Bimmer na Landcruiser V8

Niambie criteria uliotumia kuonesha mtu fulani anafuata mkumbo?

Kwamba mtu akienda kununua iphone 13 pro max anafuata mkumbo ila wewe unaeenda kununua S21ultra hufuati mkumbo.

Umetumia nini kujua huyo wa iphone amefuata mkumbo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabisa nimesema wengi na siyo wote. Watu wengi wanaonunia iPhone wanafuata mkumbo ili tu aonekane naye ana iPhone lakini hawajui kuzitumia.

Na ndiyo hao wanaolalamika kuwa oo iPhone sijui kila kitu ni cha kulipia mara kwenye iPhone hauna uhuru au hauwezi kufanya hiki na hiki kama kwenye android. Ukiuliza kwanini sasa umenunua iPhone hana majibu anajiumauma tu so waliofuata mkumbo wanajulikanaga tu.
 
Mkuu hili wala sidhani kama litakuwa na mjadala mrefu.

Ukiona gari imeandikwa 180 na imefungwa saizi ya tairi sahihi basi hiyo gari haiwezi kuvuka 180.

Ukiona gari imeandikwa 180 na inavuka 180 basi kuna mawili. Moja gari imefungwa tairi za saizi kubwa kuliko zinazotakiwa, mbili gari imekuwa tuned ikaondolewa speed limiter.

Speaking from experience, last week tulikuwa tunapeleka gari Toyota Premio Tanga mjini. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa ile gari tairi zilizofungwa ni 175/70R14 na ukisoma kile kibati cha pale mlangoni tairi zinazotakiwa ni 185/70R14.

Ile gari tukisoma speed kwenye google map ilikuwa inatuletea speed ndogo kuliko speed inayoonesha kwenye dashboad. Around 55Km/h kulikuwa na difference ya 4Km/h.

Speaking of Passo na Bus aiseee hizi ni story za vijiweni. Speed ni universal.

Basi na passo zote zikianza at point A na zikaaccelerate kwa 100Km/h wote watafika point B at the same time.

Asikudanganye mtu eti 100 ya Basi ni kubwa kuliko 100 ya Passo.

Huo ni uongo wa mchana kweupe.

Huwa nacheka sana watu wanapoleta hoja za hivyo eti mzunguko wa tairi nk. Wakati 50km/h ya treka, passo na V8 zinafanana

Tofauti inakuja kwenye kuifikia hiyo 50km/h ila zote zikimaintain same speed, then zitafika destination at the same time

Ni sawa mtu anasema Kilo moja ya mawe na kilo ya pamba ipi nzito
 
Sawa kabisa mkuu unajua kila gari inategemea na malengo na mfuko wako ukoje! Ukiwa na uwezo wa kusatisfy mahitaji ya gari husika unaweza hata agiza 2021 BMW X7 ukaipeleka kwenye mamito na makorongo ya huko site!

Ikiua kifaa unaandika cheque ya million 15 unaagiziwa fasta! Umepasua sample unaandikia tu $5000 unaletewa wala haina shida! Mwenye hesabu kali hawezi kuishi humo!

Walioko cost concious ndio hao wanaotumia Hilux! Wapo watu wenye hela za kununua Amarok ila hawanunui kwani wao hawajui kwamba Amarok ina mvuto zaidi na gari ya hadhi zaidi!
Ukiwa na M40 unamvuta mnyama amarok

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Labda VX.R ya petrol ila ya Dizeli ni mchumba kwa 3 series.
Aisee nahisi kwa hapa nyumbani TZ Diesel ndio moto zaidi.. Sababu dashboard inasogea zaidi ya 180kph.. Petrol nyingi hazivuki hapo 180kph..

Halafu sasa hata 316i nayo ni 3 series.. Hii sidhani kama inaweza LC200..
Kwenye kusprint labda..
Ila marathon V8 ni hatari.. Unahitaji engine kubwa kidogo kupambana naye bila kuichosha gari..!
 
Ok sawa.. Hapo nilichokuwa na maanisha ni hiki..
Euro Emissions zinapanda siku baada ya siku.. European cars wameshakuwa na technology kubwa zaidi kabla ya Toyota.. Kwao kumeet hizo standards sio ishu sana.. Euro emission 5 ilifanya DPF kuwa mandatory kwenye diesel cars.. Toyota wakati huo gari flagship ni LC150 na LC200.. Sasa angalia early models za hizo gari jinsi zilivyopata shida na vumbi kwenye engine.. Diesel chafu.. Actually mpaka hivi karibuni Toyota ame recall baadhi ya gari HiLux ili kufix hiyo ishu..Engine ikipita kwenye vumbi kuna sensor zinapata shida..new model HiLux sio kama HiLux ilipojenga jina enzi hizo..

Toyota Supra iv.. Engine yake 2jz Gte.. Bonge la engine na sifa zake zinajulikana kote.. Umeona new Supra.. Engine B58 kutoka kwa Bimmer.. Why hawajaweka their legendary engine wahangaike kusource mpya!!kwa standards za leo za emissions ni ngumu sana 2jz Gte kumeet..!

Kwenye sensors.. Toyota Landcruiser ya 1990 haina sensors kama Landcruiser ya 2010.. Kwahiyo sio kwamba hawakuwa na sensors.. Zilikuwepo.. Chache sana.. Ila sasa hivi engines za Toyota unakuta zina sensors nyingi.. Yote hii ni kuhakikisha gari zinakuwa na clean emission hazichafui mazingira.. Ukishaanza kuwa na vitu vingi kwenye gari.. Unaongeza chance ya kitu kimoja kuzingua.. Kwahiyo hata Toyota magari yao sio reliable kama ya zamani..!

Kwahiyo tangu zamani gari ya mzungu ilikuwa imetengenezwa kwa technology kubwa.. Halitaki vitu chini ya standard.. Toyota aliinvest vitu basic..
Sasa game inachange na Toyota anaanza kuonyesha weakness zake ikija mambo ya technology..!
Emmission standards zimebadilika tofauti na zamani. za miaka ya 90 zio za miaka ya 2000. Za zamani huwezi ku import Europe sasa ivi kwa sababu hazimeet hizo standards. Ndio maana Toyota akawa na engines mpya ambazo zinatumika Euro na hasa kwa kutumia brand ya Lexus, engine hizo hizo tunaziona kwenye toyota saiv na bado toyota hauzi Europe.

2jzgte ni engine moja babkubwa kwa perfomance, lakini sababu ya kwanini toyota hawakuiweka kwenye Supra mpya, sio kwamba emmissions (ingawa haikuwa certified tangu mwanzo kukubalika in Europe) bali ni engine ya zamani mno, Toyota wameachana na Inline 6 engines na wamehamia kwa v6, kwao kuanza development upya ya kuweka 2jzgte sio cost efficient (inabidi waanze from scratch wakati assembly ya hio engine imeshauliwa) na ndio wakaamua kwenda na BMW engine, in short wamechukua BMW wakaibandika badge ya Supra the same wamefanya kwa FT86 ambayo ni subaru.

Sensors za emmission zina collect data ku make sure gari ina run kwenye standards zilizowekwa, sioni vipi zinachangia katika ubovu wa chombo zaidi ya kukwambia tu kama gari yako ita fail emmission test n.k Mfano Oxygen sensor, ina collect data ECU inapewa taarifa mafuta iongeze au ipunguze, lakini o2 sensor kama o2 sensor hai control physicial device. Sasa general rule ni kwamba ukiongeza vitu manake unaongeza more things to fail, lakini sio in a sense kwamba its not reliable. Umeongeza tu idadi ya vitu ofcourse uta repair vingi kuliko alokuwa na vichache.

Nakubaliana na wewe kuwa toyota ana vitu basic, Haziendani kabisa na wengine, wapo nyuma na wamejiekea nyuma makusudi. Wao kama kitu kinafanya kazi vizuri kwanini wafanye njia nyengine? wanaona bora wakiache ivo ivo. Sasa wenzao wanakwenda na technology, kama wanaweza kuweka bluetooth brakes (jokes) kwanini wasiweke?

Tutizame Air suspension vs Coil Springs, chances za ku fail air suspension ni high kuliko coil springs, sasa toyota hapo anaona ah wacha niweke coil springs, RR na wenzake wacha tuweke Air Suspension for ride comfort anaenunua RR ana uwezo wa kununua Air suspension nyengine tu.
 
Kwamba BMW isifananishwe na Land Cruiser kisa tu Land Cruiser ni Toyota? Ndicho wabongo wengi wanachoponda hiki!
Wanafeli sana humo!

Yani ni sawa na kudharau tajiri eti kisa ni msukuma hajivungi ila akikaa na matajiri wenzie wachaga aonekane tajiri kweli ni mchaga tu! Yani mwenye pesa anasemwa mchaga tu wakati msukuma ana mawe pia!

Watu wanadharau Land Cruiser sababu ni Toyota ila interms of comfort haiwezi pishana na gari lolote la kisasa! Land cruiser zina Airbags, Air Suspensions na burudani zote sijui apple car play na android auto! Yani ni gari zuri kwa kweli ila watu wanaleta dharau za kishamba wakihisi Landcruiser imekakamaa kama Passo ama IST😅
 
Aisee safi sana.. Madini tupu..
Sasa hiyo ya 2jz kuwa ngumu kumeet emission uichukue pia ni sababu.. Hiyo ya assembly kuwa imeshavunjwa ni sawa..
Ila kumbuka B58 ni inline six sio V6.. Toyota anazo V6 hata leo.. Ila hajaziweka kwenye Supra..!

Sasa sensors zinatuma data then data inadisplay hapo kwenye dashboard.. Kwahiyo kama taa ya check engine inawaka.. Then teyari kuna tatizo.. Sensor hizo ndio chanzo..
Pia gari za kijerumani zinaposemwa unreliable sio kwamba bodi itabonyea.. Chassis itapinda.. No.. Ni hiyo mifumo yake ya umeme na tech ndio inasababisha unreliability.. Ila ukikutana na engines za zamani za kijerumani zipo reliable kweli... Mimi Bimmer yangu ina 250k odometer.. Na inapull kama train ya umeme..!

Sure kwa Toyota hataki mbwembwe.. Ndio maana anapata shida kuuza Europe..
Air suspension kwa mazingira yetu bora kumkubali Toyota na coils zake..!
 
Wanafeli sana humo!

Yani ni sawa na kudharau tajiri eti kisa ni msukuma hajivungi ila akikaa na matajiri wenzie wachaga aonekane tajiri kweli ni mchaga tu! Yani mwenye pesa anasemwa mchaga tu wakati msukuma ana mawe pia!

Watu wanadharau Land Cruiser sababu ni Toyota ila interms of comfort haiwezi pishana na gari lolote la kisasa! Land cruiser zina Airbags, Air Suspensions na burudani zote sijui apple car play na android auto! Yani ni gari zuri kwa kweli ila watu wanaleta dharau za kishamba wakihisi Landcruiser imekakamaa kama Passo ama IST😅
Toyoda anatumia engine za BMW
 
Hahaha aisee hapana.. Interior ya LC200 ipo very outdated..!
Huwezi kusema haipishani na gari yoyote ya kisasa..!
 
Mkuu, leo unaweza nunua Samsung ya daraja la juu kabisa, na iPhone pia kwa wati mmoja, chukua iPhone ya 2.5 million na Samsung ya 2.5 million, mje muuze mwakani ndio utajua Samsung zinavyo poromoka thamani haraka ukilinganisha na iPhone. Sio napondea Samsung nimezitumia na inatumia ila ikija kwenye value iPhone kamkata gape mbali
Value for money ni iPhone sababu tayari jamaa walishajipambanua sokoni! Kuna kitu kinaitwa brand positioning ni muhimu sana kukielewa kabla hujaingia sokoni na bidhaa yako! Inaweza kukutajirisha mapema au kukunyongesha mapema sana sokoni.

Hii utaliona kwenye mifano hii miwili.

Tecno walipoingia sokoni walikuja na kujitambulisha kama simu za hali ya chini za bei nafuu na vilikuja kama vitochi! Brand ilipoenea na kukubalika wakataka wafanye product line extension waingie katika soko jipya la smartphone. Ukumbuke walishaingia sokoni na tusimu twa bei rahisi na ile hali ilishakaa vichwani mwa watanzania. So hata walipokuja kuingia katika ulimwengu wa smartphone hali ikawa vile vile😅 watu wanazizarau simu zao!

Iphone wao tokea wanaanza walijiposition kama kampuni ya kitajiri kwa watu wanaojielewa kuwaletea simu ambazo ziko highly innovative na zenye muonekano wa kitajiri sababu wali invest high in research n development! Tokea na mwanzo bei zao ziko juu tu na watu wamejengwa kiimani kuona iphone ndio finest products. Wametengeneza ecosystem ambayo wana kila kitu chao tu na iOS yao so hii ndio competitive advantage walionayo from start to date! Apple anaweza tengeneza cheap phone ila ikauzwa ghali tu kuliko better phones from competitors. Pricing Strategy yao ni “Profit maximization” toka wameanza.

Unapoingia kinyonge sokoni utakuwa mnyonge always watu wanajua wewe kampuni la kinyonge. Unapoingia kama tajiri jua kwamba utaendelea kwa kasi sana always jikubali jiweke juu wewe ni wa juu.

Washona suti wengi kama sutibega wamejiposition tu na kujibrand na wewe ukienda kwake utalipa suti laki 7 ila suti hio hio kwa fundi Julius anakushonea kwa laki na 20 tu! Wengine wanashonea kwa mafundi mtaani wanakuja uza kwa bei ghali! Ni kucheza na mindset tu ya mteja.
 
Hahaha aisee hapana.. Interior ya LC200 ipo very outdated..!
Huwezi kusema haipishani na gari yoyote ya kisasa..!
Amenities mzee sio dashboard! Kwani toyota kujaza vioo kwenye dashboard unadhani ni kitu kigumu sana kwake ikawe kama mercedes eqs?

Ac hupulizwi? Redio huwashi? Rear view cam huoni? Speedometers haina? Toyota anajali fx zote upate tu hanaga ku complicate mambo
 
Amenities mzee sio dashboard! Kwani toyota kujaza vioo kwenye dashboard unadhani ni kitu kigumu sana kwake ikawe kama mercedes eqs?

Ac hupulizwi? Redio huwashi? Rear view cam huoni? Speedometers haina?
Hahaha akijaza hivyo vioo tuu mwisho wa reliability yake..!
Kuna touch screen na pangusa screen..!
 
Hahaha akijaza hivyo vioo tuu mwisho wa reliability yake..!
Kuna touch screen na pangusa screen..!
Hahahaha hatakagi complications mjapani! Yani anapenda vitu viwe in its simplistic forms!
Mjerumani yeye ndio anaeovercomlicate mambo yani gari inakuwa ikiharibika kitu kimoja ni chain of problems! Sahizi gari zake kupunguza turning radius ameweka system ya tairi la nyuma linakata kona nalo😅😅😅

Usiombe uko kwenye machaka ya Kibondo huko mara timming yake imecheza 😅 utaita maji mma!
 
Back
Top Bottom