Benki ya Dunia: Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine umesababisha hasara ya dola bilioni 60

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Uharibifu wa majengo na miundombinu ya Ukraine kutokana na uvamizi wa Russia umefikia hasara ya takriban dola bilioni 60 na utaongezeka zaidi kadri vita vinavyoendelea, Rais wa Benki ya dunia David Malpass amesema Alhamisi.

Malpass ameuambia mkutano wa Benki ya dunia kuhusu mahitaji ya msaada wa kifedha wa Ukraine kwamba makadirio ya awali ya gharama “finyu” za uharibifu hayajumuishi gharama za kiuchumi zinazoongezeka za vita vya Ukraine.

Malpass amesema “ Vita bado vinaendelea, kwa hivyo gharama zinaongezeka.”

Rais wa Ukraine akihotubia kwa njiya ya mtandao mkutano huo uliofanyika mjini Washington , ameelezea gharama kubwa zaidi na mahitaji ya kifedha. Amewambia washiriki katika matamshi yaliyotafsiriwa kuwa Ukraine inahitaji dola bilioni 7 kwa mwezi kufidia hasara ya kiuchumi iliyosababishwa na uvamizi wa Russia dhidi ya nchi yake.

Tutahitaji mabilioni ya dola kuijenga upya nchi baadaye,” Zelensky amesema.

Amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuiondoa Russia mara moja kwenye taasisi za kifedha za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Benki ya dunia na Shirika la kimataifa la fedha(IMF) na nyinginezo, na kusema nchi zote “lazima ziwe tayari mara moja kuvunja uhusiano wote na Russia.”

Mkutano huo ambao ulifanyika kando ya mikutano ya IMF na Benki ya dunia ya majira ya baada ya msimu wa baridi ulijumuisha maafisa wa fedha kutoka nchi kadhaa, akiwemo waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen, ambaye awali amesema Marekani itaongeza mara dufu ahadi yake ya msaada wa moja kwa moja usiokuwa wa kijeshi kwa Ukraine hadi dola bilioni 1.

“Nimejitolea kufanya kazi na washirika wetu kusaidia katika mahitaji ya kiuchumi ya Ukraine kwa muda mfupi na mrefu. Katika mkutano huo, nimeelezea ahadi ya ufadhili mwingine wa Marekani wa dola milioni 500 ili kuisaidia Ukraine kuendelea na shughuli muhimu za serikali, kama vile mishahara, pensheni na program nyingine za msaada wa kijamii zenye umuhimu ili kuepuka kuzorota kwa hali ya kibindamu nchini Ukraine,” amesema Yellen.

Waziri mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal, ambaye alihudhuria mkutano huo ana kwa ana, amesema pato la taifa la Ukraine linaweza kuporomoka kwa asilimia 30 hadi asilimia 50, na hasara ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja ni jumla ya dola milioni 560 kufikia sasa.

Kiwango hicho ni zaidi ya mara tatu ya ukubwa wa uchumi wa Ukraine, ambao ulikuwa sawa na dola bilioni 155.5 mwaka wa 2020, kulingana na takwim za Benki ya dunia.

Source: Korea Times

optimize.jpg
 
Yani hapo ndio utajua wamagharibi sio watu wazuri hata kidogo..kinachotokea Ukraine kilishatokea nchi saana,lakini leo hii Ukraine inaonekana km imeonewa na inahitaji msaada..Je mbona mpaka leo zipo nchi nyingi hao Wamerekan na Nato wameziharibu na zina hali mbaya kiuchumi na kibinadamu lakini hakuna msaada wowote?nazidi kuwachukia hawa watu.
 
Mrusi Kamatia hapo hapo Kwa Asad ,Gadafi,Iraq hawakuona leo wameona
Putin kandamiza mpaka Mashoga Yatoke yote kuropoka
Mungu ibariki Urusi
Ukraine haijawahi kushambulia Marekani wala kufadhili magaidi walioshambulia balozi za Marekani na Trade centre Kule Marekani na kufadhili akina Osama bin Laden

Akina Gadafi ,Sadam Hussein nk tofauti.Walibomolewa kwa uhalifu wao wa kufadhili ugaidi

.Ukraine ndio maana anasaidiwa usilinganisha na hiyo migaidi mingine
 
Ukraine naye anabomolewa sababu anataka kufadhari NATO na shughuli zake za kiharifu dhidi ya URUSi lakini anapigwa kwa sababu Analipa gharama za KUSALiTi wa mkataba wake Wa Warsaw ambapo alikiri mwenyewe hatafungamana na yeyote iweje awe msaliti wa maandishi yake.hivyo kila maamuzi yana gharama zake hizo ndo gharama anazolipia kwa maamuzi yake.
 
Ukraine haijawahi kushambulia Marekani wala kufadhili magaidi walioshambulia balozi za Marekani na Trade centre Kule Marekani na kufadhili akina Osama bin Laden

Akina Gadafi ,Sadam Hussein nk tofauti.Walibomolewa kwa uhalifu wao wa kufadhili ugaidi

.Ukraine ndio maana anasaidiwa usilinganisha na hiyo migaidi mingine
Sawa sawa
FB_IMG_16505433022315053.jpg
 
Russia will have to pay for war reparations as a precondition for lifting economic sanctions imposed on her, after all, she is the one who provoked the war.
 
Russia will have to pay for war reparations as a precondition for lifting economic sanctions imposed on her, after all, she is the one who provoked the war.
Inawezekana. Endapo kweli Wast wakiamua Russia alipe kwa miundombinu aliyoisambaratisha Kule Ukraine inawezekana.

Kivipi?

Mpaka Sasa,Gharama ya Miundombinu ya Ukraine iliyoharibiwa Ni $ 60B kwa mjibu wa IMF na WB.
Kwa upande Mwingine,Zaidi ya $ 309B za Hazina ya Urusi imeshikiliwa kwenye mabenki ya Marekani. Zaidi ya $ 308B ya fedha zinazomilikiwa na matajiri wa Urusi wenye mafungamano na PUTIN zimeshikiliwa nchini Uswizi. Pia Zaidi ya Meli ya Kifahari 78 zinazomilikiwa na OLIGARCH wa Urusi ambazo kwa pamoja Zina thamani ya $ 50B zimekamatwa kwenye Mataifa mbalimbali ya Ulaya,Asia,Amerika Kusini na Amerika Kaskazini.

Kama watazitaifisha zote na kuijenga Ukraine Basi Fedha zinatosha kuijenga Ukraine x 10.

Wasiwasi wangu

Nina mashaka makubwa kwamba,baada ya Vita kuisha Kuna uwezekano wa Mataifa mengi kuendelea Uhusiano wa kiuchumi na Urusi huku wakiiacha Ukraine kivyake.
 
Russia will have to pay for war reparations as a precondition for lifting economic sanctions imposed on her, after all, she is the one who provoked the war.
Kama pande zote zilitimiza makubaliano yao sawa , kama si hivyo hakuna kinachomhusu urusi........waliomtuma Ukraine ndio haohao itabidi wachukue jukumu la kuijenga hio nchi
 
Inawezekana. Endapo kweli Wast wakiamua Russia alipe kwa miundombinu aliyoisambaratisha Kule Ukraine inawezekana.

Kivipi?

Mpaka Sasa,Gharama ya Miundombinu ya Ukraine iliyoharibiwa Ni $ 60B kwa mjibu wa IMF na WB.
Kwa upande Mwingine,Zaidi ya $ 309B za Hazina ya Urusi imeshikiliwa kwenye mabenki ya Marekani. Zaidi ya $ 308B ya fedha zinazomilikiwa na matajiri wa Urusi wenye mafungamano na PUTIN zimeshikiliwa nchini Uswizi. Pia Zaidi ya Meli ya Kifahari 78 zinazomilikiwa na OLIGARCH wa Urusi ambazo kwa pamoja Zina thamani ya $ 50B zimekamatwa kwenye Mataifa mbalimbali ya Ulaya,Asia,Amerika Kusini na Amerika Kaskazini.

Kama watazitaifisha zote na kuijenga Ukraine Basi Fedha zinatosha kuijenga Ukraine x 10.

Wasiwasi wangu

Nina mashaka makubwa kwamba,baada ya Vita kuisha Kuna uwezekano wa Mataifa mengi kuendelea Uhusiano wa kiuchumi na Urusi huku wakiiacha Ukraine kivyake.
Hayo mengine yote ni sawa ila nina uhakika 💯% kwamba mataifa ya magharibi hayawezi kuitelekeza Ukraine kwa sababu ingekuwa hivyo wangeiacha toka mwanzo.

Pili hii ndio fursa pekee nzuri waliopata ya kuimaliza kabisa Russia na usije shangaa hizo pesa za Russia ndizo watakazotumia kuikarabati Ukraine.
 
Back
Top Bottom