Sishangazwi hata kidogo na jambo hili. Tumezidi kujikomba umangani mpaka inatia aibu. Naona mkuu wa kaya baada ya kuona kimeanza kunuka Ulaya na Marekani wameshaanza kumstukia, sasa kageuza uso anatembeza bakuli nchi za kiarabu. Ndiyo sababu kila kukicha yuko huko na anadiriki 'kuwabembeleza' waje kuwekeza Tanzania kiasi cha kuwapa 'uhuru' wa kuitumia nchi yetu na rasilmali zake kwa namna wanayotaka wao. Hata wamasai sio kitu mbele ya maswahiba wake wa kiarabu; wanahamishwa kutoka kwenye ardhi yao ili wapewe waarabu, ndege zinabeba wanyama wetu kupeleka huko Arabuni mchana kweupe. Sembuse leo wakija kutulipua ataweza kufurukuta?
Tuamke nchi imeshauzwa. Waswahili husema ukiona manyoya jua kashaliwa... Kazi ni kwetu sisi wenye uchungu na nchi yetu kufanya mabadiliko kabla hatujageuzwa wote kuwa watumwa nchini mwetu.
Inawezekana, timiza wajibu wako - Mwalimu Nyerere.