Binti Mariam

Binti Mariam

pole sana shostito wangu Mentor...i can feel wht u r going through...tayari huyo ashakua shemeji yako n there is nothing you can do to change that..maumivu yako yataisha tu..huwa wanasema ''Time is the best healer''..n a strong mind can separate the body from suffering..pole sn
 
Last edited by a moderator:
kumbe Mentor tumesoma wote kibo primary. . .yaani umenikumbusha mbali, mwalimu kasa, ndosi, c malya, mwalimu makule, baadae mama minja wa kilimanjaro alibadilishana shule na mama nkya. . .dah! Those gud old times mzee.
 
Last edited by a moderator:
kumbe Mentor tumesoma wote kibo primary. . .yaani umenikumbusha mbali, mwalimu kasa, ndosi, c malya, mwalimu makule, baadae mama minja wa kilimanjaro alibadilishana shule na mama nkya. . .dah! Those gud old times mzee.
 
Last edited by a moderator:
We kaka wala usiumize kichwa na wala usipatwe na mawazo mbona hapo hakuna zambi yoyote? mimi niliwahi kuhudhuria harusi ya aina hiyo, wakaka wa familia moja wameoa wadada wa familia moja.....ila wao walikuwa mapacha...yaani mapacha wanaume wakaoa mapacha wanawake.......na mpaka leo maisha yao ni mazuri na wanaelewana vizuri tu......tena wakaka ni watu wa huko huko kaskazini.....

Unachotakiwa kufanya ni kupeleka posa kwa kina mary na wala haitakataliwa, nakuambia ukweli....ni kitu cha kawaida tu...na huwa inawafanya mnakuwa karibu zaidi kama familia.....hiyo kitu inatokea sana tu labda hujawahi kuona wewe lkn si kitu kigeni na wala hakuna cha kushangaza hapo........
sasa hao wadada wamepishana matumbo watu wanoa mapacha waliokaa tumbo moja seuze hao? we endelea na mchakato wako wa kumuoa mary bana achana na hofu za kijingajinga....
 
Duh! Yaani kusema hiyo kauli umeikopa kutoka mdomoni mwangu vile Mzee...Tofauti ni kuwa kwangu mii huu si mzaha🙂
Ahahahaha maana mary.. anaonekana kalelewa akaleleka.Mila zikizuia ntamuomba atupe ruhusu nikusindikize kijana kwa Mary

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
nakumbuka nikiwa darasa la sita, miaka ya nyuma kidogo kipindi hicho naishi mkoani tanga...nilishawahi kushuhudia watoto wawili wa kiume wa familia moja(by then walikuwa wanaishi us), wakioa mtu na dadaye wa familia nyingine...wale jamaa walikuwa ni mapacha na ndoa yao ilifungwa kanisani pale kkkt kisosora kwa mch. Mtoi (enzi hizo).
niaminivyo mimi sioni kama kuna kasoro katika hili, yes mary ni shemeji yako lakini si shemeji in a sense kwamba ndiye mke wa kaka yako.

kwa wanyakyusa hilo jambo halikubaliki, labda kwasababu huyo mary ni mchanganyiko wa kisukuma pia....
 
kwa wanyakyusa hilo jambo halikubaliki, labda kwasababu huyo mary ni mchanganyiko wa kisukuma pia....


hakuna cha unyakyusa wala nini. hizo ni enzi hizo bana, ebu ampe mimba uone kama wazazi watakataa......yeye ni uoga wa bure tu
 
So sad,hahaha hiyo inaitwa timing maana for sure mimi naamini bro alikuwa anajua kinachoendelea bt atafanyeje wakati na yeye keshafall tena kwa mkubwa
 
Nakumbuka nikiwa darasa la sita, miaka ya nyuma kidogo kipindi hicho naishi mkoani Tanga...nilishawahi kushuhudia watoto wawili wa kiume wa familia moja(by then walikuwa wanaishi US), wakioa mtu na dadaye wa familia nyingine...wale jamaa walikuwa ni mapacha na ndoa yao ilifungwa kanisani pale KKKT Kisosora kwa Mch. Mtoi (enzi hizo).
Niaminivyo mimi sioni kama kuna kasoro katika hili, yes Mary ni shemeji yako lakini si shemeji in a sense kwamba ndiye mke wa kaka yako.

Huu ni utaratibu tu ambao tumejiwekea na si sheria kwamba kama kaka yako akioa sehemu basi wewe usiowe, imekuwa hivi kwa kuwa sisi ni binadamu na tuna mapungufu kutokana na assumption kwamba endapo itafikia uhusiano ume-fall apart kwenye pair moja bado hii pair nyingine itaendelea kuwa sehemu ya watu wa karibi hivyo bado interaction itaendelea kuwepo na wahusika watazidi kuumia once wanatakapokutana katika event za furaha na huzuni maana hiyo pair nyingine ni ndugu zao. Lakini kwa ujumla, if all other things remain constant hakuna shida kuoa nyumba moja kwani mila na desturi hata kisheria hairuhusiwi ndugu moja kuoana
 
Binti Mariamu

Weekend hii kwangu ilikuwa ya tafakuri nyingi zisizo na majibu na msongo mkubwa wa mawazo. Ilikuwa weekend yenye kuumiza na ya kujiuliza sana juu ya mustakabali wa maisha yangu ya mahusiano.

Nilienda kwenye send off ya mchumba wa kaka yangu.

Kwanza nitangulize samahani kwa dada zangu wapenzi gfsonwin, AshaDii na Paloma na shostito zangu mimisa na BelindaJacob kwa kutowahi kuwasimulia jambo hili lililokuwa linanitesa moyoni kwa muda mrefu..huenda wangenipa ushauri wa kunifaa…

Moshi, Kilimanjaro 1994


Baba alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kilimanjaro kama Mkuu wa Polisi Wilaya ya Moshi Mjini. Mwaka huo huo alikuja Afisa Mifugo mpya wa Wilaya. Tulikuwa tukiishi karibu maeneo ya Shanty Town. Afisa mifugo huyu alikuwa na watoto watatu. Wa kwanza ni binti mkubwa (dada Pendo), wa pili ni binti mwingine mrembo zaidi (Mary) na mdogo wao wa kiume (Michael).

Nilikuwa naingia darasa la nne.

Dada Pendo alikuwa anaingia darasa la sita na Mary ndo alikuja kuanza darasa la Kwanza wakati Michael alikuwa bado mdogo kuanza shule ya msingi hivyo yeye alienda shule ya awali ya St. Margeth maeneo ya kule kule shanty town.
Pendo, Mimi na Mary tulienda shule moja ya Kibo primary enzi hizo mwalimu mkuu ni mama Nkya.

Tulipatana sana na Mary kwani licha ya kucheza pamoja nlikuwa nikimfundisha sana hesabu. Na kwa vile tulikuwa majirani basi tulishirikiana kwa mambo mengi…hadi nilipomaliza shule ya msingi tulikuwa na urafiki mkubwa sana.

Sekondari nilipangiwa Kibaha na hata huko bado niliendelea kuwasiliana na Mary. Tuliwasiliana zaidi kama marafiki na kwa kipindi kile hakuna kati yetu aliyekuwa akiwaza mapenzi (atleast kwangu sikuwa nikiwaza kabisa).

Dada yake na ndugu wengine walifahamu jinsi tulivyokuwa tunapatana na Mary mpaka hadi wazazi wake wakawa wanatuita wachumba.

Mary ni binti aliyelelewa vizuri kwao. Nashindwa kuamua nimeliona hilo zaidi kwake kwa kuwa tu tulikuwa majirani au ni kweli ni mmoja wa mabinti waliofunzwa wakafundika.

Mary ameniona at my best and worst moments..na katika nyakati zote hizo bado tuliendelea kuwa marafiki.

Nakumbuka utotoni nilikuwa nikitoroka nyumbani kwenda kucheza mpira uwanja wa Ushirika. Siku moja nilirudi usiku baba akanichapa nje ya nyumba yetu huku Mary akiniona. Of course pamoja na kuona aibu sikuacha kutoroka, ila siku mbili baadaye nilirudi nyumbani jioni. Mary aliponiona tu akanikimbilia akanipeleka kwao nkanawa miguu halafu kama nusu saa hivi nikatoka nje na yeye akaniaga kwa nguvu ili wajue nlikuwa kwao namfundisha…

December, 2009

Baada ya kumaliza chuo tuliendelea sana kuwasiliana na Mary. Wakati huu mawasiliano yetu yalibadilika kwenda more personal. Kwa bahati nzuri she was as single as I was. Tukawa tunawasiliana sana..calls. sms na safari za mara kwa mara kwenda Arusha ambako ndiko aliko kwa sasa.

Ghafla mwaka 2010..

Mary akanitext kuniambia kuwa kuna kitu kinaendelea kwa dada yake. Kwanza dada yake alimuambia kuwa amepata boyfriend ila hata yeye mwenyewe Mary atakuwa anamfahamu sana tu. Hakuhisi chochote hadi aliponitumia ujumbe huo mfupi. Alikuwa ni kaka yangu.

Sijui ni lini walianza mahusiano yao lakini kwa vyovyote vile walijua mimi na Mary tulikuwa more than friends. Ni mara nyingi nilikuwa namuambia bro naenda Arusha kumsalimia Mary. Kwani yeye alidhani nilikuwa naenda kucheza naye karata? Au kuruka kamba? <machungu> Ndiyo sikumuambia exactly uhusiano wetu ulipofika ila ni kwa sababu haukuwa muda muafaka.

Kaka yangu akanizunguka akaenda kumchumbia dada Pendo.

Nakumbuka Mwaka juzi nilipoenda tena Arusha Mary alitaka nimpe mimba tu lolote na liwe alimradi tu tuvunje mipango yao. Alinisisitiza sana ila nilimkatalia…how I wish I just did it <majuto>.

Muda ulienda haraka mara tukaitwa utambulisho wa shemeji yetu kama familia.

Ilikuwa kama miaka ile tulipokuwa tunaishi wote Moshi. With the exception ya mimi, watu wote walikuwa na furaha sana. Nilishindwa kujua kwa nini kaka yangu aliamua kunifitini vile <usaliti>.

Ghafla tukaenda kupeleka posa kwa kina Mary…mtoto mchanganyiko wa Kisukuma na Mnyakyusa..yaani mchangamfu ila adabu tele. Acha tu!!!!! <machungu>

I wish ningemkubalia Mary wazo lake kipindi kile..sasa Mary ni shemeji yangu.

Mary, kwa yeyote atakayekuja kukuoa..am sure amepata mke mwema. Sijaona binti mwenye nidhamu kama wewe. Mcheshi na mwenye kupenda watu.

Jumamosi hii ndiyo tulikuwa Morogoro, walipo wazazi wa Mary, kwenye send off party ya binti yao, dada Pendo, ambaye mwisho wa mwezi ujao atakuwa officially shemeji yangu and hence make Mary officially out of bounds for me.

Ndo nimerudi kutoka Morogoro jana..na sasa nipo kazini,


Wasalaam wapendwa,
Mentor.


Kumbe mshua wako ni polisi ( aliwahi kuwa polisi? ). Dah siwapendi polisi!
 
Babu zangu yaani mtu na mdogo wake wameoa familia moja mbaya ni pale labda baba mdogo au uncle ameoa familia hiyo na wewe uende hapo hapo haileti picha.

Ila kwa issue ya mtu na dada yake hakuna mbaya tena ni wasukuma sidhani kama kuna shida

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
what i know if itwasnt meant for you...............hata ufanyeje huipati.
simply go for another one, imagine what if ukalazimisha kumapa mimba halafu akajifungua kitu kisichoeleweka, ama kila akiazaa mtoto anakufa could you resist it??

ama je akajakupata ulemavu wakati wa kuzaa ambao ungekuwa ni wa kudumu na ambao ungegharimu kuuhudumia akiwa kitandani maisha yake yote usingejuta??

basi ukiwaza hivyo utaacha hili lipite huku uukimwomba Mungu kwa wakufanana na wewe.
 
Sioni kizuizi chochote kwani wewe na kaka yako kuoa familia moja kuna shida gani...unless ni elimu mpya mujini hapa!
 
Guyz kwani kuoa sehemu alipo oa kakako kunakua na tatizo?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom