Biodisc

Internet italeta mengi.

Hivi vya biodisc hata na mimi nilikumbana navyo lakini wote wale wamefeli kuniconvince kwamba ina uwezo wo wote wa kimiujiza.

Afadhali ingekuwa laki moja ningefumba macho na kufanya majaribio, lakini $700 mpaka $800 ina maana target group yao ni wafanyakazi wenye mishahara mikubwa. Vile vile bei kubwa labda inaweza kuhamasisha watu kwamba kitu hichi ni genuine!
 
jamani tuwe makini na mpinga kristo yote hii ni kazi yake akuna lolote nimewaikukutana magomeni yani ni wizi mtupu eti inakukinga na mionzi yoyote asa ya cm akajaribu kunipa mifano niweke cm mfukoni nikaweka akaniambia ninyooshe mikono akawaanaishusha chini kwa nguvu mara akaniambia nitoe cm mfukoni nimyooshe mikono tena akawa anashusha tena mikono kwa nguvu akaniuliza umeona tofauti gani?

nikamwambia akuna tofauti kwani wakati cm ipo mfukoni ulishusha mkono kwa nguvu kidogo ila nilipotoa cm ulishusha kwa nguvu zaidi ndio tofauti niloiona
 
hii kitu nimekutana nayo na jamaa yangu school mate amenipiga shule sana, nikatafakari sana niakaona hainiingi akilini, kama ni biashara ya kawaida kwanini isiende katika misingi ya kawaida ya marketing and distribution, kwanini iwe ni issue ya man to man. na kwanini iwe based asia sana na sio ulaya au america. aaah wapi sidanganyiki
 
hawa watu kwa kweli ni matapeli, mimi nilipewa somo na mama yangu kuhusu hawa jamaa ila nikampuuza. nilipomuuliza baadae akasema eti ni matapeli.
 
Hi. Mimi naitwa Dr. Said. Miaka minne ilopita nilikutana na dada mmoja wa kichini kwenye mtandao akawa ananielezea kuhusu product ya Bio Disc. Nikiwa mwanafunzi wa udaktari wakati huo ilibidi nifanye utafiti kuelewa hiyo Bio Disc ni nini. Unaweza kuenda kwenye blog yangu ( Bio Disc Review – Is it Legit or Just Another Scam?) Nimeelezea vizuri Bio Disc ni nini na inafanya kazi vipi na watu waliotumia wanasemaje.
Dr. Said, nimetembelea hiyo blog yako, sijaona kama umeeleza chochote zaidi ya cut 'n' paste toka web za biodisc.
Nilitegemea wewe, kama ni dr wa ukweli, unapojitambulisha kama dr, unajustify udaktari wako, dr wa nini na umeupata wapi na lini.
Nilitegemea kukuta medical testimonial ya wagonjwa wako, lakini umetuleta ile ile crap ya wenyewe?.
Kwa vile hapa JF ni uwanja wa majadiliano na kuchangia mawazo, tueleze kile unachojua wewe na sio kutupeleka huko kwenye blog yako ya cut and paste.

Binafsi nimesema nilikuwa na tatizo fulani, nikaingizwa line ya biodisc kwa matumaini ya kupata nafuu, it was nothing, nil haina lolote, japo nimekiri wenzangu wanadai inawasaidia.
 
These are the guys that tell all those who participate in their marketing activities that money is not everything and money is the only thing. Kuanzia wanavyosalimiana mpaka wanavyoendesha mambo yao, haikawii kugundua kuwa ni yale yale ya siku zote, GRAND SECRET!. Anyway, niliambiwa ni network marketing at its best.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom