Biblia ina makosa? Nachanganyikiwa!

Biblia ina makosa? Nachanganyikiwa!

2samwel 24:1 vs 1nyakati21:1

maandiko haya hayakinzani, bali yanazungumzia tukio lilelile kutoka pembe mbili tofauti za kiteolojia (mchango wa Mungu kama Mwenye Mamlaka Makuu na Shetani kama mtenda uovu).
Ili kuelewa vyema kwa nini vifungu hivi vinakamilishana badala ya kukinzana, angalia mambo yafuatayo:
* Mamlaka Makuu ya Mungu (2 Samweli 24:1): Katika mtazamo wa Kiyahudi, Mungu ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya kila kitu. Hakuna kitu kinachotokea bila Yeye kuruhusu. Mungu alipokuwa na hasira na Israeli, aliruhusu jaribu hilo litokee ili kuleta nidhamu na hukumu.
* Chombo cha Jaribu (1 Mambo ya Nyakati 21:1): Kitabu cha Mambo ya Nyakati kinamweleza mtendaji wa moja kwa moja wa jaribu hilo, ambaye ni Shetani. Shetani ndiye aliyetumia kiburi cha Daudi na kumshawishi atekeleze wazo hilo.
* Kipengele cha Historia na Uandishi: Kitabu cha Mambo ya Nyakati kiliandikwa baadaye sana (baada ya utumwa wa Babeli), ambapo uelewa wa kiroho wa wana wa Israeli ulikuwa umepanuka zaidi kutofautisha kati ya matendo ya Mungu na ushawishi wa moja kwa moja wa Shetani.
Mfano Sawa Katika Biblia:

Hali hii inafanana sana na kisa cha Ayubu:
* Shetani ndiye aliyemtesa na kumpiga Ayubu (Ayubu 1-2).
* Lakini bado Ayubu na maandiko yanasema Mungu aliruhusu hayo yatokee kwa ajili ya kusudi fulani.
Kwa hiyo, 2 Samweli 24:1 inaonyesha sababu kuu na idhini ya Mungu, wakati 1 Mambo ya Nyakati 21:1 inaonyesha mshawishi na mtendaji wa moja kwa moja (shetani)
 
Mnahangaika sana kumtetea huyo Mungu wa kufikirika na Biblia yake ya kutungwa na wajinga wa kale.

Huyo Mungu kama yupo, aje ajitetee mwenyewe na kujieleza.

Aje ajiongelee mwenyewe na kujidhihirisha kama ana huo uwezo.

Sio ninyi mnahangaika kumtetea na kumuelezea.

Atoke huko alipo aje.
 
Usiseme maneno ya hekima mbele ya mpumbavu maana atadharau hekima ya maneno yako.

Mtumishi nakukumbusha kitabu cha mithali
 
2samwel 10:18 vs 1nyakati 19:18

maandiko haya hayakinzani bali yanatofautiana katika kile kilichofanyiwa hesabu (vitengo vya kijeshi au aina za magari).
Tofauti hii ya namba kati ya 2 Samweli 10:18 (magari 700) na 1 Mambo ya Nyakati 19:18 (magari 7,000) inafafanuliwa kwa namna kuu mbili za kiwasilisho na kitaaluma za Maandiko Matakatifu:

1. Tofauti ya Vitengo vya Kijeshi (Unit of Measurement)
* 2 Samweli 10:18 inazungumzia "magari 700" – hapa inamaanisha viwanda/vitengo vya magari ya vita (chariot divisions/squadrons). Kila kitengo kilikuwa na magari 10.

* 1 Mambo ya Nyakati 19:18 inazungumzia "magari 7,000" – hapa inataja jumla ya idadi ya askari au magari yenyewe yaliyokuwa ndani ya vile vitengo 700 (700 \times 10 = 7,000).

* Kwa mfanano wa kisasa, ni sawa na kusema "Jeshi liliharibu vikosi 10 vya vifaru" au "Jeshi liliharibu vifaru 100". Yote mawili ni ukweli mmoja uliotajwa kwa lugha tofauti za kijeshi.

2. Makosa ya Waandishi wa Zamani (Scribal Errors / Copyist Errors)
* Katika lugha ya Kiebrania cha kale, namba hazikuandikwa kwa tarakimu kama leo (700 au 7,000), bali ziliandikwa kwa kutumia herufi za alfabeti ya Kiebrania ambapo alama au kielezi kidogo tu juu ya herufi kinaweza kubadilisha thamani kutoka mia saba kwenda elfu saba.
* Waandishi (scribes) walipokuwa wakinakili vitabu hivi kwa mkono kutoka kwa vile vya asili, makosa madogo ya kiufundi (copyist errors) yalitokea kwenye namba, lakini hayaharibu au kubadilisha maana wala ukweli wa tukio lenyewe la kihistoria—kuwa Daudi alishinda vita dhidi ya Washami (Wa
ashuru).
 
Siku ya 33 nasoma hii Biblia, lakini kila nikiendelea mbele ndio kwanza nachanganyikiwa na madudu yaliyomo humu! Wakristo wote mnasema hiki kitabu kimeandikwa na watu waliyovuviwa Roho Mtakatifu.
Kama ni roho mtakatifu inakuaje ameshindwa kuandika kitabu kikanyooka.? Yani humu ndani kuna makosa kibao..

Mwanzo 22:1 inasema Mungu alimjaribu Ibrahimu amchinje Isaka. Lakini Yakobo 1:13 inakataa katakata ikisema Mungu hamjaribu mtu yeyote.

Asa tushike nini hapo? Inamaana huyo Roho mtakatifu alisahau alichoandika Mwanzo hadi akaja kujikana kwenye Yakobo? Hilo ni kosa la wazi kabisa linaloonesha jinsi kitabu hiki kilivyojaa stori tu za kutungwa na wanadamu..

Marko 10:46 inasema walipokuwa wanatoka Yeriko, alikuwepo kipofu mmoja tu kando ya njia, jina lake Bartimayo. Lakini ukifungua Mathayo 20:30, kwenye muujiza ule ule, mahali pale pale, anadai walikuwa vipofu wawili.

Kitabu cha Mungu wa kweli hakiwezi kuwa na madudu na sarakasi kama hizi. Hizi ni stori tu za kupokezana zilizotungwa bila uhakiki wowote.

Kwenye 2 Samweli 24:1, Mungu ndiye aliyemfanya Daudi kwenda kuhesabu watu wa Israeli. Lakini ukifungua 1 Mambo ya Nyakati 21:1 habari inabadilika mchana kweupe ikisema Shetani ndiye aliyesimama na kumfanya Daudi ahesabu watu.
Kwamaana hiyo huyo roho mtakatifu ni punguani sana.

Kwenye 2 Samweli 10:18 inaandikwa wazi kabisa kuwa Daudi akaua watu wa magari mia saba miongoni mwa maadui zake.

Lakini ukifungua 1 Mambo ya Nyakati 19:18, kwenye vita ile ile, mahali pale pale na maadui wale wale, idadi inapaa na kuwa magari elfu saba. Sifuri nzima ya ziada imetoka wapi? Roho wenu alikuwa amelewa kiasi gani hadi ashindwe kuhesabu namba ya magari kwenye tukio moja la kihistoria?.

Kwakweli Sarakasi hizi zinaonyesha jinsi hadithi hizi zilivyotungwa bila hata kufanyiwa uhakiki
Inajadiriwa ziko contradictions kama 700 kwenye hicho kitabu, mwisho wa siku ni wewe tu utaamua mwenyewe kusuka au kunyoa au ufunike kombe 😁
 
Biblia imeandikwa kwa mafumbo na isingeandikwa kwa mafumbo hakuna ambaye angeenda kanisani
Ufunuo 6:13 - "Nazo nyota za mbingu zikaanguka juu ya ardhi kama matunda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapotikiswa na upepo mkali."

Kuna fumbo gani hapo? maana nyota ni kubwa sana kuliko dunia, fikiria jua liangukie dunia😁
 
Pole yako

Tatizo unasoma ili uikosoe na siyo ili uielewe.

Soma kama kwamba unatafuta majibu au ukweli wa mambo.
Nimeisoma Biblia tena kuliko hata wewe.

Nimeisoma Biblia kama somo la Bible Knowledge nikiwa Seminary. Na nikapata daraja A.

Nimeisoma Biblia nakuichambua vizuri sana.

Kuna logical contradictions nyingi sana kwenye Biblia. Kitu ambacho kinatengeneza logical inconsistency.

Na taarifa zenye logical inconsistency haziwezi kuwa na ukweli.

Ukweli unataka taarifa zisizo na utata wa kimantiki, taarifa zisizo na mkanganyiko wowote ule. Ukweli unataka logical consistency.

Hiyo Biblia imejaa logical contradictions za kutosha.

Na baadhi yake hizi hapa...👇
downloadfile-7.jpg
 
Mnahangaika sana kumtetea huyo Mungu wa kufikirika na Biblia yake ya kutungwa na wajinga wa kale.

Huyo Mungu kama yupo, aje ajitetee mwenyewe na kujieleza.

Aje ajiongelee mwenyewe na kujidhihirisha kama ana huo uwezo.

Sio ninyi mnahangaika kumtetea na kumuelezea.

Atoke huko alipo aje.

Nakuombea sana ndugu Mungu akupe neema ya kulijua neno lake, very soon atashuka mwenyewe kujitetea kama alivyofanya kwa Eliya..

kasome 1wafalme 18:20-40 uone jinsi Mungu alijitetea kwa miungu ya baali
 
Biblia uwezi ukaelewa kama huna hekima au huna Roho mtakatifu

Uwezi ukaielewa.

Sema wewe ndiyo unaelewa Madudu ila yenyewe iko sawa kabisa.
Ni roho Mtakatifu ndiye aliwaambia Wasabato wasali Jumamosi, wasile kitimoto na Kambale halafu akawaambia wengine wasali Jumapili na wale tu kitimoto na Kambale?
Roho Mtakatifu ndiye aliwaambia Wakatoliki pombe haina shida halafu akawaambia wengi pombe ni dhambi?
Roho Mtakatifu ndiye aliwaambia mashahidi wa Yehova mungu sio utatu halafu akawaambia wengine ni nafsi tatu??
 
Nakuombea sana ndugu Mungu akupe neema ya kulijua neno lake, very soon atashuka mwenyewe kujitetea kama alivyofanya kwa Eliya..

kasome 1wafalme 18:20-40 uone jinsi Mungu alijitetea kwa miungu ya baali
Ashuke na sasa hivi kama ana huo uwezo.

Mambo ya kusema "very soon" halafu hashuki. Sitaki.

Ashuke sasa hiviiiii!!!

Kama kweli alimshukia huyo Elia , Na sasa hivi aje anishukie Infropreneur.

Kama huyo Mungu yupo, Aje ajitetee hapa kwa Infropreneur.

Namsubiri.
 
Naomba niende nje ya hoja.

Biblia ni kitabu cha utamaduni wa watu wa ulaya kilicholetwa kuutoa utamaduni wa kiafrika na kuuingiza wa kizungu ili kurahisisha utawala wa sheria kwa mkoloni, (usiue, usiseme uongo, usidhini, usitamani cha mwenzako n.k) .

Baada ya ukoloni kuisha huu utamaduni umeendelea kiwepo hivyo basi kuwa makini

All in all biblia sio kitabu kibaya
Agano la kale ni kitabu cha utamaduni wa Kiyahudi ila ukweli wazungu walijuwa kuitumia Biblia vizuri kwa ujumla wake kwa manufaa yao.
 
Nimeisoma Biblia tena kuliko hata wewe.

Nimeisoma Biblia kama somo la Bible Knowledge nikiwa Seminary. Na nikapata daraja A.

Nimeisoma Biblia nakuichambua vizuri sana.

Kuna logical contradictions nyingi sana kwenye Biblia. Kitu ambacho kinatengeneza logical inconsistency.

Na taarifa zenye logical inconsistency haziwezi kuwa na ukweli.

Ukweli unataka taarifa zisizo na utata wa kimantiki, taarifa zisizo na mkanganyiko wowote ule. Ukweli unataka logical consistency.

Hiyo Biblia imejaa logical contradictions za kutosha.

Na baadhi yake hizi hapa...👇View attachment 3691284
unaonekana upo vzuri kufatilia habari za Mungu ila shetani anakupoteza mwelekeo ili uasi..anakuwekea akilini mwako mawazo mabaya ya kulikosoa neno la Mungu na ww kwa sababu unaenenda kimwili(unatumia akili) badala ya kuongozwa na Roho mtakatifu basi unaishia kukosoa tu

ebu fanya maamuzi leo, muombe Mungu akujalie uwezo wa kujazwa Roho mtakatifu uone kama utakua na huo uwezo wa kuyaona hayo makosa unayoyaona kwa akili zako
 
2samwel 10:18 vs 1nyakati 19:18

maandiko haya hayakinzani bali yanatofautiana katika kile kilichofanyiwa hesabu (vitengo vya kijeshi au aina za magari).
Tofauti hii ya namba kati ya 2 Samweli 10:18 (magari 700) na 1 Mambo ya Nyakati 19:18 (magari 7,000) inafafanuliwa kwa namna kuu mbili za kiwasilisho na kitaaluma za Maandiko Matakatifu:

1. Tofauti ya Vitengo vya Kijeshi (Unit of Measurement)
* 2 Samweli 10:18 inazungumzia "magari 700" – hapa inamaanisha viwanda/vitengo vya magari ya vita (chariot divisions/squadrons). Kila kitengo kilikuwa na magari 10.

* 1 Mambo ya Nyakati 19:18 inazungumzia "magari 7,000" – hapa inataja jumla ya idadi ya askari au magari yenyewe yaliyokuwa ndani ya vile vitengo 700 (700 \times 10 = 7,000).

* Kwa mfanano wa kisasa, ni sawa na kusema "Jeshi liliharibu vikosi 10 vya vifaru" au "Jeshi liliharibu vifaru 100". Yote mawili ni ukweli mmoja uliotajwa kwa lugha tofauti za kijeshi.

2. Makosa ya Waandishi wa Zamani (Scribal Errors / Copyist Errors)
* Katika lugha ya Kiebrania cha kale, namba hazikuandikwa kwa tarakimu kama leo (700 au 7,000), bali ziliandikwa kwa kutumia herufi za alfabeti ya Kiebrania ambapo alama au kielezi kidogo tu juu ya herufi kinaweza kubadilisha thamani kutoka mia saba kwenda elfu saba.
* Waandishi (scribes) walipokuwa wakinakili vitabu hivi kwa mkono kutoka kwa vile vya asili, makosa madogo ya kiufundi (copyist errors) yalitokea kwenye namba, lakini hayaharibu au kubadilisha maana wala ukweli wa tukio lenyewe la kihistoria—kuwa Daudi alishinda vita dhidi ya Washami (Wa
ashuru).
Hivi Joshua aliwezaje kusimamisha Jua ?😁
 
sasa kitabu ambacho kinatakiwa kiwakomboe watu ili wasiende kuchomwa moto kwa nini kiandikwe kwa mafumbo ili watu wapate shida kuelewa na munasema Mungu ana upendo?
Usiogope,
Kwenye mafundisho ya Kiyahudi hata hakuna moto wa milele (Jehanamu). Hilo ni fundisho lilitongenezwa na Wakristo.
 
unaonekana upo vzuri kufatilia habari za Mungu ila shetani anakupoteza mwelekeo ili uasi..anakuwekea akilini mwako mawazo mabaya ya kulikosoa neno la Mungu na ww kwa sababu unaenenda kimwili(unatumia akili) badala ya kuongozwa na Roho mtakatifu basi unaishia kukosoa tu

ebu fanya maamuzi leo, muombe Mungu akujalie uwezo wa kujazwa Roho mtakatifu uone kama utakua na huo uwezo wa kuyaona hayo makosa unayoyaona kwa akili zako
Shetani alitoa wapi uwezo wa kupoteza watu?

Shetani alipata wapi uwezo wa kuasi?

Nani alimpa mamlaka Shetani ya kupotezea watu uelekeo?

Huyo Mungu HAKUJUA kwamba Shetani atakuja kuasi amdhibiti mapema na kumzuia?
 
Ufunuo 6:13 - "Nazo nyota za mbingu zikaanguka juu ya ardhi kama matunda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapotikiswa na upepo mkali."

Kuna fumbo gani hapo? maana nyota ni kubwa sana kuliko dunia, fikiria jua liangukie dunia😁
Huenda sio aya zote zenye mafumbo fafanua zile aya alizoandika mwenye Uzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom