Bmw 3series GT au 5series GT

Hapa tukianza kuandika watasema tunamchukia Mjerumani. Ila kusema kweli hizo BMW kama una pochi nene ni gari tamu sana.

Tuanze na BMW.
BMW 3 series ya mwaka 2013 ni F30 ni Generation ya 6 ya 3 series na iliishia 2020 ikapokelewa na G20.

Kwa 5 series huo mwaka 2013 ilikua Generation ya 6 pia ambayo ni F10 ila yenyewe ilianza 2010 ikaisha 2016 ikapokelewa na G30.

Tuje GT.
GT kwenye BMW ni Kirefu cha Gran Turismo, wengine wanasema Grand Tour. Kilichobadirika sana ni body style (imekua crossback sio sedan), suspensions zimekua more comfort, sportier look, ila performance usitegemee muujiza ni almost sawa na original wake.

Kuhusu availability ya spare, GT wanashare parts nyingi na original wao ila pia wana baadhi ya parts ni unique yaani ni za GT tu sasa izo kidogo itakua challenge kuzipata maana hapa Dar kuziona GT kwa mwezi unaweza pishana nazo mbili tu.
 
Mzee hii 5 GT hata ya 2015 bei yake inaendaje?
 
BF wanakupa 2014 GT kwa Mil 18 kabla ya Ushuru.

View attachment 2935461


Hafu Ushuru Mil 15 za Tanzania.

View attachment 2935464

Jumla kama 32 hivi.
Ahsante sana mkuu.

Kuna janki flani nilimcheki na hii gari nilikariri tu hio GT, ila nilipenda muonekano, na nilikuwa najiuliza hii ni bmw model ipi?

Perfomance yake iko vipi compare na 3 series ambayo ni saloon?
 
Ahsante sana mkuu.

Kuna janki flani nilimcheki na hii gari nilikariri tu hio GT, ila nilipenda muonekano, na nilikuwa najiuliza hii ni bmw model ipi?

Perfomance yake iko vipi compare na 3 series ambayo ni saloon?
Tofauti kidogo sana kwanza zina engine ndogo izo GT ni 2.0L mostly, tofauti na sedan zake ni hizi ni fastback yaani shape zilitaka kua kama X6. Pia GT wheel base ndefu, zipo juu kidogo, kuna mabadiriko kwenye suspension basi.

Ukitaka performance nenda M version. Mfano M3.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…