Binti Mariam

Binti Mariam

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,334
Reaction score
23,940
Binti Mariamu

Weekend hii kwangu ilikuwa ya tafakuri nyingi zisizo na majibu na msongo mkubwa wa mawazo. Ilikuwa weekend yenye kuumiza na ya kujiuliza sana juu ya mustakabali wa maisha yangu ya mahusiano.

Nilienda kwenye send off ya mchumba wa kaka yangu.

Kwanza nitangulize samahani kwa dada zangu wapenzi gfsonwin, AshaDii na Paloma na shostito zangu mimisa na BelindaJacob kwa kutowahi kuwasimulia jambo hili lililokuwa linanitesa moyoni kwa muda mrefu..huenda wangenipa ushauri wa kunifaa…

Moshi, Kilimanjaro 1994

Baba alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kilimanjaro kama Mkuu wa Polisi Wilaya ya Moshi Mjini. Mwaka huo huo alikuja Afisa Mifugo mpya wa Wilaya. Tulikuwa tukiishi karibu maeneo ya Shanty Town. Afisa mifugo huyu alikuwa na watoto watatu. Wa kwanza ni binti mkubwa (dada Pendo), wa pili ni binti mwingine mrembo zaidi (Mary) na mdogo wao wa kiume (Michael).

Nilikuwa naingia darasa la nne.

Dada Pendo alikuwa anaingia darasa la sita na Mary ndo alikuja kuanza darasa la Kwanza wakati Michael alikuwa bado mdogo kuanza shule ya msingi hivyo yeye alienda shule ya awali ya St. Margeth maeneo ya kule kule shanty town.
Pendo, Mimi na Mary tulienda shule moja ya Kibo primary enzi hizo mwalimu mkuu ni mama Nkya.

Tulipatana sana na Mary kwani licha ya kucheza pamoja nlikuwa nikimfundisha sana hesabu. Na kwa vile tulikuwa majirani basi tulishirikiana kwa mambo mengi…hadi nilipomaliza shule ya msingi tulikuwa na urafiki mkubwa sana.

Sekondari nilipangiwa Kibaha na hata huko bado niliendelea kuwasiliana na Mary. Tuliwasiliana zaidi kama marafiki na kwa kipindi kile hakuna kati yetu aliyekuwa akiwaza mapenzi (atleast kwangu sikuwa nikiwaza kabisa).

Dada yake na ndugu wengine walifahamu jinsi tulivyokuwa tunapatana na Mary mpaka hadi wazazi wake wakawa wanatuita wachumba.

Mary ni binti aliyelelewa vizuri kwao. Nashindwa kuamua nimeliona hilo zaidi kwake kwa kuwa tu tulikuwa majirani au ni kweli ni mmoja wa mabinti waliofunzwa wakafundika.

Mary ameniona at my best and worst moments..na katika nyakati zote hizo bado tuliendelea kuwa marafiki.

Nakumbuka utotoni nilikuwa nikitoroka nyumbani kwenda kucheza mpira uwanja wa Ushirika. Siku moja nilirudi usiku baba akanichapa nje ya nyumba yetu huku Mary akiniona. Of course pamoja na kuona aibu sikuacha kutoroka, ila siku mbili baadaye nilirudi nyumbani jioni. Mary aliponiona tu akanikimbilia akanipeleka kwao nkanawa miguu halafu kama nusu saa hivi nikatoka nje na yeye akaniaga kwa nguvu ili wajue nlikuwa kwao namfundisha…

December, 2009

Baada ya kumaliza chuo tuliendelea sana kuwasiliana na Mary. Wakati huu mawasiliano yetu yalibadilika kwenda more personal. Kwa bahati nzuri she was as single as I was. Tukawa tunawasiliana sana..calls. sms na safari za mara kwa mara kwenda Arusha ambako ndiko aliko kwa sasa.

Ghafla mwaka 2010..

Mary akanitext kuniambia kuwa kuna kitu kinaendelea kwa dada yake. Kwanza dada yake alimuambia kuwa amepata boyfriend ila hata yeye mwenyewe Mary atakuwa anamfahamu sana tu. Hakuhisi chochote hadi aliponitumia ujumbe huo mfupi. Alikuwa ni kaka yangu.

Sijui ni lini walianza mahusiano yao lakini kwa vyovyote vile walijua mimi na Mary tulikuwa more than friends. Ni mara nyingi nilikuwa namuambia bro naenda Arusha kumsalimia Mary. Kwani yeye alidhani nilikuwa naenda kucheza naye karata? Au kuruka kamba? <machungu> Ndiyo sikumuambia exactly uhusiano wetu ulipofika ila ni kwa sababu haukuwa muda muafaka.

Kaka yangu akanizunguka akaenda kumchumbia dada Pendo.

Nakumbuka Mwaka juzi nilipoenda tena Arusha Mary alitaka nimpe mimba tu lolote na liwe alimradi tu tuvunje mipango yao. Alinisisitiza sana ila nilimkatalia…how I wish I just did it <majuto>.

Muda ulienda haraka mara tukaitwa utambulisho wa shemeji yetu kama familia.

Ilikuwa kama miaka ile tulipokuwa tunaishi wote Moshi. With the exception ya mimi, watu wote walikuwa na furaha sana. Nilishindwa kujua kwa nini kaka yangu aliamua kunifitini vile <usaliti>.

Ghafla tukaenda kupeleka posa kwa kina Mary…mtoto mchanganyiko wa Kisukuma na Mnyakyusa..yaani mchangamfu ila adabu tele. Acha tu!!!!! <machungu>

I wish ningemkubalia Mary wazo lake kipindi kile..sasa Mary ni shemeji yangu.

Mary, kwa yeyote atakayekuja kukuoa..am sure amepata mke mwema. Sijaona binti mwenye nidhamu kama wewe. Mcheshi na mwenye kupenda watu.

Jumamosi hii ndiyo tulikuwa Morogoro, walipo wazazi wa Mary, kwenye send off party ya binti yao, dada Pendo, ambaye mwisho wa mwezi ujao atakuwa officially shemeji yangu and hence make Mary officially out of bounds for me.

Ndo nimerudi kutoka Morogoro jana..na sasa nipo kazini,

Wasalaam wapendwa,
Mentor.

Last edited by a moderator:
Mapenzi huhatibu urafiki kaka yangu. Huwezi jua Mungu kakuepusha na lipi. Endelea kumuheshimu japo inabidi ukae mbali kidogo manake hamkawii kuharibu. Curiosity killed the cat.
 
Hivi taratibu na mila zinasemaje!? uncle wangu alioa wake wawili watoto wa baba na mama mmoja tena wanaofuatana... Was anything wrong,?? hadi leo life goes on and they're old..
 
Hiyo heading ilinituma kwenye thread ya AmKATRINA ya juzi, na hivi alisema Id yake inaanzia na capital M nikajua ni wewe shemejii.....!!!!
 
Last edited by a moderator:
Dah, hapa ndipo unapotamani muda urudi nyuma ufanye maamuzi mengine bt t z too late.. No way out mkuu heshima kwa shem wako ichukue nafasi tuu
 
Mambo ya akina rachel na leah. Yakobo alitapeliwaje?
Sipati picha. Shemeji namuogopa kuliko -----.
Hivi taratibu na mila zinasemaje!? uncle wangu alioa wake wawili watoto wa baba na mama mmoja tena wanaofuatana... Was anything wrong,?? hadi leo life goes on and they're old..
 
......mhhh vifua vinabeba mazito!!! pole sana mdogo wangu Mentor.
Hebu niulize, ni kwamba hairuhusiwi kuoa ukoo mmoja? kwa vipi?
nijuzeni nisije fanya madudu mie.
 
Last edited by a moderator:
Mapenzi huhatibu urafiki kaka yangu. Huwezi jua Mungu kakuepusha na lipi. Endelea kumuheshimu japo inabidi ukae mbali kidogo manake hamkawii kuharibu. Curiosity killed the cat.

[SIZE=3 [USER=20070]King'asti[/USER], am soooo down right now! Hebu niambie Mungu kaniepushia na lipi? Umeshawahi kumuona Mary wewe? Have you King'asti? Usingejaribu kusema maneno hayo.

She is a lady and a half! I tell you ndiyo ana negatives zake but she is worth every dime man...a lady to fight for! Yaani ukimuoa umepata mke mwema yule wa Mithali 31! Na anafanya mambo yake kutoka moyoni...daaah!

anyway, najua itakuwa rahisi kumsahau kwa sababu ya geographical locations zetu! Sijui hiyo siku ya harusi itakuwaje... #sijui[/SIZE]

Hivi taratibu na mila zinasemaje!? uncle wangu alioa wake wawili watoto wa baba na mama mmoja tena wanaofuatana... Was anything wrong,?? hadi leo life goes on and they're old..

Baba V, hata mimi namfahamu mzee mmoja kule Mbulu ameoa wake watatu na wote ni ndugu wanaofuatana. Nadhani mila yao inaruhusu ila kwetu sidhani kama hili litakubalika. Kuna mtu aliwahi kuniambia ingewezekana kama wote tungeoa siku moja.

Kwa sasa hata sitaki kuliwazia hilo, I just want to forget and move on... #timeHelpME
 
Last edited by a moderator:
Ghafla mwaka 2010..

Mary akanitext kuniambia kuwa kuna kitu kinaendelea kwa dada yake. Kwanza dada yake alimuambia kuwa amepata boyfriend ila hata yeye mwenyewe Mary atakuwa anamfahamu sana tu. Hakuhisi chochote hadi aliponitumia ujumbe huo mfupi. Alikuwa ni kaka yangu.

Sijui ni lini walianza mahusiano yao lakini kwa vyovyote vile walijua mimi na Mary tulikuwa more than friends. Ni mara nyingi nilikuwa namuambia bro naenda Arusha kumsalimia Mary. Kwani yeye alidhani nilikuwa naenda kucheza naye karata? Au kuruka kamba? <machungu> Ndiyo sikumuambia exactly uhusiano wetu ulipofika ila ni kwa sababu haukuwa muda muafaka.

Yaani miaka yote hiyo hujawahi kuomba ndo ukaja kupata mshtuko baada ya bro wako kutangaza nia jimboni!!! wewe ulizembea mwenyewe unapaswa kujilaumu
 
......mhhh vifua vinabeba mazito!!! pole sana mdogo wangu Mentor.
Hebu niulize, ni kwamba hairuhusiwi kuoa ukoo mmoja? kwa vipi?
nijuzeni nisije fanya madudu mie.

Sio ukoo da Paloma, hii ni familia moja!!!:smash:
 
Last edited by a moderator:
Yaani miaka yote hiyo hujawahi kuomba ndo ukaja kupata mshtuko baada ya bro wako kutangaza nia jimboni!!! wewe ulizembea mwenyewe unapaswa kujilaumu
Fidel80 mbona sijaona uzembe wangu hapo bro?

Kila kitu kinaenda na muda....na kama yote yangeenda sawa basi labda mwakani ndipo tungefunga ndoa. But ilitubidi tusitishe plans zote mwaka 2010 pale tu alipoambiwa kuwa dada yake na kaka yangu ni an item!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kwani hairuhusiwa kuoa shemeji? watu wanaoa watoto wa baba mdogo/mkubwa iwe shemeji tu! Usiumize moyo fuatilia kwa undani ujue dini/mila na desturi zinasemaje.
 
pole sana kweli ni machungu hasa upande wako
siamini kama ndo utakuwa mwisho wako na mary.

hata hivyo mweleza kaka yako, mwambie ili ajue
ni jinsi gani amekuumiza.
 
Hivi huwa hairuhusiwi kuoa sehemu moja katika mila zetu sisi watanzania?
 
Fidel80 mbona sijaona uzembe wangu hapo bro?

Kila kitu kinaenda na muda....na kama yote yangeenda sawa basi labda mwakani ndipo tungefunga ndoa. But ilitubidi tusitishe plans zote mwaka 2010 pale tu alipoambiwa kuwa dada yake na kaka yangu ni an item!!!!

Hukuweka mambo yako wazi kama kweli unampenda Mary ukawaacha ndugu zako na ndugu zake wawe wana hisi hisi tu
 
......mhhh vifua vinabeba mazito!!! pole sana mdogo wangu Mentor.
Hebu niulize, ni kwamba hairuhusiwi kuoa ukoo mmoja? kwa vipi?
nijuzeni nisije fanya madudu mie.

Vipi mkuu Paloma na wewe una mtihani kama wa ndugu ya Mentor?. Mila na desturi za kwetu Tanzania zinatofautiana toka kabila moja na jingine. Mfano, kuna kabila mkoa wa Mara, sitalitaja maana sio langu na pia sina utani nao na nisije wakwaza, mtu/mwanaume anaweza/anaruhusiwa kuoa hata wake wawili toka familia moja ya baba na mama passipo shida yoyote na wanaishi na kushare mme mmoja, na ni bahati nimepata kushududia hilo.

Aidha pia, nimewahi kuwaona wengine mtu na ndg yake kama mkuu Mentor na ndg yake walioa katika familia moja, yaani watoto wa baba mmoja ila mama mbalimbali na hadi sasa wanaishi na hao walau ni ndg zangu pia.

Kuhusu ndg yangu Mentor, siwezi jua mila, tamaduni, malezi na mapokea yake yanasemaje, hivyo inaweza kuwa ngumu ama vinginevyo maana hata ukimusoma kimaandishi utaona kuwa kuna shida/ugumu.
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka nikiwa darasa la sita, miaka ya nyuma kidogo kipindi hicho naishi mkoani Tanga...nilishawahi kushuhudia watoto wawili wa kiume wa familia moja(by then walikuwa wanaishi US), wakioa mtu na dadaye wa familia nyingine...wale jamaa walikuwa ni mapacha na ndoa yao ilifungwa kanisani pale KKKT Kisosora kwa Mch. Mtoi (enzi hizo).
Niaminivyo mimi sioni kama kuna kasoro katika hili, yes Mary ni shemeji yako lakini si shemeji in a sense kwamba ndiye mke wa kaka yako.
 
Back
Top Bottom