Nina milioni 6: Nahitaji partner wa biashara

Kassym

Member
Dec 2, 2018
6
9
Ninayo milioni 6 kwa ajili ya biashara. Nahitaji partner wa kufanya nae biashara. Partner ni lazima awe tayari kuwekeza kiasi hicho hicho cha pesa kwenye biashara. Yaani jumla tuwe na milioni 12.

AINA YA BIASHARA
Nipo tayari kufanya biashara yoyote kati ya hizi;
1) Alluminium
2) Kuuza spare za pikipiki na bajaji
3) Welding
4) Ufundi simu na kuuza vifaa vya simu
5) Car wash
6) Njoo na wazo lingine

KWANINI NAHITAJI PARTNER?
Sababu hizi zinafanya nihitaji partner
1) Kuongeza mtaji
2) Kuongeza msimamizi mwingine wa biashara mwenye uchungu na nia ya dhati ya kuiendeleza kwa kuwa atakuwa ameweka pesa yake

Aliye na mtaji kama huo au chini kidogo ya hapo na yupo tayari kuwekeza pamoja na mimi tafadhali karibu pm au hapa kwenye uzi. Tutatengeneza makubaliano ya kisheria kabla ya kuanza biashara. Wale wenye maoni na ushauri pia nawakaribisha. Nipo Dar.
 
Huo mtaji mbona unatosha kabisa kuanzisha biashara yako mwenyewe! Mimi nakushauri upambane mwenyewe, badala ya kutafuta partinership na mtu ambaye humfahamu.

Kwanza unatakiwa ufahamu biashara nzuri ni ile unayoanza na mtaji mdogo, halafu baadaye ikishaimarika na kuzoeleka ndiyo unaongeza sasa mtaji.
 
Kibongo bongo Bora ufanye peke yako. Ni ngumu sana kumpata partner muaminifu asilimia Mia moja, wapo ila wachache sana.
Unless anataka kulia kilio cha mbwa..haya mambo ya partnership kibongo bongo ni ngumu..ndugu tu wakishea biashara wanagombana sembuse mtu baki...halaf huo mtaji mbona unatosha kuanza biashara moja wapo kati ya hizo alizotaja...start small akikua ndo ataweka pesa nying.
 
Ninayo milioni 6 kwa ajili ya biashara. Nahitaji partner wa kufanya nae biashara. Partner ni lazima awe tayari kuwekeza kiasi hicho hicho cha pesa kwenye biashara. Yaani jumla tuwe na milioni 12.

AINA YA BIASHARA
Nipo tayari kufanya biashara yoyote kati ya hizi;
1) Alluminium
2) Kuuza spare za pikipiki na bajaji
3) Welding
4) Ufundi simu na kuuza vifaa vya simu
5) Car wash
6) Njoo na wazo lingine

KWANINI NAHITAJI PARTNER?
Sababu hizi zinafanya nihitaji partner
1) Kuongeza mtaji
2) Kuongeza msimamizi mwingine wa biashara mwenye uchungu na nia ya dhati ya kuiendeleza kwa kuwa atakuwa ameweka pesa yake

Aliye na mtaji kama huo au chini kidogo ya hapo na yupo tayari kuwekeza pamoja na mimi tafadhali karibu pm au hapa kwenye uzi. Tutatengeneza makubaliano ya kisheria kabla ya kuanza biashara. Wale wenye maoni na ushauri pia nawakaribisha. Nipo Dar.
Achana na biashara ya partnership na wabongo utapoteza muda na pesa uskoy

Ungana na Mshana Jr muende China mwezi March, kwa hiyo 6M yako huko utapata Elimu, Exposure na mzigo kidogo wa kuanzia kazi

Na kama hivo haivitoshi utapata fursa ya kuijua vizuri hiyo biashara ya vifaa vya simu maana utakuwa umeenda jikoni kabisa
 
Huo mtaji mbona unatosha kabisa kuanzisha biashara yako mwenyewe! Mimi nakushauri upambane mwenyewe, badala ya kutafuta partinership na mtu ambaye humfahamu.

Kwanza unatakiwa ufahamu biashara nzuri ni ile unayoanza na mtaji mdogo, halafu baadaye ikishaimarika na kuzoeleka ndiyo unaongeza sasa mtaji.
Nachukua huu ushauri. 🙏🏽
 
Achana na biashara ya partnership na wabongo utapoteza muda na pesa uskoy

Ungana na Mshana Jr muende China mwezi March, kwa hiyo 6M yako huko utapata Elimu, Exposure na mzigo kidogo wa kuanzia kazi

Na kama hivo haivitoshi utapata fursa ya kuijua vizuri hiyo biashara ya vifaa vya simu maana utakuwa umeenda jikoni kabisa
🙏🏽
 
Back
Top Bottom