Bimmer na Landcruiser V8

Haha lazima mkubali kuwa Bimmer hajamzidi LC kwenye kila kitu. Vivyo hivyo kwa upande wa simu kuna baadhi ya android kama Samsung ambazo zimezizidi iPhone baadhi ya vitu.
Yes nakubaliana.. Kila mmoja ana strength zake.. Ila usiseme hawawezi kufananishwa..!
Ukifananisha nguvu..luxury.. Mjerumani..!
Ukija kwenye uimara.. Practical kwa hapa nyumbani TZ.. Mjapani..!
 
Mimi sio mgonjwa wa BMW au Audi ila hayo magari ni mazito bara barani yanashika road utadhani yapo kwenye reli niliwahi tembea na Q 7 moja kutoka nayo SA bara bara ya Botswana niliivulia kofia yaani ngoma haitetemeki kama imewekwa kwenye sumaku Nata, Mahalapye na pahalapye ngoma ilikua moto balaa harafu nazipita hizi zingine kama zinarudi...mimi ni mgonjwa wa Mercedes-Benz ila BM wametuzi mno sasa kufananisha na Toyota sijui ipi na hapo nimeendesha pia Porsche cayenne diesel turbo ya 2016 kutoka huko huko...
 
Huu Mkonga si ndio una 1hz? Kama ndio engine yake akae ashindane na premio kwanza
 
Nyie ndo mnadhani bimmer zote ni 3 series.

Hamjui kama kuna Bimmer zimeshapita levels za VXR.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niambie criteria uliotumia kuonesha mtu fulani anafuata mkumbo?

Kwamba mtu akienda kununua iphone 13 pro max anafuata mkumbo ila wewe unaeenda kununua S21ultra hufuati mkumbo.

Umetumia nini kujua huyo wa iphone amefuata mkumbo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishu inakuja ivi, Unanunua shock ya harrier 1.4M lakini itachukua mda mrefu zaidi mpaka kubadilisha uki compare na hio 1.3M ya X3. Unaweza kuta umebadilisha shock up mara 2 kwa X3 wakati harrier yako umebadili mara moja tu. In toyota vitu vina take time na being too abused mpaka kusumbua compared to Bimmer/Merc/Audi.

Kuhusu maintaiance bill, mi naona ukienda kwa Authorised dealer kufanya maintainance lazima tu virungu viwe vikali. Ata ukienda na carina.

Nna mdogo wangu ana altezza 3sge inamsumbua fuel pump, alinambia alienda kariakoo kwenye duka wanalouza vitu vya toyota original, akaambiwa fuel pump ni laki nane. Siwezi confirm ukweli wa bei, mana moyoni nilijisemea isijekuwa kaambiwa 80,000 huyu. Maana mi nilinunua ya kawaida (sio duka hilo ni uku visiwani) 40,000 huu ni mwaka wa nne sijapata kesi yoyote ya fuel pump.
 
Anachowazidi LC hao wengine ni reliability tu. Hamna kingine. Luxury, speed, handling, ride quality muonekano etc LC hawagusi wajerumani. Labda kwa entry model zao.
Suala sio reliability.

Yeye akivunja suspension ya LC kesho analetewa mpya anaifunga kazi inaendelea. Ila kwa Bimmer unawaza wapi utaanza nunua spare.

Ila rate ya kuharibika hayo madude ipo palepale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You couldn't identify well those vehicles mkuu,hizo labda zilikuwa ni 1hz kama ni 70 series,sidhani kama serikalini wana VDJ labda iwe mtumba hata coaster huwezi kuikuta 1hd-fte ya serikali.
 
Umemaliza na huu ndio ukweli, haitokaa Toyoda akaipiku BMW . Sema wapambe wa toyota wanakuwa wanalingamisha gari zisizo lingana mtu anakuja linganisha 3 Series na V8 Badala ya kulinganisha na BMW X5 M competition na hiyo V8 zao
Kama ishu ni reliability na durability gari ya kufa na kuzikana, Toyota yupo juu tena mbali sana mbele ya germans.

Kama ishu ni muonekano mzuri, features nyingi, luxury, modern technology, apo toyota sio uwanja wake ata kidogo.
 
Kama ishu ni reliability na durability gari ya kufa na kuzikana, Toyota yupo juu tena mbali sana mbele ya germans.

Kama ishu ni muonekano mzuri, features nyingi, luxury, modern technology, apo toyota sio uwanja wake ata kidogo.
German ana vingi zaidi kuliko Mjapan..
 
You couldn't identify well those vehicles mkuu,hizo labda zilikuwa ni 1hz kama ni 70 series,sidhani kama serikalini wana VDJ labda iwe mtumba hata coaster huwezi kuikuta 1hd-fte ya serikali.
Hiyo private inaweza kuwa VDJ..
Yeye bado anayo advantage..
1.1VD kwenye VDJ imekuwa de-tuned..
2.Dashboard inalimit 200kph
3.Center of gravity ipo juu kulinganisha na Xtrail..!
 
German ana vingi zaidi kuliko Mjapan..
sikatai kuwa ana vingi, na nimevitaja hapo baadhi. Ila Reliability na durability anawaburuza wenzake. Yeye kama alikuwa na tech ambayo alitumia miaka 90 na ikawa inafanya kazi vizuri, basi kwenye gari la 2021 anaweza aktumia tech hio hio. Toyota kama toyota hazishindani na german cars kwa izo sifa nyingine, huko kawaekea LEXUS. Yeye gari zake zikutoe point A to B tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…