufanya ili ushinde kesi pale Kisutu ni kuajiri wakili wa utetezi mkali sio kilaza!! baaasi, unashinda kesi hata kama ni ya kuua!
 
uchunguz wa ugaid unafanyka ndani ya one week na watuhumiwa wa kimataifa wanaachiwa?????its amazing
 
Uktaka kujua huu ni mkakat wa siri wa serkali angalia guest apo chni waliotumwa kupma upepo watanzania tuamke 2015..hakuna kuwarudsha hawa watu madarakan
Wewe acha kutunga hoja za kihuni mbona alipokamatwa lwakatare na ugaidi hukuongea haya nawakati guest walikuwa wengi.
 
huyu LEMA NDIO ATAKUWA AMELIPUA KANISA..SIO BURE CHADEMA MAGAIDI,,
 
Back
Top Bottom