Biodisc | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biodisc

Discussion in 'JF Doctor' started by KakaKiiza, Sep 26, 2010.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Wataalam wa tiba mbadala mimi naomba kueleweshwa kuhusu hii tiba mbadala ya kutumia kifaa maalumu kijulikanacho BIODISC,Biodisc nimeambiwa nimaji ya chemchem ambayo yamekuwa compressed nakugandishwa kitaalam nakuwa kama kitako cha glass ambacho ukikiweka katika maji yale maji yanakuwa tiba Mimi wasiwasi wangu je hakuna madhara ya baadae yatokanayo na kifaa hiki?? Na hiki kifaa kinauzwa bei ya $700 Tunaomba wenye ufaamu na ilitujuzeni.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280


  Bio Disc haijatengezwa kwa maji ya chemchem, bali imetengenezwa kwa aina 13 za madini asilia yanayopatikana ardhini na kuunganishwa kwa
  kutumia utaalam maalum uitwao NANO FUSION kwa kuchomwa kwa joto la hali ya juu mpaka kuibadili molecular formular yake, kama
  vanavyotengeneza vifaa viitwavyo super conductors.

  Muunganiko huu wa madini mbalimbali yaligandamizwa kwenye mgandamizo mkubwa yazalisha nguvu za asili ziitwazo "Scalar Energy" ambazo hupatikana kwenye chemchem mbalimbali zitoazotiba, yaani chemchem zenye healing powers.
  Hii biodisc inafanya kazi kwa kuzihamisha hizo scala energy kwenye kimiminika chochote kilicho karibu kwa kutumia nguvu za uvutano kama zile za kwenye sumaku inavyozalisha umeme kwa kuzunguka anti-clockwise.

  Hivyo ukiiweka hiyo biodisc chini ya chupa ya coca cola, itaikata gesi na kibadili ladha within a fraction of a second hivyo wanadai ikinywa kimiminika chochote kilichopitiwa na biodisc, zile nguvu zinaakisiwa kwenye kimiminika husika, hivyo ukinywa iwe ni maji, soda, chai, unakuwa umekunywa hizo scala energy hivyo zina nguvu ya utabibu.

  Mimi binafsi ninamatatizo Fulani, hivyo nikaambiwa biodisc itanisaidia, nikanunua seti nzima, bahati mbaya kwangu haukunisaidia chochote, lakini nawaona wenzangu wakinishuhudia jinsi ilivyowasaidia, hivyo kunauwezekano ili ikusaidie, ni lazima uwe na imani nayo. Nahisi mimi haikunisaidia kwa vile niliitilia mashaka kuwa hizi nguvu za kwenye biodisc ni nguvu za giza.

  Ukinunua complete set, inavyo vifaa 7 navyo ni Amezcua Biodisc, Amezcua Shower Shell, Amezcua Pewter Bio Disc, Amezcua Straw Tube, Allah Chi Pendant, Om Chi Pendant, Anahata Chi Pendant.

  Hizi pendant zinavaliwa kama urembo, tatizo zina miungu wa Waislamu, Allah, Wahindu Om na wawatu wa Indonesia Anahata.
  Kitendo cha kukosekana pendant ya God, ai Jesus au hata yenye alama ya msalaba, kulinitia mashaka kuhusu uwezo wa nguvu hizo na niposearch kwenye net, nikakuta vifaa vyote hivyo, vinatoka kwenye single source na formular yake ni top guared secret!.

  Bei ya kiwandani ni $ 500, hizo nyingine ni gharama za kusafirisha na faida ya ajenti wao. Tembelea http://www.biodisc-energy.com/
   
 3. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Mie nililetewa vitu hivyo nikashawishika kuvinunua. Lakini nikaamua kufanya uchunguzi kidogo na haya ndio niliyong'amua.

  Kwanza nilishtukia namna wanavyovitafutia soko. Wanatumia mtindo unaoitwa PRODUCT-BASED-PYRAMIDS, ambao una namna kama ya DECI na pyramids nyingine. Kwa nini kama ni kitu kizuri tusione kwenye TV kama vile wanavyotangaza bidhaa nyingine au kwenye magazeti? Kuna dawa nyingi zinazotangazwa kwenye vyombo hivyo kama dawa za kikohozi (Goodmorning, Cofta, Vicks Kingo n.k.), dawa za maumivu, dawa za malaria n.k.

  Product based pyramids zinawaahidi wasambazaji comissions kadiri wanavyopata wasambazaji wengine na kadiri wanavyouza wao wenyewe. Hatari ya hizi ni kwamba, hawa wasambazaji wa mwanzo wanaanza zaidi kwa jazba wakidhani wana bidhaa zenye "miujiza" fulani, na hivyo wanatumia nguvu nyingi sana kuzitafutia soko, na wakati mwingine kuziweka katika "stock" yao, na kujikuta wana overstock, na kupata hasara. Pia wana exploit udugu au urafiki au wa karibu au heshima ya cheo kwa ajili ya kutimiza malengo hayo ya biashara. Mara nyingi watasambazia ndugu zao na marafiki zao, kwa ile trust waliyo nayo kwao. Hata viongozi wa dini mpaka Maaskofu (kama ilivyokuwa kwa DECI) wanaweza kutumia dhamiri za waamini wao zinazowaamini kujiinua katika level ya wauzaji na kuongeza comission. Ethics za marketing za namna hiyo zina mashaka.

  Pili hata bei yake naona ni ya juu sana. $700 ni kwenye maeneo yaTSh 1m ambayo kama mtu unaitoa kwa ajili tu ya kuondoa gesi ya Coca cola na kutafuta nguvu hiyo, naona ni jazba zaidi na kufuata mkumbo wa kitu kipya kuliko tiba inayodaiwa kuwemo ndani ya hiyo bio disc. Questionable in terms of Value for Money.

  Tatu, nadhani hizo scalar energy ni ambiguous na hazieleweki zinatibu nini hasa. Kama si mgonjwa mahututi, TZS 1m kwa ajili tu ya kuwa na tiba ya kitu kisichoeleweka: kisukari, kansa, ngoma etc. ni matumizi mabaya ya pesa.

  Nne, kama ni masuala ya tiba, tunataka tuone madaktari waliobobea wanaeleza maelezo ya kina na kisayansi kuhusu tiba hiyo. Badala yake ni hao marketers ndio wanazinadi kwa ushabiki zaidi kuliko utaalamu. Hivi tunataka na mambo ya tiba yawe kiholela. BEWARE matapeli wanatafuta chance hizo.

  Mie nimeshaletewa na nikatafakari sana, na nikapeleleza hata namna zinavyouzwa nikapata mashaka hayo. But wenye kuiamini endeleeni, lakini mkijipa nafasi kutafiti kidogo mtaona mashaka pia.
   
 4. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Hivi walikueleza kama hiyo tiba mbadala ni kwa wagonjwa tu? Wa magonjwa gani? Mfano wa waliopona mnao?

  Au ni kwa kuzuia magonjwa? Magonjwa gani? Yote? Ni formula ya kuishi bila magonjwa?

  Na hao miungu, naona kuna ka-ushirikina pia, inakuwa kama zindiko fulani hivi!!!!! nina mashaka na hayo.
   
 5. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  hivi vitu ni wizi mtupu.Hiyo science mbona hatuioni kwenye scientific papers, tunaona tu iko sokoni, halafu kwa mtindo wa mteja kutafuta mteja.Yaani ukishaingizwa mjini na wewe unatafuta wa kumuingiza mjini.Halafu hii disc inafanya kila kitu utasikia inasaidia gari kutumia mafuta vizuri, ina..........matumizi yake kama uganga wa kienyeji.Unatakiwa utembee nayo mfukoni na kulala nayo kha!.
   
 6. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Pcman, nakubaliana kabisa nawe: WIZI MTUPU!!!
   
 7. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Watanzania tunakurupuka na tunadanganyika kwa haraka.
   
 8. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Kakakiiza umeridhika na michango hii?
   
 9. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Nimefurahi sana kwa michango yenu mimi nimeletewa na Representative wa hapa muarabu mmoja akawa ananieleza mafanikio yake najinsi nitakuwa najipatia $250 kila mwezi endapo nitawainiza watu wawili wakulia na wakushoto!!Wakanii takwenye semina hapo Hidaryplaza mambo mengi lakini akilini ikawa inadunda kwanza nikafikiria $700 nikaona parefu si masihara!!Hila PCMan umenifurahisha sana but thank you all:becky:
   
 10. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Thanks.
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  wizi... achana nao!!

  kama unapata ya bure ya kuvaa ...poa!!
   
 12. Dr. Said

  Dr. Said JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 204
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60
  Hi. Mimi naitwa Dr. Said. Miaka minne ilopita nilikutana na dada mmoja wa kichini kwenye mtandao akawa ananielezea kuhusu product ya Bio Disc. Nikiwa mwanafunzi wa udaktari wakati huo ilibidi nifanye utafiti kuelewa hiyo Bio Disc ni nini. Unaweza kuenda kwenye blog yangu ( Bio Disc Review – Is it Legit or Just Another Scam?) Nimeelezea vizuri Bio Disc ni nini na inafanya kazi vipi na watu waliotumia wanasemaje.
   
 13. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,543
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  asanteni hata mimi nimekutana na hii kitu
   
 14. J

  JazzBand Member

  #14
  Nov 18, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 15
  ha naiona forever living tena na man to man presentation wenyewe wanaita multi level marketing jinsi unavyoweza kuleta wengine ndivyo unavyofanikiwa niliwahi kuchomoka gnld nikanaswa forever meneja wangu nimekutana nae amehamia kwa wachina ananishawishi tena kaka na dada zangu asavali uamke mapema ukanunue ulimi machinjioni utauza supu na hela utaiona. asante muanzisha mada
   
 15. elimumali

  elimumali Senior Member

  #15
  Nov 18, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Namshukuru muanzisha mada pia. Nimeelimika, kwani maswali niliyokuwa najiuliza yamejibiwa katika mada hii kuhusu tiba hii. Naomba kuchangi kuwa katika tiba inatubidi tuamini kuwa zipo dawa zinazoweza kuwatibu baadhi ya watu na wengine zisiwatibu. Vile vile tuamini kuwa katika biashara hata kama ni ya kweli, utapeli bia haukosekani maana wahusika hutafuta mianya ya kujiongezea kipato. Thanks Dr. Said for your review.
   
 16. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hinduism =western New Age Movement against God and science. watch out. Freemansons in the business of making money.
   
 17. b

  bob giza JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi kuna jamaa alianza namm slow slow mthailand flani hadi baadae akaja bongo wakanialika kunako semibna yao pale ppf tower ule ukumbi wa mikutano juu ya ile parking pale..nikaendawasikiliza nikaskuti mmmhh hela yenyewe ilivo ngumu nikaona uzushi nikampotezea jamaa..alinilink na muhindi mmoja baada ya yeye kurudi thai yule dada akawa ananisumbua ananiulizia vp deal nikamwambia nimeghaili akanishawishi weeee alivoona sidanganyiki akaamua kuuchuna..kifupi hii kitu ni ofyo ofyo tuu..haieleweki unawesa fananisha na hii serikali ya mkwere maake inafanana na biashara kama hizi ..
   
 18. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2010
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ni usanii tu hamna kitu.
  Hata mimi nimewahi kualikwa na Mhindi mmoja, the meeting was conducted at ROYAL PALM HOTEL. Hebu jiulize; KWANINI KILA MARA WANABADILISHA UKUMBI WANAPOKUTANA NA WATU WENGI IN THEIR SO CALLED seminars?

  Wakati unapokuwa na maswali kwa mwenyeji wako kabla hujahudhuria unaambiwa "njoo tu kwenye BUSINESS PRESENTATION ndo utajua kila ki2".

  Katika kuhudhuria kwangu niligundua yafuatayo; 1. WATZ WENGI WALIOHUDHURIA (Incl WASOMI WAZURI) HAWANA UWEZO WA KUCHAMBUA KWA HARAKA. -walishangilia kwa hamasa kubwa pumba zote zilizozungumzwa, esp Pyramid scheme.

  2. COORDINATORS (HOST) NI WAASIA TU. BIG WHY?

  3. WANASEMA ZINAUZWA DUNIANI KOTE PASIPO UTHIBITISHO NA REFERENCE ZA UHAKIKA. Reference zote zipatikanazo kwenye mtandao wao ni za kwao wenyewe.
  Kuna nchi makini kama RWANDA imepiga marufuku kuingiza bidhaa hizo.

  3. Hii ni aina mpya ya HIRIZI KUTOKA MASHARIKI YA MBALI. Je iweje ni tiba kwa mtu (magonjwa yote), mafuta ya gari, mafuta ya kujipaka, vinywaji nk? -HIVI NI VITU AMBAVYO MUNGU MUUMBA TU NDIO ANAWEZA KUFANYA.

  4. Mara kadhaa msemaji alirudia "this is not related to satanism or witchcraft"-SWALI NI JE NANI ALIKUWA AMEMUULIZA?
  Hitimisho langu ni kuwa "it's related to powers of darkness and withcraft FOR MAKING PEOPLE BLIND TO TRUST GOD AND MAKING THEM POOR". Kama mchangiaji mmoja alivyoeleza kuwa alinunua "pack" na akataja majina ya vifaa vilivyomo na jinsi vinavyoonekana. Maana ya majina hayo na sura zilizopo kwenye vitu hivyo ndio uhalisia wenyewe.
   
 19. i

  ifolako Member

  #19
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si ajabu Hapa Yahaya Husein katia mkono wake!
   
 20. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  mimi nilidhani ni Dr wa ukweli kumbe na wewe uko kwenye promotion, maana nimecheck hiyo unayosema ni website yako na naona watu wa Singapore na Malaysia, sasa sijuhi hiyo reseach yako ndio ulifanyia huko?
   
Loading...