Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Natamanani sana kufanya hii biashara . Mtaji ninao ila uzoefu sina
Ninataka nitoe mikoani nije niuze Dar
 
Natamanani sana kufanya hii biashara ...mtaji ninao ila uzoefu sina
Ninataka nitoe mikoani nije niuze dar
Kama unaipenda, fanya. hakuna chuo cha uzoefu bali unakuja kutokana na kufanya kazi. kujifunza ni muhimu kwa kila hatua. tafuta taarifa za masoko mara kwa mara/kila siku. kujikwaa na kuanguka kupo but taarifa sahihi zitakuokoa
 
Mimi ni mlimaji wa mahindi na pia ninategemea kuwa mzalishaji wa kati wa bidhaa za mahindi. Niko Dodoma na nnazifahamu ABC za biashara ya mahindi hapa.Tuwasiliane
 
Mkuu biashara ya mpunga ni nzuri ukiifanyia timing!
Mimi nina nunua mpunga napiga stoo!
Halafu mwezi dec - March unaukoboa unauza mchele faida x150%!

mkuu Thegame , naomba unipe uzoefu wako katika hii biashara ya mpunga, kuu-stock, then kuukoboa.
Hasa kuhusu hiyo 'timing' yake, na changamoto zake.

Natanguliza shukrani
 
kwa kukushauri nunua mchele na c mpunga ili pesa izunguke.Kwa gunia moja,garama ya kununua hadi kusafirisha kwa mfano kati ya mbeya na dar ni kati ya 135000 hadi 14000.Ukiuza unauza kati ya 160000 hadi 180000.Kwa kila gunia kuna faida kati ya 20,000 hadi 40,000.kwa hela yako unapata gunia 37 na unauza kwa jumla jumla ndani ya siku 3-5.Je,kwa mwezi utauza mara ngapi ?

Mkuu Pompiduu Sengiyumva , please naomba kuifahamu hii biashara ya mchele. Mfano kwa mtu aliepo Dar, na anataka kufanya hiyo business kwa mara ya kwanza, nini waweza kumshauri? Wapi pa kuanzia kuchukua mzigo? Kuhusu soko kwa hapa Dar? changamoto ni zipi?

Ahsante
 
habar ndugu wa JF mm nimuajiliwa nahtaj msaada wenu wa mawazo kuhusu biashara hii ya mpunga nimekopa 4m katika taasisi ya fedha ili niweze kufanya biashara hii malengo yangu kununua gunia za mpunga 100 kwa bei ya elfu 40 katika bonde la mpimbwe maarufu kwa kilimo hcho.kisha kuyauza mazao mwezi okt novemba au dec ambapo soko lake huwa zur sna kwa uzoefu nilionao kwa bei ambzo hupanda nakufikia gunia 1 tsh 60-75 bei hii ilikuwepo msimu wa mwaka jana licha ya zao hli kupatikana kwa wingi msimu uliopita tofaut kbsa na msimu huu mpunga haupatkan kwa wingi.

Ombi langu kwa wadau wa jukwaa hili naomba nisaidiwe mbinu mawazo kwa wote wafanyabiashara na wasio wafanyabiashara waliowahi kufanya biashara kma hii changamoto na nini cha kufanya ili niweze kufikia malengo yangu nawasilisha msaada wako unahitajika sana.

Mkuu ben mjukuu , please tunaomba mrejesho na uzoefu wako kaka. Ulifikia wapi hii bizna?
 
Wadau nataka kujua kuhusu biashara ya mchele ... Masoko yako vp .. Na upatikanaji wake .. Na mtaji wake .. Mwenye ujuzi anisaidie
 
Wanajamvi,habari zenu.

Naomba mwenye ujuzi kuhusu biashara ya mazao anijuze vitu kadhaa,by the way nataka nipate uelewa kidogo kuhusu biashara ya mazao hususan NAFAKA

Mimi ni mmoja kati ya wanaosubiri ajira toka serikalini baada ya kuhitimu chuo.Mpaka sasa nimeshakaa muda mrefu bila ajira ukiacha dili ndogondogo za hapa na pale,nimechoka kukaa bila kuwa na kitu maalum cha kufanya.

Nimepata wazo,na mimi nianze biashara ya mazao yaani niwe nasafiri kwenda vijijini kuchukua/kununua mazao(NAFAKA) Mfano;Ufuta,mahindi,karanga,alizeti na mpunga.

Tatizo ni kwamba sijawahi kufanya biashara yoyote ile,hivi karibuni nilizungumza na rafiki yangu mmoja ambaye yupo kijijini(DODOMA),Yeye anafanya biashara ya mpunga/mchele.ananunua huko kijijini na kuleta mjini.na kuna mjomba wangu yupo hapa mjini,yeye ana store ya mazao hususan Ufuta kwa sasa(maana ndo msimu wake),ananunua na kuuza.

Mjomba yupo tayari kuniunganisha na mtu anayeenda vijijini kununua ufuta anayemfahamu/anayemuamini niende nae vijijini akanifundishe kazi,na rafiki yangu yupo tayari niungane naye kwenye biashara ya mpunga,Wote wawili niliwauliza maswali kadhaa ambayo ningependa na nyinyi wanajamvi mchangie.(mengine sikuyauliza kabisa japo yapo hapo chini)

1. Mtaji wa kuanzia wa mpunga/ufuta minimum inaweza kuwa kiasi gani?

2. Bei ya kununua mpunga/ufuta vijijini

3. Gharama za usafirishaji wa mpunga/ufuta

4. Vifaa vya muhimu vya kwenda navyo vijijini mfano;vifaa vya kuhifadhia/packaging kama magunia nk. na gharama zake.

5. Inachukua muda gani kujaza mzigo wa pesa kama 1,000,000/= kwa mpunga/ufuta

6. Faida kwa kila gunia la ufuta/mpunga

7. Upatikanaji wa soko(DODOMA)

8. Bei ya kuuza kwa kila gunia la ufuta/mchele namaanisha kwa kilogram.

9. Challenges/risks za biashara hii ya ufuta/mpunga

10. Matakwa ya kisheria na kodi (mfano VAT) Ipoje?

11. Mengineyo,ambayo sijayaorodhesha hapo juu,tafadhali

NB: Wote wawili walikuwa na uelewa juu ya debe maarufu kama "mozambique" .hili debe lipoje?,kwa nini litumike?,bei ya hlo debe ni kiasi gani? lina tofauti gani na debe la kawaida?

Natanguliza shukurani.
 
Huja sema mtaji ulio nao!
Pia fupisha Maelezo , jikite Kwenye point wengine hawawezi kusoma maelezo malefu
Mtaji ninaoweza kupata hauzidi 1,000,000/=,by the way nnachotaka ni kujua hii biashara inaendeshwa vp angalau kwa muhtasar.
 
mtaji ninaoweza kupata hauzidi 1,000,000/=,by the way nnachotaka ni kujua hii biashara inaendeshwa vp angalau kwa muhtasar.
Mkuu,

Kabla sijatoa ushauri wangu kwako kwanza nianze kwa kukupongeza kwa WAZO ulilolipata.

Lakini pia kwa maswali ulioainisha hapo juu, kwa mtu aliyemakini tayari una majibu kwa maswali yote maana umesema tayari una jamaa zako wa karibu wanaofanya biashara hiyo na tayari wameonyesha nia ya kukubeba yaani wapo tayari kukuonyesha njia. Nitashangaa sana kwa mtu ambaye tayari anafanya biashara hiyo then hawezi kukupa majibu ya maswali uliyouliza hapo juu.

USHAURI: Mtaji ulonao ni Pesa sawa lakini kwa biashara ya mazao hiyo haitoshi na kwakuwa unayo hiyo tu nikisema nikutajie kiasi ambacho unaweza kuanza nacho na ukajisikia inafanya kazi nitakuwa kama nakukatisha tamaa hivi.

Sasa basi huo mtaji ulonao (1mil) itakulazimu ujiunge na mmoja wa hao jamaa zako ulowataja ili akubebe tu hapa nina maana kwamba mwende naye huko vijijini ambapo yeye anapata mzigo mnunue kwa maana kwamba atajulikana kwa wauzaji kuwa anayenunua ni yeye (mwenyeji wao) kumbe ndani ya mzigo kuna vigunia vyako 4-5, mkija kwenye masoko anapouza huyo jamaa yako mwachie auze yeye na baadaye anakutolea pesa yako, hapo utaona mtaji na faida yako.
Ninakupa wazo hili kutokana na ufinyu wa mtaji wako.

Kwa kufanya hivyo, utakuwa unatunisha mtaji wako, lakini pia utakuwa unapata uzoefu ktk Kazi hiyo.

Baada ya muda mtaji wako utakuwa umeongezeka, lakini pia utakuwa mzoefu ili baadaye uweze kupeperuka kwa mbawa zako.
 
Ooh ingebidi awe na kiasi gani asante mkuu.
 
nina mtaji fulani yaani hapa ninawaza cha kufanya my ig problem is time kazi inanibana sawaza nitafanyaje nahisi umasikini utaniandama milele lolz
Mkuu,

The good investment ever is to invest in yourself.

Anza na hilo kwanza ili uondoe huo uoga ulionao, ili baadaye uwe MJASIRIAMALI. Mjasiriamali hana uoga kama huo ulonao, vinginevyo utaajiriwa milele.

NOTE: Yeyote ambaye hakuwahi kuanguka maana yake hakuna siku aliyojaribu kusimama ili kutembea.
 
N
mtaji ninaoweza kupata hauzidi 1,000,000/=,by the way nnachotaka ni kujua hii biashara inaendeshwa vp angalau kwa muhtasar.
Ninao uzoefu Kwenye mchele ambao kwa kawaida faida huwa ni sh 100-200 sometimes huwa hata pungufu ya hiyo @ 1kg
Kwahiyo hela unaweza nunua 900 au 800 .
 
N
Ninao uzoefu Kwenye mchele ambao kwa kawaida faida huwa ni sh 100-200 sometimes huwa hata pungufu ya hiyo @ 1kg
Kwahiyo hela unaweza nunua 900 au 800 .
Shukran kwa mchango mkuu, hyo sio mbaya kwa faida.na kesho ntaenda kuongea na jamaa yangu anayefanya biashara ya mpunga/mchele.
 
Back
Top Bottom