Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Mimi nionavo CCM wanamtengenezea Magufuli mazingura magumu ya Utawala wake..Huyu mzee ana nia njema sana ya Wananchi ila sasa atakwama upande mwingine wa mambo ya nje.
 
Mchungaji Msigwa nakupongeza kwa kutukumbusha nukuu muhimu kabisa

"huwezi kuyatatua matatizo kwa akili za kiwango kilichoyatengeneza"

Nyerere alitufelisha kwa kutokuwa flexible pale IMF walipompa masharti ya jinsi ya kuendesha uchumi.

Alichoking'ang'ania nyerere kimetusababisha tumefilisika kuanzia kichwani (ubongo) Jambo ambalo linatugharimu sana kwenye maamuzi yetu yajayo yanayotutia umasikini wa kipato.

"would you make a system make you kill your brother??"

unaacha trilion of money unaenda kuokata mifuko ya rambo fery siku ya kumbukumbu ya uhuru wa nchi yako.

Ukiitwa kichaa una site saiba loo craimu.
pumbafu kabisa.
 
Ni jambo baya kubaka demokrasia ni jambo baya zaidi kutegemea wengine. Ni upumbavu mkubwa kujivika kilemba cha ukoka kama chanzo cha kuimarisha kusaidiwa. Tutende haki ndani ya nchi yetu,anayestahili kwa haki si kwa hila apewe. Tuukatae upuuzi wa kutegemea wengine. Tunastahili kusaidia si kusaidiwa
 
Hivi mbona nchi kama uganda au zimbabwe huwa hawapewi misaada ya kijinga jinga kama hii na bado mambo yao yanaenda fresh tu?ebu turudishe urafiki wetu na wachina,tufanye kazi kwa bidii kama wao afu tuachane na mambo ya kwenda washngton kupiga magoti kuomba 900bil.
 
MCC hawajui kuwa kuna nchi mbili Zinazounda jamhuri ya muungano wa Tanzania? Kwa nini misaada yao wasingeondoa tu kile kipande cha Zanzibar tu? Kwa nini washupalie na TANZANIA bara?
Kwani rais wa Zanzibar Na Bara si wanaongozwa Na mwenyekiti mmoja wa chama.?
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

========================
s.

The Board deferred a vote on the reselection of Tanzania and Lesotho for compact eligibility until relevant governance concerns in both countries have been addressed.
Utegemezi taabu. Yaani tunalinganishwa na Lesotho kwenye utawala!
 
inabidi kama nchi tukikosa misaada ya maendeleo kwa sababu ya uchu wa madaraka wa viongozi inabnidi hata ile mishshsra na posho zao viongozi wastaafu nazo zipungue kutoka 80% ya current salary, maan hatuwezi kuwa tunakosa fedha za maendeleo kwa sababu ya watu tu wachache wao hawana madhara wanakula wanashiba cc tunapata shida inabidi hii impact iende hadi kwao nao wa fill hili joto la kukosa hizi fedha kama nchi masikini kama hii, huu ni uzembe wa hali juuu
 
Safi sana!

Hiyo misaada huwa ni fedheha tu.

Kwani hatuwezi kuishi bila misaada?
 
Hivi mbona nchi kama uganda au zimbabwe huwa hawapewi misaada ya kijinga jinga kama hii na bado mambo yao yanaenda fresh tu?ebu turudishe urafiki wetu na wachina,tufanye kazi kwa bidii kama wao afu tuachane na mambo ya kwenda washngton kupiga magoti kuomba 900bil.
Hawakutimiza masharti tangu mwanzo ndiyo maana hawamo katika mpango huo
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

========================
au hujui maana ya defer. wameahirisha uamuzi..kwa hiyo mtifuano znz ukiisha wataamua. cyber crime legislation haina shida wataelewa wakiringa tunafanya kwa hela zetu.
 
Mbona nao wana sheria kama hizo za kulinda vyao. Asange yuo wapi? Si wangemwacha kwa vile wana demokrasia. Hawa ni kuachana nao tu.
Kwa hiyo kwako ww na wengine wenye cariba yako mnaona ni sawa kwa ubakaji wa demokrasia unaoendelea zanzibar na udikteta wa sheria ya mtandao?
 
Kile kityengo cha MCiT/MCiCi pale MoFinancia ndo redudant our kuna visent vya kuki-service mpaka hapo mambo yatakaporekebishwa?.

Redundance redundance redundance
 
Hebu tuwe waelewa humu ndani tunaitwa great thinkers! with due respect nchi zinazopewa msaada wa MCC zinalingana na TZ kiuchumi kweli? Hebu angalia baadhi hizi nchi Cote d'Ivoire,Kosovo, Senegal,Togo,Sri Lanka,Nepal,Niger and Philippines.kama Serikali itaamua kuchapa kazi with six landlocked countries zimetuzunguuka tuna Madini,Gesi,Mbuga za Wanyama zaidi ya kumi kilimo,Uvuvi bado tunaomba ni matusi makubwa sana kwetu bora tunyimwe misaada hatustahili hata kidogo kusaidiwa hatuna umaskini huo tufunguke vichwa.
 
kumbe msaada bado upo . Mi nilidhani tumenyimwa kabisaaaa. Wanachotaka wao ni sisi kurekebisha kasoro fulani fulani kisha watautoa. Nadhani wataweka bank kifaida kwa muda kwa ajili yetu hadi tumalize hizo kasoro. Kwa hiyo wanaopata msaada huo sasa itakula kwao. Sisi fungu letu litawekwa bank kifaida hadi hapo tutakapomaliza hizo kasoro. Siunajua tena kinachokaa bank kwa muda huzalisha. Siku wakaianza kutukumbukatutapata na faidha yake toka bank. Patamu hapo! Ndiyo maana waswahili husemaharaka haraka ya kupata misaada sasa haina baraka. wanaopata sasa itakua kwao.

aisee, kwani makubaliano yanahusu na faida ya bank kutokana na hizi pesa?
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

========================

Kuna sehemu nyingine wamespecify reasons!

Kwanini umejump ktk conclusion kuwa issue ya Zanzibar na cyber crime law kuwa ndio sababu! Kwanini usingewasilisha tu kama jinsi ilivyoandikika?
 
Imekuwa suspended,Maalim Seif akiwa rais wa Zenji,kikao cha dharura kitaitwa ili kui-reaffirm Tanzania after a magnifient shift of power from an incubent CCM party to CUF,the main opposition party in Islands of Zanzibar.
So people stop worring about tha 900+billions from MCC,let them keep the money
 
Kwa kuanzia tupunguze bajeti ya serikali ili ilingane na makusanyo yetu ya kodi. Haiwezekani tupange bajeti ya Trillion 27 wakati mapato yetu ni Trillion 12!

Sipendi kuona yanayoendelea Zanzibar lakini pia sipendi kuona financial embarrassment tunayofanyiwa na MCC.

Jambo la msingi ni lazima tujitegemee.

Mkuu pitia Azimio la Zanzibar kujitegemea iliondolewa rasmi.
 
Naam! Haya ndio matokeo ya kutegemea 'wajomba.' Wajomba wamesema hapana,sijui watawala wetu watatoa kauli gani 'ya kujitetea.'
 
Back
Top Bottom