Bibi wa bwana harusi kuhudhuria harusi ya mjukuu wake, hii imekaaje?

Bibi wa bwana harusi kuhudhuria harusi ya mjukuu wake, hii imekaaje?

Ziroseventytwo

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
9,446
Reaction score
17,927
Kwa mila na destuti za Kichagga, bibi wa bwana harusi haruhusiwi kuhudhuria harusi ya mjukuu wake. Hii Tabia imeleta mgogoro kwenye familia moja hapa Moshi baada ya bibi mmoja kulazimisha kuhudhuria harusi ya mjukuu wake itakayofanyika Dar es Salaam tarehe 30/05/2015.

Bwana harusi mtarajiwa ambaye alilelewa na bibi yake mpaka alipomaliza kidato cha nne, ametishia kuahirisha harusi hiyo kama bibi huyo hataruhusiwa kuhudhuria kwenye harusi.

"Oteh" nkiwicho, hapana ni vibaya. Bibi kuhudhuria harusi! Hapana. Yeye ashiriki akiwa nyumbani, apewe vinywaji na vyakula ale na anywe na majirani na marafiki zake. Huo ndio utaratibu. Lakini bibi huyo yeye anasema kwa nini asipewe nafasi hiyo kama mlezi kwa kuwa ni kweli alimlea? Swala hili litaamuliwa kesho kutwa na wazee wa mila na viongozi wa dini.

Hili limekaaje?
 
Huyo anayeoa nguvu anazo maana wachaga hamjiwezi siku hizi
 
Wachagga hamuishiwi vijimambo..Juzi kati kati mungu aliharibiwa then ikafuatiwa na kukodi wanaume toka Kenya leo mmekuja na stori za miiko aisee mwaka huu wa uchaguzi tutaona mengi
 
Ebu tutafsilie vizuri kwa mila na desturi zenu kuna uharamu gani kwa bibi wa bwana harusi kuudhuria harusi ya mjukuu wake?
 
Ebu tutafsilie vizuri kwa mila na desturi zenu kuna uharamu gani kwa bibi wa bwana harusi kuudhuria harusi ya mjukuu wake?

Mimi hili sakata linanishangaza pia. Nisaidie wewe kwa uzoefu wako uliwahi kuudhuria harusi ukamwona bibi/babu wa bwana/bib harusi? Mimi sikumbuki kuona hii kitu.
 
Hakuna ubaya kuhudhuria,Mila na desturi zingine zisokua na mashiko tuachane nazo,hongera kwa huyo kijana kuweka msimamo bibi ahudhurie,anajua vile huyo bibi alihangaika sababu yake,so aachwe na maamuzi yake.
 
Mwacheni Bibi wa watu ahudhurie Harusi ya Mjukuu wake
Mlikuwa wapi kumlea huyo mtoto mpaka leo mnamkaeaza Bibi yake
km na mm ndio mhusika sitakubali sherehe bila kumuona Nyanya yangu
 
Mimi hili sakata linanishangaza pia. Nisaidie wewe kwa uzoefu wako uliwahi kuudhuria harusi ukamwona bibi/babu wa bwana/bib harusi? Mimi sikumbuki kuona hii kitu.

Kwa sisi wamakonde hakuna shida yoyote kwa bibi au babu wa bwana harusi kuudhuria harusi ya mjukuu wao, isipokuwa tu tuliowengi mijini wazazi wetu na mabibi zetu wako vijijini, sasa saa zingine inakuwa ngumu kuwasafilisha wazazi wako wote wakati mmoja kuja kuudhuria harusi, au saa zingine unakuta bibi zako na babu zako wamezeeka sana kiasi kwamba kusafiri kwao ni tatizo lingine, kuna sababu nyingi sana za mabibi kutoonekana kwenye harusi ikiwemo kifo na km zingine nilizozitaja, lakini hii ya wachaga kutooudhuria kwenye harusi za wajuu zao kuwa ni haramu inashangaza sana ni kama kuwanyanyapaa mabibi zao
 
Hii ya bibi na babu kiukweli mimi sijaisikia, ila ninachojua, ni kabila la Wachagga walioupokea Ukristo na mguvu sana na wakaachana na mila zao karibu zote!. Ukristo ulifundisha kuwa kufanya sex ni dhambi, hivyo hii imewaletea Wachagga wengi tatizo la 'inhibition' kwenye sex, hivyo kwenye harusi za Kichagga, wazazi huhudhuria kanisani tuu kwenye ndoa, halafu hawakupaswa kuhudhuria kwenye reception, bali wazazi walipelekewa vinywaji na vyakula vyao nyumbani 'nekia risso' kwa hoja ya lengo la sherehe ya reception ilikuwa ni kusherehekea ndoa!.

Yaani baada ya harusi kufungwa, ilikuwa inapaswa kufuatia na 'ndoa' kisha ndipo watu wanakuja kusherekea ndoa!. Kufuatia sex kuhesabika ni ndambi, wazazi hawapaswi kusherekea ndoa ya binti yao!. Hadi leo kwenye harusi nyingi za Wachagga, kwa vile harusa hufungwa kanisani na kuelekea moja moja ukumbini bila kupita hotelini kufanya ndoa, then kabla muziki haujafunguliwa na kucheza kwa kushikana kama ishara ya ndoa hakujafanyika, then wazizi wa bibi harusi huaga na kuwaacha mkiselebuka!.

Hii ya bibi ndio naisikia leo!.

Pasco
 
Ya kwangu bibi alihudhuria na ndiye amenilelea na ninatokea huko huko uchaggani si Rombo lakini.
 
Kwa mila na destuti za Kichagga, bibi wa bwana harusi haruhusiwi kuhudhuria harusi ya mjukuu wake. Hii Tabia imeleta mgogoro kwenye familia moja hapa Moshi baada ya bibi mmoja kulazimisha kuhudhuria harusi ya mjukuu wake itakayofanyika Dar es Salaam tarehe 30/05/2015.

Bwana harusi mtarajiwa ambaye alilelewa na bibi yake mpaka alipomaliza kidato cha nne, ametishia kuahirisha harusi hiyo kama bibi huyo hataruhusiwa kuhudhuria kwenye harusi.

"Oteh" nkiwicho, hapana ni vibaya. Bibi kuhudhuria harusi! Hapana. Yeye ashiriki akiwa nyumbani, apewe vinywaji na vyakula ale na anywe na majirani na marafiki zake. Huo ndio utaratibu. Lakini bibi huyo yeye anasema kwa nini asipewe nafasi hiyo kama mlezi kwa kuwa ni kweli alimlea? Swala hili litaamuliwa kesho kutwa na wazee wa mila na viongozi wa dini.

Hili limekaaje?
Mpendwa mleta mada, JF ingekuwa mtandao wa wachagga mada yako ingekuwa na maana.Unapomalizia thread yako kwa maneno: Hii limekaaje, unataka mwanajf wa shinyanga aseme nini ilhali hajui miiko na desturi za wachagga? Pamoja na hayo, wachagga wote, kuanzia Siha mpaka Tarakea wanatofautiana sana kilugha, kimila n.k.Hiyo ya bibi kukatazwa kuhudhuria harusi ya mjukuu wa kiume ilikuwepo mwika, mamba, marangu, kilema na kibosho zamani hizo, kwa sasa hakuna anayehangaika na hiyo mila.
 
Mila na tamadun zingine ni tabu tupu yani,sasa hasihudhurie ili iweje?.
 
Back
Top Bottom