Biashara ya Digrii kutoka Uingereza na Marekani ni Ugonjwa kwa watu wengi

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
2,150
4,754
Na Dr. Mathew Mndeme

UTANGULIZI
Kwenye miaka ya 1990 kuja hadi around 2015, nchi za Ulaya na hasa Uingereza na Marekani vilikumbwa na tatizo kubwa sana la uhamiaji haramu (illegal migration). Kulikuwa na wimbi kumbwa sana la wahamiaji hasa kutoka nchi za Afrkika na Asia. Watu wengi walikuwa wanaingia kwenye hizi nchi kwa utaratibu ambao ulionekana ni wa kihalali lakini walipofika walikuwa hawafanyi kile kilichowapeka. Badala yake wanapotelea kusikojulikana na mfumo wa nchi na kuzamia bila kurudi makwao.

MCHONGO WA VYUO
Moja ya njia kuu iliyokuwa inatumika sana na wahamiaji hawa ni kutafuta usahili (admission) ya vyuo vikuu na “scholarships” hivyo kuwafanya kupata “student visa” kirahisi. Kulikuwa na maelfu ya vyuo hewa/fake vilivyokuwa vinafanya hii biashara ya kuingiza watu. Cha kukusitikisha viko vingi vilivyokuwa vinajitambulisha kama vya “vyuo vya kikristo” almaarufu kama “Bible/ Theological Colleges/Schools”. Hivi vilipewa majina mazuri mazuri ya kimbinguni na kibiblia na kutoa diploma na degree zenye majina yanayovutia utadhani yanatoa pepo. Nani hatavutiwa na cheti kimeandikwa “Diploma/Degree in Demon Rebuking, Church Planting and Speaking in Tongues”?

Waliokuwa "wanachangamkia hizi fursa" walikuwa wanalipa pesa nyingi kupata admission. Ukishafanikiwa kuingia unapiga vibarua mtaani kisha unalipa tena kiwango kikubwa kupewa cheti hewa kuwa ulisoma na kumaliza. Ili kuonesha umesoma, vyuo vilikuwa vinaweka hadi rekodi fake ya mahudhurio darasani.

Kwa mfano, report moja ya Kamati ya Bunge la Mabwenyenye la Uingereza (House of Commons) ya mwaka 2009 ilionesha “wanafunzi hewa” walikua wanalipa kama million 3 kupata admission na kama milioni 8 kupata cheti fake. Taarifa nyingine ya mwaka 2004 ilionesha kuwa kati ya vyuo 400 ambavyo maafisa wa uhamiji waliamua kuvitembelea kupata uhalali wake wa kuingiza watu, walikuta 100 ni vyuo hewa. Report nyingine ya mwaka 2009 ya bunge hilo, ilionesha kwa miaka kdhaa vyuo fake zaidi ya 2000 vilikuwa vimetumika kuingiza wahamiaji haramu Uingereza.

Serikali ya Uingereza ilichukua hatua kali za kuzuia uhamiaji haramu ikiwa ni pamoja na idara ya uhamiaji kuorodhesha vyuo vilivyokuwa na uhalali kuingiza watu. Pia serikali ilifuta mamia ya vyuo vilivyokuwa vinafanya biashara hii haramu. Kwa mfano, wakati wa uongozi ya David Cameroon (2010 – 2016), serikali ilifuta vyuo fake zaidi ya 700.

Baada ya vyuo hivi kudhibitiwa, “upateli” wa utoaji degree hewa ulipata sura nyingine. Kwa kuwa haikuwezekana tena watu kwenda kufuata “elimu hizi hewa” huko Ulaya na Marekani, vyuo fake vimeanzisha ama matawi au kuwa na wawakala kwenye nchi za Kiafrika. Biashara hii imeshika kasi sana na imetujazia watu wenye diploma na degree fake, hasa PhD fake, za kumwaga mitaani.

Hizi degree ninazoziongelea sio kama zile za kununua cash (PhD za heshima) ambazo “mamia ya watumishi na wapendwa” wanazo. Hizi zina aina fulani ya uhalali kwamba mtu amesoma ila kwa mtindo uliojaa umagumashi au kwa utaratibu usiokidhi viwango vya mtu kupewa degree.

Moja ya mtindo unaotumiwa na vyuo hivi ni kutumia “mawakala” ambao ni wenyeji kuandaa sherehe za mahafali hapahapa nyumbani na wahusika kupewa degree. Wanatafuta watu wenye majina au heshima kwenye jamii ambao wanatumika kama “wavaa majoho ya kutisha” kutunukia “wahitimu” degree. Wakati mwingine wanatuma wawakilishi (hasa watu weupe) kuja kufanya zoezi hilo la kutunuku degree. Degree zao zina majina mazuri sana kama waliopata tickets za kuingia mbinguni.

"WAPENDWA" NA "WATUMISHI"
Kinachosikitisha sana, wengi wa wateja wa biashara hii ya degree ni “watumishi” wa makanisa ya ki-Pentecost na hata yale ya Protestant. Imefika mahali imekuwa ni mtindo kwamba ukiwa mchungaji au askofu hainogi bila pia kuitwa “Dr Nahiii Nabii na Mtume wa Karne ya 22”.

Ukitaka kuona uzito wa tatizo hili, orodhesha maaskofu na wachungaji wote unaowajua wanaitwa "Dr Nanihii" au wanaosema wana degree au masters fulani. Kisha nenda online tafuta maandiko yao ya Masters au PhD na majina ya vyuo walivyosoma. Kwa hakika kabisa, wengi wao hutapata chochote cha elimu hiyo kinachowahusu. Kikubwa labda utapata mahubiri yao Youtube na kauli nyingine nyingine walizotoa zikawapa umaarufu. Ukibahatika kupata vyuo vilivyowapa hizo PhDs, tafuta majina yao na angalia vimesajiliwa wapi au uhalali wao. Utashangaa.

Wapendwa na Watumishi wenye hizi degrees za michongo huwa hawaongelei kabisa vyuo walivyosoma, na walisoma au alitafiti nini hasa. Hupenda kujitambulisha kwa picha za majoho mazuri mazuri, kutaja yale majina matamu ya degree walizopewa, na kauli za "kujisifu au kumshukuru Mungu kwa kuwainua". Pamoja na kukiri wana degree hii au ile au wana PhD, wakifungua kinywa huoni kabisa maarifa waliyonayo wala uelewa wa mambo unalingana na kiwango cha elimu wanachodai wanacho. Wanaongea vitu kimichongo sana kama zilivyo degree zao.

Labda ujue tu kwamba, kwa dunia ya sasa hakuna chuo kikuu kinampa mtu degree ya Masters au PhD nyuma ya pazia. Lazima taarifa za mwanafunzi husika zipatikane mtandaoni. Hii ni pamoja na jina la chuo na idara aliyosoma, shahada aliyosoma, andiko (thesis/dissertation) aliyoandika, utafiti wake ulihusu nini, andiko au machapisho (publications) yake yatapatikana mtandaoni, na alisimamiwa na nani kwenye huo utafiti. Ukikosa sehemu kubwa ya taarifa hizi, jibu la authenticity ya hiyo degree tayari unalo.

MASWALI YA KUJIULIZA
(1) Kwanini tunataka elimu za “mchongo”?
(2) Kwanini tunataka hadhi tusiyoistahili?
(3) Kwanini tunataka ngazi ambazo hatujazifikia au tunajua hatuna uwezo wa kuzifikia?

Maswali haya na mengine yana umuhimu zaidi kwa wale wanaopata elimu hizi kwa migongo ya imani (ukristo). Hivi "imani" na maandiko vinawapa uhalali gani kuwa na elimu, titles, heshima, au hadhi za “mchongo”?

Unapataje amani kutembea unaitwa “Dr Mwenye Upako wa Kutisha” au kuijitambulisha una degree au masters fulani huku ukijua huna elimu husika, na mbaya zaidi maarifa uliyonayo hayawakilishi elimu unayotaka watu wajue unayo? Hii "amani" kama unayo, ni ya aina gani na inatoka wapi?

Mungu na atusaidie tuisimamie kweli ya Mungu .
 
BIASHARA YA DEGREE ZA THEOLOGY TOKA ULAYA NA MAREKANI: UGONJWA UNAOTAFUTA “WATUMISHI” NA "WAKRISTO" WENGI

Na Dr. Mathew Mndeme

UTANGULIZI
Kwenye miaka ya 1990 kuja hadi around 2015, nchi za Ulaya na hasa Uingereza na Marekani vilikumbwa na tatizo kubwa sana la uhamiaji haramu (illegal migration). Kulikuwa na wimbi kumbwa sana la wahamiaji hasa kutoka nchi za Afrkika na Asia.

Watu wengi walikuwa wanaingia kwenye hizi nchi kwa utaratibu ambao ulionekana ni wa kihalali lakini walipofika walikuwa hawafanyi kile kilichowapeka. Badala yake wanapotelea kusikojulikana na mfumo wa nchi na kuzamia bila kurudi makwao.

MCHONGO WA VYUO
Moja ya njia kuu iliyokuwa inatumika sana na wahamiaji hawa ni kutafuta usahili (admission) ya vyuo vikuu na “scholarships” hivyo kuwafanya kupata “student visa” kirahisi. Kulikuwa na maelfu ya vyuo hewa/fake vilivyokuwa vinafanya hii biashara ya kuingiza watu.

Cha kukusitikisha viko vingi vilivyokuwa vinajitambulisha kama vya “vyuo vya kikristo” almaarufu kama “Bible/ Theological Colleges/Schools”. Hivi vilipewa majina mazuri mazuri ya kimbinguni na kibiblia na kutoa diploma na degree zenye majina yanayovutia utadhani yanatoa pepo.

Nani hatavutiwa na cheti kimeandikwa “Diploma/Degree in Demon Rebuking, Church Planting and Speaking in Tongues”?

Waliokuwa "wanachangamkia hizi fursa" walikuwa wanalipa pesa nyingi kupata admission. Ukishafanikiwa kuingia unapiga vibarua mtaani kisha unalipa tena kiwango kikubwa kupewa cheti hewa kuwa ulisoma na kumaliza. Ili kuonesha umesoma, vyuo vilikuwa vinaweka hadi rekodi fake ya mahudhurio darasani.

Kwa mfano, report moja ya Kamati ya Bunge la Mabwenyenye la Uingereza (House of Commons) ya mwaka 2009 ilionesha “wanafunzi hewa” walikua wanalipa kama million 3 kupata admission na kama milioni 8 kupata cheti fake.

Taarifa nyingine ya mwaka 2004 ilionesha kuwa kati ya vyuo 400 ambavyo maafisa wa uhamiji waliamua kuvitembelea kupata uhalali wake wa kuingiza watu, walikuta 100 ni vyuo hewa.

Report nyingine ya mwaka 2009 ya bunge hilo, ilionesha kwa miaka kdhaa vyuo fake zaidi ya 2000 vilikuwa vimetumika kuingiza wahamiaji haramu Uingereza.

Serikali ya Uingereza ilichukua hatua kali za kuzuia uhamiaji haramu ikiwa ni pamoja na idara ya uhamiaji kuorodhesha vyuo vilivyokuwa na uhalali kuingiza watu.

Pia serikali ilifuta mamia ya vyuo vilivyokuwa vinafanya biashara hii haramu. Kwa mfano, wakati wa uongozi ya David Cameroon (2010 – 2016), serikali ilifuta vyuo fake zaidi ya 700.

Baada ya vyuo hivi kudhibitiwa, “upateli” wa utoaji degree hewa ulipata sura nyingine. Kwa kuwa haikuwezekana tena watu kwenda kufuata “elimu hizi hewa” huko Ulaya na Marekani, vyuo fake vimeanzisha ama matawi au kuwa na wawakala kwenye nchi za Kiafrika.

Biashara hii imeshika kasi sana na imetujazia watu wenye diploma na degree fake, hasa PhD fake, za kumwaga mitaani.

Hizi degree ninazoziongelea sio kama zile za kununua cash (PhD za heshima) ambazo “mamia ya watumishi na wapendwa” wanazo. Hizi zina aina fulani ya uhalali kwamba mtu amesoma ila kwa mtindo uliojaa umagumashi au kwa utaratibu usiokidhi viwango vya mtu kupewa degree.

Moja ya mtindo unaotumiwa na vyuo hivi ni kutumia “mawakala” ambao ni wenyeji kuandaa sherehe za mahafali hapahapa nyumbani na wahusika kupewa degree. Wanatafuta watu wenye majina au heshima kwenye jamii ambao wanatumika kama “wavaa majoho ya kutisha” kutunukia “wahitimu” degree.

Wakati mwingine wanatuma wawakilishi (hasa watu weupe) kuja kufanya zoezi hilo la kutunuku degree. Degree zao zina majina mazuri sana kama waliopata tickets za kuingia mbinguni.

"WAPENDWA" na "WATUMISHI"
Kinachosikitisha sana, wengi wa wateja wa biashara hii ya degree ni “watumishi” wa makanisa ya ki-Pentecost na hata yale ya Protestant. Imefika mahali imekuwa ni mtindo kwamba ukiwa mchungaji au askofu hainogi bila pia kuitwa “Dr Nahiii Nabii na Mtume wa Karne ya 22”.

Ukitaka kuona uzito wa tatizo hili, orodhesha maaskofu na wachungaji wote unaowajua wanaitwa "Dr Nanihii" au wanaosema wana degree au masters fulani. Kisha nenda online tafuta maandiko yao ya Masters au PhD na majina ya vyuo walivyosoma.

Kwa hakika kabisa, wengi wao hutapata chochote cha elimu hiyo kinachowahusu. Kikubwa labda utapata mahubiri yao Youtube na kauli nyingine nyingine walizotoa zikawapa umaarufu. Ukibahatika kupata vyuo vilivyowapa hizo PhDs, tafuta majina yao na angalia vimesajiliwa wapi au uhalali wao. Utashangaa.

Wapendwa na Watumishi wenye hizi degrees za michongo huwa hawaongelei kabisa vyuo walivyosoma, na walisoma au alitafiti nini hasa. Hupenda kujitambulisha kwa picha za majoho mazuri mazuri, kutaja yale majina matamu ya degree walizopewa, na kauli za "kujisifu au kumshukuru Mungu kwa kuwainua".

Pamoja na kukiri wana degree hii au ile au wana PhD, wakifungua kinywa huoni kabisa maarifa waliyonayo wala uelewa wa mambo unalingana na kiwango cha elimu wanachodai wanacho. Wanaongea vitu kimichongo sana kama zilivyo degree zao.

Labda ujue tu kwamba, kwa dunia ya sasa hakuna chuo kikuu kinampa mtu degree ya Masters au PhD nyuma ya pazia. Lazima taarifa za mwanafunzi husika zipatikane mtandaoni.

Hii ni pamoja na jina la chuo na idara aliyosoma, shahada aliyosoma, andiko (thesis/dissertation) aliyoandika, utafiti wake ulihusu nini, andiko au machapisho (publications) yake yatapatikana mtandaoni, na alisimamiwa na nani kwenye huo utafiti. Ukikosa sehemu kubwa ya taarifa hizi, jibu la authenticity ya hiyo degree tayari unalo.

MASWALI YA KUJIULIZA
(1) Kwa nini tunataka elimu za “mchongo”?
(2) Kwa nini tunataka hadhi tusiyoistahili?
(3) Kwa nini tunataka ngazi ambazo hatujazifikia au tunajua hatuna uwezo wa kuzifikia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msumari wa MOTO huu...........
 
Mkuu hali ya Watumishi kuwa na degree fake haiwakoseshi amani wahusika kwa sababu hawamtumikii Mungu. Hao ni mawakala wa shetani kwa hiyo wana amani ya shetani kwa kujisifu kuwa na ujuzi wasiokuwa nao.
 
Utashi wa watu umekufa, wizi, rushwa, uongo na ubadhirifu ndio vimeshika kasi. Taifa linaangamia!
 
Kuna jamaa yangu muda si mrefu atakuwa tajiri. Maana ana kipaji cha kuhubiri, halafu akaingia zake darasani kwa miezi michache; Wamarekani wakamtunuku shahada yake ya theolojia!

Nawaza na mimi sijui nikasome! 🤔 Tena ukichukulia na ule msemo wa wajinga ndiyo waliwao!! Yaani ni kukemea tu mapepo, viwete kutembea, na wenye magonjwa kupona; kupitia maji, sabuni, na mafuta yenye upako!
 
Hongera kwa kuliona hili. Degree, Masters na PhD za michongo Tanzania zimejaa kibao hasa kwa WACHUNGAJI NA WANASIASA
 
Hakika michongo imenoga Kwa watumishi kujibandika madregee ili kuwachota vizuri wagalatia wasiojua hili wala lile
 
Hili andiko mujarab kabisa! Nakiri kanisa naloabudu nimewahi kua na kiongozi wa dhehebu mwenye Phd ila anayotenda hata hayafanani!
 
Back
Top Bottom