Bomba la Mafuta: Kenya wamkomalia Museveni

Bomba la Mafuta: Kenya wamkomalia Museveni

Apunguziwe gharama kwa expense ya nani? Mlipa kodi wa Tanzania? NO,NO,NO,NO.Kama anaona biashara yake haitalipa aende kwingine

Mkuu hapana returns ya bomba.ni kubwa na sisi hatutakuwa tunaagiza mafuta arabuni pia fidia wanatoa kampuni inayojenga bomba sio serikali ya tz
 
Mkuu hapana returns ya bomba.ni kubwa na sisi hatutakuwa tunaagiza mafuta arabuni pia fidia wanatoa kampuni inayojenga bomba sio serikali ya tz
😛😛😛😛😛😛😛 ! Kaka yangu unampigia mbuzi gitaa! He is not at that level.
 
This is marvelous project which Tanzania need to acquire, hapa ndo tutajua picha halisi ya EAC, kiuhalisia Ugada-Tanga route ni option nzuri zaidi, kama uganda wanataka wauze wese lao 2018 basi Uganda -Tanga is the only option kwani bandari tayari ipo, na ni safe zaidi ukilinganishwa na hiyo bandari ya Lamu ambayo kwanza haijaanza kujengwa na ipo karibu sana na somalia ambayo ni risks kubwa kutoka kwa alishabaab. Lakini tuko kwenye dunia ya ushindani, na kenya wako serious na hii project kwa njia yeyote ile, kwa hiyo huu ni wakati muafaka wa Mh magufuri na muhongo kutumia ushawaishi wao kwa mseveni ili tuweze kupata hii project, wasije wakaa wakijidanga kuwa bandari ya tanga au route ta uganda to tz ni safe, mara ohh vita vya kagera , maa ohh tumesign MOU then tukae kimya bila kufuatilia tukisubiri mseveni atatoa cake hii direct kwa tz tutakuwa tunajidanganya. Ni lazima sasa kuanzia sasa tuanze kufuatilia the whole process ya mradi huu kabla ya mseven na uhuru hawjakutana tena uganda, tutume Muhongo aende UG akiwa na proposal nzuri ya route yetu akajaribu kumuweka sawa Mseven, ili asibadili mawazo, pia kama tukitaka kumpata mseveni tuangalie jinsi ya kumpa some kicksback, au tuangalie jinsi ya kufanya biashara na mseven, hata kwa kusema tanzania imetenga bandari ya tanga kuwa bandari maalumu ya wafanyabishara wa uganda, hata mizigo yote ya UG tunaangalia jinsi ya kuwapunguzia ushuru. At the same time, we have good relationship with China, tunaweza tukamtumia balozi wa china atusaidie kuwaconvice CNOOC just to stick with Tanzania-uganda route wanapofanya final evaluation, am sure tukiwa na backup ya CNOOC na Total itakuwa easy kuwatoa Tullow na kenya easily. Tusikubali just to give up so easily , i'm sure CNOOC wakipigwa mkwara na wanavyoheshimu mamlaka yao ya china na uhusiano wa Tz basi hii issue itakuwa easy sana, Kazi kwenu Magufuli na Muhongo.

Makuu una wazo zuri lakini don't think.unaweza.ku manipulate china which is a world power now pia china imewekeza kenya kuliko ilivowekeza Tanzania recently
 
😛😛😛😛😛😛😛 ! Kaka yangu unampigia mbuzi gitaa! He is not at that level.

Hahhahhahaajhaajaj akili.za vijana wa lumumba tutazidi.kuwaelimisha
Elimu
Elimu
Elimu
Tusikate tamaa mkuu
 
Kenya wajue washapigwa bao nafahamu Museveni bado hajamalizia fidia ya vita vya kagera hapo ndio pa sisi kumbana total wameshasema wao wana pesa ya kujenga mradi wote Kenya wamecheza pata potea Museveni anahisi atakuwa salama zaidi akishirikiana na Tanzania kuliko Kenya angalia mgogoro wa kisiwa wanachogombea
Museveni hatakubali lipite Kenya! Usalama wa Kenya ni Mdogo! Hujuma ya Alshabab kwa Kenya inafanya Tanzania kuwa salama zaidi!
Magufuli anaaminika zaidi kuliko Kenyata! Hiyo ni factor nyingine!
 
Hahhahhahaajhaajaj akili.za vijana wa lumumba tutazidi.kuwaelimisha
Elimu
Elimu
Elimu
Tusikate tamaa mkuu
Mkuu mie siko huko kwenye utani wa jadi! It is not real about generalization ya vijana wa Lumumba but him as a person na jibu lako zuri lenye elimu!
 
Mwambani Economic Corridor ni mega project ya Tanga-Matadi Railway yenye 8,500km. (Indian-Atlantic oceans ). Bomba la Uganda ni sehemu ya hii mega project
 
Tanzania bado tuna advantage maana tayaari tuna uzoefu wa ujenzi wa bomba la mafuta TAZAMA tuna uzoefu wa uendeshaji wa bomba kama hilo kwa miaka mingi lakini pia bomba hilo likipita Tanzania kuna uwezekano wa kuliunganisha na nchi zote kusini mwa Africa pale itakapobidi. Itakuwa karibu kuunganisha Rwanda Burundi Zambia na other land locked countries.

Hivyo kwa vyovyote tupo kwenye advantage zaidi ya Kenya
 
Tembea ndani ya hoja, acha unafki wa CDM-huu ni muda wa maendeleo na c muda wa siasa za kipumbavu pumbavu, mnatuboa cc ambao hatuna vyama.
kwan hoja ni CDM?! nakuuliza we mbumbumbu
 
Kikao cha jana kampuni ya Total ilieleza sababu za kuhamishia mradi Tanzania ikiwemo, Tanzania gharama za fidia ziko chini ukilinganisha na kenya, pili wakijenga kenya itabidi pia wajenge bandari katika eneo la lamu tofauti na Tanzania ambapo bandari ipo tayari. Mradi kwa Tanzania utaenda kasi ili ukamilike kabla ya 2018 ambapo uganda itaanza kusafirisha mafuta yake.

Kenya wamejibu na kusema kuhusu fidia kenya itashughulikia kwahiyo hiyo sio sababu na ujenzi wa bandari wamesema Tayari kuna ujenzi wa bomba la kutoka sudan ya kusini kwenda lamu hivyo hilo sio tatizo kwani haitakuwa sehemu ya huo mradi. Kuhusu uharaka wa mradi wamesema wanao mradi wa ujenzi wa reli mpya unaoenda kwa kasi hivyo nahuo utakuwa na kasi ileile.

Sasa sie tumejipangaje kupangua hoja za kenya ili mradi uendelee kuwa Tanzania?
mu7 asije kutuchezea shari maana hua ana kigeugeu. yabidi tuwe makini na hawa wakenya maana wakiona nyama wao ni sawa na fisi. vizuri pia magufuli alimkumbusha mu7 in public kuonyesha fadhila kwa kuwasaidia wao kumng'oa nduli amin. tusiwe watu wa kutenda wema na kuondoka hii ni enzi tofauti..enzi ya unyang'au. watu hawana kumbukumbu ya mema.
 
sisi tuko busy kupora madaraka, juz tumepora zanzibar leo bahati mbaya jiji la dar limetuponyoka
Mkuu halijawaponyoka bali wameamua kulitoa tu na kujaribu kidogo kubalance ile sensa ya wana CCM wa visiwani, kwani hila zoote zili ratibiwa na kutekelezwa mchana kweupe peee!. Baadhi ya halmashauri zimeporwa kwa hila kama hizi na hakuna aliye piga kelele.
 
Mkuu vipi swala la umbali halihusiki hapo kweli? Mahana naona kutoka kibale hadi kagera kuna kuna wilaya moja tu ya mbarara hapo kati kati, wakati ukielekea Kenya kuna wilaya takribani tano!
UGANDA WAMEONA VITU HIVI TANZANIA;

1. UNAFUU, Uganda wanaona Tanga tayari kuna bandari, kwa hiyo hakuna gharama za ujenzi wa bandari.

2. MUDA, kitendo cha Tanga kuwa na bandari tayari imeshapunguza muda wa umalizikaji wa mradi, makadirio mradi utaanza biashara mpaka 2018. Uganda wanaona Kenya hakuna bandari kwa hiyo mradi utachukua muda mrefu kumalizika.

3. UZOEFU WA BANDARI, bandari ya Tanga ni kongwe kwa wateja tayari wameshaizoea, hata maofisa wa bandari ya Tanga wanauzoefu wa kutosha. Lamu, Kenya hakuna bandari watakapojenga itachukua muda mrefu wateja kuizoea.

4. USALAMA, hapo utakubaliana nami kwamba hali ya usalama Kenya ni shwari, lakini mashambulizi ya kujitoa mhanga/kushtukiza yanayoendelea Kenya zidi ya Al-Shabaab yanaitia wasi wasi Uganda. Ikumbukwe mradi unagharimu pesa nyingi sana.

5. UHUSIANO MZURI WA KIDIPLOMASIA UGANDA-TANZANIA(vita ya Kagera), hapa pia utakubaliana nami MUSEVENI analipa fadhira kwa Tanzania.

NYONGEZA;
Serikali ya sasa ya Tanzania ipo makini chini ya uongozi wake MAGUFULI. Hapo suala la ufisadi halina nafasi katika mradi huu.
 
Kikao cha jana kampuni ya Total ilieleza sababu za kuhamishia mradi Tanzania ikiwemo, Tanzania gharama za fidia ziko chini ukilinganisha na kenya, pili wakijenga kenya itabidi pia wajenge bandari katika eneo la lamu tofauti na Tanzania ambapo bandari ipo tayari. Mradi kwa Tanzania utaenda kasi ili ukamilike kabla ya 2018 ambapo uganda itaanza kusafirisha mafuta yake.

Kenya wamejibu na kusema kuhusu fidia kenya itashughulikia kwahiyo hiyo sio sababu na ujenzi wa bandari wamesema Tayari kuna ujenzi wa bomba la kutoka sudan ya kusini kwenda lamu hivyo hilo sio tatizo kwani haitakuwa sehemu ya huo mradi. Kuhusu uharaka wa mradi wamesema wanao mradi wa ujenzi wa reli mpya unaoenda kwa kasi hivyo nahuo utakuwa na kasi ileile.

Sasa sie tumejipangaje kupangua hoja za kenya ili mradi uendelee kuwa Tanzania?

Total ambao wanagharimia mradi mzima mbona wamejieleza vizuri tu, upande wa Kenya kuna unpredictable risks chungu mzima na linapokuja suala la kulipa fidia kwa wenye aridhi uwezi kujua litaisha ishaje hapa watadai hilo ni suala dogo sana, lakini wakumbuke masuala ya aridhi nchini Kenya yana matatizo yake ambayo si madogo , vile vile suala la usalama kuna hatari za bomba kuvamiwa na mashfta na Al Shabaab huwezi kuli sweep ukweli huo under the carpet kwa kujifanya halipo.

Total na M7 wakumbuke kwamba majeshi ya Uganda na Kenya yapo Somalia hivyo mradi huo uta attract attention ya Al Shabaab in no time.

Halafu hili suala la kusema watajenga Bandari fasta hizo ni ndoto za mchana, hapa wanazuga eti wana uwezo wa kujenga Bandari kwa kasi wanayotumia kujenga reli, hapo hawasemi kwamba reli kwa kiasi kikubwa inagharimiwa na Serikali ya Uchina na wajenzi ni Wachina in case Wachina wanasusia jamaa watakwama tu, cha muhimu hapa Total na M7 wawe makini na ahaadi ambazo ni too good 2 be true which is TRUE.
 
Mkuu vipi swala la umbali halihusiki hapo kweli? Mahana naona kutoka kibale hadi kagera kuna kuna wilaya moja tu ya mbarara hapo kati kati, wakati ukielekea Kenya kuna wilaya takribani tano!

Cha muhimu hapa M7 anapaswa awe na msimamo imara, hasiwe a flip flopper - mi nafikiri jamaa wanamfuata fuata baada ya kuhisi kwamba M7 is too whobbly kama hiyo ina ukweli ndani yake au la - remains 2 be seen.
 
Usikute Waganda wanatutumia kama njia ya ku-negotiate na Kenya.

Nikweli kabisa lakini pia sisi tuna gesi ya kutosha ambayo waganda wanaihitaji sana kwa maendeleo yao kwa haraka. Akibana yeye na sisi tunabana. Hicho ndio kinachomchanganya mganda.
 
Cha muhimu hapa M7 anapaswa awe na msimamo imara, hasiwe a flip flopper - mi nafikiri jamaa wanamfuata fuata baada ya kuhisi kwamba M7 is too whobbly kama hiyo ina ukweli ndani yake au la - remains 2 be seen.

Narudia tena huu mkataba umefanyika kwa makubaliano kwamba sisi tunawapelekea gesi wao wanatuletea mafuta ukiangalia kimsingi wakenya wanarukaruka tu.
 
Mwambani Economic Corridor ni mega project ya Tanga-Matadi Railway yenye 8,500km. (Indian-Atlantic oceans ). Bomba la Uganda ni sehemu ya hii mega project

Ni kweli mkuu, lakini ni Watanzania wangapi wanajua ukweli huo, si ajabu hata baadhi ya Viongozi wetu hawajawahi kulisikia hilo, mimi nilijua mradi huo kutokana na shughuli zangu!
 
Back
Top Bottom