Bibi Tina wa Mwananyamala

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,773
699,341
1.png

Nimeiona hii picha kwa mstuko... Huyu bibi namjua ni rafiki na Bibi Tina aliyekuwa mama mwenye nyumba wangu Mwananyamala mwaka 2000 kuelekea 2001, kama sie basi naomba radhi
Nilihamia mwaka huo nikitokea Mtoni kwa Aziz Ally.

Nikatapa vyumba viwili kwa Bibi Tina... Vyumba vyangu vilikuwa upande mmoja vimeungana na vya Bibi.. Nyumba ilikuwa na jumla ya wapangaji 7.

Kuhamia tu baada ya siku mbili nikapata habari pale mtaani kuwa siku tatu zilizopita kuna mtoto alikuwa kapotea na kuja kupatikana kwa Bibi Tina chumbani... Habari ile ilikuwa bado ya moto.

Kwa mshangao wangu jioni ya siku hiyo bibi aliniita chumbani kwake na kunisihi nisiamini lolote la ule mtaa kwakuwa watu wana roho mbaya sana na wanaweza kukusingizia lolote.

Nikamwambia ni sawa ila kesho yake nikamtest kwa kuchoma UDI chumbani kwangu jioni... Hata kabla UDI haujafika nusu aliingia sebuleni mpaka mlango wa chumbani macho yamemtoka pima.

Akasema nyumba yake haichomwi UDI na kama napenda basi yuko tayari kurudisha kodi..... Nikapata jibu
Maisha yakaendelea ila majirani wakanitonya kuwa bibi ana tabia ya kuingia kwenye vyumba vya wapangaji wakiwa hawapo na hawajui anaingiaje.... Niliweka mtego wangu na kumdaka...

Tukayamaliza.. Baada ya hilo tukio wapangaji wakaniambia tena bibi huwa na tabia ya kuweka kibakuli kidogo cha alminium kwenye dirisha langu chumbani kwa nje kila jioni na kukiondoa kila asubuhi... Nilipogundua ni kweli nilikimwagia mkojo wa janaba na ikawa ndio mwisho wa kukiona pale kile kibakuli
Siku moja usiku wa kuanzia saa tatu pale kwenye kibaraza chake kukawa na maandalizi yasiyoeleweka..

Huyo bibi pichani alikuwepo na babu mmoja pia.. Eti walikuwa wanamsaidia bibi Tina kufanya usafi.. Niliingia kwangu na kulala lakini ilipofika saa nane usiku nikasikia kelele za vishindo chumba cha pili ambacho kilikuwa sitting room ya bibi.. Mimi nikatoka chumbani na upanga..

Kipindi hicho ishu za kuvunjiwa Mwananyamala ilikuwa kitu cha kawaida kabisa
Kufika sebuleni nikasikia sauti zinatoka chumba cha pili kwa bibi.. Nilichowaza ni kwamba majambazi wamemuingilia tayari na wnahamisha vitu na wakitoka kwake ni kwangu

Nilinyanyua panga na kupiga ukutani kibapabapa.. Nilirudia mara tatu kisha nikasikia kimya kabisa.. Sikulala mpaka alfajiri kuona kilichompata bibi na je kama kuna wapangaji wengine walisikia lile sekeseke... Mungu wangu wenzangu walikuwa hawajui lolote...

Nikasubiri kichambo cha bibi sasa maana usiku alikuwa hapendi kelele kabisa... Cha ajabu hakuamka mpaka naenda kazini na alinikwepa kwa siku tatu mfululizo na wala hakuwa kavunjiwa.....

Mambo yakazidi kuwa moto kuna dada mmoja anaitwa Tina (wajina wake) alisimamishwa kazi hivyo akawa hana hela ya kodi.. Walipelekeshana sana na bibi mpaka serikali za mitaa lakini dada hakuhama.. Ikafika mahali bibi akawa anammwagia ndoo za maji kwenye makochi na kitandani lakini dada anaanika na kukomaa.. Bibi alipoona amegota kumtoa akaanza kumtumia nyoka ama panya.. Ikawa tabu tupu

Mwishoni Tina akaanza kuumwa.. Aliumwa kama mwezi hivi ugonjwa usiojulikana na alipozidiwa majirani tukachanga arudishwe kwao... Siku anapelekwa UBUNGO miguu na mikono vikawa vimekakamaa havikunjuki... Waliompeleka ilibidi wanunue siti 3

Alfajiri ya Siku ya tatu tangu kuondoka Tina bibi alikuja na kunigongea na kuniambia habari za msiba wa Tina... Yeye alikuwa hana simu na hata kama angekuwa nayo kutokana na bifu lake na marehemu asingeweza hata siku moja kupewa taarifa yeye.. Asubuhi nikawapa majirani taarifa wakashangaa sana na tulipopiga simu kijijini Iringa wakatuambia ni kweli na walikuwa wanajiandaa kutupa taarifa....

Mambo yakazidi kuwa moto.. Baada ya msiba wa Tina kupita akaendelea na visa vyake vya kuingia vyumbani mwa wapangaji.. Safari hii akiingia kwenye chumba cha mwalimu binti mtu wa Tanga...

Kule hakuweza kutoka mpaka mwenye chumba akaja.. Huyu binti naye alikuwa kamili hivyo akamshushia bibi kipondo kisha akaita askari wa Oysterbay... Wakaja askari wa kike na wa kiume.. Yule askari wa kike akamuomba bibi atoke waende kituoni lakini akagoma.. Askari akasema usinitanie akatumia nguvu kumvuta lakini akaishia kupinda mkono mmoja

Mambo ni motooo.... Askari akapelekwa Mwananyamala hospital analia huku bibi analindwa na mtutu.......

Askari kufikishwa Mwananyamala hana tatizo ila mkono haukunjuki.. Huku nyumbani bibi akabembelezwa yaishe hapelekwi polisi.. Alipokubali tu na kutoka nje kule hospital mambo poa... Askari hakurudi tena kwa bibi... Ila wakaja askari vichaa..

Nani wa Mwananyamala anamkumbuka Henjewele wa Oysterbay? Huyu ndio alimtia bibi Tina pingu na kumpeleka lupango... Akafunguliwa kesi ya trespassing... Akakaa mpaka kesho yake tukamtoa na mwalimu akahama wiki ileile

Bibi Tina kuna kijana mpangaji alikuwa anampenda sana anaitwa Evarist.. Huyu kijana alikuwa anafanya kazi maeneo ya vijana.. Kwahiyo alikuwa anadamka alfajiri na kurudi usiku.. Hakuwa na demu wala mchumba.. Basi huyu alikuwa anachotewa maji na bibi na sometimes hata kupewa chakula...

Baadae alikuja kuhamia binti wa ndugu yake bibi Tina, alikuwa anamuita bibi mama mkubwa.. Huyu akapewa chumba cha ndani next to Evarist.... Taratibu na kwa siri wawili hawa wakawa wapenzi... Bibi hakupenda kabisa hii habari
Kwanza akamuita Evarist na kumkandia sana yule binti kuwa ni malaya nknk...

Lakini jamaa hakuelewa somo... Kisha akamuita binti na kumkandia jamaa kuwa hana kitu ni fukara.. Lakini haikusaidia.. Siri ya kutaka kuwaachanisha ni kwamba bibi alikuwa anajisevia usiku kwa Evarist... Jamaa alikuwa haishiwi na ndoto za ngono... Bibi aliwafanyia visa mpaka walihama alfajiri...

Na maranyingi alipenda sana kutuma panya na nyoka weusi... Yani saa kumi na mbili jioni panya anaingia kwako na kukuuma au usiku anakuja na kukuvuta kende.... Visa vilikuwa vingi mpaka wakatimkia Tabata

Huku episodes zikawa haziishi.. Kuna wakati wapangaji tulikuwa tunaamka wote tuko hoi sana na tuna matope ama michanga miguuni....
Huku na huku mara paaap nikaopoa mtoto wa kingazija mweupe pee kama Mwarabu wa muscut... Hapa ndio mambo yakawa motoooo...

Ilianza kwa yeye kuja weekend tunaenda Jolly club pembeni ya las Vegas kucheza kuch kuch hotae.. Halafu tunarudi home kumalizia na KWICHI KWICHI hatari.... Jumamosi yote hatutoki ndani... Hili jambo bibi hakulipenda ila akawa mvumilivu

Mtu wangu huyu akanifundisha na kunifunulia mengi nikaongeza na ya kwangu basi ikawa ni michezo ya kuwindana na kushindana.... Yani bibi Tina ilikuwa ni lazima usiku atembelee wapangaji wake vyumbani na kucheza nao sometimes katitu

Mngazija wangu akahamia rasmi... Moto ukawa ndio kama umetiwa petrol.. Ikawa yeye ni mwendo wa UDI na marashi makali... Basi ukija bibi yuko hoi... Siku moja akaniita... Akaniambia babu nakupenda sana lakini huyu mvaa pedi wako sitaki kumuona hapa ATANIUA.. niko tayari nikupe hela akapange kwingine lakini siko tayari kumuona tena hapa..

Hili lilikuwa kubwa kuliko tulihama wiki ile ile bila taarifa... Mimi nilidamka kwenda kazini huku mwenzangu kajifungia ndani anapaki kimya kimya... Kuja saa sita nikaenda kumuaga bibi.. Niliacha kodi ya miezi miwili.. Cha ajabu akaniambia anajua kuwa nahama... Sikujali nikaita gari

Wakati wa kutoa vyombo akafunga mlango mkubwa akatutaka tutolee mlango mdogo just imagine.... Lakini wakati tunatoa vyombo akawaita wale wazee wawili mmoja wapo ni huyo hapo pichani.. Wakaanza kufagia pale nje kwa pozi sana..

Kwahiyo kama mmebeba kabati inabidi muwasubiri.. Halafu wanachofagia hakionekani.. Vyombo vya kutoa dk 20 tulimaliza lisaa kwa kero zao za kufagia visivyoonekana...

Bibi alikuwa na watoto watano lakini kila mwaka alikuwa anakufa mmoja... Wa mwisho ni mama Whit alikufa 2012.. Huyu alikuwa anaishi hapo hapo... Bibi Tina alikuwa ni never miss Kanisani akivaa msalaba mkubwa kama wa nabii Tito na miwani kubwa kama sight mirrors za land rover 110

Kesho nitaenda kumsalimia kama bado yuko hai
 
Inaendelea......
Askari kufikishwa Mwananyamala hana tatizo ila mkono haukunjuki.. Huku nyumbani bibi akabembelezwa yaishe hapelekwi polisi.. Alipokubali tu na kutoka nje kule hospital mambo poa... Askari hakurudi tena kwa bibi.

Ila wakaja askari vichaa.. Nani wa Mwananyamala anamkumbuka Henjewele wa Oysterbay? Huyu ndio alimtia bibi Tina pingu na kumpeleka lupango... Akafunguliwa kesi ya trespassing... Akakaa mpaka kesho yake tukamtoa na mwalimu akahama wiki ileile

Bibi Tina kuna kijana mpangaji alikuwa anampenda sana anaitwa Evarist.. Huyu kijana alikuwa anafanya kazi maeneo ya vijana.. Kwahiyo alikuwa anadamka alfajiri na kurudi usiku.

Hakuwa na demu wala mchumba.. Basi huyu alikuwa anachotewa maji na bibi na sometimes hata kupewa chakula... Baadae alikuja kuhamia binti wa ndugu yake bibi Tina, alikuwa anamuita bibi mama mkubwa.. Huyu akapewa chumba cha ndani next to Evarist.

Taratibu na kwa siri wawili hawa wakawa wapenzi... Bibi hakupenda kabisa hii habari

Kwanza akamuita Evarist na kumkandia sana yule binti kuwa ni malaya nknk... Lakini jamaa hakuelewa somo... Kisha akamuita binti na kumkandia jamaa kuwa hana kitu ni fukara.. Lakini haikusaidia.. Siri ya kutaka kuwaachanisha ni kwamba bibi alikuwa anajisevia usiku kwa Evarist... Jamaa alikuwa haishiwi na ndoto za ngono... Bibi aliwafanyia visa mpaka walihama alfajiri... Na maranyingi alipenda sana kutuma panya na nyoka weusi..

Yani saa kumi na mbili jioni panya anaingia kwako na kukuuma au usiku anakuja na kukuvuta kende.... Visa vilikuwa vingi mpaka wakatimkia Tabata
Huku episodes zikawa haziishi.. Kuna wakati wapangaji tulikuwa tunaamka wote tuko hoi sana na tuna matope ama michanga miguuni....

Huku na huku mara paaap nikaopoa mtoto wa kingazija mweupe pee kama Mwarabu wa muscut... Hapa ndio mambo yakawa motoooo... Ilianza kwa yeye kuja weekend tunaenda Jolly club pembeni ya las Vegas kucheza kuch kuch hotae.. Halafu tunarudi home kumalizia na KWICHI KWICHI hatari.

Jumamosi yote hatutoki ndani... Hili jambo bibi hakulipenda ila akawa mvumilivu
Mtu wangu huyu akanifundisha na kunifunulia mengi nikaongeza na ya kwangu basi ikawa ni michezo ya kuwindana na kushindana.... Yani bibi Tina ilikuwa ni lazima usiku atembelee wapangaji wake vyumbani na kucheza nao sometimes katitu

Mngazija wangu akahamia rasmi... Moto ukawa ndio kama umetiwa petrol.. Ikawa yeye ni mwendo wa UDI na marashi makali... Basi ukija bibi yuko hoi... Siku moja akaniita... Akaniambia babu nakupenda sana lakini huyu mvaa pedi wako sitaki kumuona hapa ATANIUA.. niko tayari nikupe hela akapange kwingine lakini siko tayari kumuona tena hapa.

Hili lilikuwa kubwa kuliko tulihama wiki ile ile bila taarifa... Mimi nilidamka kwenda kazini huku mwenzangu kajifungia ndani anapaki kimya kimya... Kuja saa sita nikaenda kumuaga bibi.. Niliacha kodi ya miezi miwili.. Cha ajabu akaniambia anajua kuwa nahama... Sikujali nikaita gari

Wakati wa kutoa vyombo akafunga mlango mkubwa akatutaka tutolee mlango mdogo just imagine.... Lakini wakati tunatoa vyombo akawaita wale wazee wawili mmoja wapo ni huyo hapo pichani.. Wakaanza kufagia pale nje kwa pozi sana..
Kwahiyo kama mmebeba kabati inabidi muwasubiri.. Halafu wanachofagia hakionekani.. Vyombo vya kutoa dk 20 tulimaliza lisaa kwa kero zao za kufagia visivyoonekana.

Bibi alikuwa na watoto watano lakini kila mwaka alikuwa anakufa mmoja... Wa mwisho ni mama Whit alikufa 2012.. Huyu alikuwa anaishi hapo hapo... Bibi Tina alikuwa ni never miss Kanisani akivaa msalaba mkubwa kama wa nabii Tito na miwani kubwa kama sight mirrors za land rover 110
Kesho nitaenda kumsalimia kama bado yuko hai


JamiiForums naomba kuunganisha hii part B na ile A
 
Back
Top Bottom