Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Mbona unaniacha kwenye mataa tena mkuu? wewe ndio umekuja kusema Qur'an inasema jua linazama kwenye matope,yani jua likizama kumbe huwa linazama kwenye matope hivyo ndio Qur'an inavyofundisha. Sasa nimetaka ufafanuzi juu ya hilo matokeo yake unasema hayakuhusu wakati wewe ndio umeleta suala hili.

Usibanie elimu mkuuu,nijuze hayo matope ya wapi na hayakauki?
Mkuu mie nimemuelewa nyabhingi alikuwa anaongea sarcastically kuhusu Quran ila haimaanishi anasupport maneno hayo aliyoquote
 
vitabu vipi vya kipagani?tambua vipo vitabu vingi na magombo mbalimbali ya manabii wa kale vimepotea,ving havikujumuishwa kwenye bibilia,kumbuka bibili ni mkusnyiko wa vitabu mbalimbali vilivvyoandikwa na watu tofauttoafauti kwa vpindi tofauti vya karne.
Vya kipagani ni kama Book of jasher na book of Enock ambavyo vinakinzana na Biblia zaidi ya 70% ila bado vimekuwa Quoted na Biblia ndio maana najiuliza kivp Biblia itumie vitabu ambavyo viko termed kama vya kipagani kwa kupachikwa jina la Pseudepigraphi?? Na kama wao waliquote je na sisi tukiviquote tutakuwa tunakosea??

Hapo mkuu nimeona umesema kuna maandiko ya manabii "yalipotea" sasa najiuliza kivp maneno ya Mungu yanaweza kupotea?? Na kama yalipotea ina maana Biblia haipo kamili sababu kuna baadhi ya vitabu vilipotea??

Ok unasema pia kuwa sio vya kipagani.... Je Book of jasher na Book of Enock ni vitabu halali ingawa vinapingana na Biblia??? Na kama sio halali je sio sawa kuviita vya kipagani (Obviously maneno ya Mungu hayawezi kukinzana )

Tuwekane sawa hapo
 
Kitu kimoja ambacho najaribu kuwafunda watu wa kidini kila siku na kuwaasa

Ni kwamba mjifunze kumpenda shetani mliye simuliwa toka Enzi za utoto wenu kuwa ni adui yenu

Mkiweza hilo mtabadilika

Na ndiyo Tuzo ya kuwa Anunaki aliyekamilika

Mkuu kama ungekuwa unacheza Barcelona ningekuita Messi
 
zitto junior ,Kupitia kwa nondo za baadhi ya wadau wenye elimu ya dini hasa ya ukristo kwa jinsi nilivyowasoma,
Majibu yanaweza yakawa kama hivi
Mosi tambua biblia takatifu ni kwa ajili ya kumuunganisha mwanadamu na muumba wake,ni kwa ajili ya kumuongoza mwanadamu asiende motoni.
Ni kitabu kilichokamilika kwa kazi hiyo tajwa.
Maelezo machache ya ziada kwenye vitabu hivyo unavyovitaja ambavyo vipo nje ya Biblia haifanyi biblia kuwa haijakamilika.
Wataalam wamesema muunganiko wa maandiko ya ndani ya biblia umeongozwa na roho ya Mungu na ndo maana imekamilika.
Hivyo vitabu vingine kutokana na tafiti zimeshindwa kujithibitisha kuwa kweli,na hapa ieleweke sio lazima kitabu kizima kiwe hakijajajithibitisha bali chapter kadhaa ndani ya vitabu hivyo.Kwa hiyo kuna uwezekano wa baadhi ya chapters kulingana na tafiti za kale zilizothibitisha kuwa haya na yale kweli yametokea na hivyo sio vibaya baadhi ya chapters kukaririwa ndani ya biblia takatifu.
Ni hayo tu.
 
Mkuu, kwenye hizo reference ulizotoa, wapi umeona "VITABU VYA KIPAGANI!?" Katika kitabu cha Yohana (Injili) kuna sehemu imeandikwa hivi, "..yapo na mambo mengine ambayo YEsu aliyafanya na hayakuandikwa katika kitabu hiki, laity kama kila kitu kingeandikwa then vitabu visingetosha..." NAtaka kuonesha, yes yapo mambo mengi tu ya manabii, wafalme, makuhani nk ambayo yalifanywa, kutenda au hata kufundisha lakini hayana reference ndani ya Biblia, swali langu, hapo vitabu vya kipagani we umetoa wapi!?
Kwa mfano leo mtu akiwa anafundisha kanisani, aka fanya reference kwenye nyimbo za tenzi za rohoni, injli, mwimbieni Bwana, nyimbo za wokovu nk. Hizo reference sio za Kibiblia but again huwezi kusema hivyo vitabu ni vya kipagani! Hebu njoo tena na uthibitisho wako kwamba Biblia imeruhusu kufanya reference kwenye vitabu vya kipagani, otherwise mi umeniacha njiapanda, sijaelewa!
Ok Yuda kafanya reference ya kitabu cha Henoko ambacho nimeshakiweka humu JF kinapingana kabisa na baadhi ya mafundisho ya Biblia mfano wakati Biblia inasema dhambi ndio zilisababisha gharika yeye Henoko anasema malaika walivyozini na wanadamu ndio ikasababisha gharika maana Mungu alikwazika pia Biblia inasema Nuhu ndio alijenga safina ila Henoko anasema malaika ndio waliojenga hiyo meli..... lakini licha ya ukinzano huu kuna mistari zaidi ya 12 agano jipya ambayo ni direct copy kutoka book of Enoch ndio sasa nauliza je kitabu cha Henoko sio cha kipagani?? Na kama sio cha kipagani nani mkweli kati ya Henoko au Biblia??? Nisaidie hapa

2. Yoshua na timotheo tunaona wanavitaja kabisa na kunakili kitabu cha Yasheri..... Sasa kitabu cha Yasheri sura ya 81 kinasema pharaoh hakufa kwenye bahari ya shamu na alisalia peke yake na akamfuata Mungu wa Israel lakini ukisoma zaburi inasema Pharaoh aliteketezwa na jeshi lake baharini..... Sasa je Yasheri kukinzana na Biblia ni kosa nikikiita cha kipagani?? maana wote tunaamini maneno ya Mungu hayakinzani ikimaanisha Yasheri sio maneno ya Mungu automatically kinakuwa cha KIPAGANI si ndio maana yake

Sasa baada ya kukubaliana kuwa ni vya KIPAGANI je ni halali Biblia kuvinakili vitabu hivi ili kujengea hoja?? Na kama ni halali je na mimi nikivinakili kujengea hoja ntakuwa nakosea

Hapa ndio mzizi wa hoja wakuu
 
ok,nafikiri ungewauliza waislam au allah kuhusu hilo sababu kisayansi jua kuzama kwenye bwawa la maji ya mmatope ni upuuzi usiomithilika
Niwaulize nani tena wakati wewe ndio umetuambia kuwa Qur'an inasema jua linazama kwenye matope,maana sijawahi kusikia waislamu wakifundishana kuwa jua linazama kwenye matope.
 
Hebu jiridhishe uhusiano wa hao watu na Mungu ndio utajua maandishi yao yanaweza kua na SIFA ya KIPAGANI! Hao ni miongoni mwa manabii wa Mungu, mfano huyo Nathan ndiye aliyekwenda kumuonya mfalme Daudi baada ya kuanguka dhambini kwa kuzini na mke wa mmoja ya askari wake. Au labda neon UPAGANI ndio labda hatuelewani maana yake.
Hivyo vitabu nilivyoweka hapo hata kimoja umesoma?? Je ukikuta kinakinzana na Biblia uko tayari kuwajibika??

Ingia humu uvipakue alafu ukisoma ndio urudi kusema kama vina uhalali au lah... Utakaposoma kuwa Nuhu hakujenga safina wala Paharaoh hakufa majini na gharika halikuja sababu ya dhambi ilihali Biblia haisemi hivyo nafikiri ndio utanielewa kwanini naviita vya kipagani!!

Pseudepigrapha, Apocrypha and Sacred Writings
 
Labda angefanya hivi, aeleze kwenye hivyo vitabu vinavyo elezwa hapo sehemu inayosomeka kwamba Daudi aliwahi kuishi kindoa na mtu wa jinsia yake (ya kiume)
Mimi hiyo hakuwa hoja yangu na wala sijajikita huko bali nilichokerwa ni mtoa mada kumkataza mtu asitoe reference nje ya Biblia kuhusu tuhuma zake kwa Daudi hivyo nimeleta uzi huu maalum kabisa tujadili kwamba kivp waandishi wa Biblia wamequote vitabu nje ya Biblia tena wakaenda mbali zaidi kusema STORI YOTE MWANZO MWISHO YA DAUDI ipo kwenye vitabu A B C..... Ilihali leo hii mtu akitaka kujengea hoja kupitia vitabu hivyo mnapinga

Huu ndio mzizi wa mjadala hayo ya tuhuma nafikiri alishatoa maelezo vizuri sana tukamuelewa mkuu Elungata kwenye uzi nilioquote.

Ni hayo tu
 
Sasa watunge maneno yote yale na kujaza kitabu kisa tu wadai ni maneno ya Mungu? Wewe hilo linakuangia akilini?
Mkuu Quran na Talmud na Biblia vyote vinadai ni maneno ya Mungu lakini ukisoma unakuta vinapingana sasa cha kujiuliza je Mungu anaweza kujipinga mwenyewe?? Na kama hawezi kujipinga sasa kivipi viwepo vitabu 3 vya dini kuu za Abrahamic alafu vijipinge??

Huoni hapo mmoja ndio yuko sahihi wengine wamefoji maandiko kama anavyosema mkuu nyabhingi ?? Sasa swali linabaki je ni nani huyo ambaye ndio amefoji maneno ya Mungu??
 
Sasa watunge maneno yote yale na kujaza kitabu kisa tu wadai ni maneno ya Mungu? Wewe hilo linakuangia akilini?
labda nikwambie kwamba hawakupata tabu sana,wali-plagiarize maandiko yaliyokuwepo kabla mfano maandiko ya wamisri kwenye kitabu kinachoitwa the papayrus of ani
 
Niwaulize nani tena wakati wewe ndio umetuambia kuwa Qur'an inasema jua linazama kwenye matope,maana sijawahi kusikia waislamu wakifundishana kuwa jua linazama kwenye matope.
quran 18:86
 
Mkuu Quran na Talmud na Biblia vyote vinadai ni maneno ya Mungu lakini ukisoma unakuta vinapingana sasa cha kujiuliza je Mungu anaweza kujipinga mwenyewe?? Na kama hawezi kujipinga sasa kivipi viwepo vitabu 3 vya dini kuu za Abrahamic alafu vijipinge??

Huoni hapo mmoja ndio yuko sahihi wengine wamefoji maandiko kama anavyosema mkuu nyabhingi ?? Sasa swali linabaki je ni nani huyo ambaye ndio amefoji maneno ya Mungu??
Wewe unajua kabisa kuwa kulikuwa na mitume na walikuwa na vitabu,sasa hoja ingekuwa kipi kimepotoshwa na yapi yameongezwa katika hayo mafundisho yaliyo kwenye hivyo vitabu?
 
unajitoa ufahamu sio!!!!!!!

Until, when he reached the setting of the sun, he found it setting in a spring of dark mud, and he found near it a people. Allah said,
Nimekuuliza hayo matope yapo wapi na hayajakauka? huna majibu unaniambia niwaulize waislamu,nimekwambia sijawahi kusikia waislamu wakifundishana kuwa jua huzama kwenye matope.
 
Nimekuuliza hayo matope yapo wapi na hayajakauka? huna majibu unaniambia niwaulize waislamu,nimekwambia sijawahi kusikia waislamu wakifundishana kuwa jua huzama kwenye matope.
nimerekebisha,wanasema linazama kwenye bwawa la maji
jua linazama kwenye bwawa tokea lini?
 
Mimi hiyo hakuwa hoja yangu na wala sijajikita huko bali nilichokerwa ni mtoa mada kumkataza mtu asitoe reference nje ya Biblia kuhusu tuhuma zake kwa Daudi hivyo nimeleta uzi huu maalum kabisa tujadili kwamba kivp waandishi wa Biblia wamequote vitabu nje ya Biblia tena wakaenda mbali zaidi kusema STORI YOTE MWANZO MWISHO YA DAUDI ipo kwenye vitabu A B C..... Ilihali leo hii mtu akitaka kujengea hoja kupitia vitabu hivyo mnapinga

Huu ndio mzizi wa mjadala hayo ya tuhuma nafikiri alishatoa maelezo vizuri sana tukamuelewa mkuu Elungata kwenye uzi nilioquote.

Ni hayo tu
Upo sawa kabisa but ungerekebisha hilo neon,UPAGANI cause reference uliofanyia kwenye vitabu vyako nje ya Biblia bado waandishi wake ni watu wa Mungu, Manabii so vitabu vyao haviwezi kua vya KIPAGANI, hiyo ni kwa mtazamo wangu, sina hakika na hao wengine
 
Back
Top Bottom