Bibi Tina wa Mwananyamala

Bibi Tina wa Mwananyamala

Hivi kwa nini hivi visa vya wanga na wachawi vinaripotiwa na kutokea uswahilini na kwa watu wa vipato duni? Mbona hatujawahi kuvisikia maeneo ya Masaki, Mikocheni au Upanga?

Vv
 
Uko Haiti unakwenda kwa mganga na picha ya unaemtaka. Inawekwa kwenye bakuli la maji na maneno yanaanza, unaitwa mpaka unafika sasabunaulizwa shida yako kwake

Ninamda pesa zangu, anaulizwa utazilipa au tukuchukue?
Ninamtaka anioe ni pale pale anatoa jibu kuwa atakuoa

Ninagombania ubunge lakini huyu ndiyo kiwingu unapewa kisu ummalize huku jamaa anakata roho
Hayo hufanyika kwenye shithole countries tu na huko ndipo umasikini, maradhi na ujinga vimetamalaki.

Vv
 
Mshana kwenye uandishi tu unajua yan hua nasoma huku naombea story isiishe ni tag kwenye mwendelezo
 
Unaandika haya ukiwa kwako bila kujua Mwananyamala iko wapi na wala bila kujisumbua kufika eneo husika ili kubainisha uongo wangu wa story za kusadikika... You are so fucked up... You are just another stupid idiot
Tehehehehehehe , mkuu kwa mara ya kwanza kuona umekereka na kurusha bomu la mkono.
 
View attachment 689290nimeiona hii picha kwa mstuko... Huyu bibi namjua ni rafiki na Bibi Tina aliyekuwa mama mwenye nyumba wangu Mwananyamala mwaka 2000 kuelekea 2001, kama sie basi naomba radhi
Nilihamia mwaka huo nikitokea Mtoni kwa Aziz Ally... Nikatapa vyumba viwili kwa Bibi Tina... Vyumba vyangu vilikuwa upande mmoja vimeungana na vya Bibi.. Nyumba ilikuwa na jumla ya wapangaji 7... Kuhamia tu baada ya siku mbili nikapata habari pale mtaani kuwa siku tatu zilizopita kuna mtoto alikuwa kapotea na kuja kupatikana kwa Bibi Tina chumbani... Habari ile ilikuwa bado ya moto...
Kwa mshangao wangu jioni ya siku hiyo bibi aliniita chumbani kwake na kunisihi nisiamini lolote la ule mtaa kwakuwa watu wana roho mbaya sana na wanaweza kukusingizia lolote... Nikamwambia ni sawa ila kesho yake nikamtest kwa kuchoma UDI chumbani kwangu jioni... Hata kabla UDI haujafika nusu aliingia sebuleni mpaka mlango wa chumbani macho yamemtoka pima.. Akasema nyumba yake haichomwi UDI na kama napenda basi yuko tayari kurudisha kodi..... Nikapata jibu
Maisha yakaendelea ila majirani wakanitonya kuwa bibi ana tabia ya kuingia kwenye vyumba vya wapangaji wakiwa hawapo na hawajui anaingiaje.... Niliweka mtego wangu na kumdaka... Tukayamaliza.. Baada ya hilo tukio wapangaji wakaniambia tena bibi huwa na tabia ya kuweka kibakuli kidogo cha alminium kwenye dirisha langu chumbani kwa nje kila jioni na kukiondoa kila asubuhi... Nilipogundua ni kweli nilikimwagia mkojo wa janaba na ikawa ndio mwisho wa kukiona pale kile kibakuli
Siku moja usiku wa kuanzia saa tatu pale kwenye kibaraza chake kukawa na maandalizi yasiyoeleweka.. Huyo bibi pichani alikuwepo na babu mmoja pia.. Eti walikuwa wanamsaidia bibi Tina kufanya usafi.. Niliingia kwangu na kulala lakini ilipofika saa nane usiku nikasikia kelele za vishindo chumba cha pili ambacho kilikuwa sitting room ya bibi.. Mimi nikatoka chumbani na upanga.. Kipindi hicho ishu za kuvunjiwa Mwananyamala ilikuwa kitu cha kawaida kabisa
Kufika sebuleni nikasikia sauti zinatoka chumba cha pili kwa bibi.. Nilichowaza ni kwamba majambazi wamemuingilia tayari na wnahamisha vitu na wakitoka kwake ni kwangu
Nilinyanyua panga na kupiga ukutani kibapabapa.. Nilirudia mara tatu kisha nikasikia kimya kabisa.. Sikulala mpaka alfajiri kuona kilichompata bibi na je kama kuna wapangaji wengine walisikia lile sekeseke... Mungu wangu wenzangu walikuwa hawajui lolote... Nikasubiri kichambo cha bibi sasa maana usiku alikuwa hapendi kelele kabisa... Cha ajabu hakuamka mpaka naenda kazini na alinikwepa kwa siku tatu mfululizo na wala hakuwa kavunjiwa.....
Mambo yakazidi kuwa moto kuna dada mmoja anaitwa Tina (wajina wake) alisimamishwa kazi hivyo akawa hana hela ya kodi.. Walipelekeshana sana na bibi mpaka serikali za mitaa lakini dada hakuhama.. Ikafika mahali bibi akawa anammwagia ndoo za maji kwenye makochi na kitandani lakini dada anaanika na kukomaa.. Bibi alipoona amegota kumtoa akaanza kumtumia nyoka ama panya.. Ikawa tabu tupu
Mwishoni Tina akaanza kuumwa.. Aliumwa kama mwezi hivi ugonjwa usiojulikana na alipozidiwa majirani tukachanga arudishwe kwao... Siku anapelekwa UBUNGO miguu na mikono vikawa vimekakamaa havikunjuki... Waliompeleka ilibidi wanunue siti 3
Alfajiri ya Siku ya tatu tangu kuondoka Tina bibi alikuja na kunigongea na kuniambia habari za msiba wa Tina... Yeye alikuwa hana simu na hata kama angekuwa nayo kutokana na bifu lake na marehemu asingeweza hata siku moja kupewa taarifa yeye.. Asubuhi nikawapa majirani taarifa wakashangaa sana na tulipopiga simu kijijini Iringa wakatuambia ni kweli na walikuwa wanajiandaa kutupa taarifa....
Mambo yakazidi kuwa moto.. Baada ya msiba wa Tina kupita akaendelea na visa vyake vya kuingia vyumbani mwa wapangaji.. Safari hii akiingia kwenye chumba cha mwalimu binti mtu wa Tanga... Kule hakuweza kutoka mpaka mwenye chumba akaja.. Huyu binti naye alikuwa kamili hivyo akamshushia bibi kipondo kisha akaita askari wa Oysterbay... Wakaja askari wa kike na wa kiume.. Yule askari wa kike akamuomba bibi atoke waende kituoni lakini akagoma.. Askari akasema usinitanie akatumia nguvu kumvuta lakini akaishia kupinda mkono mmoja
Mambo ni motooo.... Askari akapelekwa Mwananyamala hospital analia huku bibi analindwa na mtutu.......

Nitaendelea.. Nitaomba Moderator aunganishe sehemu itayofuatia
Alitaka akuchezee Kumbe hakujua we mwenyewe ndio mchawi Mara laki moja zaidi yake,. Unitag basi mkuu muendelezo huo wa bibi Tina.
 
Back
Top Bottom