mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,760
- 35,205
Pamoja na wazazi wengi kuwasajili watoto wao shule za mbali na wanakoishi ili sababu ya ubora wa hizo shule ukweli ni kwamba wamekua wakiwatesa sana watoto wao.
Fikiria mtoto wa Dar es salaam anaishi pugu, gongo lamboto, kibamba, mbagala, toangoma halafu anasoma bunge primary, diamond au olympio. Huyu mtoto anaamka saa ngapi, anatoka nyumbani saa ngapi, anarudi nyumbani saa ngapi na analala masaa mangapi
Kwa wazazi ambao wanatumia au wameshawahi tumia public transport asubuhi na jioni wanaelewa jinsi vitoto vinavyokuaga vimechoka na kulala mwanzo wa safari hadi mwisho. Hivi kweli hii ina maslahi kwa mtoto au kwa mzazi?
Sasa heri hata hao wanaopanda daladala wakalala..... wapo ambao wanapandishwa bodaboda alfajiri na jioni. Tena bodaboda zenyewe hazipiti vichochoroni bali zinapita highways. Kwani lazima asome huko buana?
Wazazi tuwe na huruma na mapenzi kwa watoto wetu japo kidogo tuu. Ni hatari zaidi ya tunavyodhani jamani. Tuwatetee hawa viumbe wasioweza kujitetea
Msikilize huyu mzazi hapa ukiweza share na watu wako wa karibu wanaosafirisha watoto kwa bodaboda kuwakumbusha hatari iliyo kwa watoto wao.