Biashara ya Kubeti Michezo haina tofauti na Biashara ya kuchimba madini

Mcanada

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
982
1,904
Baada ya muda kidogo kufuatilia vifo vinavyotokana na biashara hizi mbili nimegundua kuwa utofauti uliopo baina ya biashara hizi ni kwamba Betting haiitaji mtaji mkubwa wa kifedha bali inahitaji mtaji mkubwa wa akili (Intelligence); Biashara ya Betting inatumia akili zaidi na inakupasa uwe na uwezo mkubwa wa sayansi ya hisabati, uwe na reasoning intelligence, na kubwa zaidi uwe na uwezo mkubwa wa kufanya insight analysis(uchambuzi wa kina).. wakati biashara ya madini inahitaji zaidi rasilimali watu, vitendea kazi na mtaji wa kutosha.. Katika biashara hizi mbili zote zina matokeo yanayofanana na hasara zinazofuatana..

Katika uchunguzi wangu wa kina sana Betting ni biashara yenye High risk kuliko biashara ya madini japo biashara ya madini nayo si salama kwa watu wenye moyo mdogo na uliosinyaa.. hizi biashara mbili zinahitaji kufanywa na watu wenye akili kubwa (High IQ), watu wenye mioyo mipana maana ukifanya biashara hizi kucheka ni dakika 0 na kupaniki huku ukichwagizwa na kuchanganyikiwa ni dakika 0 piaaa (Emotional Intelligence)..

USHAURI WANGU: ukijishajikagua na ukagundua wewe akili yako ni ndogo, huwezi kujicontrol kihisia usifanye biashara yoyote yenye sifa za High Risk fanya biashara ambazo ni low risk maana kuna hatari ya kufa mapema ukijiingiza kwenye biashara za namna hiyo.. ndio maana kuna biashara ni halali kwenye makaratasi tu haya ya kisheria ila kwenye uhalisia ni haramu kwa matumizi ya binadamu... hupaswi kuzifanya.. ntazitaja siku nyingine.. uwe na siku njema..
 
Betting pasua kichwa Sana,

Imagine
Umempa mancity direct win na point zake kiduchu mpk dkk ya 89 inaongoza 0:1 uku anamiliki mpira kwa Zaid ya 70%

Unaondoka zako kulala ukijua mkeka umeshatick, ushaamka na kibunda tayari.

Asbh unaamka unaambiwa mechi imeisha 3:1
IMG_20220505_040147.jpg
 
Juzi Jumamosi
Kuna dogo mmoja alikua na mkeka wa karatasi stake 2,000 unaleta mil.12.8 kule galsport.

Timu zote ngumu zimetick kabaki astonvila na bayern na wote wako nyumbani.

Kajaribu kuuingiza kwny mashine aone cash out anapata Bei gani, cashout ikasoma mil 3.5 kwa matokeo yaliyopo Hadi Sasa.

Dogo akawa anawaza kuichukua hiyo hiyo TU mil. 3.5 Ila anaiogopa mechi ya Aston Vila inaweza kuuchana mkeka.

Ikabd aseme anaichukua hiyo mil.3.5 asije kosa yote maana Hajawahi hata kuishika Iyo ela.

Wadau wakaugombania sn ule mkeka awauzie,
Kuna mzee mmoja akajitokeza na dau kubwa na kununua ule mkeka kwa mil. 6 cash, dogo kapewa ela yake na kaenda zake.

Mechi ya astonvila imeisha kashinda 3:1,akabaki anasubiriwa bayern TU mkeka mzima wa mil.12.8

Huwezi amini,
Hiyo mechi Bayern sare ya 1:1 na Yuko nyumbani ikiwa na odd chache sn kuliko mechi zote

yaani mechi yenye odds 1.2 ikauchana mkeka mzima wenye odds 6,000+
 
Wadau wakaugombania sn ule mkeka,

Huyo mzee hakudondoka presha kweli?
 
Acha kufananisha betting na madini. Sijawah kuona mtu anaebeti kamiliki guest lakini nawafahamu madon wengi waliotokana na biashara ya madini.

Anza na mzee anaemiliki WAJA, kuna dogo mwingine insta anapost sana hela, majumba na magari lakini nilishakutana nae machimboni unaweza kumsahau, wapo wengi sana.

Nakuona mpuuzi tu unavyofananisha mambo ya kihuni na kazi za watu

Betting kinachoangusha ni tamaa tu.

Nimepumzika kubet. Nilimwekea mtu Million 1 kwenye tennis ili nipate Million na point, akashindwa mbwa yule.
ukiweza kujicontrol kihisia utafanikiwa sana kwenye haya maisha
 
Nilikuwa na shida na Million ya Haraka. Nikaingia Sportybet live bet, nikatia Million. Chagua waliokuwa wanaongoza kwa set moja, odds kiduchu. Tia Million.

Ma.mae, nilichokutana nacho ni kiboko. Nikachomoa Million nyingine tu. Ile ikaenda na maji.
Screenshot_20230419-123342_1.jpg
 
Ili uifurahie betting yakupaswa uwe waangalia mechi husika.
Maana yake inabidi uwe na uelewa wa mchezo husika
Uwe na access ya kuangalia mchezo husika
Hapo ndo inakuwa rahisi kujua nini ufanye
 
Baada ya muda kidogo kufuatilia vifo vinavyotokana na biashara hizi mbili nimegundua kuwa utofauti uliopo baina ya biashara hizi ni kwamba Betting haiitaji mtaji mkubwa wa kifedha bali inahitaji mtaji mkubwa wa akili (Intelligence); Biashara ya Betting inatumia akili zaidi na inakupasa uwe na uwezo mkubwa wa sayansi ya hisabati, uwe na reasoning intelligence, na kubwa zaidi uwe na uwezo mkubwa wa kufanya insight analysis(uchambuzi wa kina).. wakati biashara ya madini inahitaji zaidi rasilimali watu, vitendea kazi na mtaji wa kutosha.. Katika biashara hizi mbili zote zina matokeo yanayofanana na hasara zinazofuatana..

Katika uchunguzi wangu wa kina sana Betting ni biashara yenye High risk kuliko biashara ya madini japo biashara ya madini nayo si salama kwa watu wenye moyo mdogo na uliosinyaa.. hizi biashara mbili zinahitaji kufanywa na watu wenye akili kubwa (High IQ), watu wenye mioyo mipana maana ukifanya biashara hizi kucheka ni dakika 0 na kupaniki huku ukichwagizwa na kuchanganyikiwa ni dakika 0 piaaa (Emotional Intelligence)..

USHAURI WANGU: ukijishajikagua na ukagundua wewe akili yako ni ndogo, huwezi kujicontrol kihisia usifanye biashara yoyote yenye sifa za High Risk fanya biashara ambazo ni low risk maana kuna hatari ya kufa mapema ukijiingiza kwenye biashara za namna hiyo.. ndio maana kuna biashara ni halali kwenye makaratasi tu haya ya kisheria ila kwenye uhalisia ni haramu kwa matumizi ya binadamu... hupaswi kuzifanya.. ntazitaja siku nyingine.. uwe na siku njema..
Unajua maana ya betting ?? Hata walioianzisha walisema ni kubashiri..sasa wewe hayo mambo ya intelligence mara sjui sayansi umeyatoa wapi
 
msingi mkuu wa betting ni bahati bana.

ipo hivi kuna dada aliniambia nifundishe kubeti kwenye simu nikamfundisha akawa anacheza direct,anacheza tu kwa kukisia au kubahatisha na mikeka mingi anashinda.wakati mimi ninaeumiza kichwa na kuzijua timu napasua mikeka.

si wanasemaga weka mechi moja au mbili kisha weka mzigo mnono,my frend naweka mpaka laki mbili odds 1.5 lakini hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom