Bomani Committee hiding the truth?

Walikuwa na Meremeta, si umeona wameifanyia nini...

ule si walisema wajeshi na hatiaye wakauuza kifisadi. Huu ni wakati wa kuanza mambo upya jamani, tutaendelea kunyonywa na hawa wazungu hadi lini? hao wazungu ndio wanafanya ufisadi wa hali ya juu zaidi ni vile tu hatujui wanatudanganya kitaalam.

Hakuna jinsi tukamiliki migodi yetu, tukazalisha, kusafisha na kuuza wenyewe?
 
Hatimaye ripoti ya Bomani imetoka na hizi ni higjhlights kutokana na Gazeti la The Guardian:-

1. Govt should have shares in every mining company
2. Formation of minerals authority to surpervise all mining activities
3. Mining loyalty to be calculated on gross value andnot net value as
is the case at the moment
4. Increase gold royalt from 3% to 5%
5. Thorough investigations on Meremeta and Tangold
6. What was the legality of the BoT paying $ 132 million to the South Africa
NedBank?

Watanzania, hivi ni nani aliyeturoga?

Tujiulize yafuatayo:-
1. Yaani ardhi na madini ni yetu na mashimo (hasara) itabaki kwetu baada ya madini kuisha;kwa nini Serikali haina share kwa niaba ya Watanzania? Au ndo wale Wanasiasa kupewa Ukurugenzi kibinafsi kwa niaba ya nchi (Kumbuka Kinana na Artumas)
2. Yaani Rais Mkapa alikuwa anafanya nini jamani? Alikuwa pale Ikulu kwa MAslahi ya nani?
3. Kwani tusingewakaribisha wawekezaji wa madini tungepata hasara gani, maana hata sasa hakuna faida yoyote tuliyokwisha ipata kama nchi ila hasara tupu!

MAONI YANGU:-
Wale wote waliokuwa Mawaziri wa Awamu ya 3 na bado wamepewa Uwaziri au Ubunge sasa (Isipokuwa JK maana tunamwachia kazi maalumu ya kurekebisha hujuma hii), Wajiuzulu kwa kukubali ujinga na upuuzi huu kufanyika nchini mwetu

Hii ripoti unasema imetoka...Imetokea wapi?
Mbona siisiki ikijadiliwa BUNGENI?
Ama imetokea Bungeni hadi Gazetini?
Naomba uwe specific pls.
Mapendekezo hayo ni mazuri lakini ni kwanini haijadiliwi bungeni?
Ama jina la SINCLAIR bado MZIMU?
 
Nilifuatilia Bunge jana, Spika alisema bado hajaipitia/isoma hiyo ripoti lakini Bunge limekubaliana kutenga siku maalumu ya kuijadili hiyo ripoti ingawa haikutajwa ni siku gani.

Hiyo habari niliyoileta hapa nimeitoa katika gazeti la The Guardian la leo tarehe 10 July. Hata wao wemechapisha kwa njia hiyo hiyo ya hints, sijui wameipata wapi.
 
..hizi Tume za Raisi ni ufujaji wa pesa na ufisadi wa aina nyingine.

..yaani muda wote huo wametumia na kuja na royalty ya 5%!??

..wananchi tuelezwe hii Tume imetumia fedha kiasi gani kuja na mapendekezo yake UCHWARA.
 
Ibrah,
Kabla ya kufariki Mwalimu alikuwa amependekeza Tanzania tuwe major share holders katika miradi yote mikubwa mikubwa kama hii ya madini. Haiingii akilini kabisa mgeni kupewa asilimia 90% ya mradi ambao ni wa manufaa kwa taifa zima. Lakini viongozi waliomfuata kuanzia Mwinyi wakawa viziwi. Sasa naona wanaanza kumpiga vijembe kuwa ujamaa ulikuwa ni ndoto.
 
Hii ripoti unasema imetoka...Imetokea wapi?
Mbona siisiki ikijadiliwa BUNGENI?
Ama imetokea Bungeni hadi Gazetini?
Naomba uwe specific pls.
Mapendekezo hayo ni mazuri lakini ni kwanini haijadiliwi bungeni?
Ama jina la SINCLAIR bado MZIMU?
ningekuwa miye ibra nisingejibu hata moja, lakini since miye siyo ibra, i think jmushi umezidi kuamrisha watu utafikiri unawalipa...lol!
 
Kinachosumbua hapa ni ufisadi na sio uendesha wa migodi, napenda kuwakumbusha yafuatayo:
1. Williamson Diamond Mine Govt ilikuwa na 50% tangu mwanzo lakini imeshuka hadi 20% kwa sasa hivi.
2.Buckreef project ambayo ilikuwa Buckreef Gold Mine Govt ina 25%
3. Bulyanhulu project ambayo sasa hivi ni Kahama Gold Mine under Burrick ILIKUWA CHINI YA STAMICO kwa 50% kama wangeingia ubia na mwekezaji yeyote.

Naweza kutaja mifano mingi sana ila hiyo michache inatosha kwa leo. Kitu cha kujiuliza ni kwanini Bulyanhulu prospect alipewa mwekezaji? (Placer Dome) na nani alikuwa waziri na kamishina wa madini? Hawa ndio wabaya wetu ambao wanasababisha uundaji wa kamati wakati wao ndio walitoa hayo maeneo kwa hao wanaotuibia.
Mkataba wa Buckreef umesainiwa na JK!!! anayebisha anitafute nitampa copy.
Kushukuka kwa % katika Mwadui imesababishwa na wanasiasa na si vingenevyo, ni juu yetu watanzania kuangaria haya mbambo critically na si kulusha mbwembwe hapa, tunaumizana wenyewe.
 
Chibingwa,

..inaelekea haya masuala ya madini na nishati una habari naye kidogo.

..hivi unaweza kutuambia tofauti ya mapendekezo ya Tume ya Jaji Bomani, na yale ya Tume ya Kipokola.

..nina wasiwasi hizi Tume zinafanya kazi kwa kujirudia-rudia. nilisoma mapendekezo ya kamati ya Lawrence Masha, nikakuta reference kibao za kazi ya Tume ya Kipokola.
 
Tonachopaswa kutambua ni hivi vifuatavyo kwani ndio adui wa maendeleo yetu na upotevu wa madini yetu:
1. Government reforms that were iniated in the early 1990s - Trade liberalization - change of the State monopoly (STAMICO) to private ownership.
2. Enabling environment through - Mineral policy 1997; Mining Act 1998; Mining Regulations 1999.

Hayo mambo niliyoyataja hapo juu ndio chimbuko la huu uozo ote tunaouona, nashauli wabunge wetu wenye uchungu na hii nchi wapie hiyo mineral policy na mining Act 1998, ili waweze kujenga hoja nzito wakati wa kujadili ripoti ya Bomani.
Mtu ambaye sijasikia akitajwa ni kamishina wa madini wa wakati huo (Mwakalukwa?) kwani ndie mshauli mkuu wa waziri Technically, yeye na wenzake nchi iliwapeleka Ghana, Botswana, Mari, South Africa kwa madhumni ya kujifunza na kuishauli serikali jinsi gani wenzetu walifanyaje kabla ya kukaribisha hawa wezi kuja kuwekeza hapa kwetu, sasa walichojifunza ndicho hicho na prospect lisence zote Mwakalukwa kasini???
WAHESHIMIWA WABUNGE NAWAPENI MAPENDEKEZO YAFUATAYO SIJUWI KAMA YAPO KWENYE MAPENDEKEZO YA MHESHIMIWA BOMANI:
1. Prospecting license yeyote ile after 50% religuish (baada ya kupunguza nusu ya eneo la utafiti), asiluhusiwe mtu yeyote au kampuni yeyote ile kuliomba bali serikali kupitia STAMICO ndio imiliki eneo hilo na itafute mtu au kampuni ya kuingia nayo ubia.
2. Bunge ilitoe tamko kwa wizara kwamba application zote ambazo bado hazijatolewa zisitolewe kuanzia sasa hivi.
3. Maeneo yote ambayo ni prospective ambayo bado wawekezaji hajafanya upembuzi yakinifu (physibility study) na ripoti yake kuwasilishwa wizarani kwa waziri husika utafiti kwenye maeneo hayo usitishwe mara moja na yakabidhiwe STAMICO
4. State monopoly iludishwe na Stamico ndio wawe wasimamizi wakuu wa shughuli za madini
5. Mwisho serikali kupitia wizara au Geological Survey of Tanzania ifanye detail evaluation ya project zote kabla ya kuingia ubia na mtu yeyote yule au kampuni yeyote ile.

Kwa kuzingatia hayo hapo ndio nchi itaweza kufaidika na hazina yake ya madini.
 
Mkuu Chibingwa,
Haya ndio maneno na wabunge wetu tafadhalini sana yatazameni maoni haya... Muhimu zaidi.. mbali na yote hayo STAMICO iwekwe moja kwa moja ktk soko la DSE..
 
Mnalaumu bure jamani. Vya dhulma hupotea bila ya huruma.Dhulma ngapi zimepita hapa. Nyumba, viwanda, mashamba nk zilitaifishwa bila ya fidia au huruma. Mwenyezi Mungu ana balance accounts zake.Hata kura za wanyonge zimeibiwa. Hao hao mafisadi wangapi walishinda uchaguzi kihalali. Dawa ni mabadiliko kamili. Miaka 50 wameshindwa hata kusambaza maji angalau ya kunywa. Sikuambii mengine.
 
Kwakweli and to be honest...

Royalty inayopendekezwa from 3-5% it is a ridicule and an embarasment to most of us tunaojua privelege kubwa Mungu aliyotupa ya kulala na kukalia madini yaha.

Viongozi wetu wanajikombakomba as if haya madini kuwa Tanzania ni favour ya mataifa ya magharibi! Wanaangalia a very short budgetary constraints badala ya kutatua matatizo ya budget finyu once and for all,only by making sure kwamba we enjoy and seriously take advantage of our mineral deposits.

Nakubaliana na members wengi madini yakaozi na wala Nyerere hakuwa mjinga, iweje leo wao wawe so desparate kutoa madini yetu bure kwa wageni?

Na mbaya zaid pale wanaposamehe kodi has VAT makapuni haya, dhambi wanayotutendea sasa, hatutakaa tuwasamehe, wao, uzao wao wa kwanza na vitukuu vyao vitaendelea kulipia dhambi hii.

Inabidi waamue kiwendawazimu hivi kwasasa, 1. waongeze royalty to at least 10% na kupata free shares to atleaset 30% na kuhakikisha kuwa ALL legitimate taxes are timely and fully paid for!

Najua wawekezaji hawa makabaila ambao wanatuona mambumbumbu watachukia na kuona mafisadi wetu wamewageuka, but the pain on our leaders will just be a short term pinch but a much hilarious and most wanted action but the owners of minerals,Watanzania!

Tunahitaji raisi atakaye tekeleza ndoto hizi, tena tunamhitaji haraka! Mungu utusikilize sala zetu!
 
Hatimaye ripoti ya Bomani imetoka na hizi ni higjhlights kutokana na Gazeti la The Guardian:-

1. Govt should have shares in every mining company

Nimesoma kuwa wamependekeza 10%, inabidi watueleze kwa nini iwe 10% badala ya say 50%. Hata Warusi hivi sasa wamechukua control ya mafuta yao na uchumi ukaanza kupendeza.

2. Formation of minerals authority to surpervise all mining activities

Hii Mineral Authority ni muhimu iwe wazi na ijitegemee. Officials wake ni muhimu wasiwe wakiteuliwa na raisi, lau kama itabidi wawe wateule wa raisi, basi wawe professionals wanaokuwa approved na bunge. Otherwise inaweza kuwa formed halafu MD akawa Lowassa, Karamagi, Chenge n.k., halafu tukarudi palepale.

3. Mining royalty to be calculated on gross value and not net value as is the case at the moment
4. Increase gold royalt from 3% to 5%

Kama tutakuwa shareholders kwa angalau 50%, royalty nafikiri haitakuwa vibaya ikabaki as a % of net value. Lakini hii iwe adjusted kulingana na kiasi gani gross value inatumika nchini. Muhimu kwetu itakuwa ni kuhakikisha kuwa mambo mengi yanafanyikia TZ ili hiyo gross value iwe imebaki TZ kwa kiasi kikubwa.

5. Thorough investigations on Meremeta and Tangold
6. What was the legality of the BoT paying $ 132 million to the South Africa NedBank?

Inabidi kuangalia hili pendekezo kiundani maana Pinda tayari alishalipindisha kuwa haliwezekaniki. Sasa sijui hayo mapendekezo yatafanyikaje.

NB: Tunaomba mwenye kuipata hii ripoti aiweke mtandaoni ASAP ili tuichambue kiundani zaidi.
 
*Fisadi yule aliyekuwa waziri wa feza awamu ya tatu anaitwa Pesambili Mramba aliwahi kutukejeli kuwa madini yaliyo ardhini kama hayachimbwi ni sawa na hasara eti huwa yanashuka value. Hivi wabunge waliokuwa bungeni last time wanakumbuka hili? na ni wao waliompigia makofi leo wanalalamika nini? kwa kweli wabunge wa chama cha mapinduzi ni wachovu kweli!
*Mimi nashauri kwa sababu serikali yetu imeshakuwa chovu haitaki kuingia katika biashara maana pesa iliyotuibia inatosha wangeruhusu hawa wawekezaji kuingia ubia na wanavijiji waliokuwa wanamiliki ardhi kupata honorary shares hizo za 40% zinazopendekezwa. Lakini???????????????????????
*Kama serikali itaona ni vizuri iendelee kuwa na share katika migodi, bado wale wanavijiji waliokuwa wanamiliki wapewe share kiasi fulani ili faida bado ibaki katika mifuko yao. Achana na biashara hii ya oh tutajenga shule na barabara na sijui zahanati. Hii ni design tu iko designated kuwaibia wanavijiji maana kile wanachodai kukiweka by any means wapende wasipende wataweka tu maana kinasaidia operations zao. Kwani watashindwa kujenga barabara wapite wapi? au wasipojenga zahanati wafanyakazi wao watatibiwa wapi? Ni viongozi wetu tu wametupiga bao la kisigino.
*Isikubaliwe kamwe mtu kuwekeza bila kuwa na mwananchi anayeshare naye tena awe ni mmoja au kampuni ya kijiji yalipo machimbo.
*La sivyo tumeliwa.
 
Chibingwa,

..inaelekea haya masuala ya madini na nishati una habari naye kidogo.

..hivi unaweza kutuambia tofauti ya mapendekezo ya Tume ya Jaji Bomani, na yale ya Tume ya Kipokola.

..nina wasiwasi hizi Tume zinafanya kazi kwa kujirudia-rudia. nilisoma mapendekezo ya kamati ya Lawrence Masha, nikakuta reference kibao za kazi ya Tume ya Kipokola.

Mkuu JokaK,
Kama bado unazo hizo ripoti zao hebu zishushe hapa zote tuzikague na kuzilinganisha na hiii ya Bomani itakapotoka.
 
WAHESHIMIWA WABUNGE NAWAPENI MAPENDEKEZO YAFUATAYO SIJUWI KAMA YAPO KWENYE MAPENDEKEZO YA MHESHIMIWA BOMANI:
1. Prospecting license yeyote ile after 50% religuish (baada ya kupunguza nusu ya eneo la utafiti), asiluhusiwe mtu yeyote au kampuni yeyote ile kuliomba bali serikali kupitia STAMICO ndio imiliki eneo hilo na itafute mtu au kampuni ya kuingia nayo ubia.

Hili linaelekea ni wazo zuri. Kama unaweza mkuu Chibingwa hebu lipanue zaidi ili tulielewe.

2. Bunge ilitoe tamko kwa wizara kwamba application zote ambazo bado hazijatolewa zisitolewe kuanzia sasa hivi.

Wazo zuri pia ila nia yake ni ipi. Fafanua kidogo.

3. Maeneo yote ambayo ni prospective ambayo bado wawekezaji hajafanya upembuzi yakinifu (physibility study) na ripoti yake kuwasilishwa wizarani kwa waziri husika utafiti kwenye maeneo hayo usitishwe mara moja na yakabidhiwe STAMICO
Hii nafikiri inaweza kuwa against contract walizosaini na pia kuharibu utendaji kama hakuna makosa. Hebu fafanua nia ya kufanya hivi ili tuwe pamoja.

4. State monopoly iludishwe na Stamico ndio wawe wasimamizi wakuu wa shughuli za madini

Nakubaliana na wewe kuhusu STAMICO kupewa nguvu zaidi. Nafikiri bado haijawa privatised ila haina meno. Muhimu ni kwa STAMICO kuundwa upya ili iwe zaidi inasimamia hisa za taifa (shareholder) badala ya kufanya tu utafiti (prospecting). Wao ndio wawe wamiliki wa Ardhi kwa niaba ya Taifa.

5. Mwisho serikali kupitia wizara au Geological Survey of Tanzania ifanye detail evaluation ya project zote kabla ya kuingia ubia na mtu yeyote yule au kampuni yeyote ile.

Wazo zuri. Hili nafikiri wanaweza kushirikiana na STAMICO kama wakiwa na hiyo mandate ya kumiliki Ardhi kwa niaba ya waTZ.
 
...acheni story zenu hapa tangu lini serikali ikafanya biashara na ikafanikiwa? hakuna haja ya serikali kujiingiza kwenye umiliki wa hizi mining,muhimu ni wahakikishe wanapata fair deal kwa nchi kupitia tax,royalties & employment kutoka kwa investors,na siyo vibaya wakiweka sheria kuhakikisha part of it lazima imilikiwe na wazawa,lakini serikali kujiingiza kwenye biashara thats no no no na uzoefu unaonyesha ni disaster tuu,wanashindwa kuendesha vitu vidogo kama mikopo ya wanafunzi jee kitu complex kama mining wataweza wapi na investor gani atakubali kushirikiana na incompetent/ mnacheza nyie....kama vipi funga migodi yote na hakuna foreigners mpaka wazawa(sio serikali) watakapokuwa na uwezo wa kuiendesha
 
....STAMICO wangeweza kufanya kazi nzuri lakini njaa na incompetency inawasumbua,na kwa nini malalamiko ni mengi sana as if sheria zina favour foreigners tuu? hata wazawa wakiamua kuingia migodini sheria ni hizo hizo tuu na hizo tax holiday zitaishia kwa wazawa wachache na sio hazina kama,kwa hiyo swala la uzawa hapa sio factor...issue ni bad deal za kina Mkapa!
 
...acheni story zenu hapa tangu lini serikali ikafanya biashara na ikafanikiwa? hakuna haja ya serikali kujiingiza kwenye umiliki wa hizi mining,muhimu ni wahakikishe wanapata fair deal kwa nchi kupitia tax,royalties & employment kutoka kwa investors,na siyo vibaya wakiweka sheria kuhakikisha part of it lazima imilikiwe na wazawa,lakini serikali kujiingiza kwenye biashara thats no no no na uzoefu unaonyesha ni disaster tuu,wanashindwa kuendesha vitu vidogo kama mikopo ya wanafunzi jee kitu complex kama mining wataweza wapi na investor gani atakubali kushirikiana na incompetent/ mnacheza nyie....kama vipi funga migodi yote na hakuna foreigners mpaka wazawa(sio serikali) watakapokuwa na uwezo wa kuiendesha

Inaelekea hujaelewa hili suala kabisa. Serikali haifanyi biashara kwa mtindo wa shareholding. Haihusiki na uzalishaji au trading. Hizo ni juu ya investor na gharama zake huziondoa kwenye mauzo. Baada ya hapo kwenye faida huko ndio tunakokutana, 50%-50%, 51%-49% n.k. Hii ndio itatoa hasara au faida directly kwa waTZ. Nafikiri ni Ibra aliyesema kuwa Botswana wanafanya hivyo at 49%.
 
Back
Top Bottom