Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Mambo ya Zanzibar ni mazito, kama sikosei Pasco ws JF amewahi kuhoji kwanini hakuna aliyekwenda mahakamani kupata tafsiri ya kisheria juu ya mambo yote haya?
CCM ndio wanaobebeshwa lawama kama ilivyo ada lakini tunasahau serikali iliyopita ilikuwa ya umoja. Kwa chochote watakachokuwa wanataka kufanya CCM naamini kuna watu wa upande wa pili wanahusishwa.
Tunaskia kwamba chaguzi zilizopita CUF walikua wanashinda lakini hatuambiwi aliyekua ananyang'anywa ushindi alikuwa anakubali kwa makubaliano gani.
Demokrasia inatumiwa vibaya wakati kuna kikundi kimeshajihalalishia kutawala iwe kwa jina la CUF au CCM. Wanasiasa watatufikisha pabaya
 
Last edited by a moderator:
Naamini ya Zanzibar yataisha lakini kama nchi tujitahidi kujitegemea ili kufikia malengo kwa muda tunaotaka.

Masharti ya misaada huwa sio mazuri na fedha huja kwa mafungu i.e tunaendelea lakini kwa speed wanayotaka wao.
Kwa kifupi tutatue matatizo wenyewe tujenge utaifa ili kuepuka kuwa controlled kimaendeleo.

Tanzania haiwezi kuishi bila ya misaada ya watu weupe! Kubali au kataa huo ndio ukweli mpaka dunia itaisha. Msaada sio pesa cash tu, misaada ni ya aina nyingi tu ambayo Tanzania inaihitaji. Ni sawa na mtoto alomalizq chuo akapata kazi na kipato kizuri, akawaambia wazee wake hataki msaada wao.

Kama ni nchi inahitaji ushirikiano mambo mingi kutoka nchi nyengine ili iweze kujiendesha. Tanzania haina utaalamu wa sayansi wa kuvumbua technolojia au utaalamu wa mambo ya usalama. Hatuna uwezo wa kulipia huduma zote hizo. Wazungu wenyewe wanabadilishana (nipe nikupe) utaalamu na habari za usalama. Sisi hatuna cha ku exchange nao. Ikiwa mbu na nzi tumeshindwa kuwadhibiti wanatuletea maradhi ya kila aina, nini tutaweza? Ikiwa toothpick na sindano ya mkono tunanunuwa kutoka nje ya nchi, tutajitegemea vipi? Hicho kigesi cha Mtwara kisifanye mukawa na jeuri. Sasa ndio naanza kufahamu kwa nini Waarabu wakawa na kiburi
 
Mkuu usidanganyike hao ndio watawala wa ulimwengu, Libya ya Gaddafi ilikuwa Donner County sasa hivi uko wapi? The world is not fair.

Kenya pia walinyimwa hi yo hi yo Banda ya machafuko ya uchaguzi. But they stood by it and now sit tegemezi
 
ahaha kwani tuliwaita watusaidie au ipo kwenye mipango yao. Ki uhalisia hawatupi bure hiyo inayoitwa misaada kuna kitu inaitwa mutual benefit, wanatupa hicho wanachoita msaada na sisi kuna vitu tunaji comit ambavyo kwao itarudisha hiyo pesa waliotoa na hata kuzidi. Kwa hiyo kama hawataki hatuna sababu ya kuwalazimisha suluhisho ni kutafuta alternatives.

Sizitaki mbichi hizi!!!!!!
 
Nafikiri wengi wetu kuna kitu hatuelewi. Hatujaweza kujitegemea 100% bado kwakuwa importation ni kubwa zaidi ya exportation. Na madeni ya nchi aliyoyaacha JK ni makubwa sana na kama alivyosema wakwepa kodi hawataacha (Mit 18:21).Hivyo basi wakati wa kutegemea mapato ya ndani ya wakwepa kodi kuendesha nchi bado sana. Bado tunahitaji muda wa kujipanga.
 
Unafurahi nini mkuu, na wakati tunaumia wote?

Wote na nani? Fedha za MCC wanazitumbua wao wenyewe,kukwamwishwa wao ndio wataathirika hata hivyo kwa mapato anayoingiza magufuli tutaweza kujiendesha pasipo walamba hao Wazungu.
 
Mheshimiwa Rais hawa wamarekani wamekutishia nyau kukunyima vijisenti vyao vya misaada, usihuzunike wala kuumia ndani ya moyo wako, watanzania tupo nyuma yako tupo tayari kula nyasi lakini tuwe huru, tunajua wanatuhitaji kuliko tunavyowahitaji, sisi tuna madini mengi hasa URANIUM ambayo bi hot cake kwao na hawapendi madini haya yaende kwa maadui zake kama URUSI, CHINA NA IRAN. sasa karibisha hawa wapinzania weka mezani mazungumzo huna muda wa kupoteza kumbembeleza mkoloni. Tuna gas, madini ya chuma, Nikel, platnum, diomond, gold, makaa ya mawe na inasadikika huenda tuna mafuta.

Kwanza misaada yao pesa zote zinarudi kwao, wanakuja wazungu kibao, P.A.YE zote zinabaki wako, kwenye manunuzi kuna misamaha, na hairuhusiwi kununua chochote km siyo kutoka kwenye makampuni yao. katika hizo trilion moja tungefaidika na nusu tu nyingine zingerudi kwao na sisi tungeshindwa kujisimamia kwenye mikataba kwa kukumbuka fadhila kwenye huo msaada wa MCC.

Sasa tutaweza kujimamia kwa sababu tutakuwa huru hatuogopi kitu.
 
Siku nchi hii itakapovunjika amani kama Burundi sababu ya masuala ya uchaguzi,tukaanza kuuana ndio mtajua kwanin wanatunyima msaada!Wakiendelea kutupa misaada huku demokrasia ikiendelea kubakwa siku yakitokea yakutokea tutaanza kuulizana walikuwa wapi kufumbia m?cho viashiria vya uvunjifu wa amani ambapo kwa wingi Africa imeonekana kuwa ni ubakaji wa demokrasia!
Hakika tusipojirekebisha,ipo siku tutawakumbuka kwa kutuonya mara kwa mara!

sijakuelewa mkuu.....tutapigana kama burundi sisi au?......huo mfanowako ni mgumu sana kuuelewa labda ulete mwingine.....halaf mambo ya demokrasiq huwa hayaelezewi na nchi nyingine....ni kama mambo ya familia yan wewe huwezi kuwa na familia yako.......halaf ukawa unategemea akili zq jirani yako hasa kwnye mambo ya uchumi.........yan asipoupa hela ya mkeo kwenda saloon unakasirika huoni hiyo ni hatari!! ni bora ukafurahi maanaduniani hakuna vitu vya bure
 
Mheshimiwa Rais hawa wamarekani wamekutishia nyau kukunyima vijisenti vyao vya misaada, usihuzunike wala kuumia ndani ya moyo wako, watanzania tupo nyuma yako tupo tayari kula nyasi lakini tuwe huru, tunajua wanatuhitaji kuliko tunavyowahitaji, sisi tuna madini mengi hasa URANIUM ambayo bi hot cake kwao na hawapendi madini haya yaende kwa maadui zake kama URUSI, CHINA NA IRAN. sasa karibisha hawa wapinzania weka mezani mazungumzo huna muda wa kupoteza kumbembeleza mkoloni. Tuna gas, madini ya chuma, Nikel, platnum, diomond, gold, makaa ya mawe na inasadikika huenda tuna mafuta.

Kwanza misaada yao pesa zote zinarudi kwao, wanakuja wazungu kibao, P.A.YE zote zinabaki wako, kwenye manunuzi kuna misamaha, na hairuhusiwi kununua chochote km siyo kutoka kwenye makampuni yao. katika hizo trilion moja tungefaidika na nusu tu nyingine zingerudi kwao na sisi tungeshindwa kujisimamia kwenye mikataba kwa kukumbuka fadhila kwenye huo msaada wa MCC.

Sasa tutaweza kujimamia kwa sababu tutakuwa huru hatuogopi kitu.

Nimesimama kuunga mkono hoja Mh Rais!!
 
Nafikiri wengi wetu kuna kitu hatuelewi. Hatujaweza kujitegemea 100% bado kwakuwa importation ni kubwa zaidi ya exportation. Na madeni ya nchi aliyoyaacha JK ni makubwa sana na kama alivyosema wakwepa kodi hawataacha (Mit 18:21).Hivyo basi wakati wa kutegemea mapato ya ndani ya wakwepa kodi kuendesha nchi bado sana. Bado tunahitaji muda wa kujipanga.

Acha uongo ndugu.....kisema kuwa hatupo tayari kujitegemea ni kujitukqna wenyewe.....maana ni sawa na kusema hatuna akili......kitu ambqcho binafsi sikikubali............
 
sijakuelewa mkuu.....tutapigana kama burundi sisi au?......huo mfanowako ni mgumu sana kuuelewa labda ulete mwingine.....halaf mambo ya demokrasiq huwa hayaelezewi na nchi nyingine....ni kama mambo ya familia yan wewe huwezi kuwa na familia yako.......halaf ukawa unategemea akili zq jirani yako hasa kwnye mambo ya uchumi.........yan asipoupa hela ya mkeo kwenda saloon unakasirika huoni hiyo ni hatari!! ni bora ukafurahi maanaduniani hakuna vitu vya bure

Acha uvivu wa kufikiri,kuna nchi zilikuwa na amani na utulivu zaidi ya Tanzania,lakini wananchi waliposema imetosha mpaka Leo ni hazijatulia,fuatilia historia ya Pakistan!Tusibweteke na amani iliyopo,tunalo jukumu la kuilinda hasa kwa kuheshimu maamuzi ya wananchi!
Mfano wako ni mfu,haina maana kuwa Mtoto hata kama wako ukaanza kumtesa au kumuua eti serikali isiingilie kisa ni familia yako,kuna limit!Hata sisi kama nchi tuna mipaka,ndio maana hatujavamiwa ila tu tumekewa vikwazo vya kiuchumi!Kama watz tujiulize,je wanachotuambia kina ukweli?Ni kwa manufaa ya nani?
 
Tanzania sasa imekosa msaada wa takriban dola 472m sawa na zaidi ya trilion 1 za MCC kutoka Marekani. Hawa MCC mwaka 2014 walisema hatua zichukuliwe kuhusu fisadi ESCROW tukagoma na Waziri SAADA na MUHONGO wakanipinga vikali sana. Sasa imeongezeka na kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na wameamua kukata huo msaada. Siumizwi na kukosa msaada, naumizwa na kukosa msaada kutokana na sababu za ufisadi na ukandamizwaji wa demokrasia. Ingejua tunakosa msaada kwa sababu tumekataa ushoga ningeona fahari sana.

Kafulila.
 
Ingekuwa ni nchi zenye demokrasia, aliyesababisha hivyo angeangushwa kwa kuhujumu maslahi ya nchi. Inakuaje kukosa 472m kwa sababu za kibinafsi kabisa, kwa nchi kama TZ, kusiwe hata news ya kujadili na wananchi. News ni nini kwao?
Watanzania hawahusiki kabisa na janga hili, lakini watabeba athari zake.
 
Back
Top Bottom