Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.
Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.
Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa kundi la waendesha bodaboda, leo Februari 27, 2024 wamelichoma moto na kuliteketeza basi linalodaiwa kuwa ni mali ya Kampuni ya Saibaba, lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha, baada ya kudaiwa kumgonga bodaboda mmoja na kusababisha kifo chake.
Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Kona ya Semkiwa, Korogwe mkoani Tanga na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya pande mbili za barabara hiyo, jambo lililosababisha foleni iliyodumu kwa takribani saa mbili.
Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya ajali iliyosababisha kifo cha mwendesha bodaboda, wenzake walijikusanya na kulizingira basi hilo, wakawaamuru abiria wote kushuka na kushusha mizigo yao kabla ya kuliteketeza kwa moto.