Bombing: Tanzania frees 3 Emiratis

Bombing: Tanzania frees 3 Emiratis

Answers to your questions are simple:

>> Very crazy Iron, how can you arrest all the people at the crime scene?!!!!!!

>>They arrested them because they were foreigners and to make matter even worse; they were Arabs i.e the usual suspects when it comes to terror charges. Umeelewa chuma?

That means walikamata randomly! Kama walikuwa wanatafuta research sample vile! Maana nilifikiri wamewakamata maana they have a reason to believe wamehusika! Kama hawakusika kabisa, then why arrest them? Na kama wamehusika kwanini wameachiwa?
 
Mimi hata sielewi tofauti ya bomu kuwa la kgaidi na la kidini nisaidieni jamani? kwani wa suni na washia kule Iraq si ugaidi na udini humo humo??? Hata sielewi kabisa jamani nisaidieni.
 
Kumbuka ya Ulimboka. Sasa hivi tunatafuta Mkenya mwingine tumuuzie kesi!

Nadhani wanatafuta mmoja aliyeendeshwa na Victor. Akipatikana mchezo umeisha, kesi itakwenda hapo, hakuna ushahidi, itafutwa, tutaambiwa tuheshimu mahakama! Watu wenye ndevu ndefu na sura za kiarabu au kisomali wakae vyema. Lolote laweza kutokea
 
Kwani unajua leo. Waarabu waliwabebesha nazi babu zako enzi zile. Kwa kifupi ni kwamba waliwazidi akili kipindi kirefu.

Na sasa wamerudi kwa style nyingine ya kutubebesha nazi kwa kupitia vichwa vibovu vya viongozi wetu
 
Yaani jeshi linakamata watu watano wote hawahusiki! Kabisa!? Sasa naamini mkuu alipigwa biti na akakatisha ziara kuja kuwatoa!
 
Kuna story ilikuja hapa kuhusu yule kijana aliyemkimbiza mmoja wa washukiwa mpaka akamkamata baada ya mshukiwa kuchoka kukimbia. Kwa kuonyesha zaidi kama alikuwa ni mshukiwa, yule kijana akawa anadai walimkuta na mfuko mwingine ambao ulikuwa na mabomu zaidi.
story ndiyo hii,

MATUKIO » ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA
ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA


ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.
Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.
Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza.
“Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana,” alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo, walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!
Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa.
“Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    102.5 KB · Views: 114
Mkuu kama ushahidi wa kuwatia hatiani haupo, unalaumu nini?

Kuna kesi nyingi sana zimefunguliwa na baadaye huko mahakamani ikaonekana mtu hana hatia, akaachiliwa. Lwakatare aliwekwa ndani kwa 'kubambikiwa' kesi lakini ilichukua muda mrefu sana mpaka kufutiwa kesi ya ugaidi, na mpaka leo hii bado yuko ndani kwa shitaka moja.

Shitaka la ugaidi ni kubwa sana kutegemea ya kuwa ndani ya wiki moja serikali itakuwa imekusanya ushahidi wa kutosha kiasi cha 'kuwafungulia' waarabu hao. Ikumbukwe ya kwamba Tanzania ilipata mikikimikiki ya ugaidi wakati Ubalozi wa Marekani ulipolipuliwa na bomu mwezi Agosti 1998. Wakati dunia nzima inahangaika kutunga sheria za kupambana na matukio ya kigaidi, sisi mpaka leo hii hatuna sheria kali za uhakika isipokuwa za 'kusuka mikanda ya video'. Kushutumiwa kwa kesi ya ugaidi kungewezesha serikali kuwaweka ndani kwa muda mrefu ili kukusanya ushahidi wa kutosha, na kutoa fursa kwa vyombo vya sheria kuangalia uzito wa kesi yenyewe kwa upana wake. Sioni sahihi kama watanzania huhusan dereva wa 'bajaj' au bodaboda wanaendelea kushikiliwa huku raia wa kigeni wameachiwa 'eti kwa kukosekana ushahidi'. Kwa nini basi na hao watanzania wasiachiwe wote? Suala zima linaleta harufu ya kuwasafisha wenye pesa wageni (wafadhili) na kuwabambikizia kesi wazawa kwa kuwa uwezo wao kipesa ni mdogo.

Enzi za Mwalimu kulikuwa na Presidential Detention Act iliyokuwa inampa mamlaka Rais kumweka ndani mtuhumiwa kwa muda mrefu bila ya kumfungulia mashitaka ikiwa anashukiwa kuhatarisha usalama wa Taifa, ama kwa kuhujumu uchumi, siku hizi tunaita kufisadi. Sheria kama hii ingeweza kutungwa na kutumika kwenye masuala nyeti kama haya. Si lazima iwe kama ilivyokuwa mwanzoni, kwamba rais ndiye awe mwenye mamlaka, lakini hata mahakama ingeweza kupewa mamlaka ya kumweka ndani mtu anayeshukiwa kwa ugaidi kwa muda mrefu zaidi na kuendelea kutafuta ushahidi (kama upo).

Haiingii akilini mwangu kabisa... tunataka yatokee mangapi ndiyo tujue wabaya wetu ni kina nani? Kama ni kuwaachia basi wawaachie wote, tujue hatuna serikali wala jeshi la polisi la kutulinda sisi wanyonge!
 
Msishabikie tu.... Ulizeni Kenya walifanywa nini
walipowakamata raia wa Emirates???? Kibaki aliomba msamaha

Wako walioshabikia jana kwa kasumba tu za kutojua serikali inaendeshwaje? na kutoa misimamo ya uki-chadema, kama CCM watawapa serikali hawa Chadema with no time wataigeuza nchi chini juu, kwa sababu hufikiri kwa tumbo. ndani ya masaa 24 tangu diplomatic row start Emirates wameachiwa.

Historia inajirudia haya si kwa Tanzania tu hata kwa mataifa makubwa kama USA na UK they do the same, ona hapa Tony Blair akiwa Waziri mkuu wa uingereza alipobwaga manyanga kwa Saudis on Arms deal corruption
Source: The Saudi-GPT deal inquiry must not be another whitewash | Andrew Feinstein | Comment is free | The Guardian

Na hivyo hivyo kwa USA in getting support to Afghanistan. more recently jirani zetu Kenya nini Mwai Kibaki alifanya kwa Emirates.

Someni duru sio mnashabikia tu kutaka kuwatia hatiani watu bila ya ushahidi (prima facie case - Prima facie also refers to specific evidence that, if believed, supports a case or an element that needs to be proved in the case. The term prima facie evidence is used in both civil and Criminal Law.)

Badala ya kutaka kuanza kumnyoshea kidole Membe tu-review utendaji na uwez0 wa mapolisi wetu ambao wamejiunga na Polisi baada ya kuzaliwa Police Lines kwenye majumba ya mapolisi. Asilimia 70% wa askari Polisi ni watoto wa mapolisi wenyewe, wanaingia Polisi kuendeleza ukilaza wa baba zao.

Ukiuliza hapa utaletewa data watoto wa makamishna wa Polisi waliopo chuo cha Polisi - Moshi hivi sasa.
 
Nilipomsikia Membe anasema anakwenda Arusha ninakujau lile NENO LIMETIMIAMchezo utachezwa hadi muendesha bodaboda aliyewapakia walipuaji Victoar Ambrose atafungwa!
Kama yule mwalimu aliyekuwa akiwapeleka watoto kwa Babu Seya alivyoachiwa huru.
 
Basi upelelezi umeishakamilika na hivyo tutegemee waliobaki kufikishwa mahakamani bila kupoteza muda.
 
Ni kigezo gani kilitumika kwa askari wa Tanzania kuwashuku wale wasaudia kuwa wamehusika? Je, ni mavazi yao, Taifa lao, dini yao, muda wa kuingia na kutoka nchini, majina yao au muonekano wao?

Je ilivyofanyika ndivyo intelijensia inavyotakiwa kufanya kazi?
 
Mimi hata sielewi tofauti ya bomu kuwa la kgaidi na la kidini nisaidieni jamani? kwani wa suni na washia kule Iraq si ugaidi na udini humo humo??? Hata sielewi kabisa jamani nisaidieni.
Mchana mwema, nikujuze kwa muhtasar vujo la IRAQ ni POWER OF DOMINATION ya nguvu la kutawala kwa kujitukuza kimadhehebu yaani kama vile huko IRELAND yaani dhehebu walowengi hawakubali kutawaliwa na walowachache.
Kweli hayo ya udini ndiyo yalowafikisha huko.!! mungu aepushe mbali balaa.

Kila la heri
 
kuna habari nilisoma sijui kama ilifika humu jamvini inasomeka kwamba balozi wa saudi nchini agoma kurudi Dar aamua kuweka kambi arusha mpaka ahakikishe watu wake wanaachiwa-naona yametimia
 
Na sasa wamerudi kwa style nyingine ya kutubebesha nazi kwa kupitia vichwa vibovu vya viongozi wetu
Respected kabila; Pole pole usiharibu siku yako mwezi jana kwenye tokeo la Boston Marathon bomu, Tangazo la kwanza kabisa wamerekaniUS na taaluma zote za kiintelijensia baada ya mripuko tu walitangaza eti Msaudi ndo mhusika na ni kijana mwanafunzi tumemkaribia kumweka nguvuni !! (hapo boston peke kuna wanafunzi zaidi ya elfu5 wa kisaudia) Looh,
Wakuu hao baada ya kupeleleza waka geuza kibao na kuomba radhi na kutoa taarifa ingine kuwa walotenda ni wa CHECHENIA/warussi. sasa mambo kama haya yanatokea kukamata mtu katika " WRONG PLACE and WRONG TIME"...
Lakini tusubiri reporti ya FBI hao mababa riwaya yao ni nini?
Tulindane tupone.
 
Si jambo la ajabu kuona hili likitokea kwetu,kule India kuna wanajeshi waliua raia,wakakamatwa na wakati wa uchaguzi Serikali ya Italy ikaomba warudishwe Italy kwa muda na baadae watarudi,wakaruhusiwa ila baada ya muda kupita Serikali ya India ikataka watuhumiwa wake na ikasema inamshikilia balozi mpaka hao watuhumiwa waje na walirudishwa,sisi hatuwezi mambo hayo kwa kuwakila kitu tunategemea kutoka kwao baada ya Serikali yetu kushindwa kujitegemea.
 
That means walikamata randomly! Kama walikuwa wanatafuta research sample vile! Maana nilifikiri wamewakamata maana they have a reason to believe wamehusika! Kama hawakusika kabisa, then why arrest them? Na kama wamehusika kwanini wameachiwa?
Mh.Iron Jioni njema hutokea kukamata randomly; Mwezi jana kwenye tokeo la Boston Marathon bomu, Tangazo la kwanza kabisa wamerekaniUS na taaluma zote za kiintelijensia baada ya mripuko tu walitangaza eti Msaudi ndo mhusika na ni kijana mwanafunzi tumemkaribia kumweka nguvuni !! (hapo boston peke kuna wanafunzi zaidi ya elfu5 wa kisaudia) Looh,
Wakuu hao baadaye kupeleleza waka geuza kibao na kuomba radhi na kutoa taarifa ingine kuwa walotenda ni wa CHECHENIA/warussi. eti wanafanana, Sasa mambo kama haya yanatokea kukamata mtu katika " WRONG PLACE and WRONG TIME"...
Lakini tusubiri reporti ya FBI hao mababa riwaya yao ni nini? Hakuna siri itakayo fichwa milele!!
good luck.
 
Back
Top Bottom