Bomani Committee hiding the truth?

Yote mnayoshauri yafanyike, yangewezekana kama taifa lingekuwa na viongozi-watumishi; na sio viongozi-watawala. Na wadanganyika tumekubali kutawaliwa, badala ya kutumikiwa.

Suala la mgawanyo wa mapato tuliliongelea sana huko nyuma; na kutoa mapendekezo kadhaa. Botswana-model ingetufaa; na hasa taifa(state, not government) lingekuwa majority shareholder kwenye kila kampuni yenye maslahi makubwa kwa ustawi wa taifa hili.
 

Koba,
Usiwadanganye wabongo. Chini ya serikali ya awamu ya tatu emphasis ilikuwa ni wawekezaji. Sheria nyingi zimewekwa na akina Mkapa, Mwinyi, kuwafavour foreigners kukiwa na ile sheria ya kuondoa haki ya serikali kutaifisha biashara yeyote ambayo imekiuka taratibu. Hakuna mzawa yeyote aliyepewa tax holiday hizo wamepewa wageni tu pamoja na wamiliki wa mihoteli ambayo inatengeneza faida tangu siku ya kwanza. Tungeweza kuimarisha STAMICO lakini hakukuwepo nia chini ya akina Mwinyi na Mkapa.
 

... sasa mbaya zaidi ni kwamba aliyekuwa Kamishna wa Madini wakati wa Mkapa ndiye DG wa STAMICO .... yaani mafisadi everywhere!
 

...wrong again,tax holiday haiangalii foreigner au mzawa wote ni sawa tuu as long as una fall katika hiyo category ya investment,na pia kama kweli tunataka kuendeleza na kupata full advantage ya madini yetu sio kuimarisha STAMICO chombo kilichojaa wanasiasa kuliko wataalam,jifunze mfano wa TBL unaweza kupata idea!
 
...wrong again,tax holiday haiangalii foreigner au mzawa wote ni sawa tuu as long as una fall katika hiyo category ya investment...

Sheria ya Tax holiday inasemaje?

Mbona hakuna anae weza kui explicate?

Si wabunge, si waandishi wa magazeti uchwara wa Bongo, si nani.

Tandika hapa hiyo sheria tuione.
 
Sheria ya Tax holiday inasemaje?

Mbona hakuna anae weza kui explicate?

Si wabunge, si waandishi wa magazeti uchwara wa Bongo, si nani.

Tandika hapa hiyo sheria tuione.

Mara ya ngapi unaiulizia hiyo sheria ya tax holiday? inaweza ikawa haipo?
 
Waheshimiwa wabunge wetu wa nchi yetu nzuri iliyobarikiwa mnapojadili maswala ya rasilimali yetu ya madini tuliyopewa na Mungu angalieni wenzetu wa Zambia walichofanya....Wanaye kina Sinclair (A.Hickman)lakini wanaangalia masilahi ya nchi yao kwanza.

 
Sheria ya Tax holiday inasemaje?

Mbona hakuna anae weza kui explicate?

Si wabunge, si waandishi wa magazeti uchwara wa Bongo, si nani.

Tandika hapa hiyo sheria tuione.



9.1 Tanzania Investment Act (TIA), 1997

In 1997 the NIPPA of 1990 was repealed and replaced by the new Tanzania Investment Act (TIA), which transferred all the tax incentives to the Income Tax, Customs and Excise and Value Added Tax statutes. The main reason for this transfer was to make the tax structure more transparent and less complicated to taxpayers. Since then Income tax holidays were abolished and the tax incentives are now granted to all investors whether local or foreigner in the form of enhanced capital deductions and allowance.

....na kama unataka details ingia hapa www.tra.go.tz then check section ya Tax incentives kuna mengi yanayoweza kukusaidia kama uko serious na business Tanzania
 
Rais hajatoa ripoti yake hadharani au yeye kusema amepokea mapendekezo hayo, hii Kamati ya Madini kwanini imetoa mapendekezo hayo kabla aliyewaagiza kusema ameyapokeea au kuyaweka hadharani? JK akija na kusema kuwa ripoti aliyoipokea haina mapendekezo hayo au yamewekwa tofauti na yeye kayaelewa vingine, si kina Bomani wataonekana wamejitega? Haya mambo ya kuscore political points yana mambo yake.
 
Ripoti ya Bomani yawaficha wabunge

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

BUNGE limeanza kujipanga kwa ajili ya kuijadili kwa kina ripoti ya madini iliyoandaliwa na Kamati ya Rais iliyoongozwa na Jaji Mark Bomani, ambayo serikali imeahidi kuyatekeleza mapendekezo yake ya msingi.

Katika hatua moja, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo (CCM) imeanza kufanya kikao cha siri kwa ajili ya kujipanga kuijadili ripoti hiyo ambayo imetoa mapendekezo mengi yanayolenga kuibadili kabisa sekta ya madini kutoka kuwa rasilimali ya kuyanufaisha makampuni ya wawekezaji na kuwa msingi wa maendeleo ya kitaifa.

Mbali ya Shellukindo, wabunge wengine wanaounda kamati hiyo ya nishati na madini ni, Dk. Harrison Mwakyembe, Daniel Nsanzugwanko, Esther Nyawazwa, Victor Mwambalaswa na Kilontsi Mporogomyi.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya Bunge zinaeleza kwamba, tayari wabunge wanaounda kamati hiyo wameshaanza kuijadili ripoti hiyo ya Bomani kwa lengo la kujiweka sawa.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya kamati hiyo vimesema kuwa kamati hiyo imewaomba baadhi ya wajumbe waliokuwa kwenye Kamati ya Rais ya Madini ili kuiwezesha iweze kuwasilisha ripoti hiyo bungeni kwa ufasaha.

Wajumbe walioalikwa kwenye kamati hiyo kutoka kwenye Kamati ya Rais ya Madini ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP).

Mmoja wa wabunge wanaounda kamati hiyo aliyezungumza na Tanzania Daima alisema; wameamua kukutana Morogoro ili kujiweka sawa na kuwa na msimamo mmoja madhubiti, hasa baada ya kuwapo kwa dalili za baadhi ya watu kutoka ndani na nje ya Bunge kuonyesha nia ya kutaka kulikwamisha Bunge na hatimaye serikali katika kuifanyia mabadiliko makubwa ya kisera na kisheria, sekta ya madini.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Shellukindo kwa njia ya simu jana ili kupata undani wa kile wanachokijadili wakati wakiwa Morogoro, mbali ya kukiri kwamba walikuwa wanakutana huko kwa shughuli maalumu ya siri kwa siku mbili, ambayo hata hivyo hakuwa tayari kuitaja.

“Tupo hapa, kuna mambo fulani fulani tunayapigia vita. Unajua na tutakuwa hapa leo na kesho,” alisema Shellukindo pasipo kutaka kuingia kwa undani kuzungumzia suala hilo.

Alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa taarifa za wao kukutana kwa ajili ya kuipitia ripoti ya Kamati ya Madini ya Rais kwa ajili ya kuijadili katika kikao hiki cha Bunge kama ilivyoahidiwa, Shellukindo, mmoja wa wanasiasa wakongwe alikataa kueleza lolote.

Hatua ya Bunge kuituma kamati yake Morogoro inakwenda sambamba na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wakati akisoma hotuba yake ya makadirio na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2008/09.

Ngeleja pamoja na kuiwasilisha mezani ripoti ya kamati ya Bomani sambamba na hotuba yake, alisema serikali ilikuwa imejipanga kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika sekta hiyo kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati hiyo ya rais.

‘‘Mheshimiwa Spika, itakumbukwa mwezi Novemba, 2007 Mheshimiwa Rais aliunda Kamati ya Kuishauri Serikali Kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini. Kamati hiyo ilimaliza kazi na kuwasilisha taarifa yake kwa Mheshimiwa Rais mwezi Mei, 2008.

‘‘Serikali imepokea na kuchambua mapendekezo ya kamati hiyo na inaandaa mpango mkakati wa kurekebisha Sera ya Madini, Sheria ya Madini na sheria nyingine zinazohusu sekta ya madini ili kuyatekeleza mapendekezo hayo. Matarajio ya wizara ni kuwa ifikapo mwezi Aprili, 2009 Sera ya Madini ya mwaka 1997 na Sheria ya Madini ya mwaka 1998 vitakuwa vimerekebishwa,” alisema Ngeleja katika hotuba yake hiyo.

Uamuzi wa rais kuunda kamati ya madini ulikuja baada ya kuwapo kwa malalamiko mengi kuhusu mwenendo wa sekta hiyo ya madini hasa baada ya kuonekana ikiwanufaisha wawekezaji wa kigeni kuliko Watanzania wenyewe.

Awali kamati hiyo ya rais, ilipewa miezi mitatu kukamilisha kazi yake kabla ya kuongezewa muda hadi kufikia miezi sita na ikakamilisha ripoti yake na ikaiwasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete Mei mwaka huu.

Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ya madini ni pamoja na Bomani, ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti, Zitto, Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe, Ezekiel Maige, Mary Kejo, Peter Machunde na David Tarimo.

Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo ilifanya kazi ya kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.

Pia ilikuwa na jukumu la kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutakiwa kutoa taarifa yenye mapendekezo, kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zitakazohusu migodi mikubwa nchini.
 
Wazalendo,
In as much the Canadians through their Envoy tried to lobby our MPs not to support reforms in the mining industry, who are the real players in the mining industry and the whole review process. Why hasn't the Bomani Report been made public? or has it? Ngereja was given two weeks to read the report by JK, what happened after that?

Issue ya pili--Hivi hatuoni ufisadi unaoendelea katika ma benki yetu huku wakurugenzi wakijineemesha na hela za watu? naomba tusilale kuna EPA ndogondogo kwenye ma benki na taasisi nyingine
 
Ilishwasilishwa Bungeni, na kitu kikwiasilishwa bungeni kinakuwa public, so itafute tu utaipata
 
Tontoh, the Bomani Report has already been made public. The President has endorsed it and handed it over to the National Assembly to do the needful. Kikwete deserves some praise for that. He has endorsed all the Bomani Team recommendations. It is now parliament's duty to give it legislative effect. Tayari baadhi ya magazeti yameanza kui"serialise"! Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ilikutana wiki iliyopita pamoja na very serious MPs (Cheyo, Zitto, Mwakyembe, Shellukindo, Manyanya, Mporogomyi) kuipitia Ripoti ya Bomani na ku"draft" recommendations za kupeleka Bungeni.
Kuhusu issue ya pili ya "viEPA" vidogovidogo, inabidi uje na hard facts ili tuzifanyiekazi, otherwise you have not assisted us much! Lazaros
 
tontoh,

....tuletee facts za hivyo tu-EPA vidogo vidogo na.............karibu sana anyway........
 
Tontoh, the Bomani Report has already been made public. The President has endorsed it and handed it over to the National Assembly to do the needful. Lazaros

Where is it that I can read it unedited? Can you post the whole report here at JF?
 
Attached is a summary of the Bomani Report. Anayetaka ripoti nzima (main report bila viambatanisho/annexes) apige simu (022) 2772611. Watakuelekeza wapi inapatikana hapa DSM.

Ripoti hii inachambuliwa hivi sasa, na uchambuzi huu utapatikana ktk tovuti ifuatayo www.policyforum.or.tz baada ya wiki moja.
 

Attachments

  • Kamati ya Madini (Bomani Report).pdf
    190.2 KB · Views: 183

Mugizi thanks,

I didn't know the report is already public.......ndo utamu wa JF huu
 


Mwanzo mzuri NPF. Ni vyema mkaitisha mjadala wa wananchi wa kuichambua ripoti husika kabla ya bunge kujadili hivi karibuni. Panahitajika mjadala wa umma mwisho wa wiki hii na mwanzoni mwa wiki ijayo ili taarifa itakapojadiliwa bungeni wabunge wapate hisia na hoja za wananchi kuhusu taarifa hiyo. Ni wakati pia wa kuwabana wabunge mmoja mmoja. Nyakati kama hizi ndipo nafasi ya AZAKI inapoonekana bayana. NPF waunganishe nguvu na LEAT, Haki Ardhi, TAMWA, Femact nk. Organized lobbying and advocacy kwenye suala hili ni kitu cha lazima. Mzinge na mzengee mpaka kieleweke!

JJ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…