Msichana mmoja [Jina tunalihifadhi] mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Ubungo Islamic amekutwa amefariki ndani ya gesti jijini Dar es Salaam.
Msichana huyo jina kapuni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Ubungo Islamic alikutwa amefariki ndani ya gesti ya Mkomboni iliyopo kata ya Hananasif, Kinondoni.
Kwa mujibu wa wahudumu wa gesti hiyo, msichana huyo aliingia ndani ya gesti hiyo akiwa na mwanaume ambaye siku tatu zilizopita aliingiza wanawake wawili tofauti ndani ya gesti hiyo.
Mmoja wa wahudumu akimuelezea mwanaume aliyekuwa na mwanafunzi huyo alisema kuwa mwanaume huyo siku tatu zilizopita alikuja na mwanamke mmoja katika gesti hiyo na kuchukua chumba namba 4, baada ya lisaa limoja mwanamke huyo alisikika akilia kwa uchungu huku akidai kurudisha pesa zake.
Siku iliyofuatia mwanaume huyo alikuja na mwanamke mwingine tofauti na kuchukua chumba namba 6 na ndani ya masaa mawili mwanamke huyo alitoka huku akilia akisema mwanaume huyo kamfanyia kitu kibaya ndio maana kaamua kumkimbia.
Jana mwanaume huyo ndipo alipotinga tena kwenye gesti hiyo akiwa na mwanafunzi huyo wa kike kwenye majira ya saa tisa mchana.
"Kwenye majira ya saa kumi tulisikia mlio kwa ndani lakini hatukufuatilia
kwa sababu tulijua ni mambo ya mapenzi lakini kadri muda ulivyozidi ndipo sauti ile ilikuwa ikipotea baadaye yule jamaa alitoka na kuondoka sisi tukijua kuwa labda wameondoka wote tulivyo kwenda kutaka kufanya usafi tulimkuta binti huyo kalala kama amekufa", alisema mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo.
Mhudumu huyo alitoa taarifa katika kituo cha polisi cha Oysterbay na walipofika walimkagua na kukuta vitambulisho vya binti huyo lakini katika mkoba wake hakukuwa na simu wala pesa.
Taarifa zilizopatikana baadae zilidai kuwa mwanafunzi huyo ameiaga dunia.
picha zaidi gonga hapa chini
NIFAHAMISHE .: PHOTO GALLERY :.