Jitu la kienyeji
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,432
- 7,965
Siku ya 33 nasoma hii Biblia, lakini kila nikiendelea mbele ndio kwanza nachanganyikiwa na madudu yaliyomo humu! Wakristo wote mnasema hiki kitabu kimeandikwa na watu waliyovuviwa Roho Mtakatifu.
Kama ni roho mtakatifu inakuaje ameshindwa kuandika kitabu kikanyooka.? Yani humu ndani kuna makosa kibao..
Mwanzo 22:1 inasema Mungu alimjaribu Ibrahimu amchinje Isaka. Lakini Yakobo 1:13 inakataa katakata ikisema Mungu hamjaribu mtu yeyote.
Asa tushike nini hapo? Inamaana huyo Roho mtakatifu alisahau alichoandika Mwanzo hadi akaja kujikana kwenye Yakobo? Hilo ni kosa la wazi kabisa linaloonesha jinsi kitabu hiki kilivyojaa stori tu za kutungwa na wanadamu..
Marko 10:46 inasema walipokuwa wanatoka Yeriko, alikuwepo kipofu mmoja tu kando ya njia, jina lake Bartimayo. Lakini ukifungua Mathayo 20:30, kwenye muujiza ule ule, mahali pale pale, anadai walikuwa vipofu wawili.
Kitabu cha Mungu wa kweli hakiwezi kuwa na madudu na sarakasi kama hizi. Hizi ni stori tu za kupokezana zilizotungwa bila uhakiki wowote.
Kwenye 2 Samweli 24:1, Mungu ndiye aliyemfanya Daudi kwenda kuhesabu watu wa Israeli. Lakini ukifungua 1 Mambo ya Nyakati 21:1 habari inabadilika mchana kweupe ikisema Shetani ndiye aliyesimama na kumfanya Daudi ahesabu watu.
Kwamaana hiyo huyo roho mtakatifu ni punguani sana.
Kwenye 2 Samweli 10:18 inaandikwa wazi kabisa kuwa Daudi akaua watu wa magari mia saba miongoni mwa maadui zake.
Lakini ukifungua 1 Mambo ya Nyakati 19:18, kwenye vita ile ile, mahali pale pale na maadui wale wale, idadi inapaa na kuwa magari elfu saba. Sifuri nzima ya ziada imetoka wapi? Roho wenu alikuwa amelewa kiasi gani hadi ashindwe kuhesabu namba ya magari kwenye tukio moja la kihistoria?.
Kwakweli Sarakasi hizi zinaonyesha jinsi hadithi hizi zilivyotungwa bila hata kufanyiwa uhakiki