Mkuu tafuta uwezekano wa wewe kuanza kuuza bidhaa au hayo matunda toka TZ. Ukweli ni kwamba hata kahawa ya TZ watu wanai-pack vizuri na kuandika kuwa ni product za kwao. Vile vile machungwa. machungwa ya Muheza wale wa kutoka jirani wanakuja wanayachuma kwa umakini ili yasipate mikwaruzo wanaya-pack na kuandika ni produce za kwao na kuuza. Sisi wa TZ tumekalia kulalamika. Na malalamiko hayaleti tija bali uchungu na akili kutokufanya kazi vizuri na kutokuona fursa zilizopo. Watu wachangamke!
Kuna mswahili mmoja anaongoza board of external trade anafikiria kazi ya board yake ni kuandaa maonyesho ya sabasaba tu.
ww si uanza sasa.........maana hyo ndo opportunity yenyewe..........
Wengi wetu wanaogopa ushuru unaotozwa na complexities za uzalishaji wa bidhaa zenye viwango vinavyohitajika huko.
Yaan hata baada ya ile mipango ya AGOA na ... inayoturuhusu kuuza bidhaa njebila vikwazo vyovyote (hasa Marekani na Ulaya) kuanzishwa bado mwitikio ni mdogo ukilinganisha na wenzetu wa Kenya na Uganda.
Nadhani Mamlaka zinazohusika kama BET, TIC, MITM, ..bado hazijatoa elimu ya kutosha kwa wajasiriamali wetu. Hata BDSP (kama AMKA) nao wanahusika kwan sector hii bado ipo nyuma sana ukilinganisha na wenzetu wa Kenya na Uganda.
Cha msingi kwa sasa ni kuanza personally pale unapoona fursa
Personally nimeanza na shamba la miembe eka kumi lazima nije export
NI miembe ya kisasa toka SUA pale.
\Piga ua galagaza lazima einde pande za mbali
Wakuu naomba ushauri wenu.
Nimekuwa nitembelea maduka mbali mbali katika nchi za Ulaya hasa UK na kukuta bidhaa kazaa za kutoka Uganda na Kenya lakini sijawahi kuona bidhaa zozote kutoka Tanzania katika maduka ya UK. Nikiwa Tanzania naona kuna matunda mengi kama Machungwa, Mahembe, Nanasi, Mapalachichi, nk zimerundikwa tu barabarani na vinauzwa kwa bei ya chini sana kulinganisha na bei ya Ulaya. Je kwa nini Watanzania hatuna akili ya kuweza kupeleka hivi vitu Ulaya na kupata soko zuri.
Mimi napenda sana ndizi Bukoba na huwa nazipata kwa urahisi sana katika Maduka ya UK zikiwa zina nembo ya (Product of Uganda). Hawa jamaa wananunua ndizi hata kutoka Bukoba na Karagwe. Sisi kwa nini tusifanye hivyo tena kutoka hata Mbeya? Waganda wanauza majimbi, viazi na hata nyanya chungu katika soko la Ulaya. Sisi tumelogwa?
Wakenya wametawala soko la maua, sisi kwa nini hatuwezi?
Naomba mawazo yenu
Cchallenge huwa ni ubora na kukidhi hizo taratibu kwenye uchumi Kama wetu ambapo umeme (refrigeration) na gas (transportation) is unreliable. Juu ya hapo miundombinu haikosupportive for a small farmer to produce at competitive volume, size, pesticides, mbolea etc all at levels that compete internationally.
A few years back nilinunua green beans Tesco (UK)... Nakumbuka kuwa very excited to see beans from Tanzania! Well, nilipofika home natoa kwa pack nakutana na udongo mwekundu kibao! Wakati quality control ya wengine isingepitisha pack ya namba hiyo... Hata kuosha tu alishindwa supplier Huyo wabTz?! Anyway, since then nikarudi kwenye kasumba yangu kuwa made in TZ is inferior quality... Najua huu ni upungufu kimtazamo hivyo ninalifanyia kazi. Naamini TZ tunaweza kuwa serious na kutengeneza vitu vyenye ubora wa kimataifa!
Mkuu usiwalaumu wale Board of External trade, nasema kusafirisha Bidhaa kwenda masoko ya ulaya haihitaji siasa wala haitaji kupigiwa pande mkuu, wale wanacheza na procedure pekee, ngoja kuna docoment moja ya procedure nilikuwa nayo nitaitafuta niwawekee humu muon kwamba hakuna short cut
Mkuu kati ya watu wanafiki na Wewe utakuwamo! Eti machungwa ya Muheza hayauzwi nje? Hivi unakijua kile wa-Kenya hawa wanakifanya na matunda kutoka Tz? Kwa taarifa yako hayo machungwa yakishafikishwa Kenya huwa wanafanya packaging kwenye makasha safi kabisa yenye nembo za Kenya! Wenzetu wanachotuzidi ni kuzingatia ubora maana EU standards siyo mchezo. Wakenya wakichukua hayo machungwa ya Muheza wanachambua vizuri kabisa wanayaosha vizuri kabisa na ku-pack. Hata maua ya arusha wanayalangua wao na kufanya packaging upya kwenye makreti safi kabisa yakifika Amsterdam kwenye mnada Wa maua yanaonekana yote yametoka Kenya kumbe kuna mengine yametoka Tz.Mkuu machungwa ya Muheza hayauzwi Ulaya hata siku moja, yale machungwa huwa wakenya wanachukua wanaenda kukamua juice zao na mengine wanauza mazima lakini ni within kenya, tembelea TAHA wakupe ni aina gani ya matunda na mboga ambazo zinaweza meet viwango vya kuuzwa Ulaya,
Mkuu kuingiza matunda au mboga ulaya si swala la kitoto hata siku moja, na huwezi jidanganya kwamba utakuwa unanua kwa wakulima wewe unasafirisha tu hakuna kitu kama hichio
Tafuta procedure za kufuata ili kuingiza matunda Ulaya ndo utagundua kwamba unacho ongea hakipo
Mdau mgogoro wa fedha ulikwamisha project yangu maana kuna mkopo nilikuwa nafukuzia ukagonga mwamba ila bado nina moyo one day itatichabari mkuu.
ni two years tangu uweke hiyo comment yako,vipi project yako ya maembe ina progress gani?natamani na mimi kufanya ya maembe na machungwa huko kisarawe...pia ukinipm ur mobile namba itakuwa poa zaidi tuangalie jinsi ya kushare bness info.
Thanx