Bila waraka wa serikali wananchi wataendelea kupata shida TRA

Bila waraka wa serikali wananchi wataendelea kupata shida TRA

Wakiingia kwa dola hawataweza kuona kwani issue kwao siyo kuwapigania wananchi bali ni dola, na dola unajua iko pale kunufaisha wanayoiendesha. Wabunge wa aina hii wakishapata kula yao wanaridhika kwani hawana woga wa kuondolewa hata kama hawasimami na wanachi. Wanajua uchaguzi ukija dola itawalinda.
Kila atakaelia atabembelezwa basi Nchi haitatawalika.
 
Jiwe alikwisha muwashia taa nyekundu kwani alikwisha muona kuwa sio mtendaji mzuri.
Samia amerithi bomu sidhani kama ana msaada sana kwake! He has no loyalty to Samia, he is just a pretender. She could as well have appointed Ndugai as her PM it would have made no difference!
If the president has not learned about the caliber of her cabinet ministers from the Kariakoo meeting, then we are heading to disaster . Mama it is time you cracked the whip as tomorrow never comes.
Mkuu hivi majaliwa anatumwa na nani kuyasema yale? Au kajituma??
 
Kikao cha wafanyabiashara wa Kariakoo , wawakilishi mikoani na waziri mkuu kimeibua uozo na mengine mazito na magumu wanayopotia wafanyabiashara wa Tanzania.. Kikao kimeisha salama kwa kukubalika kwa hoja karibia zote zilizoibuliwa na wafanyabiashara.. Furaha imetamalaki wazi kwenye nyuso zao.. Lakini...

1. Wasiwaamini sana wanasiasa akiwemo waziri mkuu.. Wanasiasa wana maneno matamu mno yenye suluhu ya muda mfupi
2. Mamlaka ya mapato inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na miongozo ya serikali kupitia waraka kwenye kila jambo.. Hivyo mteja anapobishiwa na ofisa mapato, afisa huyo analindwa na hiyo sheria bila kujali uzuri ama ubaya wake

Kamati iliyoundwa ihakikishe mapendekezo yote na maamuzi mapya yatakayotolewa yanarasimishwa na kutolewa kama waraka wa serikali kwenye gazeti la serikali.. Hii itasaidia pande zote mbili

Mikwara ya waziri mkuu itasaidia kwa muda tuu.. Litakapokuja kutokea tatizo kubwa mamlaka ya mapato itasimamia sheria na mwananchi atakosa haki kwakuwa hana chochote cha kuthibitisha
Huu ujinga wa kauli ya Rais, Makamu wa Rais, Waziri mkuu ni sheria waachane nazo
 
Seriously Hata ukimloga mtu hapo kuna ubaya gani? Nini chanzo?? Mbona mimi sijawafanyia ubaya? Mbona mimi sio adui yenu?
kwenye stori yake kuna sehemu kasema mmoja wa waliohusika katika hilo sakata keshatangulia kunako kurest in peace. Huwezi juwa kama kuna shughuli ilifanyika na wazee.
 
Nakumbuka Jiwe aliwahi toa amri ya kwamba eti Wakulima.wasibugudhiwe Kwa kusafirisha mzigo usiosidi tani 1 lakini Kwa taarifa yenu maofisa wa Halmashauri waliendelea kutoza Kodi kama kawaida na ukitoka hayo maelezo wanasema tunaomba waraka uliobadiki sheria..

Kwa hiyo TRA hawasimamii matamko ya Kisiasa Bali waraka maana wasipofanya hivyo watakiuka sheria na watakwamisha malengo ya Bajeti..

Na mwisho nimeona mfanyabishara anasema Mwigulu kwenye Kamatia anawa bypass lakini mwisho wa siku Bunge mbona Huwa Hali block sheria au mapendekezo mabaya? Hao wabunge wanajua wanachokifanya huko Bungeni kweli?

Maana Kwa dhana ya uwepo wa Bunge nimkudhibiti Nguvu ya Serikali Kwa maslahi ya Umma.
Kwa hiyo TRA hawasimamii matamko ya Kisiasa Bali waraka maana wasipofanya hivyo watakiuka sheria na watakwamisha malengo ya Bajeti..[emoji817][emoji818]
 
Kuna laana tumetupiwa sio bure! Lilipoingizwa kwenye mnada nikafanyiwa fitina likanunuliwa na watu wengine kisha nao wakataka waniuzie kwa milion kumi
Yaani Naona walitaka kukuonyeshea kuwa wanacheza na sheria Kama vile wanavyotaka ama wanavyopenda ,kujisikia.hao tra wameshawahi mto baangu mdogo 2M mwaka 95 nikiwa mdogo mpaka leo naikumbuka Ile hali.na Ni fitina za watu wenye vijicho wanaoumia kuona wengine wakiwa juu.
Viongozi wenyewe wamewachukulia uraia nchi mbalimbali watoto wao,lisu, mbowe,mahiga, nape,jk etc watt wao wapo mambele huko. Kuna kijana wa mahiga alikuwa ana operate stocks portfolio huko uswisi alifariki alisomea hukohuk,Ila nchi Kuna siku zitachapwa hawajui wanafuga bomu. Watt wao ndio wapata zile scholarship za kwenda kusoma nchi za Mana like France, German,USA,Sweden, Switzerland,Austria,etc huku watt wa wakulima wakipelekwa Russia,Cuba China etc
 
Kama kuna watu wanalitafuna na kulikwamisha hili taifa TRA wanaongoza
 
Wee acha tuu, uchungu wa ile gari sijui utaniisha lini! Kuna wakati huyo Peter nikamwambia kwa kunizungusha huku hamuoni mnaitia serikali hasara? Maana gari inaoza hapo ilipo, ningelipa nilicho nacho nikachukua gari ingiingizia mapato kwa njia nyingi pia akajibu kuwa SERIKALI HUWA HAIPATI HASARA, sanasana nikishindwa kulipa wataligawa kwenye taasisi zenye uhitaji

Halafu huyo Peter bado ukamuachia Mungu au!?

Hata kumuadabisha kidunia tuu ilikuwa ngumu
 
Kuna hili la mtu anapoanza biashara tuu anaanza kuhesabiwa kodi, yaani mtu anakadiriwa kimaelezo.
Biashara iko mahala gani?
Unaingiza capital kiasi gani?
Unategemea kuwa na mauzo kiasi gani?
Una gari?Una familia? Una nyumba?
Blah blah blah…..

Wewe utalila kiasi kadhaa cha kodi, Bum control number hii hapa.

Mpaka leo siwaelewi TRA kwenye hili, wana theory sana.
 
Kesi yangu ilikuwa genuinely kuonewa.. Tatizo lilianzia kwenye road license.. Baada ya kumaliza kulipia kwa wakala pale TRA Mwenge jumla ya 920,000 nikatakiwa kuingia TRA ndani kuchukua sticker yangu
Kufika ndani nikaambiwa siwezi kupata sticker maana gari yangu ni ya wizi! Nikawaambia ni mwizi gani anaweza kujileta alipilie RL nikaambiwa niende makao makuu nikapate ufafanuzi
Nikaenda siku hiyohiyo pale TRA ghorofa ya kwanza, nakuambiwa si ya wizi bali walikosa neno la kuweka kwenye mfumo, bali ilisajiliwa kimagumashi hivyo nifanye utaratibu isajiliwe kihalali.. Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, Jumatatu yake nikakamatwa
Waliosajili kimaghumashi si hao hao TRA?
 
Waliosajili kimaghumashi si hao hao TRA?
Wakishakuamulia hata ufanyeje hutoboi.. Utaambiwa lete ushahidi utapeleka mpaka na wa ziada majibu yakitoka utaambiwa ni sawa lakini sisi tumeamua hivi.. Kuwashinda hawa jamaa mpaka uwe na ukwasi wa kutosha kuweka wanasheria nguli
 
Hivi mkuu unataka kuniambia yale yote yaliyosemwa jana kuanzia mama bonge na hata yule jamaa kutoka Tanga waziri mkuu hayafahamu?

Pamoja na furaha waliyoipata wananchi kwa kusikia yale ambayo wamesemewa mbele ya waziri mkuu, mkuu wa TRA, waziri wa fedha na viongozi wengine waliokuwepo pale, bado nashangaa sana kama ni kweli hawajui kuhusiana na hayo matatizo wananchi wanayoyapitia.

Pamoja na tume kuundwa, bado kulikuwa na nafasi ya hatua nyingin zaidi kuchukuliwa pale pale kabla ya mkutano ule kwisha.

Kuna shida kubwa sana kwa viongozi na mfumo tulio nao wa uongozi na ndiyo maana Maghufuli alikuwa very popular. Kwasababu ingekuwa yeye jana angekuwepo pale na amin nakwambia, kuna watu wangetumbuliwa pale pale bila huruma.

Mfumo tulionao ni mbovu sana na sheria zetu zinazotungwa na watu dizaini kina Taletale, maji marefu, musukuma na wengine wa kuongozwa bungeni kwa nguvu, hazitaleta tija kwa maendeleo ya Taifa.

Kuna watu waliongea vizuri sana, lakini kwa viongozi ni kama mbuzi anawapigia gitaa!

Kuna aliyezungumzia kuhusu sheria za mapato Tanzania hizo za TRA ambazo zinapelekea “loopholes” za rushwa.

Ndiyo maana kuna aliyesema hata watoto wao hawataki tena kuwarithisha biashara, badala yake wapate kazi TRA ambapo watendaji wake wanatajirika kwa rushwa.

Ukiwa mfanyabiashara, inataka moyo kuishi Tanzania. Sheria mbovu zilizopo, ni hasara kwa Taifa. Serikali inakosa mapato pia maana watendaji wanatumia sheria hizo mbovu kujitajirisha wao binafsi.

Kuna aliyesema kuhusu polisi anayewanyanyasa, waziri mkuu akamwambia amtaje kama mara mbili hivi lakini sidhani kama hata kuna hatua zitachukuliwa hatua zozote.

Haya matatizo ni ya kumalizwa na bungeni kupitia sheria na katiba mpya ni muhimu. Tunachukulia simple sana kwenye kuchagua wabunge kumbe hatujui hapo ndo kwenye mzizi wa fitna.
 
Mwaka 2014 October gari yangu ilikamatwa na vijana wa Majembe pale Mtaa wa Rufiji Kariakoo kwa Tuhuma ya kuingizwa nchi bila utaratibu.. Wale vijana wakaniambia wanataka milion tatu waniachie

Nikawagomea kwakuwa kesi yangu tayari nilikuwa nimeshairipoti TRA.. Lakini kuepusha usumbufu nikataka kuwapa laki tano wakagoma nikapanda dau mpaka milion MOJA wakagoma kabisa wanataka 3M

Kiongozi wao anaitwa Charles naambiwa alishakufa akasema .. Wewe fanya maskhara gari utaipoteza hii.. Na ikawa hivyo[emoji24]
Tulienda mpaka TRA makao makuu .. Nikakutana na ofisa wa investigation anaitwa Peter nikajieleza lakini akaniambia twende yard kwanza pale W9.. Tukaenda W9 nikaipaki gari hapo na kupewa kikaratasi kimeandikwa SEIZURE NOTE! nikaambiwa nikitunze vizuri maana hicho ndio mbadala wa gari

Niliipambania gari yangu kwa miaka 8 kwa maumivu na gharama kubwa na kila aina ya ushahidi lakini uamuzi wa TRA ni kwamba mimi nilikuwa na makosa hivyo nilipe jumla ya milion 12 kodi na adhabu

Mwaka jana ukatoka waraka wa kusamehewa penalty lakini nilipe kodi tu nitoe gari
Kufika kwa maofisa nikaambiwa kodi sio million sita tena bali wanapiga kws viwango vya sasa! Mmh tukavutana sana hatimaye nikawashinda lakini ikaja ishu ya storage, kuja kupiga hesabu nadaiwa milion 27 ukijumlisha na ile milion 6 inakuja jumla milion 33.. Gari iliishia kupigwa mnada kwa milion 6[emoji24]
mimi niliwahi kususa gari huko. Na gari yenyewe ilikuwa ya kijerumani. Imekaa miaka kibao huko na ikaozea huko. Ikaja kupigwa mnada kwa M2.

Wale jamaa sikuwapa hata senti tano, ***** zao. Nilipewa kikaratasi kama hicho, nikachukua boda boda nikarudi nyumbani, nikachukua ki passo changu, nikaenda kukata kiu na kupooza hasira, maisha yakaendelea.
 
Pasipo na mahusiano pamoja na mawasiliano mazuri kati ya mfanya biashara na TRA.. ngoma itaendelea kuwa nzito.. TRA bado waamini wa Theory na sio practical kibiashara.. wamejaza vijana watoka vyuo wasio jua lolote kuhusu biashara zaidi ya madesa waliyosoa vyuoni
Wale vijana malengo yao ni kuwa matajiri haraka haraka tu
 
Tatizo linaanzia mbali zaidi y’a tuonavyo…Sheria wa nazo tumia TRA ambazo ndio zina waongoza pamoja na sheria zote nchini zinatungwa bungeni na kina “ msukuma”
Kaka umenena vyema sana watu wasioweza kudadavua mambo Kwa mapana awawezi elewa hili, TRA awatungi Sheria Bali wanasimamia Sheria zilizowekwa na bunge katika ukusanyaji wa mapato Kwa Io wanachokifanya ni kile ambacho Sheria imeelekeza lakin jumba bovu wanaangushiwa wao. Wananchi wanahitaji uelewa wa ziada juu ya Sheria, miongozo na utendaji kazi mzima wa TRA.
#Mchawi wa wafanyabiashara ni serikali yenyewe inayotunga sheria
 
Mwaka 2014 October gari yangu ilikamatwa na vijana wa Majembe pale Mtaa wa Rufiji Kariakoo kwa Tuhuma ya kuingizwa nchi bila utaratibu.. Wale vijana wakaniambia wanataka milion tatu waniachie

Nikawagomea kwakuwa kesi yangu tayari nilikuwa nimeshairipoti TRA.. Lakini kuepusha usumbufu nikataka kuwapa laki tano wakagoma nikapanda dau mpaka milion MOJA wakagoma kabisa wanataka 3M

Kiongozi wao anaitwa Charles naambiwa alishakufa akasema .. Wewe fanya maskhara gari utaipoteza hii.. Na ikawa hivyo[emoji24]
Tulienda mpaka TRA makao makuu .. Nikakutana na ofisa wa investigation anaitwa Peter nikajieleza lakini akaniambia twende yard kwanza pale W9.. Tukaenda W9 nikaipaki gari hapo na kupewa kikaratasi kimeandikwa SEIZURE NOTE! nikaambiwa nikitunze vizuri maana hicho ndio mbadala wa gari

Niliipambania gari yangu kwa miaka 8 kwa maumivu na gharama kubwa na kila aina ya ushahidi lakini uamuzi wa TRA ni kwamba mimi nilikuwa na makosa hivyo nilipe jumla ya milion 12 kodi na adhabu

Mwaka jana ukatoka waraka wa kusamehewa penalty lakini nilipe kodi tu nitoe gari
Kufika kwa maofisa nikaambiwa kodi sio million sita tena bali wanapiga kws viwango vya sasa! Mmh tukavutana sana hatimaye nikawashinda lakini ikaja ishu ya storage, kuja kupiga hesabu nadaiwa milion 27 ukijumlisha na ile milion 6 inakuja jumla milion 33.. Gari iliishia kupigwa mnada kwa milion 6[emoji24]
Duhhh...pole Sana
 
Back
Top Bottom