Suala lote lipo mikononi mwa Museveni. Nadhani Uganda ndiyo wenye uamuzi wa mwisho. Kama mkwere angekuwa makini siku za nyuma, wala tusingefika hapa kuanza kugombania mradi huo na wakenya. Toka mwanzo, waganda waliona unafuu wa bandari ya Tanga lakini Tanzania ilikuwa haisomeki.
Magufuli kaonyesha msimamo thabiti na Museveni ameshawishika japo kulikuwa na mazungumzo ya awali na Kenya baada ya kuona Tanzania inavuta miguu chini ya JK.
Naamini Uganda wapo wana haraka ya kuanza kuuza mafuta yao na mradi wa Tanga ndiyo inaweza kuhakikisha hilo.