Uchaguzi 2020 Bernard Membe hana kabisa mvuto!

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
1,141
2,000
Ngoja nikuulize maswali mawili:-

1. Kama umewahi kuwasikiliza wote wawili, nani muongeaji mzuri kati ya Mkapa na JK?
2. Kwa maoni yako, ni nani charismatic leader kati ya hao wawili?!

Kila mmoja ana uwezo wake, Mkapa ni great thinker na more knowledgeable kuliko kikwete, lakini Kikwete yupo very charismatic na ana fit sana na sisi wa Mujini.
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,142
2,000
Nafuatilia michango yako kidogo naota moto kwenye baridi, sasa why you do not see our serious shortcomings?, na kama shortcomings haziwi amplified zitaondokaje ili tuweze kuchukua dola?
Nakuonya kisiasa, hii kuhusu Membe - usirukie mchezo wa drafti ambao wenzako wameupanga. Ukikuta wewe vuruga panga upya kwa kuwa ule ulioukuta wamepanga hautakuwa na control nao.
Ndio maana nimesema ni speculation na nimeongelea kwa perception za watu tofauti ili tuwe na balanced discussion.

But anyway hata kma ingekua draft ya CCM haina madhara tena maana tulipata mgombea wetu so bado huwezi wapa credit upinzani kwa hilo?
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,142
2,000
Watu wasio na mipango mnafuata upepo tu.
Hakuna upepo hapo ila calculated move. Hata Nape alipogombana na mwenyekiti wake nadhani uliona wapinzani walivyoshabikia yote kwa yote kuona tu vurumai kwa adui yako ila sio kwamba walimpenda Nape.

Unakumbuka hata ugomvi wa Mwambe na Mbowe, CCM nzima ilimsupport Mwambe. Unadhani walikuwa wanampenda? Hapana Ila walitaka tu kuchochea mgogoro ili chama kipasuke.

But nadhani uliona kuanzia chaguzi za ndani Hakuna mwana CCM alichaguliwa, udiwani na ubunge wembe ule ule na hata Urais it was clear toka 2016 kwamba contender ni Lissu. Sasa ni wapi tumefuata mkumbo? Afterall Membe alipotimuliwa unakumbuka Mbowe alitoa kauli gani?

Politics is an art my friend
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,751
2,000
Kila mmoja ana uwezo wake, Mkapa ni great thinker na more knowledgeable kuliko kikwete, lakini Kikwete yupo very charismatic na ana fit sana na sisi wa Mujini.
Umejibu kwa usahihi, na nilikuuliza hayo maswali kukuonesha kwamba charisma na kujua kuongea/kutawala jukwaa ni mambo mawili tofauti kwa sababu wakati uliyekuwa umem-quote alikuwa anazungumzia suala la charismatic leadership lakini maelezo yako yalizungumzia suala la uwezo wa kuongea na kueleweka!!!

So, huyo huyo unayemuona ana-fit zaidi kwa watu wa mjini, kama he's really charimastic leader basi atafit kotekote bila kujali uwezo wake wa kuweza kuongea na watu wa makundi mbalimbali!

Na huyo mwingine, ataendelea kulazimisha kuwa a funny leader na kuishia kutoa vile anavyodhani ni vichekesho vinavyoacha maswali mengi kwa wasikilizaji kwa sababu he's not that funny but he wants to be described as a funny guy and become more attractive na kuonesha haiba nzuri kwa jamii, lakini kama hana karama ya mvuto, atabaki tu kueleweka na wengi lakini ataendelea kukosa haiba mbele yao!
 
moto wa kifuu

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
326
225
Hivi lengo la upinzani ni kumtoa Magu au ccm?
Maana mlianza kumshabikia Membe akiwa ccm
Nahisi ni Magu. Mishale mingi naona inarushwa kwake. Nadhani wanaona "aliwakwaza" kwa kusafisha uso wa chama chake. Hiyo imewapa ugumu, maana amewakosesha sera rahisi kueleweka kwa mtu wa kawaida.
 
moto wa kifuu

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
326
225
Yes kuitoa CCM automatic unamtoa Magufuli. Kumshabikia Membe maana yake kuchochea mvurugano kati ya chama na eventually kipasuke maana asingemtoa Magufuli kirahisi hivo.

Na kwa matokeo yoyote yale ingekua advantage kwa upinzani kutumia fursa kujijenga. Rejea mtifuano wa Ruto na Uhuru si unaona kina odinga wanajijenga maana wanajua jubilee inapasuka 2022!!

Kwahiyo sio kwamba tulimpenda sana Membe ila maadam angeweza kuleta mgawanyiko CCM ama kumtoa jiwe basi ndio maana tukawa tunapiga kelele mitandaoni

NB: Hizo kelele zilituisha baada ya Lissu kutua kwa kishindo Dar, upepo ukahama rasmi maana tulipata serious contender wa magufuli na CCM
Msema kweli mpenzi wa mwenyezi Mungu.
 
Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
1,141
2,000
Umejibu kwa usahihi, na nilikuuliza hayo maswali kukuonesha kwamba charisma na kujua kuongea/kutawala jukwaa ni mambo mawili tofauti kwa sababu wakati uliyekuwa umem-quote alikuwa anazungumzia suala la charismatic leadership lakini maelezo yako yalizungumzia suala la uwezo wa kuongea na kueleweka!!!

So, huyo huyo unayemuona ana-fit zaidi kwa watu wa mjini, kama he's really charimastic leader basi atafit kotekote bila kujali uwezo wake wa kuweza kuongea na watu wa makundi mbalimbali!

Na huyo mwingine, ataendelea kulazimisha kuwa a funny leader na kuishia kutoa vile anavyodhani ni vichekesho vinavyoacha maswali mengi kwa wasikilizaji kwa sababu he's not that funny but he wants to be described as a funny guy and become more attractive na kuonesha haiba nzuri kwa jamii, lakini kama hana karama ya mvuto, atabaki tu kueleweka na wengi lakini ataendelea kukosa haiba mbele yao!

Muona wangu na political strategist wote wanakubali: Magufuli ndio kiongozi aliye iimarisha CCM ambayo ilikuwa inaenda kujifia.
Na sasa hivi ndio chama imara kuliko muda wowote labda tuu wakati wa Nyerere.
Results ndizo zitakazo kuonyesha ubora wa kiongozi yeyote na sio vinginevyo. Kwa sababu hakuna formular maalumu inayofahamika kuwa sahihi kabisa kufikia unayoyataka kisisasa.

Uchaguzi huu na matokeo yake yatatupa nafasi ya kutosha kuandika daftari upya ya mifumo ya kisiasa mipya mbali tuliokuwa tukiifahamu. Hii itaongeza ufahamu kwa wengi ambao tunapenda kufuatia mienendo ya kisiasa.

Mimi ni upande wa upinzani lakini ni muhalisia katika uchambuzi bila kuweka upendeleo na kuongozwa na hisia kisiasa kwa kadiri nionavyo. Kwa umri wangu muda wa hisia ulikwisha kitambo.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,914

Hivi inawezekanaje kujua kama kweli Magufuli kaiimarisha CCM kupitia huu uchaguzi wakati uwanja wa mechi hauko sawa?
 
WILE

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
4,095
2,000
Yes kuitoa CCM automatic unamtoa Magufuli. Kumshabikia Membe maana yake kuchochea mvurugano kati ya chama na eventually kipasuke maana asingemtoa Magufuli kirahisi hivo.

Na kwa matokeo yoyote yale ingekua advantage kwa upinzani kutumia fursa kujijenga. Rejea mtifuano wa Ruto na Uhuru si unaona kina odinga wanajijenga maana wanajua jubilee inapasuka 2022!!

Kwahiyo sio kwamba tulimpenda sana Membe ila maadam angeweza kuleta mgawanyiko CCM ama kumtoa jiwe basi ndio maana tukawa tunapiga kelele mitandaoni

NB: Hizo kelele zilituisha baada ya Lissu kutua kwa kishindo Dar, upepo ukahama rasmi maana tulipata serious contender wa magufuli na CCM
Watu wasio a mipango mnafuata upepo tu.
Hakuna upepo hapo ila calculated move. Hata Nape alipogombana na mwenyekiti wake nadhani uliona wapinzani walivyoshabikia yote kwa yote kuona tu vurumai kwa adui yako ila sio kwamba walimpenda Nape.

Unakumbuka hata ugomvi wa Mwambe na Mbowe, CCM nzima ilimsupport Mwambe. Unadhani walikuwa wanampenda? Hapana Ila walitaka tu kuchochea mgogoro ili chama kipasuke.

But nadhani uliona kuanzia chaguzi za ndani Hakuna mwana CCM alichaguliwa, udiwani na ubunge wembe ule ule na hata Urais it was clear toka 2016 kwamba contender ni Lissu. Sasa ni wapi tumefuata mkumbo? Afterall Membe alipotimuliwa unakumbuka Mbowe alitoa kauli gani?

Politics is an art my friend
Nimependa ulivyomalizia tu. Tatizo its the art the current opposition lacks. Hadi sasa wenzenu wapo major league nyie mnafurahia league za mchangani. Amkeni.
 
Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
1,141
2,000
Hivi inawezekanaje kujua kama kweli Magufuli kaiimarisha CCM kupitia huu uchaguzi wakati uwanja wa mechi hauko sawa?

Katika ushindani wa kisiasa, kila advantage unayoweza kuitumia kufanikisha matokeo ya kisiasa ni sawa tuu mpaka itakapo kuwa haiwezekani Nixon case. Wewe huko uliko Trump anafanya nini kinyume na mwanasiasa yeyote ama wa ulaya au wa Africa akipata nafasi angeweza kufanya?

Siasa ndio profession pake yake ambayo haina formular maalumu ya kupata majawabu unayoyataka. The end justify the means.
A Machiavellian perspective.

Siasa sio Msikiti au kanisa it is the art of possible.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,751
2,000
Muona wangu na political strategist wote wanakubali: Magufuli ndio kiongozi aliye iimarisha CCM ambayo ilikuwa inaenda kujifia.
Na sasa hivi ndio chama imara kuliko muda wowote labda tuu wakati wa Nyerere.
Results ndizo zitakazo kuonyesha ubora wa kiongozi yeyote na sio vinginevyo. Kwa sababu hakuna formular maalumu inayofahamika kuwa sahihi kabisa kufikia unayoyataka kisisasa.

Uchaguzi huu na matokeo yake yatatupa nafasi ya kutosha kuandika daftari upya ya mifumo ya kisiasa mipya mbali tuliokuwa tukiifahamu. Hii itaongeza ufahamu kwa wengi ambao tunapenda kufuatia mienendo ya kisiasa.

Mimi ni upande wa upinzani lakini ni muhalisia katika uchambuzi bila kuweka upendeleo na kuongozwa na hisia kisiasa kwa kadiri nionavyo. Kwa umri wangu muda wa hisia ulikwisha kitambo.
Uimara gani unauzungumzia wakati wamekuwa wakitumia hila kila wakati?! Tangu Magu aingie madarakani, ni lini ametoa equal political playground kati ya CCM na vyama vya upinzani?!

Kama ni chama imara kiasi hicho kwanini kiliamua kufanya hila kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?!

Kama ni chama imara kiasi hicho, kwanini Magu alipiga marufuku shughuli za kisiasa lakini marufuku ikawa inafanya kazi kwa vyama vya upinzani pekee huku wao CCM wakiendelea kufanya siasa?!

Kama ni chama imara kiasi hicho, kwanini kimeendelea kufanya hila hadi kwenye mchakato wa uchaguzi ujao?!

Hebu jiulize: Wakati upinzani hawajafanya siasa za majukwaani tangu 2016, na hata walipojaribu kufanya vikao vya ndani walikuwa wanaletewa zengwe lakini muda wote huo CCM waliendelea kufanya siasa!!!

Yaani anafunga wapinzani mikono nyuma huku akiwa kawafunga vitambaa machoni, halafu aki-shine ndo useme ameimarisha CCM?!
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,127
2,000
Sijui kama kuna mtu mweye akili timamu angekuwa anamsikiliza Membe leo hii; hata wale wanaomsikiliza Lisu ni wale wanaopenda mambo ya umbeya tu, bila facts zozote.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom