Uchaguzi 2020 Bernard Membe hana kabisa mvuto!

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,519
Huyu jamaa, hana kabisa mvuto akiwa jukwaani.

Siasa kwake naona si jambo alilonalo kiasili.

Anajitahidi sana kuongea na kudondosha vibwagizo akiwa jukwaani, lakini wapi! Hamna kitu kabisa.

Maneno hayamtoki mdomoni kiulaini. Linganisha Lissu akiwa jukwaani na huyo Membe, ni usiku na mchana.

Sauti haina mvuto. Hana msamiati wa kutosha wa kuchotea vibwagizo kuendana na hadhira iliyo mbele yake.

Anachokiweza ni vijembe vya kimafumbo huko Twitter.

 
Ndio ujue wa-tz ni watu wa mikumbo kama vile hawamuoni siku hizi
Watz ni kama wasanii na followers wengi Instagram na ukitangaza show support kama lote hivi sasa siku ya show ndani ya ukumbi hutaamini macho yako watakao kuja ni kutoka gwambina wala sio insta na hawajawahi jiunga insta...

Membe na lissu wataponzwa na siasa za mitandaoni. Wapiga kura sio wajinga.
 
Lissu akienguliwa, huyo ndio mgombea.
Atabebwa na support ya chama.
Mbona Magufuli amepauka sana, lakini alishinda au kushindishwa?
Magufuli ana faida ya kuwa mgombea wa chama kilicho madarakani.

Ili kukiondoa chama kilicho madarakani, hususan katika mazingira yetu ambayo hayatoi fursa sawa, inahitajika kuwepo na hamasa kubwa sana.

Ili kuwepo na hamasa kubwa, ni lazima mgombea/ mshindani mkuu wa Rais aliyepo madarakani awe na uwezo wa kuwahamisha watu kwa kiwango cha juu kabisa.

Siasa ni hisia, pia.

Membe haamshi hisia za watu kama ambavyo Lissu anaweza.
 
Watz ni kama wasanii na followers wengi Instagram na ukitangaza show support kama lote hivi sasa siku ya show ndani ya ukumbi hutaamini macho yako watakao kuja ni kutoka gwambina wala sio insta na hawajawahi jiunga insta...

Membe na lissu wataponzwa na siasa za mitandaoni. Wapiga kura sio wajinga.
Mange Kimambi yalimkuta haya .... dada hatutakuangusha ... wengine wakatengeneza home made gas-mask ...siku ya siku barabara nyeupeeeeeee... wakarudi ooo tumeshinda wameandamana wao badala yetu .... 😂
 
Back
Top Bottom