Biashara ya Kusafirisha Matunda Ulaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya Kusafirisha Matunda Ulaya

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kagalala, Mar 29, 2012.

 1. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Wakuu naomba ushauri wenu.
  Nimekuwa nitembelea maduka mbali mbali katika nchi za Ulaya hasa UK na kukuta bidhaa kazaa za kutoka Uganda na Kenya lakini sijawahi kuona bidhaa zozote kutoka Tanzania katika maduka ya UK. Nikiwa Tanzania naona kuna matunda mengi kama Machungwa, Mahembe, Nanasi, Mapalachichi, nk zimerundikwa tu barabarani na vinauzwa kwa bei ya chini sana kulinganisha na bei ya Ulaya. Je kwa nini Watanzania hatuna akili ya kuweza kupeleka hivi vitu Ulaya na kupata soko zuri.
  Mimi napenda sana ndizi Bukoba na huwa nazipata kwa urahisi sana katika Maduka ya UK zikiwa zina nembo ya (Product of Uganda). Hawa jamaa wananunua ndizi hata kutoka Bukoba na Karagwe. Sisi kwa nini tusifanye hivyo tena kutoka hata Mbeya? Waganda wanauza majimbi, viazi na hata nyanya chungu katika soko la Ulaya. Sisi tumelogwa?
  Wakenya wametawala soko la maua, sisi kwa nini hatuwezi?
  Naomba mawazo yenu
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  sisi tunapenda kwenda china kuleta fongkong
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Mtafute balozi wa amani anaitwa risasi mwaulanga alisema atatoa elimu kuhusiana na hiyo kitu.
   
 4. m

  majogajo JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ww si uanza sasa.........maana hyo ndo opportunity yenyewe..........
   
 5. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Mimi nilishaanza lakini kwa bidhaa zingine ambazo nyingi naleta Tanzania, ila naona hili linanigusa kwa nini wenzetu wameweza sisi tunashindwa.
   
 6. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  kwa sababu nchi yetu imejaa watu kama wewe wasio na dynamism and initiative.
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wewe tafuta fursa lete specification ya izo bidhaa watu waende mtaani kuzisaka!
  Sasa kama umeanza kwa kulaumu hatutafika!
   
 8. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  niliona mlolongo wa mpaka kuuza embe UK nikaona ni bora niangalie soko la ndani tu
   
 9. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wengi wetu wanaogopa ushuru unaotozwa na complexities za uzalishaji wa bidhaa zenye viwango vinavyohitajika huko.
  Yaan hata baada ya ile mipango ya AGOA na ... inayoturuhusu kuuza bidhaa njebila vikwazo vyovyote (hasa Marekani na Ulaya) kuanzishwa bado mwitikio ni mdogo ukilinganisha na wenzetu wa Kenya na Uganda.

  Nadhani Mamlaka zinazohusika kama BET, TIC, MITM, ..bado hazijatoa elimu ya kutosha kwa wajasiriamali wetu. Hata BDSP (kama AMKA) nao wanahusika kwan sector hii bado ipo nyuma sana ukilinganisha na wenzetu wa Kenya na Uganda.

  Cha msingi kwa sasa ni kuanza personally pale unapoona fursa
   
 10. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu usiseme mlolongo ni taratibu waliojiwekea kuhakikisha bidhaa inayoingia soko lao imekidhi ubora.

  Don't give up so easily Narubongo try harder this time,Am sure you will get there.
   
 11. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama wakenya na waganda wameweza na wewe unakutana nao join now wakupe mbinu zilete kwa Watz ili waweze kufika hapo tatizo kubwa la watz wengi walikosa exposure tofauti wa nchi jirani.Wewe umepata hicho kitu rudi saidia watz wenzako saidia nchi yako wote kwa pa1 tutasonga mbele.
   
 12. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Kaka observations zako ni nzuri tu sana, lakini inatia shaka kama wewe ni mfanyabiashara unayeingiza bidhaa kutoka UK kuja TZ una nafasi nzuri zaidi ya kuchukua bidhaa TZ na kupeleka UK, kwa nini usifanye uchunguzi wa kutosha na kutuletea hapa ripoti kamili ya bidhaa zinazohitajika, kiasi gani zinauzwa kkule, gharama ya nauli na ushuru mwingine, taratibu kamili na vitu kama hivyo. Sisi wengine ni wakulima tu kaka, maisha yetu yote mashambani, nyie mnaokwendakwenda huko duniani ndy mnatakiwa mtupe mwanga kidogo ili tutumie hizo fursa!
   
 13. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  quality matters! unayoona mtaani unatakiwa na yale unayoyaaona uk! matunda si kununua tu na kusafirsha lazima yatunzwe ili hata mnunuaji afurahi, sisi hapa hayo hatuangalii, ndo maana hata ya mtahani hayo kuyanunua pia hayatamaniki. matunda yetu hayamwagiwi dawa hivyo utakuta mengi ya midoa kibao. sasa utachagua mpaka lini upate mazuri ya kusafirisha_
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Personally nimeanza na shamba la miembe eka kumi lazima nije export
  NI miembe ya kisasa toka SUA pale.
  \Piga ua galagaza lazima einde pande za mbali
   
 15. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni rahisi kwa mtanzania kutoa bidhaa nje na kuleta ndani kuliko kutoa ndani na kupeleka nje, urasimu.
   
 16. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu yale matunda unayo yaona mheza na pwani kule hayana viwango vya kuingia ulaya hata siku moja na huwezi pewa kibali cha kuingiza ulaya.

  - wale wanacheza na standard si mchezo na kama hulimi kwa organic farming huwezi ingiza bidhaa ulaya,

  - wale wanataka matunda na mboga zilizo zalishwa kwa organic only, yale mananasi yanayo puliziwa dawa za kufa mtu hayawezi kuingia kule,

  - na hata kenya si kwamba wananunua matunda huku halafu wanasafirisha ulaya, no wanalima huko huko kwao, matunda ya mheza hata south africa huwezi ingiza mkuu
   
 17. D

  Dangote JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimeshawah kujaribu iyo biznes dah its complicated kufanya individual labda uwe na mtaji mkubwa sana ki2 ambacho wengi ha2na,wenzetu kenya na uganda wanaweza coz wanapata sapoti kubwa kutoka serikali zao ili uweze kuuza uk ni lzm uwe na certified packing house then tz hapa logistics ni tabu sana km unasafirisha kwa air freight 2na depend kwa kenya airways ambao wanawapendelea wakenya wenzao na emirates,british,klm ni expensive haitokulipa vzuri then ha2na exposure kwa kweli coz pale unapohtaj msaada wa government officials respond haiwi nzuri sana coz they dnt i understand what kind of biznes it this so dispointing kwa kweli
   
 18. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #18
  Mar 31, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu ni kweli iko complicated sana, ila tambua kwamba ni nchi husika ndo huwa wanatoa kibali baada ya kulizika na Ubora wa Matunda hayo, na hapo hakuna cha siasa wala rushwa mkuu na hakuna short cut kabisa njia imenyoka na ni moja tu,

  - Na wanaozani serikali inaweza kuwasaidia kuingiza vitu kama matunda Ulaya wanajidanganya, wale wanaangalia Ubora na maswala ya Afya hawaangalii mambo ya Siasa kwamba Nchi fulani tuna Urafiki nayo, hawana short cut hata kidogio,

  - Tembea wale TAHA wawape procedure za ku export matunda na mboga kwenda Ulaya hapo ndo utagundua kwamba inatakiwa juhudi zako ziwe 90%,

  - Yale mananasi ya kule Pwani na machungwa ya muheza Tanga hayana viwango vya kuuzwa kwenye masoko ya Ulaya,

   
 19. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Mkuu tafuta uwezekano wa wewe kuanza kuuza bidhaa au hayo matunda toka TZ. Ukweli ni kwamba hata kahawa ya TZ watu wanai-pack vizuri na kuandika kuwa ni product za kwao. Vile vile machungwa. machungwa ya Muheza wale wa kutoka jirani wanakuja wanayachuma kwa umakini ili yasipate mikwaruzo wanaya-pack na kuandika ni produce za kwao na kuuza. Sisi wa TZ tumekalia kulalamika. Na malalamiko hayaleti tija bali uchungu na akili kutokufanya kazi vizuri na kutokuona fursa zilizopo. Watu wachangamke!
   
 20. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Tatizo mfumo wa kusubiri serikali ifanye kila kitu ndiyo uliodumaza akili wa waTZ wengi. Serikali haiwezi fanya kila kitu na kuuza machungwa. Sisi wananchi ndiyo tuuze machungwa (export) na kuchangamkia fursa zilizopo. Merci!
   
Loading...