Bimmer na Landcruiser V8

Haha lazima mkubali kuwa Bimmer hajamzidi LC kwenye kila kitu. Vivyo hivyo kwa upande wa simu kuna baadhi ya android kama Samsung ambazo zimezizidi iPhone baadhi ya vitu.
Yes nakubaliana.. Kila mmoja ana strength zake.. Ila usiseme hawawezi kufananishwa..!
Ukifananisha nguvu..luxury.. Mjerumani..!
Ukija kwenye uimara.. Practical kwa hapa nyumbani TZ.. Mjapani..!
 
Dooh kweli mkuu mimi watumiaji wa Bimmer naonaga hawana tofauti na baadhi ya watumiaji wa iPhone yaani wote wale wale tu waliokunywa uji wa mgonjwa. Hawataki kukubali kwamba kuna sehemu wamezidiwa.

Watumiaji wengi wa iPhone huwa wanadhani hakuna simu duniani kama iPhone na wanadharau sana watumiaji wa android. Wakati android hazifanani kuna Samsung kibao tu zinakalisha hizo iPhone tena za range moja.

Nimeshangaa watu wanang'ang'ania kufananisha hadi VX.R V8 na Bimmer duuh. Kuna watu ni Bimmer maniacs na huwa wanazipondea sana gari za mjep ila wanakuambia VX.R V8 ni moto wa kuotea mbali aiseee.
Mimi sio mgonjwa wa BMW au Audi ila hayo magari ni mazito bara barani yanashika road utadhani yapo kwenye reli niliwahi tembea na Q 7 moja kutoka nayo SA bara bara ya Botswana niliivulia kofia yaani ngoma haitetemeki kama imewekwa kwenye sumaku Nata, Mahalapye na pahalapye ngoma ilikua moto balaa harafu nazipita hizi zingine kama zinarudi...mimi ni mgonjwa wa Mercedes-Benz ila BM wametuzi mno sasa kufananisha na Toyota sijui ipi na hapo nimeendesha pia Porsche cayenne diesel turbo ya 2016 kutoka huko huko...
 
Sasa wakati huo LC200 hazikuwepo.. Kabla ya LC200 Landcruiser bado zilikuwa zinasifika.. Ila hazikuwa na spidi kuliko mjerumani.. Ishu ni kwamba watu wengi hawapo exposed na magari yanayokimbia.. Ndio maana Landcruiser Mkonga imesifiwa sana kwa mwendo wakati ni gari nyepesi mnoooo kwa mjerumani..!
Huu Mkonga si ndio una 1hz? Kama ndio engine yake akae ashindane na premio kwanza
 
Dooh kweli mkuu mimi watumiaji wa Bimmer naonaga hawana tofauti na baadhi ya watumiaji wa iPhone yaani wote wale wale tu waliokunywa uji wa mgonjwa. Hawataki kukubali kwamba kuna sehemu wamezidiwa.

Watumiaji wengi wa iPhone huwa wanadhani hakuna simu duniani kama iPhone na wanadharau sana watumiaji wa android. Wakati android hazifanani kuna Samsung kibao tu zinakalisha hizo iPhone tena za range moja.

Nimeshangaa watu wanang'ang'ania kufananisha hadi VX.R V8 na Bimmer duuh. Kuna watu ni Bimmer maniacs na huwa wanazipondea sana gari za mjep ila wanakuambia VX.R V8 ni moto wa kuotea mbali aiseee.
Nyie ndo mnadhani bimmer zote ni 3 series.

Hamjui kama kuna Bimmer zimeshapita levels za VXR.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimetumia iPhone 12 Pro Max na nimetumia Samsung Galaxy S20. I'd still go for Samsung aisee and a lot of people would maana iPhone users wengi wanafuata mkumbo tu.

Na ndiyo nimeamini siyo kila mtu anayeziponda iPhone eti hana uwezo wa kununua kama wafungwa wengi wa iPhone mnavyodanganyana. Kuna watu wanajua kuchambua simu.
Niambie criteria uliotumia kuonesha mtu fulani anafuata mkumbo?

Kwamba mtu akienda kununua iphone 13 pro max anafuata mkumbo ila wewe unaeenda kununua S21ultra hufuati mkumbo.

Umetumia nini kujua huyo wa iphone amefuata mkumbo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shockups OG za Toyota Harrier ni 1.4M.

Shockups OG za BMW X3 ni 1.3M.

Hizo ni shockups tu.

Set 1 ya taa za LC200 ni 1.2M.

Nenda huko Nduvini na garage za Toyota uzione hizo LC zilivyopaki.

Nilishawahi ona bill ya maintanance ya LC200 imefika 6M.

Wengi tunanunua vitu used tandale tunaona toyota ni nyepesi kuzimantain ila likija suala la kununua spare OG, tutahamia bajaj wote.

Angalia watu tunavyolia na magari kama Subaru, Mazda, Nissan n.k kwasababu hawana mambo ya kuungaunga.
Ishu inakuja ivi, Unanunua shock ya harrier 1.4M lakini itachukua mda mrefu zaidi mpaka kubadilisha uki compare na hio 1.3M ya X3. Unaweza kuta umebadilisha shock up mara 2 kwa X3 wakati harrier yako umebadili mara moja tu. In toyota vitu vina take time na being too abused mpaka kusumbua compared to Bimmer/Merc/Audi.

Kuhusu maintaiance bill, mi naona ukienda kwa Authorised dealer kufanya maintainance lazima tu virungu viwe vikali. Ata ukienda na carina.

Nna mdogo wangu ana altezza 3sge inamsumbua fuel pump, alinambia alienda kariakoo kwenye duka wanalouza vitu vya toyota original, akaambiwa fuel pump ni laki nane. Siwezi confirm ukweli wa bei, mana moyoni nilijisemea isijekuwa kaambiwa 80,000 huyu. Maana mi nilinunua ya kawaida (sio duka hilo ni uku visiwani) 40,000 huu ni mwaka wa nne sijapata kesi yoyote ya fuel pump.
 
Anachowazidi LC hao wengine ni reliability tu. Hamna kingine. Luxury, speed, handling, ride quality muonekano etc LC hawagusi wajerumani. Labda kwa entry model zao.
Suala sio reliability.

Yeye akivunja suspension ya LC kesho analetewa mpya anaifunga kazi inaendelea. Ila kwa Bimmer unawaza wapi utaanza nunua spare.

Ila rate ya kuharibika hayo madude ipo palepale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya yamenisibu, juzi kati nilikuwa na safari ya dar-dom aisee, nilitembea, gari(xtrail) ina gia 6, speed 220km/hr, mpaka nafika dom sikumbuki km kuna gari ilinikata nikiwa njiani. Nilikutana na landcruiser 70 series(VDJ76) mbili, moja STK, nyingine ya mtu binafsi(DPA/K) nadhani walibaki wanajiuliza huko.

Ila nimefika dom, juzi nafanya service nigeuze mambo mengi, ukizingatia wakati wa kuja sikufanya service mbona nimejuta, hapa nina mpango wa kurudi mdogo mdogo, nikitembea mwendo mkali basi ni 120 hivi, tena paliponyooka(maana kuna vipande mguu unasaliti akili)
You couldn't identify well those vehicles mkuu,hizo labda zilikuwa ni 1hz kama ni 70 series,sidhani kama serikalini wana VDJ labda iwe mtumba hata coaster huwezi kuikuta 1hd-fte ya serikali.
 
Umemaliza na huu ndio ukweli, haitokaa Toyoda akaipiku BMW . Sema wapambe wa toyota wanakuwa wanalingamisha gari zisizo lingana mtu anakuja linganisha 3 Series na V8 Badala ya kulinganisha na BMW X5 M competition na hiyo V8 zao
Kama ishu ni reliability na durability gari ya kufa na kuzikana, Toyota yupo juu tena mbali sana mbele ya germans.

Kama ishu ni muonekano mzuri, features nyingi, luxury, modern technology, apo toyota sio uwanja wake ata kidogo.
 
You couldn't identify well those vehicles mkuu,hizo labda zilikuwa ni 1hz kama ni 70 series,sidhani kama serikalini wana VDJ labda iwe mtumba hata coaster huwezi kuikuta 1hd-fte ya serikali.
Hiyo private inaweza kuwa VDJ..
Yeye bado anayo advantage..
1.1VD kwenye VDJ imekuwa de-tuned..
2.Dashboard inalimit 200kph
3.Center of gravity ipo juu kulinganisha na Xtrail..!
 
German ana vingi zaidi kuliko Mjapan..
sikatai kuwa ana vingi, na nimevitaja hapo baadhi. Ila Reliability na durability anawaburuza wenzake. Yeye kama alikuwa na tech ambayo alitumia miaka 90 na ikawa inafanya kazi vizuri, basi kwenye gari la 2021 anaweza aktumia tech hio hio. Toyota kama toyota hazishindani na german cars kwa izo sifa nyingine, huko kawaekea LEXUS. Yeye gari zake zikutoe point A to B tu
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom