Uwekezaji wa China nchini Morocco waleta wasiwasi wa Umoja wa Ulaya?

Uwekezaji wa China nchini Morocco waleta wasiwasi wa Umoja wa Ulaya?

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
186
Reaction score
307
Gazeti la Financial Times la Uingereza hivi karibuni limechapisha ripoti kuhusu makampuni ya China kuwekeza na kuanzisha viwanda katika Bustani ya Teknolojia ya Tangier nchini Morocco. Katika ripoti hiyo, Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya Maroš Šefčovič alirudia kauli ya “uwezo wa utengenezaji wa kupita kiasi wa China”, akielezea wasiwasi kwamba, kupitia uwekezaji nchini Morocco, China itaweza kubadilisha nchi hiyo ya Afrika Kaskazini kuwa “kituo” cha uzalishaji na usafirishaji bidhaa kinacholenga soko la Ulaya.

Tukisoma ripoti hiyo kwa makini, tutagundua kwamba, ingawa wasiwasi wa EU unaweza kuwa na “usahihi kisiasa”, lakini hauna mantiki ya kiuchumi. Shughuli za uwekezaji na ujenzi wa kiwanda wa makampuni ya China nchini Morocco, ni marekebisho ya mnyororo wa sekta ya magari duniani.

Kwanza, uwekezaji wa China nchini Morocco unatokana na upanuzi wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika, na pia ni chaguo la kimkakati kufuatia soko linalofanywa na makampuni ya China. Morocco iko karibu na bara la Ulaya, ina mazingira thabiti ya kisiasa, na miundombinu imara. Hivyo imekuwa moja ya nchi zinazovutia zaidi uwekezaji wa kigeni barani Afrika. Kwa kuwekeza katika sekta kama vile magari ya umeme, betri, na vipengele vya magari, makampuni ya China si kama tu yatakidhi mahitaji ya soko la ndani na kikanda, bali pia yatainua kiwango cha Morocco katika minyororo ya usambazaji wa kimataifa. Mchakato huu si jaribio la kuingia Ulaya kwa mlango wa nyuma, bali ni mwelekeo usioepukika ya mchakato wa kijani na mgawanyo wa viwanda duniani.

Pili, makampuni mengi ya China kuwekeza nchini Morocco pia kunatokana na juhudi za Morocco za kuboresha mazingira yake ya kibiashara. Katika miaka ya hivi karibuni, Morocco imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kusamehe kodi ya mapato ya makampuni ya nje kwa miaka mitano, ili kuvutia uwekezaji wa kigeni. Faida hizi zinapatikana kwa usawa kwa wawekezaji kutoka nchi yoyote. Kwa ukweli, makampuni makubwa mengi ya Ulaya ikiwemo Renault na Stellantis yameanzisha viwanda vikubwa vya utengenezaji nchini Morocco muda mrefu uliopita, na yamekuwa yakiota mizizi katika soko la nchi hiyo kwa miaka mingi. Makampuni ya China yana mantiki ya kibiashara sawa na wenzao wa Ulaya.

Wasiwasi wa kweli wa Umoja wa Ulaya hautokani na kinachoitwa “uwezo wa uzalishaji kupita kiasi wa China”, bali ni kutokana na hofu ya kupungua kwa nguvu yake ya ushindani ikilinganishwa na China. Hata hivyo, njia sahihi ya kushughulikia wasiwasi huo si kwa kujenga kuta ndefu au kutumia vibaya vyombo vya kujilinda kibiashara. Badala ya kutoa malalamiko na kuweka vikwazo, Umoja wa Ulaya unapaswa kutafakari kasoro ya sera zake za kiviwanda na kutafuta ushirikiano na washirika ikiwemo China na Morocco.
a86ee248b53c818e9e03920f99ec9ff2.png
 
Uwekezaji wa China nchini Morocco ni uamuzi wa kibiashara unaonufaisha pande zote hasa upande wetu Africa Ila ushindani wa kiuchumi unapaswa kujibiwa kwa ubunifu na ushirikiano, si kwa hofu au vikwazo
 
Uwekezaji wa China nchini Morocco ni uamuzi wa kibiashara unaonufaisha pande zote hasa upande wetu Africa Ila ushindani wa kiuchumi unapaswa kujibiwa kwa ubunifu na ushirikiano, si kwa hofu au vikwazo
👍👍👍👍👍
 
Back
Top Bottom